Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Anaandika Lissu:

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
 
Yale makontena aliyozuia pale bandarini atayaachia na mbaya zaidi atalipia fidia kwa fedha za walipa kodi ambao wana lundo la makodi. Tutaacha kusonga mbele na kujikuta tunarudi nyuma kulipia nothing. Huu ni ukweli japo ni mchungu sana! Uzalendo wa kweli kamwe hauambatani na faraja ya muda mfupi inayozaa msiba baadaye.

Nasisitiza kuwa tunaibiwa kwenye mikataba yetu tuliyosainiwa na miccm. Huko kwingine Magufuli anapiga tu maneno.
 
Najiuliza sana swali dogo tu kila nikiona post ya Lisu kiufupi nasubiri apost kuwa amepima yeye au kashuhudia upimaji wa huo mchanga na kajiridhisha kuwa hatuibiwi,nitamuelewa sana,tofauti na hapo aendelee kusoma takwimu na historia kwenye makaratasi hadi pale atakapo ikomboa nchi kwa takwimu na sheria
 
Sasa kwa taarifa yako wewe mpuuzi kuna kipengele kwenye mkataba kinachosema kuwa kinachochimbwa chote ni mali ya mwekezaji na sisi tutaambulia mrabaha ambao kila mwisho wa mwaka mnapeleka wakaguzi. Pia kumbuka kuwa kule ndani ya migodi mna maagent kibao mlioweka huko.

Ule mkataba aliosaini mkuu wako wa miaka 100 ndiyo chanzo cha tatizo.
 
Hilo lipo wazi kwa wafuatiliaji......nakumbuka jamaa alivyokuwa anapewa ulinzi na wananchi badala ya polisi wakati anapambana na hawa wazungu..........Zitto Kabwe alitimuliwa Bungeni kisa ishu ya madini......wakati haya yanatendeka ni kweli wanaofoka Leo walikuwa bungeni wakishabikia kumsulubu Zitto.
 
Kwenye siasa na hasa siasa za kipumbavu za ccm ni kutengeneza matatizo na kuja kujifanya wanayatatua baadae.....yaani hiki ni chama cha sanaa na wizi mtupu. Matukio mengine yapo hawayatatui mpaka watz wateseke ndipo wao wanakuja na kujifanya wanatatua.....

Magufuli was is and will never be a hero coz he is a member of corrupt system of ccm which consistently destroys watz.....

I will the very last person to agree on any move initiated by ccm
 
Najiuliza sana swali dogo tu kila nikiona post ya Lisu kiufupi nasubiri apost kuwa amepima yeye au kashuhudia upimaji wa huo mchanga na kajiridhisha kuwa hatuibiwi,nitamuelewa sana,tofauti na hapo aendelee kusoma takwimu na historia kwenye makaratasi hadi pale atakapo ikomboa nchi kwa takwimu na sheria
ukitaka kujua Tundu Lissu ni tahira hebu angalia anacho kiongea na sisi tunacho kiongea ni tofauti.
Yeye anafikiri watu wengi wana kataa kusafirishwa kwa mchnaga kumbe kikubwa kinachopingwa ni udanganyifu kwenye kilichomo kwenye mchanga... yeye alishawai kusema mikataba hii ni ya usiri sasa anaongelea nini kitu ambacho hajawai kukiona? hivi hiyo mikataba ndio inasema kuwa wawe wanadanganya kuna kiasi fulani cha dhahabu?
Hivi Tundu Lissu utahira atapona lini? Hata ACCACIA wanajua concern ya serikali ni kuhusu kiasi kilichomo kwenye mchanga au makanika na wao wanataka upimwe tena...

Lakini Tahira Lissu anapinga utafiti kwa tumbo na mdomo tuuu...
Mwenzie Zitto amenyamaza na kusema wazi kuwa utafiti hupingwa kwa utafiti..
 
185 Reactions
Reply
Back
Top Bottom