Majibu ya Kigwangalla: Kwa Nini Sikusaini Hoja ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (MB)!

Najisikia kuugua ghafla baada ya kusoma unafiki huu
na nahisi nikiendelea kuusoma nitajibu ovyo na kutukana na nitaishia kupata BAN
Bora niende kwenye kjukwaa jingine kabisa
 
Dr. Kupeng'e
Msidhani hapo mna mwanachama ni kama msukule tu...

Watu wengine ndio wanafikiri badala yake...

Ninahisi na kale kakampuni kake kalikula hela za stimulus package...

He can't think out of the box..

Good comment! nimeipenda. Asante kwa kumweleza ukweli
 
ndugu zangu wanabodi,



tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni mbunge kutokea ccm na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya ccm kwa hoja inayoletwa na mbunge wa kambi ya upinzani! Mbunge wa chama tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa bunge letu ni wa westminster, na hivyo kuna kambi ya upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na kambi ya serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa ccm tuna jukumu la kuilinda serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye party caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya chama chao. Kuna wengine wanataka bunge liwe bunge huru (ama 'an indipendent power house') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

hk.
inasikitisha jamani
 
Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic!

Really? Are you serious?
 
HKIGWANGALA hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo
msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani

una akili iliyopofuka, unafikira rojo mithiri ya ute wa yai, unatazama mambo kwa macho yaliyojazwa kiwi, una tongotongo za tamaa za madaraka kwa jasho la walalahoi wa taifa letu, anayaona mambo katika sura ya ccm kwanza, taifa baadae.

anawaza kimasikini, anajivika kilemba cha uchapakazi na kutetea vibovu, anasema anakwaza na baraza la mawaziri bila kukerwa na alieliteua baraza hilo, haiwezekani ukawa unaumizwa na rushwa halafu anaeilea rushwa akawa rafiki yako. ...huu ni unafiki, uzandiki na ubinafsi wa kiwango cha juu.
 
Last edited by a moderator:
huyu jamaa kilaza kweli huwezi amini....even the way utetezu wake alivyo oraganize hata moto wa form VI angeweza kujenga Hoja wan JF tukamwelewa.....
Mimi binafsi ninawaomba watu tunafikri ni wasomi kama wewe kabla hamjaja hap JF mjuwe this is the place of Great Thinkers....msituletee utumbo kama huu.......shame up u acting dr!!!!
 
Ndugu zangu wanabodi,

Nimeamua kuja kujibu kama ambavyo mngependa nifanye. Siyo kwamba nimekimbia JF, la hasha. Siwezi kukimbia na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Ni kwamba gadget yangu ninayotumia kwa mawasiliano ilipata mushkeri na nikawa nalazimika kutumia kompyuta na bahati mbaya sana kwa jinsi nilivyokuwa bize na ujenzi wa Taifa nilijikuta nakosa muda wa kukaa kuanza ku-surf. Nisamehewe kwa hilo.

Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.

Kuna uwezekano wa kuwa na tafsiri tofauti kutokana na pre-conceptions zetu vichwani, siwezi kulizuia hilo hata kidogo. Kwa kuwa ninakalia kiti cha uwakilishi, nina-feel ninawajibika kwenu kutoa maelezo ya msimamo wangu kwenye hili, na wala sintomumunya maneno.

Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo. Pili, naamini na ninakubali, na kwa hakika ninakerwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana za kuongoza baadhi ya ofisi nyeti za umma wametuangusha watanzania, na hivyo naunga mkono hoja ya kutaka kuwatoa hawa. Mhe. Zitto Kabwe (MB) alipokuwa akijumuisha hoja yake, alitaka serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa Wizara na Mashirika ya umma, na akasema kama serikali haikufanya hivyo kufikia J3 iliyofuata basi sisi (Bunge) tuna uwezo na WM na kwamba atapitisha karatasi ya kukusanyia saini 70 ili kukidhi matakwa ya kikanuni ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na WM; kwa tafsiri yangu ni kwamba Mhe. Mbunge alilenga kuweka presha kwa serikali, kuitaka iwajibike kwa kuwawajibisha mawaziri hao (watano) kama alivyowataja yeye. Kwanza mwanzoni nilielewa hivyo. Baadaye jinsi ilivyopokelewa na wadau mbalimbali nikaona kama hoja inahama sasa na kwamba si mawaziri hao watano wenye tuhuma mbalimbali, ni PM na kwa maana hiyo ni serikali yote Bungeni! Hili mimi siliungi mkono na silikubali. Nasema wazi hivyo kwa sababu, mimi nina imani na WM, nina imani na Rais - aliyemchagua WM, na nina imani na Mawaziri wengine wengi wazuri tu kwenye serikali hii, na msimamo wangu huu uko wazi sana tu.

Mbili, sioni sababu ya kuiingiza nchi kwenye wasiwasi wa kiutawala kiasi hiki. Na kwa kuwa wabunge wa CCM kwenye party caucus tulikuwa tayari tumeishaambiwa kwamba kuna mawaziri wameamua kujiuzulu wenyewe (tena siyo wale watano, ni wanane kabisa) kutokana na tuhuma hizo na presha kutoka kwa wabunge wa CCM na wengine, sikuona sababu ya mimi kusaini hoja ya Zitto (ambayo kikanuni ilikuwa imekosewa - kitendo kilichonidhihirishia wazi kwamba hakuwa na u-seriousness wa kutaka kweli kumuondoa WM bali ni baadhi ya mawaziri, sema alichomeka tu hiyo kauli ili kutia presha zaidi!). Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama Mhe. Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, na kimkakati zaidi angewapa wabunge wa CCM walioibua hoja hizo za kuwataka mawaziri wang'olewe na hapo angefanikisha malengo ya kumuondoa WM na serikali yake Bungeni. Kwa namna ilivyo hawezi kupata support ya wabunge wa CCM na kwa kuwa sisi ndiyo majority, hoja hiyo haitopita - na hii itaturudisha kule kule kwenye nilichokisema kule twitter kwamba hoja hii ni ......politically right but technically flawed!

Jamani, hoja ya kumuondoa WM madarakani siyo kitu kidogo, siyo kitu cha mchezo, ni lazima ujipange. Ukweli ni kwamba rafiki yangu Mhe. Zitto hakujipanga kuifanikisha (bila shaka yeye mwenyewe analielewa hili vizuri - he is smarter than this, I know him!)

Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.

Wakatabahu,
HK.

Sitaki kusoma utumbo wako. Issue imepita sasa unajitokeza kusema nini hapa! Msomi uchwara arafu DR. nahisi inatumika vibaya!
 
Shukrani Mh. Kigwangalla kwa kuja na majibu haya.

Kwanza kabisa nakubaliana na hoja yako kwamba ndani ya baraza la Mawaziri, wapo ambao kweli ni wasafi na ni ukweli usiopingika.
Ila napingana na wewe kwa kauli yako kwamba unapokua ndani ya CCM lazima ufanye mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Does this mean kwamba hata kama kuna mabovu wewe utayasupport tu? I think umuhimu wa kua ndani ya chama ni kukijenga chama, na chama kunajengeka kwa kuambiana ukweli na wakati mwingine kuwawajibisha wale wanaoenda kinyume na matwakwa ya wananchi ambao chama kinawatetea. Hiki ndio kiini cha mjadala wa kuwataka mawaziri wasio wajibikia wajiondoe.

Ni ukweli usiopingika kwamba ndani ya CCM hakuna mwenye uwezo wa kumfunga paka kengele. Wote ndani ya CCM wanaishi kwa mawazo kama yako, ya kufanya na kufuata yale yote ambayo chama kinawata kufanya, bila kuweka your value judgement. Hiki unachotuambia kwamba ndani ya vikao vyenu kuna Mawaziri 8 waliojitolea kujiuzulu sio cha ukweli na kitatokea tu kwa shinikizo kutoka vyama vya upinzani na wananchi ila sio kwa shinikizo ndani ya CCM yenyewe. Wanachama wa CCM mnaogopana na huu ni ukweli.
Kuhusu hoja yako ya kwamba kuna mawaziri ambao wanautendaji mzuri na usingependa nao wawajibishwe kwa kumshinika PM ajiuzulu, sidhani kama hili ni tatizo. Kama kuna mawaziri ambao unadhani wana utendaji mzuri sio wewe peke yako ambao umewaona. Rais ambae amewateua pia anao uwezo wa kutambua utendaji wa mawaziri wake. Hivyo kuvunjwa kwa baraza la mawaziri hakuzuii kuchaguliwa tena kwa wale mawaziri wenye utendaji mzuri. Kinachoshinikizwa hapa ni kwa PM kujiuzulu ili hao mawaziri ambao utendaji wa sio mzuri waondolewe. Imeonekana wazi kwamba hawa Mawaziri corrupt wana nguvu sana ndani ya CCM na ni lazima itafutwe sababu ambayo itamuwezesha Rais kuitumia kuwaondoa hao mawaziri, na sababu yenyewe ni PM ajiuzulu na baraza zima la mawaziri lifutike wachaguliwe upya, period.

Baadhi ya wana CCM mmefunga Rais mikono na hawezi tena kutoa maamuzi ya msingi kwa kuogopa aidha lawama au nguvu walizo nazo wana CCM wenye hela. Tumsaidie Rais katika hili. Mshinikizeni PM ajiuzulu kama hao mawaziri corrupt hawataki kujiondoa wenye. Hili ndilo jambo ambalo wapenda nchi kama wewe mnatakiwa kuliangalia na sio kuangalia tu kwamba wewe ni CCM na lazima ufuate kila ambalo CCM inalisema. Mmepewa uwezo wa utambuzi kutambua yaliyo mema na mabaya. Kwa hiyo uwingi wenu (CCM) ndani ya bunge usiwafanye kusaua karama yenu ya utambuzi wa mema na mabaya na kuendelea kuyalea yaliyo maovu.

Ni hayo tu kwa sasa.
 
Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo.
HK.

Mkuu nakubaliana na mtizamo wako na kila mtu anastahili kuheshimiwa kwa mawazo yake bila kuwa pressured

Lakini, nashindwa kuelewa mtizamo wako kwamba hii serikali haijashindwa kufanya kazi (either upo out of touch na madudu wanayofanya.., au definition yako ya kushindwa kufanya kazi ni ya juu sana na tuombe Mungu tusifike huko).., in short je unaona mambo yanakwenda sawa na hii serikali ?
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa kuja kuleta majawabu sawia!

Ingawa siwezi kuthubutu kukuita mnafiki kutokana na ukubwa wa neno hili kwa muumba, ila naona kama kuna sehemu sijakufahamu vyema kauli yako kwamba

"Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM",

Wasiwasi wangu katika hili ni je ikiwa mambo hayo ambayo kimsingi yanakubaliwa na ccm yatakuwa yanaenda kinyume na matakwa ya wananchi itakuwaje hapo? mfano tunajua kuwa uongozi ni dhamana na ubadhirifu ni kukosa unaminifu na ni dalili ya unafiki kwa kutenda kinyume na dhamana hapo inakuwaje kaka yangu hebu nijibu tafadhari?


" Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic "


Lakini pia katika dhana hiyo hiyo ya kuungana na yatokanayo na chama chetu "CCM" na kutokubali hoja iliyotoka upande wa pili, napo ninaomba unipe ufafanuzi mzuri, naamini kabisa pamoja na sababu chafu na agenda zingine za vyama vyetu vya upinzani lakini bado kuna masuala yalio sahihi na yanayogusa maslah ya umma,

Huenda hoja iliyoanzishwa kwa upande mmoja ikapelekea kuwapa ushindi wa kisiasa wapinzani lakini swali langu kwako Mh. Ni upi msimamo wako pale hoja inapoletwa na wapinzani ikawa ina maslah makubwa kwa taifa lakini itakipunguzia nguvu chama chetu CCM, utaunga mkono hoja au kupinga? na kama ni lazima uitetee serikali yako huoni kama kwa hilo huwatendei haki wananchi?

Best
Tume ya katiba
 
Ndo maana kwenye katiba mpya tunataka de_centralisation of gvt (states gvt). This will be a final soln.

Kumbe nyie wabunge wa CCM mko mjengoni kutetea serikali yenu. Hata kama imeoza. Ili kuogopa tawi ulilokalia lisianguke....

Tanzania tuachane na mfumo wa west ministers. Tufuate mfumo wa marekani wa States gvt ndo itakuwa soln kwa hii nchi yetu. Yenye walafi wengi
 
Umejieleza sana, ndani ya maelezo yako yooote umeonyesha huko tayari kuwatetea wananchi, chama chako kinawalinda wezi wa fedha za walipa kodi ambao wewe ndiye mtetezi wao bungeni, nawe unayakataa majukumu yako kwa maelezo nasikitika kukwambia ya "kijinga"!!
unawaside wezi kisa kuwa madarakani!!!! Rudia kuyasoma maelezo yako utakubaliana nami kuwa ni ya kijinga. wananchi hawakosei kukikataa ccm na mtu kama wewe mwenye mawazo mgando.
 
Well, sikutarajia ujibu tofauti na haya. Uwezo wako unatosha kwa haya ulosema, ukiendelea zaidi utabaki mtupu. Kwa mujibu wa maelezo yao:

1. Unaunga mkono ufisadi wa serikali yako na uko tayari rasilimali za nchi ziendelee kufujwa ili kuendeleza utawala wa ccm.

2. Hauna uchungu na watanzania wanaoteseka kwa kukosa huduma muhimu, hivyo hufai kuwa muwakilishi wa wananchi. Najua unatetea waliokupa nafasi ya ubunge, endelea kwani mwisho uko karibu.

Najua hakuna msafi ndani ya ccm. Kila mmoja wenu anawaza wizi na ufisadi, watanzania tumeamka na tutawawajibisha.
 
hv j.k mtu kama huyu K.N kuna haja ya kumpa hata ukuu wa wilaya? Kweli umejialibia siwez hata kukuita mh
 
asante ndugu kigwangala kwa kujivua gamba na kutuonyesha jinsi ulivyo kimawazo na vitendo asante sana koma ndugu yangu na chama chako. bra mauye anaunafuu kuliko wewe
 
Back
Top Bottom