Majibu ya shamsi vuai nahodha na mwema kuhusu mauaji ya jk arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya shamsi vuai nahodha na mwema kuhusu mauaji ya jk arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fredwash, Jan 7, 2011.

 1. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Nahodha: Vurugu ArushaKatika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amesema vurugu zilizotokea Arusha juzi ni tatizo la kisiasa ambalo pia litapaswa kushughulikiwa kisiasa.

  “Wote tunapaswa kulinda amani yetu. Tunapaswa kutuliza hali ya Arusha. Kilichotokea Arusha ni mgogoro wa kisiasa tutautatua pia kisiasa,” alisema Nahodha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, jana, jijini Dar es Salaam.

  “Biblia inasema ‘ni heri wapatanishi kwani wao watarithi nchi,’… sisi (serikali) tutawakutanisha pande zote ili tufikie muafaka na kutuliza hali ya Arusha,” alisema Nahodha.

  Alisema hatua hiyo ya maridhiano kwa sasa ni muhimu kwani, baada ya msuguano wa takribani wiki, pande mbili zinazosuguana mkoani humo, sasa zimeridhika kuwa kuna tatizo la msingi ambalo linapaswa litatuliwe.

  “Kunawakati wa kuchukia na wakati wa kufurahi, wakati wa kupenda na wakati wa kuridhiana, sasa wakati wa maridhiano umewadia,” alisema Nahodha ambaye pia anataaluma ya Udpolomasia.

  Aliendelea kufafanua kuwa, kulingana na taaluma ya migogoro, usuluhishi hufanikiwa pale tu ambapo wahusika wa pande zinazosuguana kuona na kuamini kwamba kuna tatizo.

  Alisema kuwa, kwa muda sasa zilikuwepo juhudi za kusuluhisha mgogoro wa Arusha, ambazo zilikuwa zikifanyika chini chini, lakini kutokana na hali ilivyo sasa, itabidi usuluhishi huo kufanyika kwa uwazi.

  Kuhusu muda utakaotumika kufanya usuluhishi huo kisiasa, Nahodha alisema “Nadharia ya usuluhishi wa migogoro kwanza kabisa ni kutokuwa na haraka, suala la muda utakao tumika, utategemeana na msuluhishi pamoja na wasuluhishwaji. Unaweza kutumika hata second (sekunde) moja.”

  Akijibu swali kama serikali itakuwa tayari kufuta kesi mbalimbali zinazowakabili viongozi na wananchi waliokamatwa kutokana na tukio hilo, Naodha alisema hakuna na jibu la moja kwa moja ingawa swali hilo litachukuliwa kama ushauri.

  Kuhusu uwezekano wa kutengua matokeo ya umeya Arusha, suala ambalo pia Chadema wanalilalamikia, Naodha alisema “Sina uhakika kama tatizo la msingi lililopo Arusha linatokana na Umeya. Lakini katika mazungumzo tukibaini kuwa hilo ndiyo tatizo basi tutalifanyia kazi.”IGP Mwema Kigugumizi
  Naye IGP Said Mwema ambaye pia alikuwepo katika mkutano huo, alionekana kupata shida ya kujibu maswali mengi yaliyoulizwa na waandishi juu ya polisi kutumia nguvu nyingi.

  Alikwepa kujibu pia swali la waandishi wa habari iwapo kuna polisi anayeshikiliawa kutokana na kusababisha vifo vya raia wawili.

  Waandishi waliuliza maswali baada ya Waziri Naodha kumaliza kuzungumza, ambapo baada ya kuyaandika maswali ya waandishi alimtaka IGP kuanza kutoa majibu kwa yale maswali yanahusu moja kwa moja polisi.

  Katika awamu ya kwanza ya kujibu maswali hayo, IGP hakujibu swali lililomtaka kueleza endapo madhara yaliyotakana na fujo hizo, ni madogo, makubwa au yanalingana na yale ya taarifa alizodai kuwa ni za kiintelijensia, ambazo walizitumia kutoa tamko la kisitisha maandamano.

  Kuhusu madai kwamba kuna kikosi cha polisi kutoka Ukonga jijini Dar es Salaam, Chuo cha Polisi Moshi (CCP) na Manyara vilivyopelekwa Arusha kudhibiti vurugu, alisema:

  “Hakuna askari tuliowachukua sisi kutoka Ukonga, suala la polisi kutumia askari wangapi na kutoka wapi, hilo ni suala la taaluma ya polisi na hatuwezi kutangaza kwa kuwa hayo ni mambo ya security (kiusalama)."

  Hata hivyo alisema kuna wana askari wa ziada na akakiri kuwai kuna vikosi vingine vilipelekwa Arusha juzi ili kuongeza nguvu ya kulinda usalama wa raia kuanzia jana.

  “Sisi kuweka mpaka askari wa reserve (waakiba) mngetupongeza, kuongeza askari sisi hiyo ni issue ya kiusalama, kuna mpaka askari waliondoka jana (juzi) kwa sababu ya ku-project hali leo (jana).

  Alisema kutokana na hali ilivyo katika mkoa huo, maafisa mbalimbali wa polisi walitumwa kwenda Arusha ili kuchunguza hali ilivyo.

  Juu ya kuwepo kwa mkanganyiko wa amri ya kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ya kuruhusu maandamano pamoja na aliyoitoa ya kusitisha amaandamano, IGP.

  “Kwa taarifa yenu kuna barua ya ruhusa na katazo la maandamano hayo kutoka kwa RPC wa Arusha, nilichokifanya mimi ni kutoa msisitizo tu,” alisema IGP Mwema.


  My take: hii inaonyesha ni jinsi gani serikali yetu inavyofanya kazi kama mwili usiokuwa na mawasiliano na vioungo vyake.... viongozi wa chadema wako mahakamani... waziri mwenye dhamana tena pembeni akiwa amekaa na kamadna wake anasema swala litashughulikiwa KISIASA kwa kuwa ni mgogoro wqa kisiasa sasa hapo sio kuingilia kazi ya mahakama.. na hayio majibu ya kujing'ata ya mwema ndio yamenichefua kabisa... serikali yetu HAINA ADABU.
   
 2. v

  van helsing Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  VUAI na MWEMA kama kweli wana busara na wanahitaji tuwakumbuke,,,WA-JI-U-ZU-LU kwa kushindwa kazi.
   
Loading...