Majibu ya hoja za Lissu kuhusu ruzuku ya Chadema

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Anaandika TUNDU LISSU:

Advocate Mahinyila salaam,

Nafikiri una tatizo moja kubwa: unaelekea kuamini kila tuhuma inayoelekezwa CHADEMA na wanachama wetu wa jana na juzi.

Sijakusikia ukijipa tahadhari ya kujiuliza swali moja rahisi: hivi kwa nini wahamaji wetu hawa wanagundua maovu ya ndani ya CHADEMA pale tu wanapoondoka na kuhamia CCM???

Lipo lingine ambalo nadhani pia ni swali muhimu la kujitahadharisha na maneno ya wahamaji hawa: ni kwa nini 'wimbi' hili la wahama chama lipo CHADEMA tu kwa sasa???

Nitaanza na swali la kwanza na mtaniwia nikiwarudisha nyuma kidogo katika historia ya chama chetu. Tukifahamu historia ya masuala haya hatutayumbishwa na makelele ya akina Mwita Waitara wa sasa na wajao.
Katika wahama CHADEMA wa kwanza kabisa, Dr. Amani Walid Kabourou, Katibu Mkuu na baadae Makamu Mwenyekiti wetu alikuwa ni maarufu zaidi.

Huyu alihama mwaka 2006, mara baada ya kupoteza ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005.

Dr. Kabourou alihama akiwa Makamu Mwenyekiti wetu, takriban miaka miwili baada ya timu ya Mh. Mbowe na Dr. Slaa kuchukua uongozi wa CHADEMA.

Heshima pekee ya Dr. Kabourou, kwa kuzingatia haya ya waliofuata baadae, ni kwamba yeye aliondoka bila kusema sana. Angalau mimi sikuwahi kumsikia akiyoyoma kama hawa wa baada yake.

Hizi tuhuma za ruzuku na 'Uchagga' dhidi yetu zilianza na Makamu Mwenyekiti wetu aliyerithi mikoba ya Dr. Kabourou, marehemu Chacha Zakayo Wangwe.

Chacha alikuwa rafiki yangu mimi tangu tulipokutana kwa mara ya kwanza mwaka 2003, wakati wa harakati za kudai haki za wananchi wa Nyamongo dhidi ya Mgodi wa Dhahabu wa North Mara sasa.

Nilimkuta akiwa diwani wa Kata ya Tarime Mjini kupitia NCCR-Mageuzi. Tayari alikuwa na kesi kumi na moja za kubambikiziwa na Mgodi na maswahiba wao maCCM, wakiongozwa na kaka yake mwenyewe Peter Wangwe 'Keba', wakati huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

Mwaka uliofuata Chacha alifungwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi minne. Nilijitolea kuwa wakili wake katika rufaa ya Mahakama Kuu Mwanza. Kitu ambacho wengi hawakijui ni kwamba gharama zote za usafiri wa kwenda Mwanza na baadae Tarime kumtetea kwenye kesi kumi zilizobaki zilitoka kwenye mifuko binafsi ya Mwenyekiti Mbowe.

Tulishinda rufaa na kupangua kesi nyingine zote kumi katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime. Chacha hakuwahi kuchangia shilingi moja katika kesi zake zote, hata ya ubunge ya 2006.

Kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005 mimi binafsi nilifanya kampeni sana Tarime. Na baada ya kutatua tatizo la ubambikiziaji wananchi kesi za uongo, tuliwasambaratisha maCCM na Chacha alichaguliwa kwa kura nyingi kuliko mbunge mwingine yeyote wa upinzani.

Kwa hiyo Chacha Zakayo Wangwe aliingia bungeni akiwa na umaarufu mkubwa ndani na nje ya Chama. Kwangu binafsi tatizo lilianzia hapo.
Kwanza alianzisha ugomvi mkubwa ndani ya Chama wilayani Tarime. Ndani ya mwaka mmoja aligombana na viongozi karibu wote wa CHADEMA Wilaya waliomsaidia kupata ubunge.

Ndani ya mwaka huo huo, alihama jimboni na kuhamia Dar. Chacha aliyenyanyaswa sana na Wazungu wa Nyamongo akawa anaenda jimboni Tarime kwa 'lifti' ya ndege za Wazungu wa Mgodi wa Nyamongo. Mengine sitayasema hapa.
Mwaka huo huo, kufuatia kukimbia kwa Makamu Mwenyekiti Kabourou, Chacha akawa Makamu Mwenyekiti wetu.

Mwaka huo huo wa 2006, Chacha akaanza kuwaambia wananchi wa Tarime waliokuwa wanamhoji sababu za kukimbia Jimbo, kwamba sio lazima agombee ubunge mwaka 2010 kwani atakuwa ana 'majukumu makubwa ya kitaifa.'
Haukupita muda Chacha Zakayo Wangwe akatangaza kuwa anataka kugombea Uenyekiti wa Chama Taifa ili kuondoa 'Uchagga' na kugawa ruzuku hadi wilayani badala ya kuliwa na watu wa Makao Makuu.

Hapo ndipo zilipoanzia tuhuma za 'Uchagga wa CHADEMA' na 'ulaji wa ruzuku.' Wakati huo tulikuwa na wabunge watano wa kuchaguliwa na Viti Maalum sita, na ruzuku haikuwa inafika hata milioni 50

Kuhusu ruzuku

Kitu cha kwanza cha kuelewa ni kwamba ruzuku yetu haijawahi kutosheleza hata mahitaji ya kawaida ya uendeshaji chama.
Kila inapotokea kuna uchaguzi wa marudio au Uchaguzi Mkuu wowote ule, matumizi yamekuwa ni makubwa kuliko mapato yetu ya ruzuku na michango ya wabunge.

Tunapowapiga sana wabunge wetu, tuwe tunakumbuka pia kwamba nje ya ruzuku, wabunge wetu wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha mapato ya chama hasa nyakati za Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio.

Kwa sababu ya upungufu huo wa mapato, hasa kila wakati wa Uchaguzi Mkuu, tumelazimika kukopa pesa kwa ajili ya kampeni kwa mapatano kwamba madeni hayo yatarudishwa baada ya Uchaguzi Mkuu.

Sasa ni vyema tujiulize, katika hali halisi ya Tanzania hii, ni akina nani hasa ambao wako, na wamekuwa, tayari kukikopesha chama??? Ni wachache sana, kwa sababu za wazi kabisa: hofu ya kunyanyaswa na mapolisi au uhamiaji au TRA.

Nimekuwa naingia kwenye vikao vya Kamati Kuu tangu mwaka 2004, na ninaweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba hakuna kikao cha Kamati Kuu kilichokaa kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, ambacho hakikumwambia Mwenyekiti wetu atafute pesa za kampeni hata kwa kukopa, ili tuweze kununua vifaa vya kampeni au kulipia huduma zinazohitaji malipo.

Chopper, magari, pikipiki, bendera, mabango na kila aina ya vifaa vingine vya uchaguzi vinapopatikana kila Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, huwa hatuna utamaduni wa kuuliza au kujiuliza vifaa hivi vyote vitakuwa vimegharimu kiasi gani, na pesa hiyo itakuwa imetoka wapi.
Hata hivyo, kila baada ya Uchaguzi tunapoanza kulipa madeni ya waliotukopesha kwa maagizo ya Kamati Kuu ya Chama, kunakuwa na kelele kubwa kwamba ruzuku ya chama inaliwa na viongozi wakuu, hasa Mwenyekiti. Na kila anayehama chama na kukimbilia CCM anarudia rudia tuhuma hizo mpaka watu wetu wanaanza na wao kuzirudia rudia.

Na lengo kubwa la mashambulizi haya, miaka yote, ni Freeman Aikaeli Mbowe, huyo huyo ambaye kila uchaguzi ukifika tunamwomba atutafutie pesa za kampeni.

MaCCM wanajua wanachokitaka kwenye kampeni hii ya kumchafua Mwenyekiti wetu. Wapambe wao, hasa wahamaji hawa, nao wanajua. Je, sisi wanachama wa CHADEMA tunaozirudia rudia tuhuma hizi tunajua hii ngoma tunayoicheza???

Naambiwa CAG naye amehoji juu ya matumizi ya ruzuku yetu. Ni kweli. Lakini ni kweli pia kwamba CAG amezungumzia pesa za ruzuku ambazo hatujawahi kuzipata tangu tuanze kupata ruzuku.
Na kwenye suala la ruzuku, maafisa wa Ofisi ya CAG wametuhumiwa kutoa taarifa yao bila kutupa sisi fursa ya kujibu 'audit queries' zao, kama inavyotakiwa na sheria na taratibu za ukaguzi wa mahesabu.

Tunapaswa hapa kukumbuka kwamba CAG na maafisa wake ni wateule wa Jiwe na/au watumishi wa serikali ambao, kwa mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, wanashinikizwa sana kutafuta namna ya kuiumiza CHADEMA. Kwa hiyo, badala ya kumeza kila kinacholetwa kwa jina la CAG, tunahitaji angalau kujihadhari na taarifa hizo kwa kuuliza maswali muhimu juu ya usahihi wake.

Kumalizia hoja hii ya ruzuku

Tumeijibu tangu ilipoanza kuibuliwa na marehemu Chacha Wangwe mwaka 2006/07. Tumeijibu wakati tunashughulikia 'Mkakati wa Mabadiliko' wa akina Zitto na Kitilla Mkumbo. Tumejieleza na kujieleza.

Lakini maCCM na wapambe wao wana malengo yao ya kutaka tuendelee kujadili ruzuku ya CHADEMA. Inawauma kwamba tangu mwaka 2005 tulipoanza kuonyesha aina mpya ya kampeni za kisiasa.
Tangu wakati huo, mafanikio yetu yamekuwa makubwa zaidi. Kutoka chama chenye wabunge 5 mwaka 2000 hadi chama kikuu cha upinzani chenye wabunge 72 mwaka 2015 ni mafanikio makubwa.

Ruzuku yetu imeongezeka pia, hata kama bado haikidhi mahitaji yetu yote. Wakati najiunga CHADEMA mwaka 2004, ruzuku yetu ilikuwa milioni 5.6 kwa mwezi. Leo ni takriban milioni 250 kwa mwezi.
Haya ni mafanikio makubwa. MaCCM wanajua hivyo lakini hawawezi kusema hivyo hadharani. Hawafurahishwi nayo. Ukitaka kujua wanatuonaje angalia mambo yote wanayotutendea. Mauaji, vipigo, vifungo vya kusingiziwa, ukiukaji wa haki za kisiasa, propaganda chafu, n.k.

Kuhusu kifo cha marehemu Chacha Zakayo Wangwe

Hii pia ni propaganda chafu iliyoanzishwa na maCCM. Ulizeni watu wetu wa Tarime kilichotokea mara baada ya kifo cha marehemu Chacha. Ghafla msiba ule ukawa wa akina Wassira na maCCM wenzao.

Ukweli ni kwamba tuhuma hizi zilianzishwa na Wassira na genge lake wakati wa msiba huo. Vijana wa CCM walitolewa Bunda, Musoma na maeneo mengi nje ya Tarime na kuletwa kuja kumfanyia fujo Mwenyekiti wetu msibani.

Ndugu zake Chacha, wale wale waliokuwa wakimbambikizia kesi ili afungwe wakati wa uhai wake, wakawa sasa ndio wenye uchungu naye akiwa amekufa. Hata hivyo, wananchi wa Tarime walielewa kilichokuwa kinaendelea.

Ndio maana kwenye uchaguzi wa marudio baada ya kifo cha marehemu Chacha, tuliwapiga vibaya. Na ndio maana Tarime imeendelea kuwa ngome kubwa ya CHADEMA.

Inatosha tu kujiuliza kama kweli tungekuwa tumemuua Chacha, haya maCCM kwa jinsi wanavyotuchukia wangetubakiza kwa hii miaka kumi??? Tunatakiwa kujielewa, tusije tukajikuta tunacheza ngoma ya maadui zetu wakubwa.

Nizungumzie swali langu la pili: Kwa miaka zaidi ya kumi sasa, CHADEMA ndio adui nambari moja wa maCCM. Dhambi yetu kubwa ni ile ile iliyokuwa dhambi kubwa ya NCCR-Mageuzi kati ya mwaka 1995 na 2000; na CUF kati ya 2000 na 2005.

Ni dhambi ya kuwa chama kikuu cha upinzani. Ni dhambi ya kuwa na mafanikio makubwa kwenye uchaguzi. Ni dhambi ya kupendwa na kuungwa mkono na wananchi.

Kwa sababu ya dhambi hiyo, ni lazima tushambuliwe na kuchafuliwa na kufanyiwa kila aina ya fujo na hila.

Tusipolielewa hilo ni rahisi sana kukatishwa tamaa na haya ya akina Waitara wa juzi, jana na wanaokuja mbeleni.

Ili tusibabaishwe na haya ya Magufuli na watu wake na hawa maYuda Iskariote, tukumbuke tu tulikotoka.

Tulikuwa na Amani Walid Kabourou kama Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Aliondoka na kujiunga na maCCM. Tulisonga mbele.

Tulikuwa na Zitto Zuberi Kabwe, Naibu Katibu Mkuu na Naibu KUB. Tulimwondoa na tukasonga mbele.

Tulikuwa na Mzee Saidi Arfi, Makamu Mwenyekiti na mrithi wa marehemu Chacha. Alitoroka na kujiunga nao, haikuwa mwisho wetu.

Tulikuwa na Dr. Wilbrod Peter Slaa, Katibu Mkuu na mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo. Alitukimbia katikati ya vita lakini hatuku-surrender. Tulisonga mbele.
Hawa wanaomkimbilia Jiwe, huyu anayetuogopa hadi kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa, wanatubabaishaje???

Mwisho, kwa yote ambayo nimeyasema hapa, sina maana sisi ni malaika tusiokuwa na doa lolote. Tuna mapungufu mengi ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi ili kuyaondoa.

Mengine ni ya kujitakia; mengine ni ya kutakiwa na maadui zetu. Tupembue yapi ni ya kwetu wenyewe na yapi ni ya maCCM. Yote tuyatafutie dawa.
 
Anaandika TUNDU LISSU:
Advocate Mahinyila salaam,
Nafikiri una tatizo moja kubwa: unaelekea kuamini kila tuhuma inayoelekezwa CHADEMA na wanachama wetu wa jana na juzi.
Sijakusikia ukijipa tahadhari ya kujiuliza swali moja rahisi: hivi kwa nini wahamaji wetu hawa wanagundua maovu ya ndani ya CHADEMA pale tu wanapoondoka na kuhamia CCM???
Lipo lingine ambalo nadhani pia ni swali muhimu la kujitahadharisha na maneno ya wahamaji hawa: ni kwa nini 'wimbi' hili la wahama chama lipo CHADEMA tu kwa sasa???
Nitaanza na swali la kwanza na mtaniwia nikiwarudisha nyuma kidogo katika historia ya chama chetu. Tukifahamu historia ya masuala haya hatutayumbishwa na makelele ya akina Mwita Waitara wa sasa na wajao.
Katika wahama CHADEMA wa kwanza kabisa, Dr. Amani Walid Kabourou, Katibu Mkuu na baadae Makamu Mwenyekiti wetu alikuwa ni maarufu zaidi.
Huyu alihama mwaka 2006, mara baada ya kupoteza ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005.
Dr. Kabourou alihama akiwa Makamu Mwenyekiti wetu, takriban miaka miwili baada ya timu ya Mh. Mbowe na Dr. Slaa kuchukua uongozi wa CHADEMA.
Heshima pekee ya Dr. Kabourou, kwa kuzingatia haya ya waliofuata baadae, ni kwamba yeye aliondoka bila kusema sana. Angalau mimi sikuwahi kumsikia akiyoyoma kama hawa wa baada yake.
Hizi tuhuma za ruzuku na 'Uchagga' dhidi yetu zilianza na Makamu Mwenyekiti wetu aliyerithi mikoba ya Dr. Kabourou, marehemu Chacha Zakayo Wangwe.
Chacha alikuwa rafiki yangu mimi tangu tulipokutana kwa mara ya kwanza mwaka 2003, wakati wa harakati za kudai haki za wananchi wa Nyamongo dhidi ya Mgodi wa Dhahabu wa North Mara sasa.
Nilimkuta akiwa diwani wa Kata ya Tarime Mjini kupitia NCCR-Mageuzi. Tayari alikuwa na kesi kumi na moja za kubambikiziwa na Mgodi na maswahiba wao maCCM, wakiongozwa na kaka yake mwenyewe Peter Wangwe 'Keba', wakati huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Mwaka uliofuata Chacha alifungwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi minne. Nilijitolea kuwa wakili wake katika rufaa ya Mahakama Kuu Mwanza. Kitu ambacho wengi hawakijui ni kwamba gharama zote za usafiri wa kwenda Mwanza na baadae Tarime kumtetea kwenye kesi kumi zilizobaki zilitoka kwenye mifuko binafsi ya Mwenyekiti Mbowe.
Tulishinda rufaa na kupangua kesi nyingine zote kumi katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime. Chacha hakuwahi kuchangia shilingi moja katika kesi zake zote, hata ya ubunge ya 2006.
Kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005 mimi binafsi nilifanya kampeni sana Tarime. Na baada ya kutatua tatizo la ubambikiziaji wananchi kesi za uongo, tuliwasambaratisha maCCM na Chacha alichaguliwa kwa kura nyingi kuliko mbunge mwingine yeyote wa upinzani.
Kwa hiyo Chacha Zakayo Wangwe aliingia bungeni akiwa na umaarufu mkubwa ndani na nje ya Chama. Kwangu binafsi tatizo lilianzia hapo.
Kwanza alianzisha ugomvi mkubwa ndani ya Chama wilayani Tarime. Ndani ya mwaka mmoja aligombana na viongozi karibu wote wa CHADEMA Wilaya waliomsaidia kupata ubunge.
Ndani ya mwaka huo huo, alihama jimboni na kuhamia Dar. Chacha aliyenyanyaswa sana na Wazungu wa Nyamongo akawa anaenda jimboni Tarime kwa 'lifti' ya ndege za Wazungu wa Mgodi wa Nyamongo. Mengine sitayasema hapa.
Mwaka huo huo, kufuatia kukimbia kwa Makamu Mwenyekiti Kabourou, Chacha akawa Makamu Mwenyekiti wetu.
Mwaka huo huo wa 2006, Chacha akaanza kuwaambia wananchi wa Tarime waliokuwa wanamhoji sababu za kukimbia Jimbo, kwamba sio lazima agombee ubunge mwaka 2010 kwani atakuwa ana 'majukumu makubwa ya kitaifa.'
Haukupita muda Chacha Zakayo Wangwe akatangaza kuwa anataka kugombea Uenyekiti wa Chama Taifa ili kuondoa 'Uchagga' na kugawa ruzuku hadi wilayani badala ya kuliwa na watu wa Makao Makuu.
Hapo ndipo zilipoanzia tuhuma za 'Uchagga wa CHADEMA' na 'ulaji wa ruzuku.' Wakati huo tulikuwa na wabunge watano wa kuchaguliwa na Viti Maalum sita, na ruzuku haikuwa inafika hata milioni 50
Kuhusu ruzuku. Kitu cha kwanza cha kuelewa ni kwamba ruzuku yetu haijawahi kutosheleza hata mahitaji ya kawaida ya uendeshaji chama.
Kila inapotokea kuna uchaguzi wa marudio au Uchaguzi Mkuu wowote ule, matumizi yamekuwa ni makubwa kuliko mapato yetu ya ruzuku na michango ya wabunge.
Tunapowapiga sana wabunge wetu, tuwe tunakumbuka pia kwamba nje ya ruzuku, wabunge wetu wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha mapato ya chama hasa nyakati za Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio.
Kwa sababu ya upungufu huo wa mapato, hasa kila wakati wa Uchaguzi Mkuu, tumelazimika kukopa pesa kwa ajili ya kampeni kwa mapatano kwamba madeni hayo yatarudishwa baada ya Uchaguzi Mkuu.
Sasa ni vyema tujiulize, katika hali halisi ya Tanzania hii, ni akina nani hasa ambao wako, na wamekuwa, tayari kukikopesha chama??? Ni wachache sana, kwa sababu za wazi kabisa: hofu ya kunyanyaswa na mapolisi au uhamiaji au TRA.
Nimekuwa naingia kwenye vikao vya Kamati Kuu tangu mwaka 2004, na ninaweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba hakuna kikao cha Kamati Kuu kilichokaa kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, ambacho hakikumwambia Mwenyekiti wetu atafute pesa za kampeni hata kwa kukopa, ili tuweze kununua vifaa vya kampeni au kulipia huduma zinazohitaji malipo.
Chopper, magari, pikipiki, bendera, mabango na kila aina ya vifaa vingine vya uchaguzi vinapopatikana kila Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, huwa hatuna utamaduni wa kuuliza au kujiuliza vifaa hivi vyote vitakuwa vimegharimu kiasi gani, na pesa hiyo itakuwa imetoka wapi.
Hata hivyo, kila baada ya Uchaguzi tunapoanza kulipa madeni ya waliotukopesha kwa maagizo ya Kamati Kuu ya Chama, kunakuwa na kelele kubwa kwamba ruzuku ya chama inaliwa na viongozi wakuu, hasa Mwenyekiti. Na kila anayehama chama na kukimbilia CCM anarudia rudia tuhuma hizo mpaka watu wetu wanaanza na wao kuzirudia rudia.
Na lengo kubwa la mashambulizi haya, miaka yote, ni Freeman Aikaeli Mbowe, huyo huyo ambaye kila uchaguzi ukifika tunamwomba atutafutie pesa za kampeni.
MaCCM wanajua wanachokitaka kwenye kampeni hii ya kumchafua Mwenyekiti wetu. Wapambe wao, hasa wahamaji hawa, nao wanajua. Je, sisi wanachama wa CHADEMA tunaozirudia rudia tuhuma hizi tunajua hii ngoma tunayoicheza???
Naambiwa CAG naye amehoji juu ya matumizi ya ruzuku yetu. Ni kweli. Lakini ni kweli pia kwamba CAG amezungumzia pesa za ruzuku ambazo hatujawahi kuzipata tangu tuanze kupata ruzuku.
Na kwenye suala la ruzuku, maafisa wa Ofisi ya CAG wametuhumiwa kutoa taarifa yao bila kutupa sisi fursa ya kujibu 'audit queries' zao, kama inavyotakiwa na sheria na taratibu za ukaguzi wa mahesabu.
Tunapaswa hapa kukumbuka kwamba CAG na maafisa wake ni wateule wa Jiwe na/au watumishi wa serikali ambao, kwa mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, wanashinikizwa sana kutafuta namna ya kuiumiza CHADEMA. Kwa hiyo, badala ya kumeza kila kinacholetwa kwa jina la CAG, tunahitaji angalau kujihadhari na taarifa hizo kwa kuuliza maswali muhimu juu ya usahihi wake.
Kumalizia hoja hii ya ruzuku. Tumeijibu tangu ilipoanza kuibuliwa na marehemu Chacha Wangwe mwaka 2006/07. Tumeijibu wakati tunashughulikia 'Mkakati wa Mabadiliko' wa akina Zitto na Kitilla Mkumbo. Tumejieleza na kujieleza.
Lakini maCCM na wapambe wao wana malengo yao ya kutaka tuendelee kujadili ruzuku ya CHADEMA. Inawauma kwamba tangu mwaka 2005 tulipoanza kuonyesha aina mpya ya kampeni za kisiasa.
Tangu wakati huo, mafanikio yetu yamekuwa makubwa zaidi. Kutoka chama chenye wabunge 5 mwaka 2000 hadi chama kikuu cha upinzani chenye wabunge 72 mwaka 2015 ni mafanikio makubwa.
Ruzuku yetu imeongezeka pia, hata kama bado haikidhi mahitaji yetu yote. Wakati najiunga CHADEMA mwaka 2004, ruzuku yetu ilikuwa milioni 5.6 kwa mwezi. Leo ni takriban milioni 250 kwa mwezi.
Haya ni mafanikio makubwa. MaCCM wanajua hivyo lakini hawawezi kusema hivyo hadharani. Hawafurahishwi nayo. Ukitaka kujua wanatuonaje angalia mambo yote wanayotutendea. Mauaji, vipigo, vifungo vya kusingiziwa, ukiukaji wa haki za kisiasa, propaganda chafu, n.k.
Kuhusu kifo cha marehemu Chacha Zakayo Wangwe. Hii pia ni propaganda chafu iliyoanzishwa na maCCM. Ulizeni watu wetu wa Tarime kilichotokea mara baada ya kifo cha marehemu Chacha. Ghafla msiba ule ukawa wa akina Wassira na maCCM wenzao.
Ukweli ni kwamba tuhuma hizi zilianzishwa na Wassira na genge lake wakati wa msiba huo. Vijana wa CCM walitolewa Bunda, Musoma na maeneo mengi nje ya Tarime na kuletwa kuja kumfanyia fujo Mwenyekiti wetu msibani.
Ndugu zake Chacha, wale wale waliokuwa wakimbambikizia kesi ili afungwe wakati wa uhai wake, wakawa sasa ndio wenye uchungu naye akiwa amekufa. Hata hivyo, wananchi wa Tarime walielewa kilichokuwa kinaendelea.
Ndio maana kwenye uchaguzi wa marudio baada ya kifo cha marehemu Chacha, tuliwapiga vibaya. Na ndio maana Tarime imeendelea kuwa ngome kubwa ya CHADEMA.
Inatosha tu kujiuliza kama kweli tungekuwa tumemuua Chacha, haya maCCM kwa jinsi wanavyotuchukia wangetubakiza kwa hii miaka kumi??? Tunatakiwa kujielewa, tusije tukajikuta tunacheza ngoma ya maadui zetu wakubwa.
Nizungumzie swali langu la pili. Kwa miaka zaidi ya kumi sasa, CHADEMA ndio adui nambari moja wa maCCM. Dhambi yetu kubwa ni ile ile iliyokuwa dhambi kubwa ya NCCR-Mageuzi kati ya mwaka 1995 na 2000; na CUF kati ya 2000 na 2005.

Safi. Mungu ibariki CDM
 
Hata Idd Amin hakuangushwa madarakani na wanajeshi wa Tanzania bali aliangushwa na wanajeshi wake ambao walijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

CHADEMA itaangushwa na wanachama na viongozi wake wanaokihama chama na kujiunga na vyama vingine.

Siasa za chama Kikuu cha Upinzani nchini zina muda wa uhai kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi na CUF.

Hata vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF vilipoanza kupukutika, kuna viongozi wao waliojitokeza na kupiga bla bla huku wakiukataa ukweli kama anavyofanya Tundu Lissu.

Maelezo ya Tundu Lissu yanasadifu ukweli unaosemwa kuwa CHADEMA ni chama cha Mbowe. Yaani chama kinamwagiza Mbowe akakope popote kwa mtu yeyote halafu baada ya kukopa hawaambii amekopa wapi na kiasi gani bali anachowaambia ni kiasi anachotaka walipe. Gosh!

Maisha ya CHADEMA kama chama kikuu cha Upinzani yako ukingoni.

Waingereza wana msemo usemao, ''Beware the last kicks of a dying horse''.

Swali la kujiuliza kwa sasa ni hili, Baada ya Uchaguzi Mkuu 2020, Chama gani kitakuwa ni chama kikuu cha upinzani baada ya CHADEMA?
 
Last edited:
Hata Idd Amin hakuangushwa madarakani na wanajeshi wa Tanzania bali aliangushwa na wanajeshi wake ambao walijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Siasa za chama Kikuu cha Upinzani nchini zina muda wa uhai kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi na CUF.

Maisha ya CHADEMA kama chama kikuu cha Upinzani yako ukingoni.

Swali la kujiuliza kwa sasa ni hili, Baada ya Uchaguzi Mkuu 2020, Chama gani kitakuwa ni chama kikuu cha upinzani baada ya CHADEMA?
Mtumwa wa historia!!
 
Iddi amini si mwenyekiti wa ccm na msaidizi wake maliyamungu anae amua nani aishi nani apelekewe kodi
 
Anaandika TUNDU LISSU:
Advocate Mahinyila salaam,
Nafikiri una tatizo moja kubwa: unaelekea kuamini kila tuhuma inayoelekezwa CHADEMA na wanachama wetu wa jana na juzi.
Sijakusikia ukijipa tahadhari ya kujiuliza swali moja rahisi: hivi kwa nini wahamaji wetu hawa wanagundua maovu ya ndani ya CHADEMA pale tu wanapoondoka na kuhamia CCM???
Lipo lingine ambalo nadhani pia ni swali muhimu la kujitahadharisha na maneno ya wahamaji hawa: ni kwa nini 'wimbi' hili la wahama chama lipo CHADEMA tu kwa sasa???
Nitaanza na swali la kwanza na mtaniwia nikiwarudisha nyuma kidogo katika historia ya chama chetu. Tukifahamu historia ya masuala haya hatutayumbishwa na makelele ya akina Mwita Waitara wa sasa na wajao.
Katika wahama CHADEMA wa kwanza kabisa, Dr. Amani Walid Kabourou, Katibu Mkuu na baadae Makamu Mwenyekiti wetu alikuwa ni maarufu zaidi.
Huyu alihama mwaka 2006, mara baada ya kupoteza ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005.
Dr. Kabourou alihama akiwa Makamu Mwenyekiti wetu, takriban miaka miwili baada ya timu ya Mh. Mbowe na Dr. Slaa kuchukua uongozi wa CHADEMA.
Heshima pekee ya Dr. Kabourou, kwa kuzingatia haya ya waliofuata baadae, ni kwamba yeye aliondoka bila kusema sana. Angalau mimi sikuwahi kumsikia akiyoyoma kama hawa wa baada yake.
Hizi tuhuma za ruzuku na 'Uchagga' dhidi yetu zilianza na Makamu Mwenyekiti wetu aliyerithi mikoba ya Dr. Kabourou, marehemu Chacha Zakayo Wangwe.
Chacha alikuwa rafiki yangu mimi tangu tulipokutana kwa mara ya kwanza mwaka 2003, wakati wa harakati za kudai haki za wananchi wa Nyamongo dhidi ya Mgodi wa Dhahabu wa North Mara sasa.
Nilimkuta akiwa diwani wa Kata ya Tarime Mjini kupitia NCCR-Mageuzi. Tayari alikuwa na kesi kumi na moja za kubambikiziwa na Mgodi na maswahiba wao maCCM, wakiongozwa na kaka yake mwenyewe Peter Wangwe 'Keba', wakati huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Mwaka uliofuata Chacha alifungwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi minne. Nilijitolea kuwa wakili wake katika rufaa ya Mahakama Kuu Mwanza. Kitu ambacho wengi hawakijui ni kwamba gharama zote za usafiri wa kwenda Mwanza na baadae Tarime kumtetea kwenye kesi kumi zilizobaki zilitoka kwenye mifuko binafsi ya Mwenyekiti Mbowe.
Tulishinda rufaa na kupangua kesi nyingine zote kumi katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime. Chacha hakuwahi kuchangia shilingi moja katika kesi zake zote, hata ya ubunge ya 2006.
Kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005 mimi binafsi nilifanya kampeni sana Tarime. Na baada ya kutatua tatizo la ubambikiziaji wananchi kesi za uongo, tuliwasambaratisha maCCM na Chacha alichaguliwa kwa kura nyingi kuliko mbunge mwingine yeyote wa upinzani.
Kwa hiyo Chacha Zakayo Wangwe aliingia bungeni akiwa na umaarufu mkubwa ndani na nje ya Chama. Kwangu binafsi tatizo lilianzia hapo.
Kwanza alianzisha ugomvi mkubwa ndani ya Chama wilayani Tarime. Ndani ya mwaka mmoja aligombana na viongozi karibu wote wa CHADEMA Wilaya waliomsaidia kupata ubunge.
Ndani ya mwaka huo huo, alihama jimboni na kuhamia Dar. Chacha aliyenyanyaswa sana na Wazungu wa Nyamongo akawa anaenda jimboni Tarime kwa 'lifti' ya ndege za Wazungu wa Mgodi wa Nyamongo. Mengine sitayasema hapa.
Mwaka huo huo, kufuatia kukimbia kwa Makamu Mwenyekiti Kabourou, Chacha akawa Makamu Mwenyekiti wetu.
Mwaka huo huo wa 2006, Chacha akaanza kuwaambia wananchi wa Tarime waliokuwa wanamhoji sababu za kukimbia Jimbo, kwamba sio lazima agombee ubunge mwaka 2010 kwani atakuwa ana 'majukumu makubwa ya kitaifa.'
Haukupita muda Chacha Zakayo Wangwe akatangaza kuwa anataka kugombea Uenyekiti wa Chama Taifa ili kuondoa 'Uchagga' na kugawa ruzuku hadi wilayani badala ya kuliwa na watu wa Makao Makuu.
Hapo ndipo zilipoanzia tuhuma za 'Uchagga wa CHADEMA' na 'ulaji wa ruzuku.' Wakati huo tulikuwa na wabunge watano wa kuchaguliwa na Viti Maalum sita, na ruzuku haikuwa inafika hata milioni 50
Kuhusu ruzuku. Kitu cha kwanza cha kuelewa ni kwamba ruzuku yetu haijawahi kutosheleza hata mahitaji ya kawaida ya uendeshaji chama.
Kila inapotokea kuna uchaguzi wa marudio au Uchaguzi Mkuu wowote ule, matumizi yamekuwa ni makubwa kuliko mapato yetu ya ruzuku na michango ya wabunge.
Tunapowapiga sana wabunge wetu, tuwe tunakumbuka pia kwamba nje ya ruzuku, wabunge wetu wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha mapato ya chama hasa nyakati za Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio.
Kwa sababu ya upungufu huo wa mapato, hasa kila wakati wa Uchaguzi Mkuu, tumelazimika kukopa pesa kwa ajili ya kampeni kwa mapatano kwamba madeni hayo yatarudishwa baada ya Uchaguzi Mkuu.
Sasa ni vyema tujiulize, katika hali halisi ya Tanzania hii, ni akina nani hasa ambao wako, na wamekuwa, tayari kukikopesha chama??? Ni wachache sana, kwa sababu za wazi kabisa: hofu ya kunyanyaswa na mapolisi au uhamiaji au TRA.
Nimekuwa naingia kwenye vikao vya Kamati Kuu tangu mwaka 2004, na ninaweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba hakuna kikao cha Kamati Kuu kilichokaa kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, ambacho hakikumwambia Mwenyekiti wetu atafute pesa za kampeni hata kwa kukopa, ili tuweze kununua vifaa vya kampeni au kulipia huduma zinazohitaji malipo.
Chopper, magari, pikipiki, bendera, mabango na kila aina ya vifaa vingine vya uchaguzi vinapopatikana kila Uchaguzi Mkuu au chaguzi za marudio, huwa hatuna utamaduni wa kuuliza au kujiuliza vifaa hivi vyote vitakuwa vimegharimu kiasi gani, na pesa hiyo itakuwa imetoka wapi.
Hata hivyo, kila baada ya Uchaguzi tunapoanza kulipa madeni ya waliotukopesha kwa maagizo ya Kamati Kuu ya Chama, kunakuwa na kelele kubwa kwamba ruzuku ya chama inaliwa na viongozi wakuu, hasa Mwenyekiti. Na kila anayehama chama na kukimbilia CCM anarudia rudia tuhuma hizo mpaka watu wetu wanaanza na wao kuzirudia rudia.
Na lengo kubwa la mashambulizi haya, miaka yote, ni Freeman Aikaeli Mbowe, huyo huyo ambaye kila uchaguzi ukifika tunamwomba atutafutie pesa za kampeni.
MaCCM wanajua wanachokitaka kwenye kampeni hii ya kumchafua Mwenyekiti wetu. Wapambe wao, hasa wahamaji hawa, nao wanajua. Je, sisi wanachama wa CHADEMA tunaozirudia rudia tuhuma hizi tunajua hii ngoma tunayoicheza???
Naambiwa CAG naye amehoji juu ya matumizi ya ruzuku yetu. Ni kweli. Lakini ni kweli pia kwamba CAG amezungumzia pesa za ruzuku ambazo hatujawahi kuzipata tangu tuanze kupata ruzuku.
Na kwenye suala la ruzuku, maafisa wa Ofisi ya CAG wametuhumiwa kutoa taarifa yao bila kutupa sisi fursa ya kujibu 'audit queries' zao, kama inavyotakiwa na sheria na taratibu za ukaguzi wa mahesabu.
Tunapaswa hapa kukumbuka kwamba CAG na maafisa wake ni wateule wa Jiwe na/au watumishi wa serikali ambao, kwa mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, wanashinikizwa sana kutafuta namna ya kuiumiza CHADEMA. Kwa hiyo, badala ya kumeza kila kinacholetwa kwa jina la CAG, tunahitaji angalau kujihadhari na taarifa hizo kwa kuuliza maswali muhimu juu ya usahihi wake.
Kumalizia hoja hii ya ruzuku. Tumeijibu tangu ilipoanza kuibuliwa na marehemu Chacha Wangwe mwaka 2006/07. Tumeijibu wakati tunashughulikia 'Mkakati wa Mabadiliko' wa akina Zitto na Kitilla Mkumbo. Tumejieleza na kujieleza.
Lakini maCCM na wapambe wao wana malengo yao ya kutaka tuendelee kujadili ruzuku ya CHADEMA. Inawauma kwamba tangu mwaka 2005 tulipoanza kuonyesha aina mpya ya kampeni za kisiasa.
Tangu wakati huo, mafanikio yetu yamekuwa makubwa zaidi. Kutoka chama chenye wabunge 5 mwaka 2000 hadi chama kikuu cha upinzani chenye wabunge 72 mwaka 2015 ni mafanikio makubwa.
Ruzuku yetu imeongezeka pia, hata kama bado haikidhi mahitaji yetu yote. Wakati najiunga CHADEMA mwaka 2004, ruzuku yetu ilikuwa milioni 5.6 kwa mwezi. Leo ni takriban milioni 250 kwa mwezi.
Haya ni mafanikio makubwa. MaCCM wanajua hivyo lakini hawawezi kusema hivyo hadharani. Hawafurahishwi nayo. Ukitaka kujua wanatuonaje angalia mambo yote wanayotutendea. Mauaji, vipigo, vifungo vya kusingiziwa, ukiukaji wa haki za kisiasa, propaganda chafu, n.k.
Kuhusu kifo cha marehemu Chacha Zakayo Wangwe. Hii pia ni propaganda chafu iliyoanzishwa na maCCM. Ulizeni watu wetu wa Tarime kilichotokea mara baada ya kifo cha marehemu Chacha. Ghafla msiba ule ukawa wa akina Wassira na maCCM wenzao.
Ukweli ni kwamba tuhuma hizi zilianzishwa na Wassira na genge lake wakati wa msiba huo. Vijana wa CCM walitolewa Bunda, Musoma na maeneo mengi nje ya Tarime na kuletwa kuja kumfanyia fujo Mwenyekiti wetu msibani.
Ndugu zake Chacha, wale wale waliokuwa wakimbambikizia kesi ili afungwe wakati wa uhai wake, wakawa sasa ndio wenye uchungu naye akiwa amekufa. Hata hivyo, wananchi wa Tarime walielewa kilichokuwa kinaendelea.
Ndio maana kwenye uchaguzi wa marudio baada ya kifo cha marehemu Chacha, tuliwapiga vibaya. Na ndio maana Tarime imeendelea kuwa ngome kubwa ya CHADEMA.
Inatosha tu kujiuliza kama kweli tungekuwa tumemuua Chacha, haya maCCM kwa jinsi wanavyotuchukia wangetubakiza kwa hii miaka kumi??? Tunatakiwa kujielewa, tusije tukajikuta tunacheza ngoma ya maadui zetu wakubwa.
Nizungumzie swali langu la pili. Kwa miaka zaidi ya kumi sasa, CHADEMA ndio adui nambari moja wa maCCM. Dhambi yetu kubwa ni ile ile iliyokuwa dhambi kubwa ya NCCR-Mageuzi kati ya mwaka 1995 na 2000; na CUF kati ya 2000 na 2005.
Ni dhambi ya kuwa chama kikuu cha upinzani. Ni dhambi ya kuwa na mafanikio makubwa kwenye uchaguzi. Ni dhambi ya kupendwa na kuungwa mkono na wananchi.
Kwa sababu ya dhambi hiyo, ni lazima tushambuliwe na kuchafuliwa na kufanyiwa kila aina ya fujo na hila.
Tusipolielewa hilo ni rahisi sana kukatishwa tamaa na haya ya akina Waitara wa juzi, jana na wanaokuja mbeleni.
Ili tusibabaishwe na haya ya Magufuli na watu wake na hawa maYuda Iskariote, tukumbuke tu tulikotoka.
Tulikuwa na Amani Walid Kabourou kama Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Aliondoka na kujiunga na maCCM. Tulisonga mbele.
Tulikuwa na Zitto Zuberi Kabwe, Naibu Katibu Mkuu na Naibu KUB. Tulimwondoa na tukasonga mbele.
Tulikuwa na Mzee Saidi Arfi, Makamu Mwenyekiti na mrithi wa marehemu Chacha. Alitoroka na kujiunga nao, haikuwa mwisho wetu.
Tulikuwa na Dr. Wilbrod Peter Slaa, Katibu Mkuu na mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo. Alitukimbia katikati ya vita lakini hatuku-surrender. Tulisonga mbele.
Hawa wanaomkimbilia Jiwe, huyu anayetuogopa hadi kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa, wanatubabaishaje???
Mwisho, kwa yote ambayo nimeyasema hapa, sina maana sisi ni malaika tusiokuwa na doa lolote. Tuna mapungufu mengi ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi ili kuyaondoa.

Mengine ni ya kujitakia; mengine ni ya kutakiwa na maadui zetu. Tupembue yapi ni ya kwetu wenyewe na yapi ni ya maCCM. Yote tuyatafutie dawa.
Tundu Lissu umechambua kwa ukweli mtupu kuhusu hili sakata la kumwandama Mwenyekiti Mbowe.........

Hebu tujiulize maswali yafuatayo mepesi

La kwanza, ikiwa ni kukaa muda mrefu kwenye uenyekiti, ni kwanini hawa wanaopiga hizo kelele hawawagusi akina Wenyeviti Mrema wa TLP na John Momose Cheyo wa UDP ambao ndiyo wamedumu kwa muda mrefu zaidi na wamevigeuza vyama vyao kama Mali yao binafsi??

La pili, ni kwanini wale walio mstari wa mbele wa kutaka Mbowe ang'atuke uenyekiti ni wanaccm kindakindaki na wala siyo wanaChadema??

Jibu ni jepesi tu kuwa wanaccm wanakosa usingizi kwa ufanisi wa Chadema chini ya uenyekiti wa Mbowe, kwa hiyo wanafanya kila linalowezekana kuweza kumng'oa kwenye nafasi hiyo

Lengo lao kuu wanaccm na vibaraka wao ni kutaka "kupandikza" Mwenyekiti mamluki kwenye Chama hicho kikuu cha upinzsni nchini cha Chadema
 
Last edited:
Back
Top Bottom