Majibu ya Sitta kwa Dr Slaa: Asema Dr Slaa Mnafiki, Dikteta

Namheshimu sana Mzee wangu Sitta lakini hoja yake kuhusu wembamba wa safu ya uongozi wa Chadema, hasa kama hoja yake ya msingi kwanini Chadema hawapo tayari kutawala ni hoja nyembamba sana; isitoshe hao viongozi kama Kawawa, alikuja kuwa KAWAWA baada ya TANU kukamata uongozi; Fundikira alikuja kuwa FUNDIKIRA baada ya TANU kukamata uongozi; same applies kwa orodha ya viongozi wote including Mwalimu; vinginevyo kabla ya hapo, wote walikuwa wanaharakati waliojiunga TANU 1954, na kuja kutwaa madaraka ya nchi miaka saba tu baadae (1954 - 1961); Kinachohitajika na chama cha siasa ni LEADERSHIP, it could be one charismatic leader ambae anazaa followers who later proceed to become LEADERS as well; Mwalimu was the only LEADER wa TANU, and it is because of his influence, he attracted others who later became leaders, ingawa none kwa kiwango chake;

YESU na MTUME wote hawa walikuwa viongozi, and we all know how they influenced people from different walks of life who later became followers...then leaders..., both BELIEVERS AND NONE BELIEVERS; It has to begin from somewhere;

Ninaandaa makala kumjibu Mzee Sitta, kama mwanachama mwenzake wa CCM ninayeamini katika dhana ndani ya chama chetu kwamba kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi. Kwanini nataka fanya hivi? Kwa sababu nina amini kwamba BILA CHADEMA MADHUBUTI, CCM MAKINI HAIWEZEKANI!

Hiyo para yako ya pili ungeindoa kwani haileti maana wala kuongeza uzito kwenye hoja yako kwani ni masuala ya imani zaidi.
 
\


Bwana mkandinga unachanganya mambo pengine kutokana na kuzidiwa na mapenzi kupita kiasi,unaweza kuonyesha kwa ku quote ni wapi mzee sitta amaeonyesha kudharau kazi ya u dj au ni wapi mimi ama mzee sitta tumesema kwa kuandika kwamba free aliwahi kuwa Dj?

mzee sitta kwa mfano alichosema mchango wa bwana mbowe kwenye mambo ya burudani hauwezi ukadharauliwa wakati unataja cv yake.

Na kuhusu elimu unaweza kunisaidia kujua kiwango cha elimu ya mbowe na mambo aliyosomea?
Kim kwanza dharau hazifai.. kuniita Mkandinga wakati unalijua jina langu umeanza na dharau na ndivyo ulivyo hata ya Sitta huwezi kuyaona kwa sababu dharau ni hulka yako wakati wewe mwenyewe huna kitu, sii elimu wala maisha lakini unapenda sana kuzungumzia ya wengine. Sisi wote tumeisoma hotuba ya Sitta na kama amesema vinginevyo hatuwezi sote kuwa wajinga kiasi hicho..
 
Hiyo para yako ya pili ungeindoa kwani haileti maana wala kuongeza uzito kwenye hoja yako kwani ni masuala ya imani zaidi.

Lessons juu ya uongozi zipo nyingi sana kwenye Biblia na Quran na hakuna tatizo lolote kutumia experiences husika kwani leadership limekuwa ni suala universal, unless you have something else in mind; Otherwise ukipata muda jaribu kutafuta kitabu hiki:

THE BIBLE ON LEADERSHIP: FROM MOSSES TO MATHEW - MANAGEMENT LESSONS FOR CONTEMPORARY LEADERS [BY LORIN WOOLFE]; ISBN:0-8144-06823;

Pia suala la imani hata katika siasa lipo, kwa mfano, imani ya CCM ni pamoja na:

-Binadamu wote sawa;
-Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake;
-Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru;
 
Namheshimu sana Mzee wangu Sitta lakini hoja yake kuhusu wembamba wa safu ya uongozi wa Chadema, hasa kama hoja yake ya msingi kwanini Chadema hawapo tayari kutawala ni hoja nyembamba sana; isitoshe hao viongozi kama Kawawa, alikuja kuwa KAWAWA baada ya TANU kukamata uongozi; Fundikira alikuja kuwa FUNDIKIRA baada ya TANU kukamata uongozi; same applies kwa orodha ya viongozi wote including Mwalimu; vinginevyo kabla ya hapo, wote walikuwa wanaharakati waliojiunga TANU 1954, na kuja kutwaa madaraka ya nchi miaka saba tu baadae (1954 - 1961); Kinachohitajika na chama cha siasa ni LEADERSHIP, it could be one charismatic leader ambae anazaa followers who later proceed to become LEADERS as well; Mwalimu was the only LEADER wa TANU, and it is because of his influence, he attracted others who later became leaders, ingawa none kwa kiwango chake;

YESU na MTUME wote hawa walikuwa viongozi, and we all know how they influenced people from different walks of life who later became followers...then leaders..., both BELIEVERS AND NONE BELIEVERS; It has to begin from somewhere;

Ninaandaa makala kumjibu Mzee Sitta, kama mwanachama mwenzake wa CCM ninayeamini katika dhana ndani ya chama chetu kwamba kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi. Kwanini nataka fanya hivi? Kwa sababu nina amini kwamba BILA CHADEMA MADHUBUTI, CCM MAKINI HAIWEZEKANI!

Bahati mbaya sana Nyerere was a lone rider save a handful members such as Sokoine, Kawawa sijui na kina nani tena? Most of his followers have proved notorious to this nation exactly his opposite. Many of them have deliberately and repeatedly raped the party constitution and sometimes the national constitution too. To many they are defectors but unfortunately they don't know nor are they ready to know. What do you call a party whereby most of its leaders do not respect its creed i.e. constitution? They tell lies, practice corruption, etc. in broad day light and bless such practices with words such as takrima, hakuna ushahidi wa vitendo vya rushwa, mafisadi wana nguvu sana! Kweli? Mchambuzi nieleweshe please!!!
 
Mimi nawaambieni hakuna mtu manafiki kama slaa mtakuja kuniambia hapa yule mzee anaramani zake pale mahali pakupiga pesa tu kumlisha yule mchumba wake

Umeamua kuchekesha wana JF huyo mchumba gani tena si wameshafunga ndoa? Hata hivyo huyo mwana mama anakula tembo mmoja kwa siku mpaka Dr. Slaa ashindwe kumlisha kwa kipato chake cha sasa?
 
Mzee Sitta anazidi kujidhalalisha afadhali angekaa kimya tu. Yaani anaudhi hadi basi. Tena hajielewi hayo maelezo yake yanazidi kukijenga CHADEMA
 
Bahati mbaya sana Nyerere was a lone rider save a handful members such as Sokoine, Kawawa sijui na kina nani tena? Most of his followers have proved notorious to this nation exactly his opposite. Many of them have deliberately and repeatedly raped the party constitution and sometimes the national constitution too. To many they are defectors but unfortunately they don't know nor are they ready to know. What do you call a party whereby most of its leaders do not respect its creed i.e. constitution? They tell lies, practice corruption, etc. in broad day light and bless such practices with words such as takrima, hakuna ushahidi wa vitendo vya rushwa, mafisadi wana nguvu sana! Kweli? Mchambuzi nieleweshe please!!!

Kwa kweli haiingii akilini, na sijui ni kwanini viongozi wa CCM wanahamaki wanapoona Chadema wanazidi kusambaa kama moto wa nyika; kuhusu suala la rushwa kama ulivyojadili kidogo, inashangaza kwanini tunakuwa na vyombo vya TAKUKURU na DPP separately kwani jambo hili ndilo linapunguza kasi ya kushughulikia ufisadi, kwani TAKUKURU haiwezi kushughulikia kesi yoyote bila ya DPP kukamilisha kazi zake; Ni vigumu kuelewa kwanini wabunge wanaoonyesha uzalendo na nchi yao hawapeleki masuala kama haya kama Hoja Binafsi ili zijadiliwa na ikiwezekana in the process, muswada wa kurekebisha hili upitishwe; Vinginevyo uwepo wa TAKUKURU na DPP maana yake ni kama vile suala la Ufisadi limewekewa mazingira ya Checks and Balance? Ni madhaifu kama haya ndio yanazidi kukigharimu CCM;
 
Sita ni mnafiki, wala hana jipya. Wenzake akina mwakyembe wanajipambanua. Siwaelewi kabisa Sita na Olesendeka pamoja na Kilongo Anna. Kama kinyonga vile.
 
Jamani, huyu mzee nilikuwa namheshimu tena sana lakini kwa hoja hii kwamba CHADEMA haina safu ya uongozi ya kutosha ni upotoshaji wa hali ya juu. Unajua, tatizo la CCM tena lipo kwa wazee sana wa aina ya akina Six ni moja. Wao wamelishwa sumu na chama hiki mfu kiasi cha kudhani kwamba nchi lazima iongozwe na baraza la mawaziri lenye mawaziri na manaibu waziri 60, makatibu wakuu na manaibu makatibu wa kuu wa wizara zaidi ya 60, n.k. Wanasahau kwamba idadi ya viongozi wa serikali ni matokeo ya mfumo wa chama katika kuongoza nchi.

CCM inatumia vyeo kama zawadi kwa wanachama wake na siyo mkakati wa kujipanga kiuongozi na kujiletea maendeleo. Binafasi bado nina imani kwamba CHADEMA inaweza kujipanga vizuri na kukamata dola bila wasiwasi na dalili nzuri ni namna walivyojipanga bungeni na kubeba majukumu mazito pamoja na uchache wao. Watanzania wengi wasomi katika kila nyanja wamechoka na hiki chama cha CCM na bila shaka endapo CHADEMA itakamata dola watashirikiana vema nacho katika kujenga safu nzuri ya uongozi na kuwaletea maendeleo wananchi.

USHAURI WANGU KWA DR. SLAA BAADA YA MAJIBU YA SIX:
Dr. Slaa katika maelezo yako umeonyesha kuwa Mzee Six akikujibu utatoa data au uthibitisho zaidi wa kuonyesha jinsi mzee huyu alivyo mnafiki na asivyofaa kuwa kiongozi wa nchi hii. Tafadhali nakuomba ufanye hivyo kwani pasipo kufanya hivyo tutastukia mzee huyu yupo magogoni na hapo ndipo kitakuwa kilio na kusaga meno.
Tangu Mzee SITTA azuia mjadala huru wa wa RICHMOND na kitendo anachofanya cha kujenga makundi ndani ya ccm kwa manufaa yake kisiasa ,hakika sitaki kumsikia.
 
:flypig::flypig::flypig::flypig:HAKIKA SIPENDI HALI YA KISIASA INAVYOENDELEA NDANI YA NCHI HII HUSUSANI NAMNA NCHI ISIVYOONA HURUMA DHIDI YA DAMU ZA WATZ
 
:llama:Kwa nini huyu Mzee SITTA haachi kuongea sana dhidi ya DR.?Je anadhani kwa hali yoyote anayoweza kuongea dhidi ya huyu DR.aweza kuwafanya watu waamini anachosema?Je ana sababu za kujibizana nae ktka eneo lolote?Je hajui kuwa watz. walio wengi wanatambua uozo wake na chama chake cha zamani? Hivi anafikiri itawaingia akilini watu kwa kauli kwamba amekuwa akifuatwa na kila chama ili agombee nafasi ya u Rais? Hivi haoni kuwa ni jambo la kushangaza ati aitwe kugombea wakati hata misingi ya chama haijui na wala hajakitumikia wala kuwatumikia watu na jamii ya tz kwa ujumla?Haoni aibu kwa maneno yake yasiyo tija kwa kudhani ni yeye tu anaepaswa kugombea tu?Kwa nini yeye wakati maadili yake ni sifuri?Anakumbuka alivyowaumiza watz .kwa suala la mikataba feki mingi chini ya uongozi wake wa Mhimili mkubwa kabisa? yaani BUNGE?.ASIJICHANGANYE WALA KUWATIBUA NYONGO WA TANZANIA.NAMPA USHAURI
 
Kuwa Mh Slaa ni DIKITETA, nimeshasema mara nyingi huko nyuma. Ni vyema na Vingunge wanisaidie.

Dhambi kubwa isiyosameheka ni kumpa nchi huyu DIKITETA. wATANZANIA MKATAENI HUYU DIKITETA KWA NGUVU ZOTE.
 
Sijaelewaa Dr Slaa aliposema mama SITTA alimpigia simu kumuomba msaada,alimaanisha nini?
 
Kuwa Mh Slaa ni DIKITETA, nimeshasema mara nyingi huko nyuma. Ni vyema na Vingunge wanisaidie.

Dhambi kubwa isiyosameheka ni kumpa nchi huyu DIKITETA. wATANZANIA MKATAENI HUYU DIKITETA KWA NGUVU ZOTE.

Sifa yake nyengine ni kwamba haambiliki nadhani hata kanisani walishindwa kumvumilia tabia zake.
 
zamani nilikuwa nakuita mheshiwa kutokana na busara zako lakini nimekuja kugundua ya kuwa nilikuwa nakosea sana na sasa nitakuwa nakuita kaka kutokana na kuwa mambo unayoyasema kwa sasa hupaswi kuitwa mheshimiwa tena hebu jiulize ni kweliu kuwa ukitaka kujua uimara wa mtu je ni lazima utumie maneno ya kukejeli mfano chadema ni wacheza disco? hilo moja lakini jambo la pili ni kuwa kama alivyo sema Dr silaa pindi mwalimu anapewa uhuru na wakoloni alikuwa na stuff wa kutosha? kama ni hapana je aliwapata wapi hilo jingine unaposema nchi hii suala la majimbo haliwezekani kutokana na utofauti wa kiuchumi kwa sehemu mbalimbali ta taifa hili je ni nani aliyeleta tofauti hizi kama siyo ninyi chama tawala hilo pia jingine jambo jingine ni kuwa unasema ya kuwa uliangalia sera za chama cha dcm ukabaini kuwa kinaangalia kuwa wewe ni nani na unatoka wapi kwangu mimi naamini hata hiyo sera ya dcm inaonekana huifahamu vizuri kwani kama ungekuwa unajua mfumo mzima wa chama usingesema yote haya hata mimi mwenyewe ambaye sijakuwa sana kisiasa kaka nakupiga bao kwa njia hii inaonekana ya kuwa ulipo hapo ukikosa urais 2015 uaweza kuanzisha chama chako kwa sababu zote hizi kwangu mimi inatosha sasa kukuita kaka na siyo mheshimiwa
naomba kuwasilisha
 
Kama kweli Sita have attempted kugombea aina yoyote ya uongozi nje ya ccm kama Slaa alivyodai, basi he is finished ndani na nje ya chama. He has no any credibility. For a long time nilikuwa nawaona watu wadesign ya Sita ndani ya ccm kama wanafiki. Kwa mtazamo wangu, Sita siyo mnafiki tena bali "alikuwa" mnafiki, huyu jamaa sasa hivi is in another level, yaani he has lost his discretion (which means amepoteza uwezo wakutofautisha kati ya uchungu na utamu). Namshauri either atafute hoja nyingine yenye maslahi ya taifa au anyamaze, taharabu zake zinatia kinyaa, vinginevyo he is nothing but just a loose puppet.
 
Yafuatayo ni majibu ya Waziri Sitta kuhusu kauli ya Dr Slaa aliyoitoa Majuzi mkoani Iringa

Nimesikitishwa na kauli za jazba na mwangwi wa kiwewe za Mhe Dr W Slaa alipokuwa Iringa juzi hadi kuniita mnafiki, mwongo, mtu wa hatari n.k

Hali hii inatia mashaka juu ya uwezo wa kiongozi huyo wa kisiasa kuhimili kukosolewa ambayo ni sifa muhimu ya maisha ya mwanasiasa yeyote hususani anapojinadi kuwa anaweza kuchukua madaraka ya kuiongoza nchi.

Kauli zisizo na staha alizozitoa Dr Slaa dhidi yangu kama vile sifai hata uongozi wa kata zinadhihirisha mambo mawili:

Dr Slaa ni dicteta. Hana uvumilivu. Ana hulka ya kujiskia kwamba mawazo yake hayapingwi.
Ni mzushi asiyeogopa kusema na kupindisha mantiki ya jambo ili tu kushinda hoja. Iweje mtu aliyenibembeleza nigombee uraisi kupitia chama chake mwaka juzi leo aseme sifai kuongoza hata kata kwasababu tu nimetamka ukweli juu ya udhaifu wa chama chake cha siasa?

Niliyoyasema pale Karagwe majuzi katika uchambuzi wangu wa vyama vya siasa nchini ni kwamba CHADEMA wamekuwa hodari wa kukosoa na kuishambulia CCM na serikali zake lakini wanasau kuwa ili wawe mbadala kwa kuiongoza nchi hawana budi kurutubisha safu yao ya uongozi nawe na watu wakutosha kuweza kushika madaraka ya ngazi mbalimbali za uongozi wa Taifa. Kuukataa ukweli kwamba safu ya uongozi wa CHADEMA ni nyembamba ni kujidanganya tu.Kupita mikoani kutangaza kwamba matatizo yote ya wananchi yanatokana na CCM ni kazi rahisi na ina mvuto wake kisiasa lakini mwanasiasa makini hana budi kwenda mbele zaidi ya hapo.

Hana budi kutuambia wapiga kura mipango ya chama chake inayoeleweka na inayotekelezeka na iliyo makini kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo ya nchi. Ahadi za alinacha za tiba bure, elimu bure bila kuonyesha vyanzo halisi vya mapato ni porojo tu. Kusema kwamba raslimali za nchi kama vile gesi asilia, madini, makaa ya mawe, utalii zinatosha kuondoa umaskini ni nadharia tupu ambayo uhalisia wake hauna budi kubainishwa kwa mikakati dhahiri na thabiti ya kiutawala (uendeshaji) inayoweza kuchuma utajiri huo kwa ufanisi, kwa uendelevu na kwa faida ya wengi1. Kuhusu mwenyekiti Mh Mbowe – MB

Katika hotuba yangu sikukejeli uzoefu wa Mhe Mbowe, wala sijasema Mhe Mbowe ni mcheza disko. Niliuchambua wasifu wa viongozi wa CHADEMA na kutamka uzoefu wa Mhe Mbowe katika vitega uchumi vya burudani hii siyo kudharau bali ni kutamka ukweli tu.Huwezi kuuelezea wasifu wa Mhe Mbowe bila kuelezea mchango wake mkubwa katika tasnia ya burudani.Mmoja wa maraisi maarufu wa marekani (USA)alikuwa ni mcheza sinema Ronald Reagan.Na hapa Tanzania tulikuwa na mzee R. Kawawa ambaye alianzia katika tasnia ya uigizaji, kwa hiyo Mhe Mbowe au Dr.W. Slaa anaweza akawa Rais wetu kwa maana ya kupigiwa kura za uchaguzi wa demokrasia.Kumudu au kutoyamudu madaraka hayo ni suala tofauti. Tathmini yangu ilihusu safu nzima ya uongozi wa CHADEMA kwa ujumla wao.Ni safu nyembamba mno.

2. Kujiunga na CHADEMA

Kama alivyosema Dr. Slaa Chadema walifanya jitihada ya kunishawishi niingie CHADEMA 2010 na niwe mgombea wao wa Urais. Jambo hili nililitafakari na kutafuta ushauri kwa watu wangu wa karibu na nikabaini kwamba:-

CHADEMA wana migawanyiko yao ya uongozi tena ni ya hatari kwasababu ni ya kikanda za nchi – yaani nani anatoka wapi.

Kutokana na yaliomo katika ilani yao ya uchaguzi 2010 – 2015 nilibaini mambo ya kiitikadi ambayo siyakubali kama vile sera ya majimbo. Sera ya majimbo inawezekana katika nchi ambazo ni tajiri na pia isiyo na tofauti kubwa ya hali ya maisha baina ya kanda mbalimbali za nchi kama vile Marekani (USA). Kuleta majimbo Tanzania ambako kuna tofauti kubwa za kimaendeleo baina ya Kaskazini, Mashariki, kati, Kusini na Magharibi ni kusababisha nchi ichanike vipande vipande.

Huduma bure za elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na huduma bure za afya kwa wote ni ndoto na ni ghilba kwa wananchi. Isitoshe siamini kwamba kazi ya Serikali yoyote Duniani ni kuwalea Wananchi kwa umaskini huku ukiwaahidi huduma za bure badala ya kuwaendeleza wajitume na waongeze kipato ili wamudu gharama za maisha. Kwa hiyo nisingeweza kuwa mgombea Uraisi ndani ya chama ambacho itikadi zake za msingi sikubaliani nazo.

Baada ya hapo nisingeweza eti baada ya uchaguzi Mkuu niombe kugombea Uspika kupitia chama cha CHADEMA.

3. Kuhusu CCJ

Kama ilivyo kawaida kwa vyama vya siasa kutafuta wagombea bora, CCJ ni miongoni mwa vyama vilivyonifuata mimi na baadhi ya wanasiasa wakati wa maandilizi ya uchaguzi mkuu. jambo hili si la siri wala la ajabu na Nimelizungumza hili mara nyingi. Isitokee katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mtu kutoka chama kumoja cha siasa na kujiunga na chama kingine haiwezi kusemwa kuwa ni uhaini. Na kama Ningeridhika na mambo yao ningejiunga na CCJ mwaka 2010 lakini sikufanya hivyo. Pia ni uzushi usio na msingi kunihusisha na uanzishaji wa chama hicho. Waanzilishi wa chama hicho cha siasa wanajulikana na wapo hai, ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania kuanzisha au kujiunga Binafsi na chama chochote cha siasa.

4. Madai mengine

Eti nilitamka kwamba ningehamia chadema na Wabunge wa CCM 55 ni porojo za Dr. Slaa kama ulivyo usemi ningeihama CCM siku chache kabla ya kuvunjwa Bunge la 9.

Inashangaza kwa Dr Slaa kukejeli uendeshaji wa bunge la 9 ambalo ndilo lililowapa fursa watu kama yeye kujulikana na kujipatia umaarufu.

Haya madai ya mimi nikiwa Spika kukwamisha uchunguzi wa Meremeta na Richmond ni kutokana na hisia tu za chuki. Taratibu za Kibunge hazimwezeshi Spika kuwa Dikteta anayeamua nini kijadiliwe na nini kisijadiliwe. Yote yapo katika kanunu za Bunge. Maamuzi ya Bunge si lazima yawe ni ya Spika.

Kuhusu ofisi ya Mbunge jimboni Urambo mahasimu wangu ndani ya CCM na nje yake wameng’ang’ania kwa makusudi maalum kuiita ofisi ile kuwa ni ya Spika. Michoro yake na gharama zake hata ukijumuisha samani haifikii tarakimu za ajabu wanazotaja mahasimu wangu kujenga hoja istoshe ofisi hiyo haina maslahi yeyote binafsi kwangu Aidha viongozi wengine waliofikia hadhi za juu mathlani ya uwaziri mkuu nao wamejengewa majimboni ofisi zinazolingana na hiyo

Porojo nyingine binafsi kama vile kumuhusisha mke wangu kumpigia simu Dr Slaa kumsihi anisaidie kisiasa ni upuuzi wa aina yake unaodhihirisha umahiri wa Dr.Slaa katika siasa za kiwango cha chini.

5. HITIMISHO

Mimi nikiwa mwanasiasa mzoefu na mkongwe nimetoa ushauri na nitaendelea kutoa ushauri kwa makundi mbalimbali nchini.Kuniambia naingilia mambo ya CHADEMA ni kichekesho.Wakiwa wao ni chama cha siasa kinachoendesha harakati za kuwania kuchukua madaraka ya kuongoza nchi ambayo mimi ni raia wasitazamie kuwa sisi wapiga kura tutaacha kuwachambua.Wanalo tatizo kubwa la safu nyembamba mno ya uongozi, Kulingana na majukumu ya kuendesha nchi.

Kujilinganisha na safu ya uongozi ya Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ni mzaha wako wapi akina R.M Kawawa, Pauli Bomani, George Kahama, Amir Jamal, Solomoni Eliufoo, Tewa Saidi, Tewa Abdallah, Fundikira wa CHADEMA? Kutembea nchi nzima kuhamasisha chuki dhidi ya serikali iliopo madarakani ni jambo jepesi lakini Watanzania walio makini wanahitaji maelezo ya mipango mbadala ya uchumi kuinua hali za maisha yao na kuiona safu ya uongozi itakayowezesha kwa dhati kubuni na kusimamia mikakati endelevu ya kuondoa umaskini kujenga uchumi imara na kuimarisha umoja wa watanzania

Kazi kwenu tuanze kumjadili mzee huyu

CHADEMA watafaidika sana wakifuata ushauri huu, hasa katika nukuu hii



"Huduma bure za elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na huduma bure za afya kwa wote ni ndoto na ni ghilba kwa wananchi. Isitoshe siamini kwamba kazi ya Serikali yoyote Duniani ni kuwalea Wananchi kwa umaskini huku ukiwaahidi huduma za bure badala ya kuwaendeleza wajitume na waongeze kipato ili wamudu gharama za maisha. Kwa hiyo nisingeweza kuwa mgombea Uraisi ndani ya chama ambacho itikadi zake za msingi sikubaliani nazo."


Huu ndio mwimbo wa CHADEMA unaoniudhi kuliko mimbo yao yote. Watanzania tafakarini kwa undani haya maneno ya mwasiasa mashuhuri kwa faida yenu na kwa kuepuka kukiingiza chama cha kitapeli IKULU.
 
Sijaelewaa Dr Slaa aliposema mama SITTA alimpigia simu kumuomba msaada,alimaanisha nini?

USICHOELEWA NI NINI? Huy mtu ni mpenda wake za watu na kilichokuwa kinaendelea ni kumtongoza mama SITTA ili apaone. Na sijui kama alimkosa!! Maana huyu ni Dr wa wa akina mama.

Sasa huo ni ujumbe fika kwa Mh Sitta kuwa usiringe nimeshakuweka mkononi kwani hata siri zako za ndani ninazo.

We acha tu, maana jahanamu nyingine WATANZANIA tunajitakia hapa hapa kwa kumuingiza Mh Slaa IKULU.
 
sitta amejibu tuhuma kwa busara sana..katibu wangu kwakweli hukuwa umejipanga. cha msingi tuyatilie maanani ushauri huu
 
Mzee wewe inaonekana una taaluma ya ualimu,unajitahidi kuwasaidia hawa vilaza wa chadema lakini bahati mbaya sana ni watu ambao hawako tayari kujifunza na kuelewa,hawa ni aina ya wanafunzi wanaoamini katika kukariri mambo ili tu wafaulu mtihani,hawako tayari kuelimika..kwa watu wa aina hii chadema ina safari ndefu sana..lakini umetimiza wajibu wako wa kutoa elimu kaka,thanx.HUNA LOLOTE NA WEWE UNASIKIZA HABARI ZA HUYU 6 NDO ALITETEA RICHMOND HUYU NI KEWLI MAIHSA BORA YANAWEZEKANA NCHI INA UTAJIRI MKUBWA KUSOMA BURE DAWA BURE ,PESA NGAPI UMESKIA ZIKO NJE YA NCHI NANI ZA WIZI HAZITOSHI KUFANYA JAMBO WE KILAZA KWELI
 
Back
Top Bottom