Majibu yaliyotolewa leo na CHADEMA, ni ushahidi tosha kuwa hela zimepigwa

Hapa ndipo ninapopishana na wengi wenu. Ushahidi ili uwe ushahidi kuna kanuni zake za kufuatwa. Hayo maneno ya tuhuma ya Waitara siyo ushahidi.

Ndiyo maana nasema kama hela ziliwekwa si hata wataje akaunti hizo hela ziliwekwa na watia sahihi walikuwa wakina nani na ni kwa nini waliidhisha hela hizo zitolewe!!??
Chadema baada Dr Slaa kuondoka imekuwa ni kikundi Cha mataahira. Sioni namna ya kukuelewesha kuhusu hili. Watia saini ili mpunga utoke nao ni washiriki wa hilo deal chafu.
Km pesa iliwekwa kwaajil yamatumizi fulani kitendo cha kubadilishwa matumizi hasa kihunihuni kwenye taasisi kubwa km chadema ni aibu.
 
Kwa upande wangu, tukisimama kwenye hoja haiwezekani tuhuma zikatolewa na upande mmoja halafu tukatoa hukumu na bado tukajiona ni sisi ni 'great thinkers'. It's a joke! Kitu kingine, morally, kama hakuna ushahidi siyo ushahidi kuwa mtu hakula hela na wala siyo ushahidi kuwa mtu kala hela. Lakini kwa utaratibu wa kisheria tunazozifuata na kuzitumia, anayetuhumu ndiye anayepaswa kuthibitisha tuhuma zake. Mfano, A akisema B ni mwizi, basi A anapaswa athibitishe kuwa B ni mwizi. Vinginevyo, inakuwa tu 'vicious calumny' ambayo kama Watanzania inabidi tuepuke na tuondokane nayo na kama hatuwezi, itakuwa ndiyo tabia yetu. Maana leo tufanya hivyo kwa X, kesho kwa Y, keshokutwa kwa Z na tutaendelea hivyo hadi mwisho wa maisha yetu.
Tabia ya kuzusha mambo imeanzishwa na viongozi wa CHADEEMA kwenye majukwaa ya kisiasa. Kwa ushahidi, hivi karibuni Msigwa, Mchungaji feki, alikiri na kuomba msamaha kwake Kinana. Hivyo basi, ni mhimu tuhuma zilizotolewa na viongozi wa chama, zijadiliwe kwenye vikao vya chama.
 
Matukio ya kufanya wanaohituhumu CHADEMA wasiaminke ni kama haya hapa chini:-

1. Mbunge Lijualikali - Ameozeshwa kwa Spika Job Ndugai na ana ukaribu sana (kifamilia) na Spika na wasaidizi wake

2. Mbunge Selasini - Ndugu wake wa damu wote walirubuniwa na CCM wakakimbia upizani, Dr. Lamwai (RIP), DC Evodius Mmanda na yeye baada ya kujulikana kuwa ni bomu linalosubiri kulipuka wanachadema walimnyima kura za uenyekiti wa Kanda ya KASKAZINI

3. Mbunge Mwambe - Naye kioo kilimmulika wakati wa uchaguzi

4. Waitara, Dr. Mollel, Patrobas, nk. wamekirimiwa uwaziri na nafasi nyingine unategemea hawa waisifie Chadema wakati wana mkate wa CCM mdomoni.

5. Yale yale ya Rwakatare, Silinde na wengine, hawana cha kupoteza maana hata wawe watiifu kwa chama madhaifu yao hayawezi tena kuwapa nafasi za kugombea hivi wakaona vipande Thelathini ni muafaka.

Hii ni UYUDA tu.

Hiki kinachofanyika cha kununua wabunge na Madiwani ni mojawapo ya miradi ya serikali ya awamu ya 5. Pole yao maana hapo ndo MFUTIKO wa kisiasa.
 
Majibu siyo ushahidi wa wizi bali viambatanisho!! Mnaosema hela zimepigwa si angalau mtaje hata Akaunti moja iliyotolewa hela na ni nani aliyeidhinisha kutolewa kwa hizo hela!!
SIgnatories si tumeambiwa ni Mwamba? na katibu ALIYEMTEUA mwenyewe na mkurugenzi wa fedha ALIYEMTEUA mwenyewe?
 
Kijualike amesha kana na kutaja Mpaka alipo oa Ila nyie bado mnataka kumlisha matango
Matukio ya kufanya wanaohituhumu CHADEMA wasiaminke ni kama haya hapa chini:-

1. Mbunge Lijualikali - Ameozeshwa kwa Spika Job Ndugai na ana ukaribu sana (kifamilia) na Spika na wasaidizi wake

2. Mbunge Selasini - Ndugu wake wa damu wote walirubuniwa na CCM wakakimbia upizani, Dr. Lamwai (RIP), DC Evodius Mmanda na yeye baada ya kujulikana kuwa ni bomu linalosubiri kulipuka wanachadema walimnyima kura za uenyekiti wa Kanda ya KASKAZINI

3. Mbunge Mwambe - Naye kioo kilimmulika wakati wa uchaguzi

4. Waitara, Dr. Mollel, Patrobas, nk. wamekirimiwa uwaziri na nafasi nyingine unategemea hawa waisifie Chadema wakati wana mkate wa CCM mdomoni.

5. Yale yale ya Rwakatare, Silinde na wengine, hawana cha kupoteza maana hata wawe watiifu kwa chama madhaifu yao hayawezi tena kuwapa nafasi za kugombea hivi wakaona vipande Thelathini ni muafaka.

Hii ni UYUDA tu.

Hiki kinachofanyika cha kununua wabunge na Madiwani ni mojawapo ya miradi ya serikali ya awamu ya 5. Pole yao maana hapo ndo MFUTIKO wa kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema baada Dr Slaa kuondoka imekuwa ni kikundi Cha mataahira.
Tangu Dr. Slaa atoke CHADEMA hao mataahira ni wangapi wameshahamia CCM. Yaani CCM huwa inashangilia kupokea mataahira. Kama CCM huwa inafurahia kupokea mataahira yenyewe iko hali gani??
 
Mkuu Allen Kilewella, utaendeleza ubishi usio na faida kwa chama chako. Na wala sina haja ya kuendeleza mjadala na mtu asiyekubali ukweli.
Nikuulize swali rahisi tu. Leo hii Mbowe akijiuzulu nyadhifa zake zote na kuwa mwanachama wa kawaida tu, jee tayari CHADEMA itakuwa imeshasafishika na kuwa safi kuongoza Tanzania?

Baada ya Mbowe kuondoka nini kitafuatia ili ionekane kwamba kila ovu la Mbowe limeshughulikiwa ipaswavyo na CHADEMA??
 
Fuatilia milioni 350 pesa ya ruzuku ya CUF jinsi ilivyoainishwa kuchukuliwa kinyume na sheria NMB na kutajwa AC zote ilizopitia mpaka AC ya mtu binafsi.

Na lijuakali afanye hivyo.
Hii hoja imewazidi kimo. Sisi hatuzungumzii kama hela zimeliwa ama la, tunachozungumzia ni ushahidi wa hizo tuhuma kwa kuwa watoa tuhuma ni wakimbizi waliotoka CHADEMA na kupewa hifadhi CCM, Hapa inajulikana wanamfuruhisha mchinja mbwa ili wazimu usiwarudie!!
 
Nikuulize swali rahisi tu. Leo hii Mbowe akijiuzulu nyadhifa zake zote na kuwa mwanachama wa kawaida tu, jee tayari CHADEMA itakuwa imeshasafishika na kuwa safi kuongoza Tanzania?

Baada ya Mbowe kuondoka nini kitafuatia ili ionekane kwamba kila ovu la Mbowe limeshughulikiwa ipaswavyo na CHADEMA??
Chama cha siasa ni kama dini yoyote kwa kuwa ni kundi la watu wenye itikadi na imani moja kuelekea kwenye maisha mema na bora. Wakati Imani kidini ni matarajio ya maisha baada ya kifo, imani kisiasa ni maisha kabla ya kifo. Kwa maana hiyo chama cha siasa, kama ilivyo dini yoyote kinapaswa kuongozwa na watu wenye kujitolea, kwa kila hali, kuwatumikia watu (dini - waumini au chama cha siasa - wanachama)

CHADEMA kama chama cha siasa hakisafishiki kwa Mbowe kujiuzuru. Itikadi na imani ya chama itaishi milele kama zilivyo dini.

Naamini ni wachache wanaotaka Mbowe ajiuzuru. Na wenye kutaka iwe hivyo ni ambao hawajui falsafa hiyo hapo juu. Yawezekana, hata viongozi wa kiasiasa hawalijui hilo. Na iwapo Mbowe hajui kuongoza chama cha siasa ni kutumikia wanachama waweze kuishi maisha ya peponi duniani, basi hana budi kujiuzuru.

Shutuma dhidi yake zinashiria kuwa anaongoza chama cha siasa kimaslahi, lakini ukimsikia anavyotetea maslahi ya watu, ni kama nabii yeyote umewahi kumsikia au kusoma habari za maisha yake.

Akijiuzuru anatoa nafasi kwa wenye nia dhabiti kuongoza chama kwani tayari ITIKADI ya CHADEMA na inachokiamini inawapa matumaini ya maisha hapa duniani, wanachama wake.
 
Kwa maana hiyo chama cha siasa, kama ilivyo dini yoyote kinapaswa kuongozwa na watu wenye kujitolea, kwa kila hali, kuwatumikia watu (dini - waumini au chama cha siasa - wanachama)

Na iwapo Mbowe hajui kuongoza chama cha siasa ni kutumikia wanachama waweze kuishi maisha ya peponi duniani, basi hana budi kujiuzuru.

Dhana sahihi ya umuhimu wa chama cha siasa ni kuwatumikia wananchi WOTE - sio wanachama tu. Ni kuwaongoza wananchi wote kwenye njia mujarab itakayowaletea fanaka kimaendeleo na kutimiza maslahi yao kibinafsi na kitaifa. Ingekuwa lengo ni maslahi ya wanachama pekee (kikundi) basi hakuna sababu ya kuwapo (raison d'être) kwa vyama vya siasa.
 
Tangu Dr. Slaa atoke CHADEMA hao mataahira ni wangapi wameshahamia CCM. Yaani CCM huwa inashangilia kupokea mataahira. Kama CCM huwa inafurahia kupokea mataahira yenyewe iko hali gani??
Wanaohama ni wale waliostuka na kujielewa. Mataahira ni waliobaki.
 
Back
Top Bottom