Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Kuliko hata mkapaa
kwa hio tunahitimisha kwamba magufuli hausiki...ni hicho tu hao kina mkapa watajiju..kwa sababu yeye kawa raisi wanasahau watu wabovu kabisa na waliosapoti ujinga ndio wanawaongoza kwenye chama chao...bora kina mkapa tunaweza kuwasamehe kwa kumpitisha raisi wetu.....sio hao wengine na nawaambie huyo lowasa ameondoka ccm kwa sababu alikatwa..angepita asingekua upinzani leo....kwa hio basi nahitimisha kusema kua lowasa na team yake iliohamia huko sio wakombozi kwa taifa hili na hawatokaa wawe wakombozi daima..kina dk slaa waliokua wanasema vitu vya kweli watu wakamdharau
 
Kwahiyo kwa sab hakupinga asipinge for good? Mbona swali rahisi tu.
Mbona jibu unalo tena rahisi sana yani ukubali kwa mikono miwili halafu unakuja kupinga kirahisirahisi ilihali unajua Madudu ambayo yamefanyika yanaathiri vizazi na vizazi na gharama yake ni kubwa na unawadanganya watanzania kuwa una uchungu wakati nawe ni sehemu ya matatizo hayo..wanafiki siku zote huwa wapo pamoja
 
Sasa kwa taarifa yako wewe mpuuzi kuna kipengele kwenye mkataba kinachosema kuwa kinachochimbwa chote ni mali ya mwekezaji na sisi tutaambulia mrabaha ambao kila mwisho wa mwaka mnapeleka wakaguzi. Pia kumbuka kuwa kule ndani ya migodi mna maagent kibao mlioweka huko.

Ule mkataba aliosaini mkuu wako wa miaka 100 ndiyo chanzo cha tatizo.
Bro umepaniki na nina wasiwasi na elimu yako
 
Kwenye siasa na hasa siasa za kipumbavu za ccm ni kutengeneza matatizo na kuja kujifanya wanayatatua baadae.....yaani hiki ni chama cha sanaa na wizi mtupu. Matukio mengine yapo hawayatatui mpaka watz wateseke ndipo wao wanakuja na kujifanya wanatatua.....
Magufuli was is and will never be a hero coz he is a member of corrupt system of ccm which consistently destroys watz.....
I will the very last person to agree on any move initiated by ccm
Punguza jazba broo, composure
 
Kwa akili yako maana ya mkataba mbovu unaelewaje? Na unipe madhara ya mkataba mbovu ili twende sawa
Labda unijuze wewe ni kipengele gani katika huu mkataba mbovu kinachowaruhusu ACACIA kutudanganya ni kiasi gani cha dhahabu kilichopo katika huu mchanga wanaosafirisha.
 
Labda unijuze wewe ni kipengele gani katika huu mkataba mbovu kinachowaruhusu ACACIA kutudanganya ni kiasi gani cha dhahabu kilichopo katika huu mchanga wanaosafirisha.
Kweli wewe fyatu umefika ugoto wa kufikiri unaulizwa swali nawe unauliza swali ambalo majibu yake ungeyapata ndani ya nini maana ya "mkataba mbovu" na siku za wikiendi jaribu kujisomea ni namna gani mikataba mizuri Inakuwa na tija kwa taifa wala janjajanja hakuna mfano mzuri Botswana na tulisaini hiyo mikataba miaka inayofanana..
 
Kweli wewe fyatu umefika ugoto wa kufikiri unaulizwa swali nawe unauliza swali ambalo majibu yake ungeyapata ndani ya nini maana ya "mkataba mbovu" na siku za wikiendi jaribu kujisomea ni namna gani mikataba mizuri Inakuwa na tija kwa taifa wala janjajanja hakuna mfano mzuri Botswana na tulisaini hiyo mikataba miaka inayofanana..
Kama nyie ndio wasomi wa upinzani mliobobea basi mwenyezi Mungu atunusuru mtakaposhika dola.

What a waste.
 
Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa

Yakhe,
Unajaribu kupinga ili kujifurahisha kwa muda tu! But the truth shall stand forever! Anachosema Tundu Lissu ni UKWELI MCHUNGU NA UTAENDELEA KUBAKIA HIVO until otherwise!!
Ripoti ya Kamati ya Mchanga wa Magufuli ni USANII uliopambwa na kukolezwa ili kumubeba Magufuli kisiasa!!!
Just try to think a little bit.Kwanza hii kamati haikuwa Transparent iliamua kujifungia na kukurupuka kama kichaa. Pili Kamati hii ilipashwa kuwashirikisha ACACIA na TMAA ili kuja na uchunguzi shirikishi kwa kutumia mashine za ACACIA ambazo wamekuwa wakizitumia miaka yote na baadaye kutumia za Tume ya Mchanga kama zipo!
Lakini yote 2 hayakufanyika na hapo ndipo shida inakoanzia na kizungu mkuti kinapoanzia!
Tayari ACACIA wameomba Tume Huru kurudia UCHUNGUZI HUO na kama CCM wataridhia basi wajue Magufuli na Serikali yake wamekwenda na maji!!!!!
 
"Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered".

wazungu walijaribu kupunguza makali wakasema hivi:
If the amount of gold in our concentrates was in line with the Committee findings, then it implies that both Bulyanhulu and Buzwagi would produce more gold than any other mine in the world. Sadly this is not the case.
......
. ....Salute
 
Na kwa kuongezea tu, namnukuu na Mh. John Mnyika (Mb) mwaka 2012...

14 Oktoba, 2012

Tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani niliitaka Serikali kueleza ni kwanini mpaka sasa kiasi cha dola milioni 20.1 zilizopunjwa kifisadi hazijareshwa na kuitaka serikali iache kutumia kisingizio cha kuundwa kwa Timu ya Majadiliano (GNT) kuchelewesha utekelezaji wa maazimio, suala ambalo Wizara ya Nishati na Madini itapaswa kueleza hatua iliyofikiwa iwapo Spika atazingatia mwito huu na kuchukua hatua za haraka.

Ifahamike pia kwamba mwaka 2011 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini niliitaka serikali kuweka wazi bungeni na kwa umma mikataba ya madini, mafuta na gesi asili katika nchini ili kuongeza tija na uwajibikaji.

Aidha nilitoa mwito mwito kwa wananchi na wabunge kuongoza marekebisho ya kikatiba na kisheria ili kuweka vifungu vya kulazimisha uwazi katika mikataba katika hizo muhimu kwa uchumi na usalama wa nchi.

Uwazi katika mikataba utadhibiti pia mianya ya ufisadi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa serikali kwa kuwa mikataba hiyo itajadiliwa na umma na hivyo kupunguza uwezekano wa viongozi kutanguliza maslahi binafsi na kuwa na mikataba bora ya baadaye yenye kuzingatia maslahi ya umma.

Usiri katika mikataba ni tatizo kwa sababu masharti kama ya kushughulikia madhara ya kimazingira na kuchangia katika huduma za jamii pamoja na kulipa kodi zinazokusudiwa yanaweza yasitekelezwe kwa ukamilifu kama hayatafahamika kwa wabunge na umma. Aidha, ipo mikataba yenye vifungu ambavyo vinakinzana na sheria nyingine ama vinalinda kupindukia makampuni dhidi ya sheria nyingine za nchi zinazotungwa masuala ambayo yanaingilia mamlaka ya bunge ya kutunga sheria na kuisimamia serikali.

Sheria mpya ya madini Tanzania ya mwaka 2010 ina kifungu kinachotaka uwazi hata hivyo kimejikita katika uwazi wa rekodi na ripoti hakijaweka bayana mfumo wa uwazi katika mikataba ya madini, sheria ya mafuta nayo haina kifungu cha uwazi katika mikataba na sheria ya gesi haipo kabisa; hali ambayo inahitaji kurekebishwa.

Pamoja na mapato uwazi katika mikataba utachangia katika kupata tija ya ziada katika uchimbaji kwa kulinda maslahi ya wafanyakazi na kuweka mfumo mzuri zaidi wa makampuni kununua bidhaa za ndani kwa majibu wa vifungu vya mikataba hali ambacho itawezesha rasilimali kunufaisha wananchi wengi zaidi.

Uwazi katika mikataba utawezesha wabunge na wadau wengine kusimamia ipasavyo taasisi za kiserikali kuhusu mifumo ya kifedha na kibenki ambayo itaongeza mchango wa sekta za nishati na madini katika kuimarisha uchumi kwa kudhibiti mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu wakati huu ambapo thamani ya mauzo imeongezeka duniani lakini mzunguko umejitika katika masoko na mabenki ya nje.

Kwa ujumla, uwazi katika mikataba utapanua pia uwajibikaji wa kuongeza umiliki wa nchi na wananchi wa michakato ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili.

Pamoja na kuwa ibara ya nne ya katiba inasema kwamba rasilimali na mali asili zote ziko chini ya usimamizi wa serikali; na ibara ya 63 inaeleza kwamba bunge ndicho chombo kikuu cha kuisimamia serikali kwa kutunga sheria na kupitisha mipango, katiba haijalazimisha mikataba ya madini, mafuta na gesi kuridhiwa na bunge hivyo katika kipindi cha sasa mikataba hiyo iwasilishwe kwa rejea na mapitio.

Katika muktadha huo, tarehe 4 Oktoba 2012 nilimtaka Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo afute taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuwa lengo la agizo lake la kupitiwa kwa mikataba yote 26 ya utafutaji mafuta na gesi asili ni “kuhakikisha kwamba endapo kuna mapungufu katika mikataba hiyo, mapungufu hayo yasijirudie tena katika mikataba mipya ya baadaye” kwa kuwa ikiachwa ilivyo italinda ufisadi na kukwaza utetezi wa rasilimali za taifa.

Nilieleza kwamba ufafanuzi uliotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini unatoa mwanya kwa mikataba mibovu kulindwa wakati ambapo kuna madai tuliyotoa toka mwaka 2011 kwamba baadhi ya mikataba hiyo imeingiwa kifisadi na mwaka huu wa 2012 zimeibuka tuhuma za vigogo wa serikali kuingiziwa fedha kifisadi katika akaunti zao za nchini Uswisi na makampuni ya nje ya utafutaji mafuta na gesi asili.

Aidha, pamoja Serikali kuwasilisha bungeni mikataba inapaswa pia kuwasilisha mipango kabambe (master plan) ya mafuta na gesi asili yenye kuzingatia mabadiliko ya kisera na kimfumo yenye kuwezesha nchi na wananchi kunufaika na rasilimali husika.

Kauli hii nimeitoa leo tarehe 14 Oktoba 2012 ikiwa ni Siku ya Kumbukumbu ya Hayati Julius Nyerere ambaye alipinga ufisadi na kutaka rasilimali za nchi zitumike kwa manufaa ya maisha ya wananchi:

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

NB: John Pombe Magufuli ni miongoni mwa wabunge/mawaziri wa CCM waliokuwa mstari wa mbele kudai mikataba ni siri haiwezi kutolewa kwa wananchi. Miongozi mwa wabunge vijana waliomtetea Prof. Sospeter Muhongo wakati huo ni Dr. Hamisi Kigwangala akiunga mkono mikataba kuendelea kuwa siri. Ajabu ni kwamba leo kwa unafiki na bila haya anao ujasiri wa kusimama bungeni na kumtuhumu Muhongo eti kwa uongo uliotukuka!

Kwa kweli Wapinzani walijitahidi sana...tatizo ni Chama cha Mapinduzi na serikali yake ambamo John Pombe Magufuli alikuwa sehemu yake kwa miaka zaidi ya 20; miaka 10 chini ya Mkapa na miaka mingine kumi chini ya Kikwete kwenye ngazi ya uwaziri. Wakati huo wazalendo kama Tundu Lissu wanawapigania wananchi hadi kusweka ndani kwa kutetea rasilimali za taifa.
.....
.....watu mna Kumbukumbu
 
..jaribu kuwa balanced.ukishindwa
hilo jaribu ktk mijadala hii kuchambua "mchele" na "pumba" uachane nazo.

..hayo mambo hayatokei tu. Kuna mahali tumejikwaa. Ni lazima tupajue, na siyo kuwa fixated na tulipoangukia.

..kwa maoni yangu, mazingira mabovu ya kisiasa yamesababishwa au yanachochewa na Mzee mwenyewe.

..kwa maoni yangu Mzee haamini ktk dhana ya demokrasia ya vyama vingi. Hili nililisema tangu hajawa "mtu mkubwa."

..Lingine nadhani haamini ktk rule of
law. Anataka yeye asimike sheria na taratibu.

..Zaidi Mzee hana uvumilivu kwa yeyote mwenye mawazo tofauti na ya kwake. Jaribu kumsikiliza jinsi anavyowaadhiri wale aliotofautiana nao kimtizamo.

..Kwa maoni Mzee ndiyo chanzo cha kuchafuka kwa hali ya kisiasa na kijamii nchini. Vilevile ndiyo kikwazo cha hali hiyo kutengemaa.

SAKATA LA MIKATABA YA MADINI.

..CCM walipaswa kuonyesha UUNGWANA kwa kukiri makosa ya kuruhusu dhuluma hii iendelee kwa miaka 15++.

..RAISI na Mwenyekiti wa CCM alipaswa kuliomba RADHI taifa kutokana na maamuzi ya serikali za CCM yaliyolitia taifa hasara.

..Raisi alipaswa kutambua mchango wa wanaharakati kuwa walikuwa sahihi na waliweka maslahi ya taifa mbele.

..Katika hili WANAHARAKATI walitakiwa kutambuliwa kama MASHUJAA wa taifa letu.

..Kama kiongozi alipaswa kuliunganisha taifa na kusititiza umuhimu wa mchango wa kila Mtanzania.


..Baada ya hapo sasa ndipo Raisi angetangaza vita dhidi ya wawekezaji wanaotuibia.

Cc Nguruvi3
Kweli wewe ni JK . . ,

Umesema vizuri sanaaa . .
 
Najiuliza sana swali dogo tu kila nikiona post ya Lisu kiufupi nasubiri apost kuwa amepima yeye au kashuhudia upimaji wa huo mchanga na kajiridhisha kuwa hatuibiwi,nitamuelewa sana,tofauti na hapo aendelee kusoma takwimu na historia kwenye makaratasi hadi pale atakapo ikomboa nchi kwa takwimu na sheria
Kwa nini wewe uiamini tume iliyopima yenyewe bila wawakilishi wa Acacia kushirikishwa.Just imagune,kama wangekuja na vipimo vile vile vya Acacia vya mwanzo,je mngewaamini?Si ngeanza kusema nao wamehongwa na Acacia?..Je hakuna uwezekano kwamba Tume imeleta yale majibu ili kuwa please wa TZ na rais?..
Ni kwa nini acacia hawakushirikishwa kama sababu ilikuwa ni kupata ukweli?,just think freely..
Ilishindikana nini kukaa na Acacia na kuunda indeprndent Committee ihusike na upimaji ili kuridhisha party zote..Yaani haiwezekani ukawaondoa Acacia kwenye hili zoezi sababu wao ni party of tha contract na chochote kitachotokea kitawaathiri moja kwa moja.
 
Lopo lopo, mbunge sijui lini kawajali wananchi wake.
Rais wa nini sijui, wakili anayejiita msomi. Sijawahi kumwelewa huyu mtu.
 
Back
Top Bottom