Majibu ya Mtendaji Mkuu wa BRELA kuhusu kinachoitwa "Kukimbiza wawekezaji" kilichoandikwa JamiiForums

Jul 19, 2020
39
128
Andiko hili nimeliona kwenye forums kadhaa, walau Wakili Msomi amekiri kwamba mfumo sasa upo stable.

Kuhusu suala linalolalamikiwa, kwanza nikiri kwamba hoja zake Ni za ukweli na changamoto hii nilishaiona since day one.

Mara kadhaa tumeeleza kuwa kuna kazi tunaendelea nayo ya system Re-designing ambayo ilianza tangu Mwezi May, 2020 ikishirikisha wataalam wa IT toka Taasisi kadhaa ndani ya Nchi yetu na inatarajiwa tukabidhiwe mfumo huo hivi karibuni, maana tupo kwenye testing (Majaribio).

Miongoni mwa maboresho hayo Ni kuunganisha mfumo wa BRELA na mifumo ya Taasisi kadhaa za serikali ikiwemo TIC, mabenki, polisi, Uhamiaji n.k. lengo kuu Ni mifumo hiyo iweze kusomana na kuondoa urasimu uliopo sasa ambao kwetu sisi tunaona ni kikwazo katika kukuza biashara.

Shida mfumo uliopo sasa haukua na flow, mteja akiwasiliana request yake inaenda kwa mtu Mpya badala ya kuanzia kwa supervisor, then amu assign mtu,au irudi kwa Yule Yule Alie process (Processing Officer).

Lakini pia, Kuna shida ya mfumo kufuta kile walichojaza wateja na hivyo kuleta changamoto Kama hizo.

Hivyo Basi wadau wetu wajue hatujalala na Soon, tunazindua upya mfumo huo ambao uta address hizo changamoto alizozianisha mwandishi(Wakili Msomi).

Lengo la BRELA Kama Taasisi Sio kukimbiza wawekezaji, Bali kuhakikisha tunakuza uwekezaji kwa kushirikiana na wenzetu wa TIC.

Na hili linajionyesha kwa jitihada kadhaa zilizokwishafanyika na zinazoendelea kufanyika ndani ya BRELA.

Changamoto zipo ili ziboreshe na kupata matokeo tarajiwa ndani ya Taasisi yoyote ile na hata ndani ya familia zetu, changamoto hazikosekani.

Kwa kumalizia,yapo mengi tunayoendelea kuyafanya, ikiwa Ni pamoja na kupitia Sheria mbalimbali ili kuziboresha, kutengeneza nyaraka mbalimbali za kiutendaji ndani ya Taasisi.

BRELA tutaendelea kupokea comments za wadau Kama hawa lengo ni kuboresha Sio tu mifumo ,Bali pia uendeshaji wa Taasisi yetu.

----
Pia soma > BRELA inakimbiza wawekezaji

------

0FF8693A-8070-438C-8D34-9215551A97CD.jpeg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI JUU YA MADAI YA BRELA KUKIMBIZA WAWEKEZAJI

Dar es Salaam, Januari, 2021 Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyosambaa katika Mitandao ya kijamii juu ya BRELA kukimbiza wawekezaji kutokana na changamoto za Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS). Wakala inatambua dhamana iliyopewa na serikali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shughuli za Uwekezaji zinaongezeka nchini, hivyo inaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali ambazo zimekua zikionekana kuwa ni kikwazo katika urasimishaji wa biashara kupitia Mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao.

Ifahamike kwamba, mwezi Mei 2020, BRELA kwa kushirikiana na wataalam wa mifumo toka Taasisi mbalimbali za serikali ilianza rasmi kubadilisha na kuboresha mfumo (System Redesigning) kwa kuzingatia changamoto zilizopo katika mfumo unaotumika hivi sasa. Mfumo huo kwa sasa upo katika hatua za majaribio na utakapo kuwa tayari utakabidhiwa kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi huku ukisimamiwa na wataalam wazawa tofauti na mfumo wa sasa unaosimamiwa na Mzabuni kutoka nje ya nchi.

Kukamilika kwa Mfumo huo kutaweza kutatua changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na Maombi kupokelewa na kufanyiwa kazi na Ofisa mmoja, Ombi kufanyiwa kazi kwa kuzingatia ombi lililofika awali (first come, first served), kuendelea kuunganisha Mfumo wa BRELA na mifumo ya taasisi nyingine kama Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Benki, Uhamiaji na Mamlaka za utoaji Leseni katika Halmashauri.

Lengo kuu ni kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi sio tu kwa wawekezaji bali wafanyabiashara wote. Aidha, katika kuhakikisha kwamba katika kipindi hiki Wadau wa BRELA wanapata huduma nzuri, Wakala imeanzisha Kituo cha Miito na Huduma kwa wateja. Kituo hiki kazi yake kuu ni kutoa usaidizi wa haraka kwa Wateja wetu wanapokwama wakati wa urasimishaji wa Biashara zao.

Ni vyema umma ufahamu kwamba, muda wa usajili wa Jina la biashara ni siku moja (1) na si zaidi ya siku tatu (3) za kazi, Usajili wa kampuni ni siku tatu (3) na si zaidi ya siku tano (5) za kazi, Usajili wa Alama za Biashara na huduma ni kipindi cha siku tisini (90) (kutokana na takwa la kisheria), maombi ya kupata Hataza ni siku mia moja na ishirini (120) (kutokana na takwa la kisheria), kupata Leseni ya Kiwanda au Leseni ya Biashara kundi A ni siku moja (1) na si zaidi ya siku tatu (3) za kazi.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI Baada ya kipindi hicho kupita kama usajili haujakamilika Mteja awasiliane na kituo cha huduma kwa Wateja kupitia namba +255 (0) 222 212 800 au kwa barua pepe maoni@brela.go.tz kwa ajili ya usaidizi wa haraka.

Hivyo basi, Wakala inawataka wadau wake kufuata taratibu za usajili ikiwa ni pamoja na ujazaji wa taarifa kwa makini na uwekaji wa viambatanisho sahihi ili kuepusha kuchelewa kwa kukamilika kwa usajili.

BRELA wakati wote tunapokea maoni ya wadau kwa lengo la kuboresha sio tu mifumo bali pia uendeshaji wa Taasisi yetu “Tunaipa utu wa kisheria biashara yako”

Imetolewa na:

KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI
 
Asante kwa maelezo mauti

Watu wa Passport pia system yao isomane na Tassimo zingine nimekaa manual Mon ujaze u print hard copy mtu apitie manually ni kama ile system ya passport imeongeza badala ya kupunguza ingekuwa inasomana na Nida nk kazi ingekuwa rahisi zaidi.

Nadhani Taasisi zote ziige hiyo system mpya ambayo brela wanataka kuizundua.
 
Wako humu hujui JF ndio kipimo cha utendaji cha serikali ? MATAGA na watendaji wote wako humu tena very active. Wengi ndio huanzisha Mada hot kupima upepo.
 
Tunashukuru Sana kwa response yenu na kufanyia kazi malalamiko yetu.

Unganisheni mifumo yenu na manisapaa pia ili badala ya mteja kwenda kuanza upya process ya leseni amalize hapo hapo na nyie mtakua wakala wa manispaa husika.

Asante.
 
Shida mfumo uliopo sasa haukua na flow, mteja akiwasiliana request yake inaenda kwa mtu Mpya badala ya kuanzia kwa supervisor, then amu assign mtu,au irudi kwa Yule Yule Alie process (Processing Officer).
Hapa pia kuna tatizo pia.

Kuna umuhimu wa kuwa na 'set unit standards' (Nimekosa jina linalofaa) kwa ajili ya ku-crosscheck hizi docs. Hii itaondoa tatizo la kila officer kukosoa anachoona kinafaa.

Hapa doc ikikaguliwa na Mr. X ikarudi kwa Mr. Y hapatakuwa na makosa tofauti tofauti ya kukosoa kwani ma-officer wote watakuwa na similar base ya kukagua.
 
Nilifanya hili zoezi la kujaza Form za Return mpaka nikachoka Na kuacha, vijana wangu wakaendelea. Sasa kufika kwenye malipo. Tukaletewa bili ya ajabu .. Bili haingalii kama kuna mwaka wewe umeshawahi kulipa return fee Na hata kama ulidaiwa penalty miaka ya nyuma Na ukalipa , Wenyewe wanakupa fee ikiwa haija zingatia malipo ya awali.

Mfano

Kama ulichelewa kuleta return mwaka 2015 Na 2016 , kisha unafanya return mwaka 2017. basi ili return ya mwaka 2017 iwe accepted kipindi hicho .. basi ilibidi ulipie Na penalty za kushindwa kuwakilisha return za mwaka 2015 Na 2016.

Sasa kutokana na kushindwa kuweka data zao vizuri , kwa sasa Mfumo unatutaka kuanza kujaza Return Tangu mwaka uliosajiliwa ..

Kisha wanakuja Na Hesabu pamoja Na penalty za miaka yote bila kujali kama kuna mwaka ulizaja return Na kufanya malipo, pia hata hawajali kuwa ulisha wahi lipia penalty siku za nyuma.

Wanadai wewe Mteja ndio upeleke ushahidi umawauliza wao hawana kumbukumbu wanaruka ruka tu.
 
Salaam WanaJf,

Andiko hili nimeliona kwenye forums kadhaa, walau Wakili Msomi amekiri kwamba mfumo sasa upo stable....
Mkuu nina masuali mawili

1. Kwanini afisa anaepokea ombi asilishughulikie hadi mwisho ndipo apeleke kwa supervisor?
Hiyo ni kwasababu kila ombi sharti liwe assigned kwa case worker na itolewe reference ya ombi.

2. Je, tatizo la system flowing ni kubwa kiasi cha kutema maombi mapema ambapo maombi mengine yaweza kuwa straight forward?
 
Wako humu hujui JF ndio kipimo cha utendaji cha serikali ? MATAGA na watendaji wote wako humu tena very active ....wengi ndio huanzisha Mada hot kupima upepo .....
Hawataki kuifungia tena? Kesi za Max zimefutwa? Kama hawajafanya hivyo wakae na unafiki wao.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI JUU YA MADAI YA BRELA KUKIMBIZA WAWEKEZAJI

Dar es Salaam, Januari, 2021 Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyosambaa katika Mitandao ya kijamii juu ya BRELA kukimbiza wawekezaji kutokana na changamoto za Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS). Wakala inatambua dhamana iliyopewa na serikali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shughuli za Uwekezaji zinaongezeka nchini, hivyo inaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali ambazo zimekua zikionekana kuwa ni kikwazo katika urasimishaji wa biashara kupitia Mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao.

Ifahamike kwamba, mwezi Mei 2020, BRELA kwa kushirikiana na wataalam wa mifumo toka Taasisi mbalimbali za serikali ilianza rasmi kubadilisha na kuboresha mfumo (System Redesigning) kwa kuzingatia changamoto zilizopo katika mfumo unaotumika hivi sasa. Mfumo huo kwa sasa upo katika hatua za majaribio na utakapo kuwa tayari utakabidhiwa kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi huku ukisimamiwa na wataalam wazawa tofauti na mfumo wa sasa unaosimamiwa na Mzabuni kutoka nje ya nchi.

Kukamilika kwa Mfumo huo kutaweza kutatua changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na Maombi kupokelewa na kufanyiwa kazi na Ofisa mmoja, Ombi kufanyiwa kazi kwa kuzingatia ombi lililofika awali (first come, first served), kuendelea kuunganisha Mfumo wa BRELA na mifumo ya taasisi nyingine kama Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Benki, Uhamiaji na Mamlaka za utoaji Leseni katika Halmashauri.

Lengo kuu ni kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi sio tu kwa wawekezaji bali wafanyabiashara wote. Aidha, katika kuhakikisha kwamba katika kipindi hiki Wadau wa BRELA wanapata huduma nzuri, Wakala imeanzisha Kituo cha Miito na Huduma kwa wateja. Kituo hiki kazi yake kuu ni kutoa usaidizi wa haraka kwa Wateja wetu wanapokwama wakati wa urasimishaji wa Biashara zao.

Ni vyema umma ufahamu kwamba, muda wa usajili wa Jina la biashara ni siku moja (1) na si zaidi ya siku tatu (3) za kazi, Usajili wa kampuni ni siku tatu (3) na si zaidi ya siku tano (5) za kazi, Usajili wa Alama za Biashara na huduma ni kipindi cha siku tisini (90) (kutokana na takwa la kisheria), maombi ya kupata Hataza ni siku mia moja na ishirini (120) (kutokana na takwa la kisheria), kupata Leseni ya Kiwanda au Leseni ya Biashara kundi A ni siku moja (1) na si zaidi ya siku tatu (3) za kazi.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI Baada ya kipindi hicho kupita kama usajili haujakamilika Mteja awasiliane na kituo cha huduma kwa Wateja kupitia namba +255 (0) 222 212 800 au kwa barua pepe maoni@brela.go.tz kwa ajili ya usaidizi wa haraka.

Hivyo basi, Wakala inawataka wadau wake kufuata taratibu za usajili ikiwa ni pamoja na ujazaji wa taarifa kwa makini na uwekaji wa viambatanisho sahihi ili kuepusha kuchelewa kwa kukamilika kwa usajili.

BRELA wakati wote tunapokea maoni ya wadau kwa lengo la kuboresha sio tu mifumo bali pia uendeshaji wa Taasisi yetu “Tunaipa utu wa kisheria biashara yako”

Imetolewa na:

KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI

Zaidi, Soma:

Attachments

  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.docx
    28.6 KB · Views: 7
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.pdf
    542.9 KB · Views: 9
Hao brela kwanini wasije na mfumo mtu akitimiza masharti na requirement siku hyo hyo akanilishe kila jambo online. Sio unajaza kila kitu online then baadae ukienda wanaendesha vitu manual.
 
Hao brela kwanini wasije na mfumo mtu akitimiza masharti na requirement siku hyo hyo akanilishe kila jambo online. Sio unajaza kila kitu online then baadae ukienda wanaendesha vitu manual.
Kwa sasa mifumo yetu bado sana kuwa "Fully Automated" mzee mama. Automation plus paperwork bado inahitajika.

Japan mifumo yao ipo computerized kwa 65% tu mpaka sasa.
 
Porojo tu hizo kwa ajili ya kujisafisha ila kwenye ground ni tofauti sana. Pia wanaofanya zile kazi kule BRELA wengi wao hawana uelewa wa Sheria ya Makampuni.
 
Kwa sasa mifumo yetu bado sana kuwa "Fully Automated" mzee mama. Automation plus paperwork bado inahitajika.

Japan mifumo yao ipo computerized kwa 65% tu mpaka sasa.
Serikalini wako slow Sana imagine hata kulipia online baada ya control number huku unakuwa umeshapata notification wao wakiingia kwenye system inakuwa iko low na hapo watataka urudi bank upange foleni Ili upewe ma receipt sasa najiuliza nini maana ya kulipia on-line aisee, maana ni kucheleweshana tu
 
Back
Top Bottom