Majibu ya Kigwangalla: Kwa Nini Sikusaini Hoja ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (MB)!

Najisikia tumbo la kuhara baada ya kusoma utetezi wa Kigwangala. Huo usaliti unaouonyesha inaonyesha nawe ni mchumia tumbo tu
 
Kwanza, hoja yenyewe siikubali.
HK.

Watu kama nyie hamfai katika uongozi.
Inaonyesha jinsi gani haupo tayari kupokea mabadiliko.
Na vile vile umeridhika na serikali yenu isiyo sikivu kwa kukumbatia walafi na makupe waliopo nchini.
Huu ndo unafiki wenyewe.
Unachumia tumbo.
 
yaani wewee unatuonyesha jinsi gani ulivyo . huna huruma garama za maisha zinapanda kila siku eti serikali ya chama chako haijashindwa lol:mad2:
 
Halafu unatuambia 'wakatabahu' as if umeandika jambo la msingi sana....

Wacha nitoke hapa nisije kula ban ya bure...
 
Mkuu kwanza heshima kwako!viongozi wengi wa nchi za dunia ya tatu hawana hulka ya kuweka mawazo yao hadharani..wengi wanatuongoza ingawa hatujui mitazamo na misimamo yao.
Kwa kuwa kwa maneno yako mwenyewe umesema huna hulka ya UNAFIKI,(hata hivyo UNAFIKI ni neno subjective) naomba nikuulize swali mmoja rahisi kabisa;Unaamini ni mawaziri gani wanadhorotesha hadhi ya chama chenu, na unadhani adhabu gani ni muafaka kwao?ukitupatia majina yao hakika hautakuwa kweli mnafiki.
Baada ya hapo maswali mengine yatafuata.
 
Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani!

Hapa nimeshikwa na tumbo la kuhala gafla.
Wewe mganga njaa huna dhamila ya kweli ya mapambano katika taifa.
Nyie ndo wapingaji wakubwa kila jambo zuri linalo letwa na upinzani kwa kisingizio kaleta wa upinzani.
Umeonyesha dhahiri sura yako.
 
Du!!!nilikuwa nakuheshimu sana kaka lakini kwa huo utumbo uliouweka hapa basi kaka ndo ivyo tena(utamalizia mwenyewe) ,,naomba unijibu swali moja tu, ivi kwako wewe nini kinaanza Chama ama utaifa??kwa iyo kwa kuwa CCM ni chama chako ubadhilifu uliofanywa haukugusi kabisaaa???kama mnazani hiyo ni hoja Zitto mmepotea, soon mtapata jibu na hasira za watu....endelea kutumikia chama kaka!!!!!!!maslahi ya Taifa lazima yaende zaidi ya chama kam CCm mnahisi bila kushirikishwa hoja haipiti bungeni itapita nje ya Bunge,,,M4C ndo inayoendelea sasa na jimboni kwako tutapita kueleza unafiki wako....
 
Bora angeandika hizi pumba kwenye Tanuru lao la Fikra...[QUOTE=Fredrick Sanga;3794099]Unatia aibu sana, ukishakuwa mbunge tunategemea uweke maslahi ya watu wa jimbo lako na taifa mbele sio chama. Msomi kabisa unaongea vitu kama hivi, tena JF. Si ungeendelea kukaa kimya tu. umejishushia heshima sana. Ngoja 2015.[/QUOTE]
 
Kigwangala, huna tofauti na Basil Mramba aliyesema potelea mbali watanzania wale majani mradi ndege ya rais inunuliwe. Mawaziri waitafune tanzania, watanzania wafe kama wanavyokufa sasa hivi kukosa huduma muhimu mradi CCM isitoke madarakani. Kweli hiyo ni busara!!!

You are after power of your party and not the performance and wellbeing of poor Tanzanians particularly thoise at the periphery. Poor Kigwangala!!!
 
Huu utetezi wako hata usingeandika tayari tulishaelewa kuwa hizo ndizo sababu za wewe kutosaini. Kimsingi sababu zako zote zimejikita katika woga na unafiki uliotukuka.

Hivi ulitaka Zitto akutafunie kila kitu?
Mara ohh hajatushirikisha ccm...ulitaka awashirikishe vipi.
Kwani Filikunjombe, Mkono na wengine wa magamba waliosaini wao walisaini vipi?

Ngoja niishie hapa tu....naona kama ban inaninukia.
 
Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

Na huu ndio unafiki wenyewe
Kwa kuwa mnakipenda sana chama chenu na serikali inayoundwa na chama chenu hata ikifanya madudu hamuwezi kuiondoa madarakani maana mnalilia sana mkate wenu
So madudu yenu hata yakiwa makubwa kiasi gani hamuwezi kusema sasa basi tumechoka
So wananchi waendelee kuvumilia uozo wenu kwa kuwa mnalinda serikali yenu ya chama tawala
Umeonyesha ulivyo mnafiki
Kile unachokiandika humu wala hakiendani na wewe kabisa na ukitishiwa tuu nyau unanyea hata kukohoa huwezi
Mnalinda ufisadi kwa kuwa mnaogopa kuiandama serikali yenu iliyojaa madudu
Unadhihirisha kuwa uko kwenye uongozi kwa sababu ya kushibisha tumbo lako na wala sio kutetea wananchi
Unawaambiaje wananchi wa jimbo lako ambao hawana madawa hospitali na madawati kwa ajili ya watoto wanaokaa chini huku mawaziri wa serikali ya chama chako wanatafuna mabilioni ya pesa na unawatetea kwa kuwa huwezi kujiunga na upinzani kuiangusha serikali yako
Unawatetea vipi wanyonge wanaoona madini yaliyoko kwenye jimbo lako yanaondoka na wao wanabakia na mashimo wakati hawaoni faida yake ilhali wewe umeamua kuwatetea mafisadi wenzako kulinda kitumbua chako kisiingie mchanga
Unawajibu nini wananchi ambao kula yao ya siku ni shida wakati wewe umekaa unahudhuria party caucus kutetea wizi na ubadhirifu wa mali ya umma
Bora ungenyamaza ungeonekana wa maana zaidi kuliko kuja kuandika pumba ambazo eti unajisafisha kuwa wewe sio mnafiki
Ni mnafiki namba moja na wala huna uchungu na wananchi wako wala huwatetei kwa lolote sana sana unawamwagia vumbi na kuwaonyesha namna unavyofaidi cake wakati wao hata mhogo wa kushindia hawana
 
Ndugu zangu wanabodi,

Nimeamua kuja kujibu kama ambavyo mngependa nifanye. Siyo kwamba nimekimbia JF, la hasha. Siwezi kukimbia na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Ni kwamba gadget yangu ninayotumia kwa mawasiliano ilipata mushkeri na nikawa nalazimika kutumia kompyuta na bahati mbaya sana kwa jinsi nilivyokuwa bize na ujenzi wa Taifa nilijikuta nakosa muda wa kukaa kuanza ku-surf. Nisamehewe kwa hilo.

Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.

Kuna uwezekano wa kuwa na tafsiri tofauti kutokana na pre-conceptions zetu vichwani, siwezi kulizuia hilo hata kidogo. Kwa kuwa ninakalia kiti cha uwakilishi, nina-feel ninawajibika kwenu kutoa maelezo ya msimamo wangu kwenye hili, na wala sintomumunya maneno.

Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo. Pili, naamini na ninakubali, na kwa hakika ninakerwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana za kuongoza baadhi ya ofisi nyeti za umma wametuangusha watanzania, na hivyo naunga mkono hoja ya kutaka kuwatoa hawa. Mhe. Zitto Kabwe (MB) alipokuwa akijumuisha hoja yake, alitaka serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa Wizara na Mashirika ya umma, na akasema kama serikali haikufanya hivyo kufikia J3 iliyofuata basi sisi (Bunge) tuna uwezo na WM na kwamba atapitisha karatasi ya kukusanyia saini 70 ili kukidhi matakwa ya kikanuni ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na WM; kwa tafsiri yangu ni kwamba Mhe. Mbunge alilenga kuweka presha kwa serikali, kuitaka iwajibike kwa kuwawajibisha mawaziri hao (watano) kama alivyowataja yeye. Kwanza mwanzoni nilielewa hivyo. Baadaye jinsi ilivyopokelewa na wadau mbalimbali nikaona kama hoja inahama sasa na kwamba si mawaziri hao watano wenye tuhuma mbalimbali, ni PM na kwa maana hiyo ni serikali yote Bungeni! Hili mimi siliungi mkono na silikubali. Nasema wazi hivyo kwa sababu, mimi nina imani na WM, nina imani na Rais - aliyemchagua WM, na nina imani na Mawaziri wengine wengi wazuri tu kwenye serikali hii, na msimamo wangu huu uko wazi sana tu.

Mbili, sioni sababu ya kuiingiza nchi kwenye wasiwasi wa kiutawala kiasi hiki. Na kwa kuwa wabunge wa CCM kwenye party caucus tulikuwa tayari tumeishaambiwa kwamba kuna mawaziri wameamua kujiuzulu wenyewe (tena siyo wale watano, ni wanane kabisa) kutokana na tuhuma hizo na presha kutoka kwa wabunge wa CCM na wengine, sikuona sababu ya mimi kusaini hoja ya Zitto (ambayo kikanuni ilikuwa imekosewa - kitendo kilichonidhihirishia wazi kwamba hakuwa na u-seriousness wa kutaka kweli kumuondoa WM bali ni baadhi ya mawaziri, sema alichomeka tu hiyo kauli ili kutia presha zaidi!). Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama Mhe. Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, na kimkakati zaidi angewapa wabunge wa CCM walioibua hoja hizo za kuwataka mawaziri wang'olewe na hapo angefanikisha malengo ya kumuondoa WM na serikali yake Bungeni. Kwa namna ilivyo hawezi kupata support ya wabunge wa CCM na kwa kuwa sisi ndiyo majority, hoja hiyo haitopita - na hii itaturudisha kule kule kwenye nilichokisema kule twitter kwamba hoja hii ni ......politically right but technically flawed!

Jamani, hoja ya kumuondoa WM madarakani siyo kitu kidogo, siyo kitu cha mchezo, ni lazima ujipange. Ukweli ni kwamba rafiki yangu Mhe. Zitto hakujipanga kuifanikisha (bila shaka yeye mwenyewe analielewa hili vizuri - he is smarter than this, I know him!)

Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.

Wakatabahu,
HK.

Kweli nimeona hoja zako si za kitaifa bali chama chako, hukufikiria hata madaktari wenzako wala wazazi wako wakiugua, unasema mawaziri watano wakati ni orodha tu ndefu . Umedhihilisha unafiki wako na kujikomba kwako na kutojua hasa kazi ya ubunge
 
Kwani si tulijua ulikuwa mkali kipindi kwasababu ya machungu ya kuswekwa Jela! It was personal, si kwa ajili ya watu! Sasa tunadhudia unalipa fadhila maana hata hukustahili kuwa mbunge tunakumbuka kwenye kura za maoni za chama chako ulipata kura chache, ulikuwa mtu wa tatu! Kwahiyo huo ubunge ulipewa!
 
hakiyamungu 2015 sikuchagui.mbunge gani hajui hata utaifa anawaza uccm aaaagh.i never see majibu ya ovyo kama haya.haya hao mawaziri watano waliojiuzuru wakowapi?
 
Back
Top Bottom