Majibu ya Hotuba ya Rais kwa waitwao wazee wa Dar

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,990
20,292
1. Hoja kwamba pesa zilitolewa kwa uamuzi wa hukumu ya sept5.2013 sio sahh kwasababu hukumu ilisema ALL AFFAIRS OF IPTL SHOULD BE HANDED TO PAP. Haikusema kama escrow monies ni party of affairs of IPTL kwasababu zilikuwa kwenye mgororo. hoja ya kusema hukumu ilisema ilikuja baada ya kikao cha Oct8.2013 kunduchi beach hotel ambacho kiliongeza maneno kwenye hukumu kwa kusema ALL AFFAIRS OF IPTL INCLUDING RECEIBLES FROM ESCROW AC SHOULD BE HANDED TO PAP. Huko ni kupotosha hukumu kwani hela za escrow zilikuwa na mgogoro kati ya Tanesco na IPTL na PAP kununua IPTL haimanishi mgogoro kati ya IPTL na Tanesco umekwisha bali PAP ingechukua nafasi ya IPTL kwenye mgogoro wa pesa za escrow. hili Rais kapotoshwa.

2. Kusema Muhongo atamtoa bada ya uchunguzi wake ikulu kukamilika ni mbinu ya kumlinda kwani mbona mawaziri wanne waliohusika ktk oparesheni tokomeza ripoti ya bunge ilitosha rais kutengua uteuzi wao na kisha rais akaunda tume ya rais uchunguzi. kwann kwa Muhongo inakuwa kinyume chake?

3. Bunge liliazimia mamlaka ya uteuzi ichukue hatua dhidi ya Maswi. Rais anasema suala la Maswi ameliacha kwa mamlaka ya nidhamu ambayo ni Katibu Mkuu Kiongozi, Hapa Rais amekwepa Jukumu lake kwani yy ndio anateua na kufukuza Makatibu wakuu. pia suala hili sio jipya kwa Katibu Mkuu Kiongozi ingetosha awe amekwisha kuchukua hatua za kinidhamu siku nyingi kama TRA walivofanya kwa wahusika tawi la Ilala.

4. Hoja kwamba kutaifisha mitambo ya IPTL kutakimbiza wawekezaji ina mapungufu kwasababu kwa mujibu wa ripoti ya CAG, PAP alifanya utapeli wa kughushi katika umiliki wa IPTL hivyo sio mwekezaji mwadilifu hivyo kutaifisha haiwezi kutisha wawekezaji. pia ifahamike kwamba wawekezaji wengi wanatoka Ulaya na Amerika na nchi hizo ndio zimezuia misaada kutaka serikali itekeleze mazimio ya Bunge na mazimio ya Bunge ni pamoja na kutaifisha mitambo hiyo. sasa inawezekanaje nchi hizo zinazotaka serikali itekeleze mazimio kwamba ndio zikimbie kuwekeza kwa sisi kutekeleza mazimio husika? hapa ni namna ya kulinda matapeli wanaokuja kwa jina la wawekezaji

5.Hoja kwamba mikataba ikiwa wazi itakimbiza wawekezaji ina mapungufu kwasababu tatu;
a. Nchi nyingi sasa duniani mikataba ipo wazi na mfano rahisi ni Ghana na bado wawekezaji hawajakimbikia kwasababu hiyo. Ndio utekelezaji halisi wa itifaki ya OPEN GOVERNANCE ambayo Tanzania tulisaini

b. Kipengele cha Usiri(Confidentiality clause) kwa mikataba yote kinasema mkataba utakuwa siri isipokuwa kwa pande za mkataba(parties of contract) na kwa mahitaji ya dola( statutory purpose). sasa statutory purpose maana yake ni mahitaji ya Serikali, Bunge na Mahakama. sasa tatizo la sasa ni pale serikali inapokataa kutoa mikataba kwa bunge kwa hoja ya kipenge cha usiri(confidentiality clause) wakati kipengele hicho kinaruhusu Bunge kuwa na mamlaka ya kuona mikataba kama part of state organ

c. Pia wawekezaji hawa wanaposaini mikataba hapa wanakwenda kutafuta mitaji kwenye masoko ya mitaji kwao(stock markets). Kule kwenye masoko ya mitaji wanaweka wanalazimika kuweka mikataba hiyo wazi na wanaweka. hivyo kwa dunia ya leo ni aibu kuendelea kufanya mikataba kuwa siri.

6. Hoja ya kodi. TRA walidai kodi kwa barua kwenda BOT. na Werema ndio aliandika barua kukataa kodi. Kwakuwa CAG alikiri ktk ripoti kuwa kodi ilipaswa kulipwa kiasi cha 23bn mana yake alosema kodi isilipwe anapaswa kuchukuliwa hatua za kutaka kusababisha hasara hiyo. ikumbukwe Basil Mramba yupo mahakamani mpaka sasa kwa kesi ya kusababisha hasara ya 11bb. inawezekanaje hawa waishie kujiuzulu?

7. Mwisho kauli ya Mhe Rais kuwa fedha zile ni za IPTL kwasababu tu ziliwekwa kwenye escrow na Tanesco badala ya kulipwa moja kwa moja kwa IPTL kutokana na mgogoro sio sahh kwasababu pesa ya mgogoro kati ya Tanesco na IPTL haiwezi kuwa ya IPTL mpaka mgogoro umalizike na mwenyewe amekiri kuwa mpaka pesa hizo zinatolewa mgogoro ulikuwa haujamalizika. ni kwa mantiki hiyo pesa hiyo haikuwa sahh kuita ya IPTL. pia hapa niongeze kwamba Mgogoro wa IPTL kutoza zaidi Tanesco capacity charge unamanisha ni dhuluma ya IPTL tangu mwanzo wa utekelezaji wa mkataba mwaka 2002 na sio 2006 kama Mhe Rais alivosema. Hii ni kwasababu mgogoro wa IPTL ku overcharge Tanesco kwenye capacity charge msingi wake ni udanganyifu wa IPTL ktk mtaji na hivyo hesabu yake inapaswa kuzingatia tangu mwanzo wa utekelezaji wa mkataba mwaka 2002 na sio 2006 escrow ilipofunguliwa. Hii inakaziwa na Uamuzi wa mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara ( International Centre For Setllement Of Investment Disputes-ISCID) wa Feb12. 2014.

David Kafulila(MB)
 
Ahahaha!! Rais sijui ndo kaongea nini leo. Yaani unatoa hukumu ya kesi kwa Jambazi mmoja kisha unawaacha Majambazi wengine waendelee ujambazi wao. SHAME ON YOU.
 
Wakati mwingine nikiona sura au jina la huyu kichwa nazi natamani kutapika... Nakubaliana na aliyewahi kusema kuwa kuna mtoto alizaliwa miaka 1950s na kichwa cha nazi na leo ni raia namba moja wa Wadanganyika..

Nawaomba Wabunge vijana wote bila kujali itikadi zenu vita ya kulinda rasimali zetu ndiyo imeanza bahati nzuri adui keshajidhirisha mchana kweupe. Sasa kazi iliyobaki kwa nyie wakina Zitto, Filikunjombe, Kigwangala, Mnyika, Mdee, Kafulila, Wenje, Bulaya, Mpina na wengine wenye mapenzi mema na nchi hii Mkirudi Bungeni anzeni na Hoja ya kutokuwa na IMANI NA RAIS WA JMT.

Najua ni kazi kubwa lakini kuwasilisha Hoja tu inatosha kufikisha ujumbe kwamba haturidhiki na mwenendo wa Rais.. Ni Changamoto kubwa lakini naamin majina yenu yataandikwa kwa wino wa dhahabu..
 
huko china rais wa sasa amewatia hatiana senior officers wa rais aliyeondoka madarakan
tuombe mungu hapa tz itokee 2016
 
Kikwete anashangaza sana huyu jamaa, pesa yote imewekwa na TANESCO halafu yeye anadai ni pesa ya IPTL!!!! Ni pesa ya IPTL kwa maamuzi ya nani!? Ya Kikwete baada ya kushauriwa na Ruge, Tibaijuka, Muhongo, Maswi, Ndullu, Chenge na Werema!? Ripoti ya CAG inaonyesha vingine na yeye kaja na yake baada ya kuichakachua hiyo ripoti kufuatia kuzugwa na mwizi Ruge.

The CAG has also established that all money in the Tegeta escrow account was supposed to be paid back to Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) because the state-owned power utility had been overcharged a total of Sh321 billion by IPTL between 2002 and 2012.

According to two senior officials from the CAG's office, who were among investigators who probed the multibillion-shilling scandal, Mr Sethi presented forged documents to the Tanzania Revenue Authority (TRA) and Business Registration and Licencing Authority (Brela) in an attempt to hide the dubious nature of the transactions.

What CAG found out in escrow deal - National - thecitizen.co.tz
 
Rais wetu ndiye mteuzi wa wahusuka wanaotakiwa kuwajibishwa, haya mambo ya kuendelea kuchunguza kusiko kuwa na mwisho! Ni kulindana, na kuendelea kuwaomba wahusika waachie ngazi. Huu ni mwendelezo wa udhaifu!
 
Kikwete anashangaza sana huyu jamaa, pesa yote imewekwa na TANESCO halafu yeye anadai ni pesa ya IPTL!!!! Ni pesa ya IPTL kwa maamuzi ya nani!? Ya Kikwete baada ya kushauriwa na Ruge, Tibaijuka, Muhongo, Maswi, Ndullu, Chenge na Werema!? Ripoti ya CAG inaonyesha vingine na yeye kaja na yake baada ya kuichakachua hiyo ripoti kufuatia kuzugwa na mwizi Ruge.

The CAG has also established that all money in the Tegeta escrow account was supposed to be paid back to Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) because the state-owned power utility had been overcharged a total of Sh321 billion by IPTL between 2002 and 2012.

According to two senior officials from the CAG’s office, who were among investigators who probed the multibillion-shilling scandal, Mr Sethi presented forged documents to the Tanzania Revenue Authority (TRA) and Business Registration and Licencing Authority (Brela) in an attempt to hide the dubious nature of the transactions.

What CAG found out in escrow deal - National - thecitizen.co.tz
Kaka siamini hata kama ulishaisoma report ya CAG kuhusu account ya ESCROW thus why bado unalazimisha kuwa ni pesa za Umma, jifunze kuwa mkweli wa nafsi yako, tusipende kuonea mtu tu kwakuwa sio wa chama au dini yetu! CAG kamwe hajasema hizo pesa ni za umma,chetu mle ni kodi tu
 
Napenda niwahamasishe wanabodi wote, hili la ESCROW hakuna kukata tamaa, hadi kieleweke liwe fundisho kwa wezi na mafisadi!
 
Kikwete anashangaza sana huyu jamaa, pesa yote imewekwa na TANESCO halafu yeye anadai ni pesa ya IPTL!!!! Ni pesa ya IPTL kwa maamuzi ya nani!? Ya Kikwete baada ya kushauriwa na Ruge, Tibaijuka, Muhongo, Maswi, Ndullu, Chenge na Werema!? Ripoti ya CAG inaonyesha vingine na yeye kaja na yake baada ya kuichakachua hiyo ripoti kufuatia kuzugwa na mwizi Ruge.

The CAG has also established that a

waweza kuwa na point,lakini mgogoro wa kwanza wa overcharge ulikua solved katika mahakama ya kimataifa,which means bill ikawa inakwenda kwa rate iliyotokana na hukumu hiyo.
sasa mgogoro wa pili ulitolewa hukumu na mahakama ipi hadi mtu akokotoe mahesabu na kudai hela yote ni ya tanesco?
 
Acha ujinga wewe, pesa ziwekwe na TANESCO halafu ziwe IPTL kwa maamuzi ya nani!? Tangu lini pesa ya wizi ikatozwa kodi? CAG na PCCB wote wamethibitisha pesa ni za umma na ziliibiwa. Acha kuandika uongo kutetea wezi na mafisadi. Weka hapa ushahidi unaoonyesha zile pesa ni za IPTL. Alikwambia nani kwamba CAG na PCCB waliandika ripoti zao kwa kuangalia chama cha wahusika au dini zao!? Acha ujinga bhanaaa!!!

Kaka siamini hata kama ulishaisoma report ya CAG kuhusu account ya ESCROW thus why bado unalazimisha kuwa ni pesa za Umma, jifunze kuwa mkweli wa nafsi yako, tusipende kuonea mtu tu kwakuwa sio wa chama au dini yetu! CAG kamwe hajasema hizo pesa ni za umma,chetu mle ni kodi tu
 
Very disappointed .
Siamini kawaachia wezi na majambazi Huru .

Bora angekaa tu ikulu asiseme kitu .
 
Kaka siamini hata kama ulishaisoma report ya CAG kuhusu account ya ESCROW thus why bado unalazimisha kuwa ni pesa za Umma, jifunze kuwa mkweli wa nafsi yako, tusipende kuonea mtu tu kwakuwa sio wa chama au dini yetu! CAG kamwe hajasema hizo pesa ni za umma,chetu mle ni kodi tu

Hiyo kodi sio ya UMMA?

Hata wewe hujaelewa somo. Kwenye hii pesa ya escrow, hakuna kodi maana mwenye wajibu wa kulipa kodi ni mmiliki wa IPTL wakati wa kupeleka VAT returns na alipopeleka income tax returns. Kama hakulipa wakati huo na TRA wakanyamaza kimya na kuendelea kukimbizana na maskini kwenye EFD, Waziri wa Fedha na Commissioner General wa TRA wana kesi ya kujibu.

Kosa kubwa hapa ambalo hata Mkuu wa nchi kalipiga danadana ni uhalali wa pesa kutolewa kwenye akaunti ilikohifadhiwa. Haikutakiwa kutoa pesa eti ndio AFFAIRS, Mahakama iliposema affairs, kwa upande wa escrow, ilimaanisha kupokea mgogoro uliokuwepo katika hali iliyopo na kuendelea kusuruhishana na Tanesco
 
Mimi binafsi sijaelewa hasa maana ya JK kukutana na kuongea na wazee wa Dar. Maana nimeishia kuona JK peke yake akiongea na sijaona mzee yoyote kuongea au kuuliza swali. Nafikiri wazee hawakutendewa haki bali wamesumbuliwa tu. Hata kama ni kusema JK ameongea na wananchi kupitia wazee wa Dar sihafiki kabisa, sababu sijaona mchango wa hao wazee kwenye maongezi hayo. Nafikiri aliyochofanya JK angeweza kufanya popote hata kama ni ikulu akiwa mwenyewe kwenye chumba maalum na kuongea na wananchi kupitia TBC na habari ingekuwa ni ileile.
 
Kaka siamini hata kama ulishaisoma report ya CAG kuhusu account ya ESCROW thus why bado unalazimisha kuwa ni pesa za Umma, jifunze kuwa mkweli wa nafsi yako, tusipende kuonea mtu tu kwakuwa sio wa chama au dini yetu! CAG kamwe hajasema hizo pesa ni za umma,chetu mle ni kodi tu
Hapo kwenye red,kama chenu ni kodi ni chenu kama umma au chenu kama nyinyi,na nyinyi ni nani, ebu fafanua.
 
Back
Top Bottom