Majibu ya Gavana Ndulu kuhusu Noti Mpya na ubora wake

Prof Benno Ndulu
Gavana
Benki kuu ya Tanzania

3 Februari 2011

Angalau angeacha kujiita "Professor" wakati ni wazi yeye si Mwanazuoni na hafundishi chuo kikuu bali ni Administrator akiwa kama Gavana wa Benki Kuu.
 
BoT: Noti mpya zachakachuliwa
• Gavana Ndulu afundisha wananchi kuzitambua noti feki

na Ratifa Baranyikwa


amka2.gif
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imekiri kuwa noti mpya ilizozitoa kuanzia mwezi uliopita zimeanza ‘kuchakachuliwa’ na wahalifu kwa kutengeneza noti bandia.
Hayo yalisemwa jana na Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya dukuduku na maswali mbalimbali toka kwa wananchi kuhusiana na noti hizo mpya.
Akizungumzia suala la kuwapo kwa noti bandia za toleo jipya, Ndulu alisema ‘wajanja’ wameishaanza kujaribu kutengeneza noti mpya kabla ya wananchi kuzifahamu vyema.
“Mimi mwenyewe tayari nimeiona moja...wanaotengeneza noti bandia hata dola ya Marekani wanatengeneza. Wajanja lazima watajaribu tu hasa katika kipindi hiki lazima watatumia fursa hiyo kabla watu hawajazijua haraka noti za toleo jipya,” alisema.
Gavana huyo aliwaasa wananchi kuwa makini katika kuzielewa alama zilizoko kwenye noti hizo za shilingi 500, 1,000, 2,000, 5,000 na 10,000.
Akielezea jinsi ya kuzitambua noti halali, Ndulu alisema kuwa kuna mstari ambao umepita pembeni, ukiuchezesha kuna lensi inayocheza ambayo imeshonewa ndani ya karatasi.
Alisema teknolojia hiyo ya lensi hiyo kuonekana ikichezacheza haiwezi kuonekana au kuigwa na wahuni wanaotengeneza noti bandia.
Alifafanua kuwa ukiiweka kwenye mwanga utaona picha ya Mwalimu Nyerere na nyuma ya noti kuna alama ya twiga inayobadilika rangi, mambo ambayo hayawezi kufanyika katika katika noti bandia.
Alisema wao kama BoT wamejipanga kutoa elimu kwa kina zaidi na kwamba mkakati huo wataendelea nao wakati wowote ambapo elimu inahitajika.
Gavana huyo alisema hatua ya BoT kubadili fedha kila baada ya miaka mitano hadi saba ni moja ya njia ya kuweka alama bora zaidi za usalama ambazo ni ngumu kuzighushi.
Pia ubadilishwaji huo husababishwa na maendeleo ya teknolojia ya uchapaji wa noti katika kuongeza uhai wa noti katika mzunguko.
Katika hilo alisema hata Marekani au Uingereza zimekuwa zikibadili noti zake kwa sababu hizo.
Akijibu maswali na madukuduku kadhaa ambayo yamekuwa yakiulizwa tangu kutolewa kwa noti mpya, Ndulu alisema miongoni mwa maswali waliyopokea ni malalamiko kuwa noti mpya zikisuguliwa kwenye karatasi nyeupe zinaacha rangi na zikiloa hutoa rangi.
Akitolea ufafanuzi suala hilo alisema kuacha rangi noti zinaposuguliwa kwenye karatasi nyeupe ni jambo la kawaida kwani noti zote zilizochapishwa kwa teknolojia maalumu inayojulikana kwa kitaalamu kama ‘Intaglio Printing’ hufanya hivyo.
Alisema aina hiyo ya uchapishaji inazifanya noti kuwa na hali ya maparuzo zinapopapaswa.
Kwa mujibu wa maelezo yake, teknolojia hiyo imetumika ili kuimarisha kingo za noti kwa lengo la kupunguza uwezekano wa kuchanika au kuchakaa kwa haraka.
“Hata dola au euro ukizisugua kwenye karatasi zinatoa rangi na kitendo hicho kinathibitisha kuwa noti hiyo ni halali…noti ya bandia haiwezi kuacha rangi ukisugua,” alisema Ndulu.
Aliongeza, “Kuna watu wanasema ukiloweka inatoa rangi, sasa ni hivi rangi iliyotumika kutengenezea haichuji, kiwandani zinapotengenezwa zinapitia kwenye jaribio kama kuzipitisha kwenye mashine ya kufulia, kuziloweka na zikitolewa hazitoi rangi.
Pamoja na watu kudai kuwa noti mpya zinaonekana kutokuwa imara kwa sababu ya wepesi wake, gavana huyo alisisitiza kwamba noti hizo mpya ni bora zaidi kuliko zile za zamani kwa kuwa zimewekewa dawa inayojulikana kitaalamu kama ‘Anti Soiling Treatment’ inayozuia zisichafuke au kuchanika kwa haraka.
Pia alisisitiza kuwa noti za zamani bado ni halali na zitaendelea kuwa katika mzunguko pamoja na zile mpya mpaka zitakapotoweka kwenye mzunguko kwa sababu ya uchakavu wake.
Alisema huenda noti hizo za zamani zikatoweka katika mzunguko kati ya miezi 12 hadi mwaka mmoja na nusu hadi pale BoT itakapoutangazia umma.
Kuhusu upatikanaji wa noti mpya nchi nzima, Ndulu alisema kuwa ipo akiba ya kutosha ya noti hizo mpya na kwamba Benki Kuu inaendelea na mchakato wa kuziingiza kwenye mzunguko kwa kupitia benki za biashara.
Hata hivyo, alisema kutokana na mtandao wa baadhi ya matawi ya benki hizo kuwa ni mpana imechukua muda mrefu kwa baadhi ya maeneo kufikiwa na noti hizo.
Mbali na hilo Ndulu pia amewatoa hofu wale wote wanaofikiri kuwa umbile dogo la noti mpya kuwa ni upungufu wa thamani na kusisitiza kuwa zina thamani licha ya kuwa na umbile hilo.
Aidha, akijibu swali ambalo wananchi wamekuwa wakijiuliza kuwa kwa nini BoT haikutoa noti kubwa zaidi ya 10,000 ili kurahisisha malipo katika biashara, Ndulu alisema kuwa BoT hawakuona haja ya kutoa noti yenye thamani kubwa zaidi kwa sasa kwani malipo makubwa yanahimizwa kufanywa kupitia njia nyingine za kibenki.
Pia alisema uchumi wetu bado haujatuelekeza kutengeneza noti kubwa zaidi ya hapo.
Akigusia gharama iliyotumika kuchapishia toleo jipya la noti mpya, Ndulu alisema ni pungufu ya asilimia 30 ukilinganisha na ile iliyotumika kuchapishia zile za zamani.
Kuhusu tatizo la kukwama kwa pesa ama kushindwa kutoka katika baadhi ya mashine za ATM, Ndulu alisema kuwa mabenki yapo kwenye utaratibu wa kuziwezesha mashine zao ziweze kusoma noti hizo mpya.
Alisema kwa sasa wenye mabenki wanazifanyia marekebisho mashine zao za ATM kwa kuziwekea programu zitakazokuwa na uwezo wa kusoma fedha hizo mpya.
Akiichambua hali ya uchumi, gavana huyo alisema kwa sasa hali ya uchumi ni nzuri na kwamba nchi ina uwezo wa kulipa huduma kwa miezi sita bila kutegemea sehemu yoyote.
Ndulu alisema kwa fedha za kigeni tu kuna kiasi cha zaidi ya dola bilioni 3.8, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na nchi yoyote ndani ya Afrika Mashariki.
Akizungumzia grafu ya uchumi, alisema kwa mwaka 2010 katika robo ya kwanza uchumi ulikua kwa asilimia saba, wakati robo ya pili ulikuwa kwa asilimia 7.1 na robo ya tatu ulikuwa kwa asilimia 6.2.
Alisema, dhahabu pekee imeongoza kwa kuingiza bilioni 1.4 wakati sekta ya utalii ambayo ilikuwa juu ya dhahabu imeingiza kiasi cha bilioni 1.3.
Kwa upande wa mauzo ya nje ya bidhaa, alisema yameingiza milioni 900, mazao ya kilimo yaliingiza milioni 400 wakati huduma za bandari zilifanikiwa kuingiza milioni 380.
Katika hilo alisema uwezo wetu wa kuzalisha fedha za nje umekua sana ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Alipoulizwa kama tatizo la umeme limeathiri vipi uchumi katika kipindi cha robo ya mwaka huu, Ndulu alisema suala hilo litatolewa ufafanuzi na waziri husika hivyo asingependa kumuingilia.
Lakini alisisitiza, “Tutakua kiuchumi zaidi ya mwaka 2010.”
Hata hivyo, takwimu na maelezo hayo ya Gavana Ndulu yanayosifia hali nzuri ya uchumi, vinapingana na hali halisi ya kupanda kwa gharama za maisha, hususan bei za vyakula mbalimbali ambazo zimepanda kwa zaidi ya asilimia 100 na kuzua malalamiko mengi kwa wananchi.
 
BoT yatetea noti za 'batiki'


*Ni zile mpya zilizotolewa hivi karibuni
*Yadai zimetengenezwa kwa teknolojia mpya
*Yadai zikisuguliwa na kuacha rangi ndio halali


Na Rehema Mohamed

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa ufafanuzi kuhusu kuchuja rangi katika
noti mpya zilizotolewa hivi karibuni na kusema kuwa hali hiyo ni ya kawaida kwa noti zilizochapwa kwa teknolojia maaluum ijukanayo kama 'Intaglio Printing'

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema aina hiyo ya uchapishaji unafanya noti kuwa na hali ya mparuzo zinapopapaswa na imetumika ili kuimarisha kingo za noti kwa lengo la kupunguza uwezekano wa kuchanika na kuchakaa kwa haraka.

Prof. Ndulu alisema miparuzo hiyo huacha rangi noti inaposuguliwa kwa nguvu kwenye karatasi nyeupe kitendo ambacho kinathibitisha kuwa noti hiyo ni halali.

"Kutoa rangi ni moja ya alama ya usalama inayothibitisha kuwa noti siyo bandia, noti hizi hazichuji zikilowekwa kwenye maji kama inavyodaiwa kwa kuwa wino uliotumika hauyeyuki kwenye maji,"alisema Prof.Ndulu

Prof.Ndulu alisema kuwa utowaji rangi huo upo hata katika noti za nje kama dola pale zinaposuguliwa ambapo teknolojia iliyotumika kutengezewewa inalingana.

Alisema kuwa noti hizo zimetengenezwa kwa teknolojia ya kuwekewa kinga dhidi ya uchafu ili kupunguza uwezekano kunasa uchafu inapokuwa katika mzunguko.

Aliongeza kuwa noti za zamani bado ni halali na zitaendelea kutumika pamoja na zile mpya mpaka zitakapopotea katika mzunguko kwa sababu ya uchakavu wake.

Akizungumzia hoja ya kuwepo noti mmoja iliyo na thamani kubwa zaidi ya ile ya sasa ya sh.10,000/-, Prof. Ndulu alisema BoT haikuona haja ya kufanya hivyo kwakuwa malipo makubwa yanahimizwa kufanywa kupitia njia nyingine za kibenki kama njia ya mitandao.

Katika siku za karibuni wananchi mbalimbali wamekuwa wakilalamika na kuhofia teknolojia iliyotumika kutengeza noti mpya zilizotolewa hivi karibuni.

Noti hizo ambazo ni ya 10,000/-, 5,000/-, 2000/-, na 1,000/- zilipokelewa kwa shingo upande baada ya kuingizwa kwenye mzunguko na BoT huku wengine wakidai zimetengenezwa kwa teknolojia dhaifu na kulinganisha na upikaji vitenge aina ya batiki.

Hali hiyo imesababisha watu wengi kutokuwa na imani nazo huku yakiwepo matukio ya msuguano katika maeneo mbalimbali ya biashara ka baadhi ya watu kuzikataa pale wanaporudishiwa chenji hususani muda wa usiku.

Hata wale wanaozipokea saa za mchana wamekuwa na mashaka nazo na kuziangalia mara mbili mbili huku wengine wakilalamika kwamba zimetengenezwakwa teknolojia ya chini inayopunguza hadhi ya noti hizo.
 
Ni majibu mazuri Professa ila tunakuomba utuambie uchapishaji wa noti hizo umegharimu kiasi gani?

Maswali mengine bwana! Hivi toka lini gharama za printing zimewahi kuhojiwa. Unataka kujua nini? Subiri uone mahesabu ya Benki then utajua kiasi kilichotumika! Hivi ni wapi duniani watu wanatoa gharama za uchapaji wa noti zao?
 
Kuna lolote la maana hawa jamaa wamechakachua na wametudanganganya...

Unataka kuniambia marekani wa uingereza wanabadilisha hela yao kila wakati??? Huo ni uongo....

Hela yetu inatengenezwa kwa bei ya chini sana na hii ndiyo shida...

Pia ile hela iliyoibiwa yapata bilioni 20... Imepatikana....????????????
 
Unapobadilisha noti zote kwa wakati mmoja unakuwa na sababu; mimi hofu yangu ni kuwa ile stimulus na fedha za ufisadi zinazoingia au kutoka kwenye mzunguko zinasababisha matatizo kwa sababu nadhani kuna hoarding ya fedha mahali fulani. Na labda baada ya kumwaga trilioni zaidi ya moja kwenye stimulus inflation ilikuwa inanukia.
 
Wabongo bwana, sa unasugua noti kwenye karatasi ili iweje??? We tumia kufaya manunuzi hayo mengine hayasaidiii... Kuiba walishaiba ndio maana wakaona wabadili hizo noti ili waweze kutuhadaa na uchafu waliokwisha ufanya!!!!
 
Gavana Ndulu kwa uapnde alieleza kuwa noti hizo kutoa rangi wakati zimesuguliwa kwenye karatasi au kulowana ni moja ya alama zake za usalama.

Hata hivyo, wakati BoT wakitangaza katika vyombo vya habari kuhusu alama za usalama (security features) katika noti hizo, hawakuwahi kutaja hilo la kuchuja kwa rangi za noti hizo kuwa miongoni mwa vigezo vya ubora wake.

Ndulu alisema rangi hiyo inyotoka katika noti hizo, huwezi kuiona katika noti bandia na kwamba teknolojia iliyotumika inasaidia noti hizo kukaa muda mrefu bila kuchakaa.
Prof Ndulu aliwaambia waandishi wa habari kuwa hata noti za zamani za Sh 5,000 na 10,000 pia zikisuguliwa kwenye karatasi huacha rangi.
“Ukitaka kujua noti halali, kama ukiisugua kwenye karatasi, lazima iache rangi na rangi inapokuwa imekolea zaidi, inaacha zaidi,” alisema Prof Ndulu na kuongeza:
"Noti bandia haziwezi kuacha rangi kwa kuwa hazikutengenezwa kitaalamu na hiyo ni njia nzuri kwa mtumiaji kugundua noti bandia na noti halali na pia noti ikiwa na rangi nyingi inakuwa ni imara na haichakai mapema".
Kuhusu kuwepo kwa noti za zamani na za sasa katika mzunguko wa fedha alisema noti zote ni halali na zitaendelea kutumika hadi zile za zamani zitakapoisha kwenye mzunguko.

Source : Gazeti la Mwananchi
 
Sijapata kusikia "upuuzi, utumbo, kinyesi cha ng'ombe" kama kusema kuwa noti kuchuja rangi ni sehemu ya usalama wa noti zenyewe. Hata mtoto mdogo huwezi kumdanganya. Itakuwa ni mara ya kwanza duniani kutumika njia hii ya usalama. Sisi watu wa kuchunwa tu.
 
Ni aibu sana kujenga hoja ya kutetea noti kutoa rangi kana kwamba imechapwa kwa stencil
 
Yaani kwa hizi pumba wanazotoa hawa viongozi wetu kila kukicha naona kama masri ii karibu haki ya mungu.eti kutoa rangi ni ishara ya ubora?hata tahaaira ukimpa hiyo atakukatalia.
 
Kwanza noti zenyewe kuna wafanyabiashara wameshaanza kuzikataa wanataka za zamani maana photocopy zake tayari ziko mzigono na watu hawajaelimishwa tofauti yake vizuri hivyo inawacost kibiashara.
 
Sijapata kusikia wala kuona sifa na kigezo cha ubora wa noti kuchuja rangi mfukoni na ukiigandamiza kwenye karatasi nyeupe inaachia rangi kama lip stick
 
UTETEZI WA NOTI MPYA ZA 10000/=

Bank of Tanzania governor Prof Benno Ndulu (L) displays new 10,000/- banknote when elaborating to the media in Dar es Salaam yesterday on the quality of the notes. With him is BoT Director of Banking Emmanuel Boaz. (Photo: Khalfan Said)

“The colour transfer especially when the notes are rubbed on a piece of paper is normal for all banknotes which have been printed using special technology known as “Intaglio Printing” which makes the notes scrape when touched,” said Prof Ndulu.

Hii siyo kuuziwa mbuzi kwenye gunia? Yaani noti mpaka ikuchafue shati ndo ujue halali. Tena wadai ikiwa mpya ndo yapaswa kutoa rangi kama ni halali. Ina maana watengenezao feki wanahitaji tu kuzifinyanga zisionekane mpya na hivyo kutotegemewa kuchuja? Nahisi kuna kanyaboya hapa
 
Benno Ndulu kaingizwa mjini sasa anatafuta pa kutokea!Sasa hivi nimechukua dollar bill mpya na kuisugua mbona haitoi rangi kama hizi noti za Ndulu? Huyu bwana anatuzuga tu!
 
halafu hatujaambiwa kama ikichafuka inasafishika ama la? maana sio ichafue na kuchafuka halafu isbaki kwenye hali yake ya usafi! Kila kitu 30% siku hizi ukiuliza kwanini makampuni ya kuchapa noti yanabadilika kila toleo jipya? jibu tunalo na liko wazi! katika ku-solicit 30%!
 
Back
Top Bottom