calmdowndear
JF-Expert Member
- Jul 12, 2011
- 605
- 273
Haya ndio majibu ya Zitto kwa Profesa KIKWETE:
Zitto kaanza kwa kusema hivi:
Our Leaders Must move away from culture of denials, cover-ups and proxies and deal honesty, sincerely and transparently with Tanzanians to regain their trust and confidence.
Tanzanians are no fools, they can see, they can hear, they can talk among themselves, they can think and they can act in the interest of their country.
[ largely borrowed from General Obasanjo's letter to President Jonathan of Nigeria ]. Found the words very relevant at the current circumstances in Tanzania
Kisha akaendelea kwa kusema hivi:
Nimemsikiliza Mhe Rais. Ninachoweza kusema ni kwamba maazimio yale hayakuwa ya Zitto Kabwe, PAC, CAG au PCCB. Yalikuwa ni maamuzi ya Bunge zima. Bunge la vyama vyote kikiwamo chama cha Rais Kikwete yaani CCM. Sisi kama Bunge tulitoa maazimio yale kwa maridhiano, uzalendo na bila kutaka kumuonea mtu yeyote.
Suala hili sasa naliacha kwa wananchi. Bunge limefanya kazi yake na Serikali ambayo ndiyo tulikuwa tunasubiri maamuzi yake imeamua hivyo. Wananchi wataamua wenyewe.
Kuweka rekodi sawa:
1. PAP ( sio IPTL ) wamelipwa tshs 306 bilioni.
2. Alizosema Rais ni zile zilizokuwa Benki kama taslimu na dhamana za Serikali.
3. Ambazo hakusema ni zile ambazo zililipwa na TANESCO baadaye.
4. Ifahamike hadidu rejea ( Terms of References ) kwa CAG kufanya uchunguzi zilitolewa na PAC, hivyo PAC ndio yenye mamlaka ya kuzisemea, kuzielezea na kuzitolea ufafanuzi.
5. Kwenye eneo hili Rais hakuwa sahihi na Ikulu inapasa kurekebisha. Jumla ya fedha ambayo PAP wamelipwa kutoka akaunti ya TegetaEscrow Ni tshs 306 bilioni.
Muhimu sana Mamlaka ya Kutafsiri Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali haipo kwa mkaguliwa ( Serikali ) Bali kwa Bunge. Bunge hufanya kazi hiyo kupitia Kamati ya PAC.