Majibu ya Kikwete ya Tuhuma za Uongozi Dhaifu Yasubiriwa kwa Hamu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya Kikwete ya Tuhuma za Uongozi Dhaifu Yasubiriwa kwa Hamu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Dec 9, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Dec 9, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Na Leon Bahati na Sadick Mtulya

  KAULI ya Rais Jakaya Kikwete kuwa anajiandaa kujibu tuhuma za udhaifu wake katika kufanya maamuzi magumu zilizotolewa kwenye kongamo lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, imewasha moto mpya baada ya waliomtuhumu kueleza bayana kuwa wanasubiri kwa hamu majibu ya kiongozi huyo wa nchi.

  Mawaziri wa zamani, Matheo Qares na Mussa Nkhangaa, mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Joseph Butiku na makada wengine wa CCM walieleza wasiwasi wao kuhusu utendaji wa Rais Kikwete hasa katika kufanya maamuzi magumu dhidi ya mafisadi wakati wa kongamamo hilo la kuadhimisha miaka 10 tangu kifo cha muasisi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.

  Ilifikia wakati walisema kama Kikwete hatafanya maamuzi magumu kabla ya 2010, basi CCM itafute mwanachama mwingine agombee urais kwa tiketi ya chama hicho, huku wengine wakisema CCM imepoteza hadhi kutokana na kutekwa na matajiri.

  Lakini Kikwete, ambaye alirejea juzi kutoka ziara ndefu iliyohusisha nchi za Jamaica, Trinidad na Tobago, Cuba na Marekani, aliwaambia waandishi wa habari kuwa hashangai kuwa watu hao wametoa tuhuma dhidi yake.

  Kikwete aliwaambia waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akisema: "Japo bado sijapata taarifa vizuri kuhusu yote yaliyozungumzwa katika kongamano hilo, siwezi kushangazwa sana, lakini ninakwenda kupata taarifa kamili na kujadiliana na wenzangu kisha nitajibu mambo yote yaliyokuwa na maana na yale ambayo hayana maana na yaliyosemwa kwa chuki, tutayapuuza tu."

  Tamko hilo la Kikwete halikuachwa lipite na wananchi mbalimbali walioongea na Mwananchi, na hasa watoaji wa tuhuma hizo.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana, makada hao walisema hawatishwi na uamuzi huo wa rais kwa kuwa ana uhuru wa kusema, huku Nkhangaa akisema atayatafakari majibu ya Rais Kikwete na ikibidi atajibu tena mapigo.

  "Kumjibu, itategemea 'nature' (aina) ya majibu yake," alisema Nkhangaa ambaye katika kongamano hilo aliweka bayana kuwa CCM sasa imetekwa na wafanyabiashara matajiri na kuachana na sera zake za kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, ndiyo maana imekuwa vigumu kuwashughulikia mafisadi.

  Alifafanua kwamba kongamano hilo halikuwa na lengo la kumchafua Rais Kikwete bali watu walitoa maoni yao kulingana na mada iliyokuwa mbele yao ya "Mstakabali wa Taifa".
  "Mjadala ulikuwa unazungumzia mustakabali wa taifa na wote walitoa maoni yao kulingana na namna wanavyoona na wala hakukuwepo na lengo la kumchafua mtu," alisema Nkhangaa.

  Matheo Qares, ambaye aliwahi kuwa waziri wa Menejimenti na Utumishi wa Umma, alisema jana kuwa jukumu la kujibu hoja atakazotoa rais ni juu ya viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

  Alisema katika hali hiyo ya malumbano hana ushauri wowote kwa Rais Kikwete na wala hawezi kutolea maoni kauli yake ya juzi kwa kuwa hilo si juu yake.

  "Sio juu yangu kumshauri ajibu au asijibu, hii ni juu yake na watu anaodhani wanaweza kumshauri," alisema Qares kwa mkato akirejea kauli ya Rais Kikwete kuwa atakaa na wenzake kuandaa majibu.

  Hata hivyo, baadaye Qares aliliambia gazeti dada la Mwananchi, The Citizen kuwa "hoja kwamba rais atajibu tuhuma hizo au la, mimi sijui, mkawaulize kina Butiku wenye hiyo foundation (taasisi) na 'walioorganize (walioandaa)' hiyo forum' (kongamano)".

  "Mambo aliyozungumza rais mimi hayanihusu, kina Butiku ndio wako katika nafasi nzuri kujibu hoja hiyo mimi sijui hayo," alisema.

  Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa dini wamemshauri Rais Kikwete asijibu shutuma zilizotolewa dhidi yake kwa sababu hazitajenga na badala yake zitachochea zaidi mgawanyiko wa kitaifa.

  "Mimi naona ni busara zaidi angekaa kimya," alisema katibu mkuu wa Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo Tanzania (CCT), Leonard Mtaita.

  "Sizungumzii tu katika suala hili la rais, bali hata viongozi wengine ambao wanalumbana kama malumbano yale ya (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utawala Bora) Sophia Simba na (Mbunge wa Same Mashariki) Anne Kilango."

  Alielezea malumbano hayo kuwa yanawachanganya wananchi na yanawagawanya kulingana na pande zinazosigana, jambo ambalo alisema ni hatari kwa umoja wa taifa.

  Mtaita aliishauri serikali kutumia vyombo vyake katika kutatua matatizo baina yao kwa sababu kuyaweka hadharani, hakujengi bali kunabomoa.

  Katibu mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Suleiman Lolila alisema asingependa kuchangia lolote kuhusu tamko la Rais Kikwete, lakini angependa kuona Tanzania inakuwa na amani.

  Katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amesema kauli ya Rais Kikwete imekata mzizi wa fitina kwa kuwa imetoa majibu sahihi kwa tuhuma dhidi yake.

  "Rais Kikwete jana (juzi) amemaliza kila kitu, sasa mambo yanakwenda. Si mnaona alivyofanya" alisema Makamba jana alipokuwa akiwatambulisha waliokuwa wanachama wa TLP mkoani Kilimanjaro ambao ni katibu mkuu, Aidani Majawanga na katibu mwenezi Shabani Mtego baada ya kujiunga na CCM.

  Bila ya kufafanua kauli yake, Makamba aliongeza kusema: "Ni kweli nitafungwa kama nisipomtetea Rais Kikwete"

  Wiki iliyopita Makamba alilazimika kutumia vitabu vitakatifu vya dini za Kiislamu na Kikristo (Msaafu na Biblia) kumtetea Rais Kikwete dhidi ya watu wanaomtuhumu anasita kufanya maamuzi magumu.

  Miongoni mwa masuala ambayo rais anaonekana kusita kufanya maamuzi magumu ni pamoja na kutowachukulia hatua watu walio chini ya mamlaka yake ambao walitajwa katika maazimio 23 ya Bunge kuwa wawajibishwe kutokana na kuhusika kwao kwa namna tofauti kwenye kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development LLC.

  Miongoni mwa watu hao ni mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah wakati watendaji wengine walio chini ya mamlaka yake wameshastaafu kwa mujibu wa sheria bila ya kuwajibishwa.

  Pia Kikwete anatuhumiwa kutokuwa imara kurejesha nidhamu kwenye chama baada ya makundi yanayopingana kushambuliana waziwazi hadharani, yakituhumiana kwa ufisadi. Badala yake halmashauri kuu ya CCM imeunda kamati ili kuchunguza kutoelewana huko kwa wanachama wake.

  SOURCE:
  Mwananchi
   
 2. H

  Haki JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good job Kikwete, usiwaogope hao Makafir. Tupo nyuma yako kwa nguvu zote.
   
 3. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Majibu gani tena hawa watu wanasubiri?

  4yrs have passed with no actions. Everyone knows that and that's the fact.

  That's the past, and he cannot change that. All he can do now is to tell us what's going to do in the next 11 months.
   
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  mbona ameisha sahau kama alisema atawajibu? anachokumbuka ni kusema kwamba anakwenda kwenye mkutano wa mazingira copenhagen, dernmark. na zaidi mkumbuke ameambia apumzike na madaktari wake na wanje pia, kwa hiyo msitakie matatizo bure wakati akijipanga kusherekea kumalizika kwa mwaka 2009 na kuukaribisha 2010 na kuwa na mapumziko safari hii katavi, hala hala mbunge Arafi wa mpanda huna Binti wa Kiburushi kweli . holiday nyingine itakuwa Mikumi.
   
 5. O

  Orche Senior Member

  #5
  Dec 9, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hizi taarifa za uvumi na uzushi za magazei ya TZ yametuchosha juu ya kijana huyu. Hakuna hasiyejua hayo, wasubiri sasa wajewatuambie kwamaba yametimia badala ya kuendelea kubadilisha vichwa vya habari tu.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,173
  Trophy Points: 280
  Mtanzania yoyote anayesubiri majibu ya Kikwete kwa kudhani kwamba yatatoa mwanga kuhusiana na uongozi wake dhaifu katika kila nyanja ikiwemo kushindwa kupambana na mafisadi, kushindwa kuipitia mikataba ya uchimbaji wa madini na pia kushindwa kutimiza ahadi zake za "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" na "Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya" anapoteza muda wake bure.

  Kikwete amepata nafasi chungu nzima za kufanya maamuzi ambayo yangerudisha imani ya Watanzania kwa uongozi wake kama Rais, lakini nafasi zote hizi amekuwa akijikanyagakanyaga na kujichanganya na kuzidi kutukatisha tamaa Watanzania.

  Kwa hiyo siku atakapoamua kuongea rasmi ili kujibu tuhuma za uongozi wake dhaifu hakutakuwa na jipya lolote la kutupa matumaini Watanzania bali ni kujikanyagakanyaga kama ambavyo ilivyo kawaida yake na kwa mara nyingine tena kutukatisha tamaa mamilioni ya Watanzania. Tunahitaji Rais mpya 2010, Kikwete kazi imemshinda na hili siyo siri kabisa.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,173
  Trophy Points: 280
  Astaghafirullah! ndiyo yamekuwa hayo tena! Nilidhani tunaongea kama Watanzania kumbe imeshakuwa ya makafir na wasiokuwa makafir! OMG! Kazi kweli kweli!
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Dec 9, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kuna watu vichwa vyao vimejaa upepo, mapepo au maji ndugu yangu, ni kuwapuuza tu!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Dec 9, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kazi ipi ambayo unamsifia JK kuifanya mpaka yeye mwenyewe umtenge na ukafiri? Hujui kwamba yeye amewekwa madarakani kwa fedha za ufisadi ndio maana anashindwa kuwachukulia hatua mafisadi? Kuwa mkweli na nafsi yako acha propaganda ambazo haziwezi kukusaidia wewe au mtu mwingine yeyote!
   
 10. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie naona viongozi wanakuwa kama wanawake waliochukuliana wanaume. Wanapigana vijembe kama kwenye miziki ya taarabu. Ishu kama hizi ndio zinachangia kwa kiwango kikubwa kurudisha maendeleo. Huyo anamuita mwenzio sanamu ya michellini huyu anamuita mwenzie hana shape. Sasa hii statement na kuitana mafisadi na wehu zinatofautiana gani.

  Mweh wacha nikale mzigo wangu nchi inaelekea kubaya naona
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  JK amenunua urais kwa fedha haramu.....sasa hawezi kufanya lolote....yeye alitaka amalizie awe rais bogus lakini Alikuwa rais....basi...hakuwa na sera wala jipya....aombee next ptes awe mwana mtandao la sivyo atakaa sana keko kama liyumba!!
   
 12. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Maoni yaliyotolewa na akina Mateo Qaresi ni sahihi kabisa. Sidhani kama JK ana sababu yoyote ya kujibu. Anachotakiwa kufanya ni kujitazama upya na kurekebisha dosari zote za utawala wake. Bado ana kipindi cha karibu mwaka mzima kujirekebisha ili amalize vizuri miaka yake mitano ya urais na kuacha legacy. Ila namshauri baada ya hapo asigombee, apumzike ale starehe. Urais umemshinda! Yawezekana yeye angependa kuendelea kuwa rais, lakini awe rais ili afanye nini? Kuna watu wenye uwezo watajitokeza na nchi itasonga mbele. Akina Makamba nao waache porojo zao za kinafiki, wasidhani kuwa wanamsaidia JK.
   
 13. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  maamuzi gani makubwa mnasubiri kwa huyu bwana zaidi ya yale aliyoyafanya wakati wa sakala la rich mond...? kwa kukubali kumtosa swahiba wake na kulivunja baraza la mawaziri, pamoja na kesi hewa zinazoendlea mahakani za zombe na epa? mimi naona hao yalikuwa maamuzi mazito sana na makubwa kuliko yote kufwanywa na raisi kwa kukubali kutumia gharama kubwa kuendesha hizo kesi na kuanza kuzurura kumba pesa kwaajili ya miradi ya maleria na ukimwi
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Simlaumu uyu mkwele tumemtwika mzigo mkubwa sana wa uaraisi,na huo ndo uwezo wake jamani.
  Vumilieni mpaka atakapoachia kijiti otherwise endeleeeni na maumivu ya kichwa na ughari wa maisha na ahadi ya maisha ya hovyo kwa kila mtanzania..............mafisadi huleeeeeeeeeeeeeeee
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Umepotea jukwaa ndugu.... hili siyo la kidini ni la siasa!
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Dec 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Ndio mjue tabia hizi siyo za wanawake tu!
   
 17. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #17
  Dec 9, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Makafir manaake nini?
   
 18. Ukweliii

  Ukweliii Member

  #18
  Dec 9, 2009
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuhuma za RASI kushindwa kufanya maamuzi ni nzito sana sana saaaaaana. Maana hiyo ndio maana ya uongozi ukishindwa hilo hufai hufai hufai.... Haijawahi kutokea kwenye historia ya TZ. Hata tu watu kuanza kufikiria Raisi aliyeko madarakani asigombee second term. Sijui anataka aambiwe nini tena. CHAGUA UPANDE

  Lazima watu wote wajulikane wako upande gani. Hakuna tishio kwa amani wala undugu. Tofauti za hoja na mtazamo tunaweza kuishi nazo ndio maana ya demokrasia na vyama vingi.
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  Dec 9, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hata mimi ninamsubiri kwa hamu nione atajibu nini.
   
 20. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #20
  Dec 9, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Shukrani Veracity kwa kutambua kuwa hakuna tabia za wanawake wala wanaume...tabia ni tabia tu. Hakuna tofauti ya Makamba na Sophia Simba...ni vijembe kwa kwenda mbele...halo halo,babu wee.
   
Loading...