Changamoto2015
JF-Expert Member
- Oct 1, 2012
- 773
- 314
Mkakati wa Kuboresha Ukusanyaji wa Mapato na Matumizi
MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA aliuliza:-
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakusanya mapato kiasi cha takribani bilioni mia nane kwa mwezi na kuna vyanzo vingine vya mapato; kila mwaka tunapitisha Bajeti ya Serikali, lakini baadaye tunaambiwa Serikali haina fedha hivyo kusababisha Halmashauri zetu kupewa asilimia 30 au asilimia 40 tu ya fedha zilizoombwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo:- (a) Je, ni lini Serikali itakuwa makini katika kukusanya na kutumia vizuri mapato yake? (b) Je, Serikali ina mkakati gani wa kupunguza misafara ya viongozi ya ndani na nje ambayo ni mikubwa sana na haina tija? Nakala ya Mtandao (Online Document) 17 (c) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha “Payroll” ya Serikali haina watumishi hewa?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. MWIGULU L. MCHEMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deogratius Aloyce Ntukamazina, Mbunge wa Ngara, kama ifuatavyo:-
(a) Mheshimiwa Spika, Serikali muda wote imekuwa katika kukusanya mapato na kudhibiti matumizi. Umakini wa Serikali katika kukusanya mapato yake unajidhihirisha wazi katika mwenendo wa ukuaji wa mapato hayo. Katika kipindi cha miaka 10, mapato ya Serikali yamekuwa kwa wastani wa asilimia 22 kwa mwaka kutoka shilingi 1,773,709 mwaka wa fedha 2004/2005 na kufikia shilingi 10,252,981 mwaka wa fedha 2013/2014. Ongezeko hilo limetokana na hatua mbalimbali za kisera na kiutawala zilizochukuliwa katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato. Ili kuwa na nidhamu na umakini katika matumizi yake, Serikali hufanya matumizi yake kulingana na mapato na kuzingatia vipaumbele vilivyoainishwa katika bajeti ambayo huidhinishwa na Bunge lako Tukufu.
(b) Mheshimiwa Spika, si kweli kwamba misafara ya viongozo ya ndani na nje haina tija. Viongozi wa Serikali na hata Chama Tawala, hufanya ziara ndani ya nchi kukagua, kuhimiza na hata kushiriki katika shughuli za maendeleo, wakati mwingine kushiriki katika kuhamasisha harambee za kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile zahanati, shule, barabara na hata VICOBA na SACCOS.
Mheshimiwa Spika, ziara za nje ya nchi pia zina tija kubwa, ziara hizo hufanyika kwa ajili ya kuonana, kujadiliana na kufanya makubaliano na washirika wetu wa maendeleo katika masuala ya misaada, mikopo na uwekezaji. Ziara hizi hutumika pia kutangaza vivutio na fursa za utalii na kwa hali hiyo, huhamasisha kuvutia watalii. Waheshimiwa Wabunge wanafahamu kuwa Mashirika ya Kimataifa ya Ulaya, Benki ya Dunia, Benki ya Ulaya, Shirika la Fedha la Kimataifa, Benki ya Maendeleo ya Afrika na hata nchi moja moja kama Uingereza, Marekani, Uchina, Japani huutaka ujumbe wa Serikali yetu kufika huko kwenye Mashirika hayo na nchi hizo kwa ajili ya kukamilisha masuala ya misaada, mikopo na hata vitega uchumi.
source:
http://parliament.go.tz/FFBDBE81-55...ploads/documents/1450874546-30 MACHI 2015.pdf