Majibu ya Zitto kwa Kamati Kuu: Mashitaka yote sio ya kweli na sijavunja Katiba

Wakuu Mzigo wote Huu hapa wa Majibu Ya Zitto Kwa kamati Kuu ya CHADEMA,Ni majibu ya Kisomi,yenye Uangavu,Yenye taswira ya Mtu mwenye Kuona Mbali,Ni majibu Yanayowaacha Mbowe na Slaa(Team) midomo wazi,Ni Majibu ambayo Wajumbe wa baraza kuu wakiyasoma/Kuyasikia basi Zitto atawabwaga Mbowe na Slaa Vibaya sana.

Kumbe utetezi anao! Na kilichomfanya akimbilie mahakamani ni nini? Mi namshauri hata akitaka aendelee kuwa CDM ameshanjea kambi aondoke akaanzishe chama chake hafu afanye siasa kama nyota inang'aa atafanikiwa tu lakini kama nyota yake ilikuwa iking'aa kwa kushirikiana na bbadhi ya Viongozi wa Chama tawala atafulia kama alivyofulia Mrema
 
Zitto is Inocent,Wachafu ni Mbowe,Slaa na vibaraka wake Saanane.Nimepitia majibu ya huyu Kijana nimeshawishika akili yake ni sawa na akili za Wabunge wote wa chadema+Slaa mwenyewe
Subiri Ben anakuja sasa hivi...usitoke baruti tu! Msando anamchimbia bosi wenu kaburi...hakuna kikao ambacho upanga wa Slaa na Mbowe haupo! Usaliti wake umerekodiwa hadi kwenye video... suala la muda tu ...
 
zito ameambiwa ajitetee ili adhabu ya kunyang'anywa kadi isimkumbe, alivyoondolewa vyeo si adhabu, ni matakwa ya nidhamu ya taasisi (chadema)

Amepotea maboya ile mbaya. mhurumieni huyu kijana.
 
Tulipokuwa wadogo tulisoma hadithi ya Chui na mwanakondoo. Hivyo hata kama hukufanya maadam wameshaamuwa basi umefanya. Kitu kimoja nakiandika kwa Bold, ​Watanzania wakipenda kitu basi wataupamba mlio kama vile walimuona mbuzi mwenyewe. Neno usaliti nahisi halijulikani maana na wengi.
 
ili kuweka kumbukumbu sawa naomba mwenye link ya ule uzi ben aliyowaumbua kisha zitto akapanic na kuanza kujibu hoja kwa jazba...btw kumuita katibu mkuu mhe tena kwa unyenyekevu halafu hapo hapo unasema huna imani nae unaamini mahakama ! Imekaaje? Kwanini amekimbilia mahakamani wakati alipaswa kuwasilisha utetezi wake ndani ya chama na kama asingeridhika bado alikuwa na nafasi ya kwenda ngazi ya juu zaidi... Huu ni wakati muafaka sasa wa kumwaga details zitakazo mchakaza mwanzo mwisho ...usaliti sasa basi...
pole kwa kuumizwa
 
Kwema Mkuu,naona unajazba sana why?

Ulivuma kipindi cha masalia 8 oclock alipoonyesha mzigo ulipo ukatoweka ghafla sasa awamu ya waraka na siri umekuja na leo mtakesha jukwaani na temamate kumbuka hzo tuhuma zina ushahidi hebu tafakari hapo kwenye vikundi ben akipewa nafasi si ataonyesha tena mzigo ulipo mheshimiwa hapo sijui atawaambiaje.

Mnachoshindwa kuona mashtaka hayo licha ya waraka yana mpaka tuhuma za u masalia waliotajana wakati ule

Haya mambo si rahisi kama kujamba peke yako pakiwa hapana mtu.

We subiri ukiona manyoya ujue kashakibliwa
 
zito ameambiwa ajitetee ili adhabu ya kunyang'anywa kadi isimkumbe, alivyoondolewa vyeo si adhabu, ni matakwa ya nidhamu ya taasisi (chadema)

Amepotea maboya ile mbaya. mhurumieni huyu kijana.
Kamanda! Siyo ndiyo vizuri mumfukuze au?
 
Zitto anapaswa kupeleka utetezi wake kwenye kamati kuu na sio humu mtandaoni.
Nini mantiki yake?
Je, ni woga, kutojiamini, mbinu, kukurupuka, kujitetea ama nini hasa?
 
Tangu lini mwizi akakubali kwamba ameiba? Nakanusha,nakanusha,nakanusha ! mwongo mkubwa wewe! Subiri cha moto!
 
Mkuu tema mate unapoanza awali kwa kusema, mzigo wote huu hapa...

Una maana umeandali wa na CHAMA CHA MIZIGO??

Mapenzi yanakuumbua kama ngoswe unayachanganya kwenye kazi ya siri kweli mnakazi

Wakuu Mzigo wote Huu hapa wa Majibu Ya Zitto Kwa kamati Kuu ya CHADEMA,Ni majibu ya Kisomi,yenye Uangavu,Yenye taswira ya Mtu mwenye Kuona Mbali,Ni majibu Yanayowaacha Mbowe na Slaa(Team) midomo wazi,Ni Majibu ambayo Wajumbe wa baraza kuu wakiyasoma/Kuyasikia basi Zitto atawabwaga Mbowe na Slaa Vibaya sana.
 
Huu ukanusha si wa kiuweledi hata kdogo, kijana hana jipya anatapatapa.
Kwann anajiamnisha sana kwa baraza kuu? Zitto kama wewe ni msafi,ziachie mamraka ngazi husika ndani ya chama ziamue.
Usafi wako tutauona sisi wananchi km kweli una ndoto za kulitumikia Taifa hili kizalendo.
 
Mkuu tema mate unapoanza awali kwa kusema, "Wakuu Mzigo wote huu hapa...

Una maana umeandali wa na CHAMA CHA MIZIGO??

Mapenzi yanakuumbua kama ngoswe unayachanganya kwenye kazi ya siri kweli mnakazi

Au mko ki div 5 zaidi chini ya katibu mkuu Prof na Waziri Dr na Naibu shahada
Mkuu tanganyika ni muunganiko wa nini tena rejea South

Wakuu Mzigo wote Huu hapa wa Majibu Ya Zitto Kwa kamati Kuu ya CHADEMA,Ni majibu ya Kisomi,yenye Uangavu,Yenye taswira ya Mtu mwenye Kuona Mbali,Ni majibu Yanayowaacha Mbowe na Slaa(Team) midomo wazi,Ni Majibu ambayo Wajumbe wa baraza kuu wakiyasoma/Kuyasikia basi Zitto atawabwaga Mbowe na Slaa Vibaya sana.
 
Huu ukanushaji na ushahidi hauna nyama zakutosha!.
na kwann anajiamnisha sana kwa baraza kuu? Zitto kama wewe ni msafi,ziachie mamraka ngazi husika ndani ya chama ziamue.
Usafi wako tutauona sisi wananchi km kweli una ndoto za kulitumikia Taifa hili kizalendo.
 
"Maelezo ya Zitto Zuberi Kabwe
Ninasikitika sana kuona wanachama wa CHADEMA wanavyoweza kutumika kwa maslahi ya kundi fulani kuharibu heshima ya viongozi wao mbele ya jamii.

Ninaomba ndugu Ben Saanane aje hapa jukwaani kuthibitisha maelezo haya ya Bwana Mamuya kutoka Arusha. Mimi binafsi nikikutana na Ben Saanane leo naweza kupishana naye maana sijawi kumwona, wala kukutana naye. Ndugu Ben Saanane nimewasiliana naye kwenye simu mara mbili au tatu kuhusu masuala yake ya kitaaluma au pale alipohisi kuonewa ndani ya chama. Sijawahi kukutana naye hata siku moja. Kama nasema uwongo yeye binafsi aje hapa kukanusha.

Mimi pamoja na wenzangu tumejenga chama hiki mpaka hapa tulipofika. Tumeingiza watu kwenye chama hiki ili kwa pamoja tuweze kujenga asasi imara kabisa ya kidemokrasia. Chama hiki kina damu yangu. Chama hiki kina muda wangu. Chama hiki kina jasho langu. Nitakuwa mtu wa mwisho kusaliti chama hiki. Sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa tofauti na CHADEMA. Sitarajii kuwa mwanachama wa chama zaidi ya CHADEMA.

Ninawasihi wana CHADEMA tuache propaganda za kuchafuana. Nguvu kubwa inayotumika kumchafua Zitto ielekezwe kwenye kujenga taasisi imara ya CHADEMA, chama chenye demokrasia, kisicho na upendeleo, chenye uwakilishi wa kitaifa na chenye kuthamini nafasi ya kila mwanachama.

Mamuya, mara kadhaa umetaka kuniona kwa sbaabu nisizozijua na imekuwa ikishindikana. Unapata dhambi kubwa sana kumwaga sumu unayomwaga kwa mtu usiyemjua wala hujawahi kukutana naye.Acha kutumika. Jisimamie. Simamia chama.

Vijana, wote wa vyama vyote, siku zote simamieni misingi (principles) na sio kusimamia watu. Watu sio mawe. Mtaja juta. Misingi inadumu. Watu hawadumu. Acheni kuramba miguu ya watu. Simamieni misingi ya chama. Misingi ya nchi yetu. Misingi ya demokrasia. Kataeni kutumika.

Angalieni, wanaozungumzia sana usaliti waweza kuta ndio wasaliti wakubwa. wanazungumzia usaliti kama 'defensive mechanism'.

Tuacheni ujinga huu. Tufanye kazi. Kazi tu ndio kipimo cha ukamanda na sio kurambaramba visigino vya watu.

Mwisho, nasikia sikia sana habari za kuchinjana. Kuuana nk. Nasikia habari hizi kwa watu wale wale wa kikundi kile kile. Moja, natoka Kigoma. Nimeaga kwetu. Nitakufa kwa amri ya Mungu. Siogopi kufa. Iwapo kifo changu kitatokana na mkono wa mtu, sidhani kama kwa mtu huyo kama hata panya atabaki nyumbani kwao. Underline this.

Pili, revolutioneries don't talk about deaths. Only cowards do.
"
  • ...Sasa huyu Traitor na mbwembwe zote hizi kilichompeleka mahakani ni nini?...Kama alivyosema mwanakijiji Zitto alitakiwa kumwagwa long time ...
 
Back
Top Bottom