Majibu ya Udalali wa Wasaidizi wa kazi za ndani. Ufafanuzi wa kina

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,034
50,956
MAJIBU NA UFAFANUZI KUHUSU UDALALI/UWAKALA WA WASAIDIZI WA KAZI ZA MAJUMBANI.

Anaandika, Robert Heriel.
Wakala wa WASAIDIZI WA Ndani.

Bila Shaka wote ni wazima humu.
Andiko hili nitaeleza muhtasari wa suala la Wasaidizi wa kazi za ndani. Mimi nikiwa Mdau, na mkurugenzi wa Kampuni inayohusika na mambo haya.

Naamini andiko hili litakuwa msaada Kwa waajiri, Wafanyakazi, wakala, na serikali na jamii itapata manufaa na hilo ndilo lengo langu.

Nilianza kazi ya UWAKALA na kufungua ofisi ya UWAKALA WA WASAIDIZI WA MAJUMBANI mwaka 2018. Hivyo mpaka sasa ninauzoefu wa miaka mitatu. Sio miaka mingi Ila inatosha Kueleza jambo.

Ofisi yangu ililenga mambo Yafuatayo;
1. Kusaidia waajiri kupata Wafanyakazi bora na Kupunguza malalamiko Yao.

2. Kuifanya kazi za ndani kupata thamani, Kwa kuwalinda, kutetea maslahi Yao, na kutoa elimu.

3. Kuondoa dhana potofu kuwa kazi za ndani ni duni. Kwani zinaweza fanywa na hata mtu wa shahada moja. Katika hili wapo Vijana wakike na wakiume wenye mpaka Degree wanaofanya kazi hizi. Kama kuna watakaohitaji ushahidi wanaweza kuniona.

4. Kupunguza unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya waajiri. Kuanzia unyanyasaji wa malipo mpaka utendaji kazi.
Wafanyakazi wengi ambao Kwa utafiti nilioufanya wanalipwa sio zaidi ya 50,000/=

Ingawaje kazi hii inachangamoto nyingi lakini zote zinasuluhu yake.

KAZI za ndani zimegawanyika katika makundi Yafuatayo;
1. Housemaid or housemanager
Huyu huhusika na masuala ya Usafi wa nyumba, Kupika, Kuosha vyombo, Kufua, kupanga nyumba.

2. Housekeeping.
Hawa huhusika na Kusafisha nyumba tuu au maofisi. Hawapiki wala hafui wala Kuosha vyombo. Huhusika na Usafi.

3. Babysitter. (YAYA)
Kukaa na mtoto, kumtunza, kumlisha chakula, kumuozesha, Kuosha vyombo vya mtoto, Kufua nguo za mtoto na kazi zote za mtoto.

4. ELDER care (KUTUNZA WAZEE)
Kumuangalia Mzee, Kufua nguo zake, Kupika chakula chake, na kumpa kampani.

5. Pet care and livestock Keeping
Kuangalia mifugo ya nyumbani, kumtunza mbwa na Paka n.k

6. Gardening. (Muangalizi wa Bustani na mazingira)
Kuangalia mazingira ya nje na Bustani.


Watanzania wengi hasa Maboss tunakasumba mbaya Sana.
Unakuta mtu anamuajiri binti au kijana anasema ni Housemaid(houseboy au housegirl) alafu anamfanyisha mikazi mingi ambayo sio majukumu yake, unakuta huyo huyo Housemaid anafanya kazi ya Uyaya(kutunza watoto) huyo huyo anafanya Housekeeping au anamuuzisha Duka binti wa watu, huyo huyo anahangaika na Kufua manguo ya familia. Alafu Mshahara unataka umlipe 50,000/= thubutu!
Hilo kwangu haliwezekaniki, na linatia uchungu mno.

Nikijaribu kuuliza Kwa nini unalipa hiyo pesa Tsh 50,000/= mtu anakujibu, ati anakula kwangu, analala kwangu, anatumia sabuni, dawa ya mswaki na kila kitu kwangu.
Basi ninawaambiaga basi asile kwako, asikae kwako na usimpe chochote, yeye aje kufanya kazi. Mlipe 250,000- 300,000 anakataa.

Utapeli kwenye kazi hii upo Sana.
Lakini chanzo cha utapeli ni kipi Hilo lazima tujiulize. Ukweli ni kuwa utapeli upo Kwa Wafanyakazi, waajiri na hata madalali.

Sababu zifuatazo zinaweza kuwa chanzo cha utapeli katika sekta hii.

1. Roho mbaya na tabia mbaya za Waajiri.
Sio waajiri wote wenye roho mbaya. Ila ukweli ni kuwa 70% wanaroho mbaya na ndio chanzo kikuu ya utapeli.
Kwanza kumlipa mtu tuu hiyo 50,000 alafu akufanyia makazi mengi ambayo mengine sio majukumu yake ni sehemu ya utapeli.
Wengine hawatoi hata mishahara, wanawapiga danadana Wafanyakazi.

Kama unaishi na binti au kijana wa watu vizuri hawezi kuondoka kienyeji hapo nyumbani. Hawezi kutoroka. Lakini unamchukulia mfanyakazi Kama mnyama Kwa nini asikufanyia naye uhuni.

Mfanyakazi anayohaki ya kuabudu.
Kupumzika na ndio maana ninawaambia waajiri kuwa ni sharti mfanyakazi alale masaa yasiyopungua nane Kwa siku.
Lazima Kwa wiki awe na siku moja ya kupumzika. Lazima Kwa mwaka awe na siku walau 28 za likizo.
Yale mnayopenda kufanyiwa lazima nanyi mfanye vivyo hivyo.

Mfanyakazi anayohaki ya kutafuta mahusiano na wenzi wa maisha. Umri wa miaka 18 ni mkubwa, ilimradi asiathiri kazi yake.
Sio unamlimit binti au kijana Kama mfugo, Hilo haliwezekaniki, huyo sio mtumwa ni mtu Kama wewe.

Huwaga nawaambia na hata leo nawaambia, binadamu kila mmoja na nafasi Yao.

Mtu Kama unakipato kidogo usichukue mfanyakazi, fanya kazi zako mwenyewe. Au mchukue ndugu yako.

Kuna Ile kasumba kuwaona Wafanyakazi WA Ndani ni wachawi, ninaoushahidi wa kutosha pia wapo waajiri wachawi,
Mtu akija ofisini kwangu akiniomba Msaidizi akisema asiwe mchawi nami namuuliza nawe sio mchawi, huendagi Kwa waganga sio kujifanya wewe ni Bora kuliko mwenzako..

Hata hivyo zipo sheria za Ofisi pia ili kuweka mambo Sawa baina ya mfanyakazi na Mwajiri wake.

2. Utapeli wa Wafanyakazi, Dhana potofu na kujiona Duni.
Wapo Wafanyakazi wasio waaminifu ambao huwaumiza waajiri wao.
Huwaumiza Kwa namna nyingi. Kwa uzoefu wangu nimebaini mambo haya;
1. Wapo Wafanyakazi huwatapeli waajiri wao nauli. Hurumiwa nauli alafu hawatokei. Huu ni utapeli common na wengi wameshafanyiwa.

2. Wapo Wafanyakazi ambao hufika mjini(kazini) Kwa lengo la kupata pakufikia kisha wakishazoea mji huondoka. Hii ndio Ile unakuta anakaa wiki au miezi miwili anaondoka.

3. Wapo Wafanyakazi ambao ni mawakala wa nguvu za Giza ambao kazi Yao ni kuzurura kwenye majumba ya watu Kwa ajili ya kukusanya vitu Kama vywele, kucha na mambo mengine Kwa shughuli za kishirikina.
Ninaoushahidi wa mambo hayo kwani Kama nilivyosema ninahusika na shughuli hii na ninawateja kwenye miji mbalimbali hapa nchini.
Huwaumiza Kwa namna gani, hii ni mada nyingine.

4. Wapo Wafanyakazi ambao huchonga dili na madalali au mawakala wasiowaaminifu kuhamishwa ili Kula hela za wateja.
Hii pia ipo Sana.

5. Wapo Wafanyakazi ambao hupanga njama na ndugu au wazazi wao kumtapeli Mwajiri Kwa kudanganya vifo au magonjwa.
Hili pia ni kundi kubwa.

6. Wapo Wafanyakazi ambao hutumika kuvunja ndoa za watu iwe kikawaida au kimazingara. Hii ushahidi upo na inatokea Sana.

7. Wapo Wafanyakazi ambao hupanga njama au hutoroka wakiwa wameiba aidha Fedha au Mali zingine.
Hii wakati mwingine waajrii huwasingizia Wafanyakazi.

8. Wapo Wafanyakazi ambao wapo kwenye Mtandao wa kuiba watoto. Hili pia ninauzoefu nalo.
Hivyo umakini ni muhimu Sana.


3. UTAPELI WA MADALALI AU WAKALA WENYE MAKAMPUNI.
1. Wapo madalali ambao hula nauli za Waajiri Kwa ahadi ya kukuletea mfanyakazi
2. Wapo madalali au mawakala hupanga njama za kumuiba mfanyakazi kutoka nyumba moja kumpeleka nyumba nyingine wajipatie pesa.

3. Wapo madalali au wakala ambao huweza kumuibia wakala mwingine mfanyakazi Kwa kumuahidifanyakazi kuwa ofisini kwake mishahara ni mikubwa.

4. Wapo madalali na Wakala hupanga njama kumuibia au kumtapeli Mwajiri.

5. Wapo madalali au wakala ambao hushirikiana na Mwajiri kumfanyisha kazi haramu mfanyakazi iwe ni kijana au binti.


Mambo haya ninayasema Kwa uzoefu sio WA kusikia isipokuwa nipo Field hivyo ninaongea Kwa uzoefu.

Umakini mkubwa unahitajika, sio Kwa waajiri pekee Yao ambao wanafikiri kuwa wao ndio wapo spesho Bali hata Wafanyakazi kwani pia wapo waajiri wahuni.

Wapo waajiri wanaowafundisha Wafanyakazi WA kike ishu za kusagana, hii iliwahi tokea, wapo waajiri wenye mambo ya kishoga, hii iliwahi kutokea.

Hivyo wazazi pia mnalojukumu la kujua huko mtoto wenu anapoenda kufanya kazi wakoje.

Au mumkabidhi kwenye Kampuni lenye kujali na kusimamiwa maadili na utu.

Baada ya kusema hayo;

Ninapenda kuwataarifu Wale wote wanaohitaji Wafanyakazi WA MAJUMBANI na maofisini ninatoa Huduma hiyo.

VIGEZO na masharti kuzingatiwa. Tutalinda haki za Mwajiri lakini pia tutalinda haki za mfanyakazi.

Kama unatabia ya kunyanyasa na kujiona wewe ndio mtu na mfanyakazi ni mnyama natangaza tuu hatutawezana.

Zingatia pia mishahara inaendana kulingana na kazi.
Kama mfanyakazi atafanya kazi za Housemaid na Babysitter utamlipa mishahara miwili Kama kazi zilivyo.

Na Kama unandugu yeyote unayehisi anafanya kazi Kwa malalamiko na usalama wake ni mdogo unaweza MPA mawasiliano yetu.

Mafunzo pia yatatolewa ili kuondoa Ile Dhana potofu na kujiona Duni. Maana wapo Wafanyakazi ambao hawataki kupewa maelekezo, wakipewa maelekezo wanadai wananyanyaswa.

Mkataba utakuwepo.

Piga simu
0693322300
Robert Heriel
TAIKON WA FASIHI
Kwa sasa Dar es salaam
 
Nabii Tito anasema kazi ya mjakazi ni kumsaidia mama mwenye nyumba kazi zote hadi za kitandani

USSR
 
Kama huna hela usiajiri beki tatu. Bongo utamkuta anamilik bek3 halafu yupo kwenye chumba na sebule.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom