Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Sema tutu CCM Mheshimiwa Mbunge. MaCCM ndiyo chama gani ?Huyo Magu Kutetea tumbo lake na CCM wenzake akiwa mbunge Mbunge hakumzuii kupigania anachokiamini akiwa Rais....Hoja zako juu ya hasara za kufanya akifanyacho ni muhimu na unao uwezo na nafasi kutumia njia mbalimbali kumfikishia hoja na tafiti zako(kumbuka utafiti hupingwa na tafiti) badala ya kusubiri tuwe na hali ya Zimbabwe.

Tanzania ni yetu sote na ni muhimu kuliko chochote ukiweza omba hatabkukutana naye na umweleze haya badala ua kuyatumia kama karata yako kisiasa (kama anavyoitumia yeye/ kwa mujibu wa maelezo yako).

Tafadhari Mheshimiwa ziweke hoja na ushauri mbele kwa maslahi ya taifa badala ya kukazania kuwa aliyepitisha mikataba ni yeye na chama chake....Kuendeleza wimbo huu ni unafiki na uzandiki mkubwa, au ulitaka mambo yabaki kama yalivyokuwa ili iwe hoja ya vyama vyetu vya upinzani kila baada ya nusu muongo.
 
Najiuliza sana swali dogo tu kila nikiona post ya Lisu kiufupi nasubiri apost kuwa amepima yeye au kashuhudia upimaji wa huo mchanga na kajiridhisha kuwa hatuibiwi,nitamuelewa sana,tofauti na hapo aendelee kusoma takwimu na historia kwenye makaratasi hadi pale atakapo ikomboa nchi kwa takwimu na sheria
Anaingelea Mikataba Mama...
Hiyo inahitaji Vipimo kwani ?
 
Aliandika TUNDU LISSU KATIKA MTANDAO WA TANZANIA 2015 AND BEYOND FORUM
26/05/2017

Na mimi ni Mtanzania pia.
Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.
Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo wa yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo, then God have mercy on us!

[HASHTAG]#PrayForTunduLissu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#PrayForTanzania[/HASHTAG]
 
Aliandika TUNDU LISSU KATIKA MTANDAO WA TANZANIA 2015 AND BEYOND FORUM
26/05/2017

Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99...


Mtunze Babako na Mamako kwanza upate Baraka, usipoteze muda na Wasaliti utalaaniwa bure, Mungu hapendi Waaliti!
 
Aliandika TUNDU LISSU KATIKA MTANDAO WA TANZANIA 2015 AND BEYOND FORUM
26/05/2017

Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99...
MaCCM MACCM ndio waliompatie dhamana ya mali KAULI AKAPELEKWA NAIROBI
 
Tundu Antipas ni mzakendo tangu zamani halafu maCCM yanakuja kujifanya mazalendo kuliko mtu yeyote wakati ndio yameiuza hii nchi na rasilimali zake kwa mabepari. Mungu anawaona nyie wachumia tumbo,
 
Ccm mawakala wa mafisadi na mabepari kwa jhingia mikataba ya kinyinyaji huku wakijinufaisha matumbo yao. Wabunge wa ccm ndo muhuri wa serikali kupitisha uchafu wote tunaouona leo
Mbwa kabisa ccm
 
Clas
Lissu is a classic example of a loose cannon. Watu kama Lissu ni wazuri sana kuongea lakini ukimkabidhi zizi mifugo yote itakufa kwa funza. He will do nothing apart from lecturing the planet earth. No wonder baada ya miaka 8 alikuwa matapishi, shamelessly.


Classic hypocrisy will never take us anywhere, a person who replaced institutional leadership with personal decree-ship will never take us anywhere, Leaders are born, the guy is typically not a leader, just a mechanical one, leadership without vision, leadership wisdom, leadership without self discipline, leadership without holding a true sense of humanity, Leadership without basic economic knowledge, leadership with zero experience in diplomatic issues, leadership with zero level of tolerance, This is not a leadership rather than a personal decree-ship. Lissu will always remain as a true patriotic person of our times.
 
Naomba majibu ya hili swali hadi leo sijapata.

Kwanini Lissu alikiwa anawetetea sana Barrick na kutishia kwamba tutashitakiwa? Alikuwa na nia ya dhati kweli ama alikuwa anatetea ulaji wake tu? Ama ilikuwa sehemu ya siasa kwamba ukiwa upinzani lazima upinge kila jambo?

Nikijibiwa nikaelewa basi kura yangu kwake.
 
Hakuna mtu amewatetea barrick kama Magufuli.

Serikali ilisema inawadai barrick usd 191 billion.

Kitu cha ajabu deni likateremshwa mpaka kuwa usd 300 million.

Yaani ni sawa na udai shilingi 630+ halafu ukubali kulipwa shilingi 1, tena ulipwe kidogo kidogo.
 
..hakuna mtu amewatetea barrick kama Magufuli.

..serikali ilisema inawadai barrick usd 191 billion....
We ni miongoni wa wale walomuamini lisu eeeh.

Punguza unyumbu brother,next time utatumbukizwa shimoni ujue Kama hujui lolote ndani ya nchi hii.

Utakua Katika kundi linaloamini Lissu ndo Rais wako baada ya 28/10.
Bila Shaka atakua Rais wa nyumbu
 
We ni miongoni wa wale walomuamini lisu eeeh.

Punguza unyumbu brother,next time utatumbukizwa shimoni ujue Kama hujui lolote ndani ya nchi hii.

Utakua Kayla kundi linaloamini Lissu ndo Rais wako baada ya 28/10.
Bila Shaka atakua Rais wa nyumbu

..Jpm ametusaliti ktk madai yetu dhidi ya barrick.

..tena alikutana na mabosi wa barrick ikulu.

..kwanini alikutana na watu/majizi waliokuwa wakituibia madini?
 
Back
Top Bottom