Majibu ya Gavana Ndulu kuhusu Noti Mpya na ubora wake

mbarbaig

Senior Member
Feb 10, 2009
151
22
BENKI KUU YA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHUSU TOLEO LA NOTI MPYA


1. Mwezi Januari 2011 Benki Kuu ya Tanzania ilitoa toleo jipya la noti za Shilingi 500, 1000, 2000, 5,000 na 10,000. Baada ya kipindi cha takriban mwezi mmoja sasa, pamejitokeza dukuduku na maswali mbalimbali kutoka kwa wananchi. Kwa kuwa ni maswali ambayo yakijibiwa yatasaidia kuelimisha jamii katika ufahamu wa noti hizi tumeona ni vyema tukayajibu kupitia kwenu.

2. Maswali yaliyopokelewa au kuandikwa katika vyombo vya habari yameonekana kutaka kutoa uelewa zaidi katika maeneo yafuatayo:

2.1 Noti mpya zikisuguliwa kwenye karatasi nyeupe zinaacha rangi na kwamba zikilowa zinatoa rangi. Je hali hii haitokani na uduni wa noti hizi mpya?

Hali ya kuacha rangi noti zinaposuguliwa kwenye karatasi nyeupe ni ya kawaida kwa noti zote zilizochapishwa kwa teknolojia maalum inayojulikana kwa kitaalamu kama “Intaglio Printing”. Aina hii ya uchapishaji (Intaglio Printing) inazifanya noti kuwa na hali ya mparuzo zinapopapaswa. Teknolojia hiyo imetumika ili kuimarisha kingo za noti kwa lengo la kupunguza uwezekano wa kuchanika na kuchakaa haraka. Miparuzo hii huacha rangi noti inaposuguliwa kwa nguvu kwenye karatasi nyeupe kitendo ambacho kinathibitisha kuwa noti hiyo ni halali. Hali hii pia ni moja alama ya usalama (security feature) inayothibitisha kuwa noti siyo ya bandia.

Aidha, noti halali hazichuji zikilowekwa kwenye maji kama inavyodaiwa kwa kuwa wino uliotumika hauyeyuki katika maji. Vilevile noti hizi zimetengenezwa kwa teknolojia ya kuwekewa kinga dhidi ya uchafu inayojulikana kitaalamu kama “Anti Soiling Treatment” ili kupunguza uwezekano wa kunasa uchafu inapokuwa katika mzunguko.
Teknolojia hizi mbili zinalenga kuongeza uhai wa noti katika mzunguko.

2.2 Je noti za zamani bado ni halali na zinaendelea kutumika?

Noti za zamani bado ni noti halali na zitaendelea kuwa katika mzunguko pamoja na zile mpya mpaka zitakapotoweka kwenye mzunguko kwa sababu za uchakavu wake. Kwa hiyo wananchi wanashauriwa kuendelea kutumia noti za toleo la zamani bila wasiwasi wowote.

2.3 Kwa kuwa noti mpya ni ndogo kuliko za zamani kwa umbo je thamani ya noti hizo siyo pungufu kulizo zile za toleo lililotangulia?

Thamani ya noti ni ile iliyoonyeshwa kwa tarakimu zilizoandikwa kwenye noti yenyewe bila kujali ukubwa wake. Kwa hiyo thamani ya noti za zamani na za sasa haitofautiani.

2.4 Kwa kuwa kumekuwa na matatizo ya upatikanaji wa noti mpya, je Benki Kuu ina mipango gani kuhakikisha noti mpya zinapatikana nchi nzima?

Benki Kuu huingiza noti mpya katika mzunguko kwa kupitia benki za biashara. Benki Kuu inaendelea kutoa noti hizo mpya kupitia benki hizo lakini kwa kuwa mtandao wa baadhi ya matawi ya benki hizo ni mpana imechukua muda mrefu kwa baadhi ya maeneo kufikiwa na noti hizo. Hata hivyo kwa kuwa biashara nchini haina mipaka, noti hizo zitaendelea kusambaa nchini kote kupitia mzunguko wa kibiashara na kuongezeka siku baada ya siku.

2.5 Je noti halali zinatofauti gani na noti bandia?

Ili kuhakiki uhalali wa noti tunawashauri wananchi kuzichunguza kwa makini noti kwa kutumia alama za usalama kama zilivyoainishwa kwenye matangazo na vipeperushi vilivyotolewa na Benki Kuu ama kuwasiliana na ofisi zetu kwa ufafanuzi zaidi pale mtu anapokuwa na mashaka na noti hizi.

2.6 Je Benki kuu ina mikakati gani ya kuelimisha jamii na hasa vijijini kuhusu toleo jipya la noti?

Mtakumbuka baada ya uzinduzi wa noti mpya tarehe 17 Desemba 2010 nilisema noti hizi zitaanza kuingizwa katika mzunguko Mwezi Januari 2011. Hii ililenga kutoa kipindi cha kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari kuhusu toleo jipya kabla ya kuliingiza katika mzunguko. Aidha Benki Kuu ina mikakati endelevu ya kufikisha elimu ya “tambua noti zako” kwa wananchi wote kupitia matangazo, semina, ushiriki katika mikusanyiko mikubwa kama Sabasaba na nanenane na kwenye masoko pamoja na minada mikubwa ya mifugo. Tovuti ya benki kuu Bank of Tanzania (BOT): Home Page : Benki Kuu ya Tanzania vilevile imetoa maelezo mazuri kuhusu kutambua alama muhimu katika noti.

2.7 Kwa kuwa Benki Kuu inabadilibadili fedha kila baada ya miaka mitano hadi saba. Je ni kwa nini isiwe na toleo la kudumu kama ilivyo kwa fedha ya Uingereza au ya Marekani?

Kubadili noti husababishwa na maendeleo ya teknolojia ya uchapaji wa noti katika kuongeza uhai wa noti katika mzunguko na kuweka alama bora zaidi za usalama ambazo ni ngumu kuzighushi. Aidha sio kweli kwamba Uingereza na Marekani hazijabadili noti zake. Kuna mabadiliko makubwa na mengi tu yaliyopita na yanayotarajiwa kwa noti za nchi hizi.

2.8 Kwa nini Benki Kuu haikutoa noti kubwa zaidi ya 10,000 ili kurahisha malipo katika biashara?

Benki Kuu haikuona haja ya kutoa noti yenye thamani kubwa zaidi kwa sasa kwani malipo makubwa yanahimizwa kufanywa kupitia njia nyingine za kibenki. Noti ya Shilingi 10,000 bado inakidhi mahitaji ya malipo ya kawaida katika biashara kwa sasa.

Ni matumaini yetu kwamba ufafanuzi huu utaondoa wasiwasi uliokuwepo na kujenga imani kuhusu noti zetu mpya. Na Benki Kuu na matawi yake iko tayari kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu noti zetu mpya pindi unapohitajika.

Asanteni sana

Prof Benno Ndulu
Gavana
Benki kuu ya Tanzania

3 Februari 2011
 
Ni majibu mazuri Professa ila tunakuomba utuambie uchapishaji wa noti hizo umegharimu kiasi gani?
 
Ebu niende "google" kwanza halafu nitarejea!

- Intaglio Printing?
- Anti Soiling Treatment?

Obuntu
 
halafu muheshimiwa benno,
mbona umechelewa sana kuyaweka hayo maelezo kaka?
 
anavyosema haichuji ana maana gani?.....kama ukiisugua kwenye karatasi inaweka rangi nyekundu kwa nini isichuje. na je, hii inamaanisha ukiisugua kwenye karatasi nyeupe kwa muda wa kutosha si rangi itaisha au?
 
Mi nakumbuka kuna mdau mmoja aliniambia hii habari ya kubadilisha hela in December 2008.

He was very specific kwamba zitabadilishwa after uchaguzi wa October 2010.

Alinipa reason moja:

There is so much money in the circulation and the central bank does not even know how much money is in the circulation.
I remember alinipa mfano wa hela za EPA zilizopo kwenye mzunguko na BOT haijui ni kiasi gani.

Then akasema kwa kuwa BOT haijui idadi ya fedha zilizopo kwenye mzunguko it becomes very hard kufanya implementation ya monetary policy and so does the Treasury to implement Fiscal Policy.

Alisema when the gvt ikitoa hela kwenye mzunguko haioni zile impacts walizokua wanazitegemea the same happens when they inject money in the economy.

I think hii ni kwa sababu hela nyingi kwenye mzunguko ni HARAMU.

Sasa hivi watu wenye billions of money watashindwa kwenda kuzibadilisha, and TRUST me there are people with billions at their homes for example Asians wengi wana tabia ya kuhoard money.

Sasa hivi wakienda nazo kwenye any bank, wanashtukiwa.

The best thing they can do ni kununua foreign currency before the deadline.

So you should expect a drop in the TZ shilling when the deadline approaches bcz demand ya foreign currency itakua kubwa and therefore its value in Tsh. itapanda juu.

NAWASILISHA
 
benno, hebu tuwekee hapa hizo alama za usalama puliizi kwa sababu nasikia noti mpya bandia ziko frontline kwenye mzunguko wa noti mpya halali
 
Ata ningekuwa mimi ningejitetea mpaka povu zitoke mdomoni.
Sababu ya kubadili izo noti mara baada ya uchaguzi wanaijua
Ikishindikana ya dowans itaundwa miradi mingi kufidia mambo ya uchaguzi na gharama zake
 
uwongo huo benno sikubaliani na wewe. sijawahi shika noti ya nchi nchi yeyote ile yenye kupukutika rangi km huu uozo wetu, eti anti soiling imekuwa bustani hii bennoooooooooooooo acha wizi mchana kweupee
 
Sio kweli kuwa lazima uzisugue ndio zitoe rangi; ukivaa shati nyeupe na ukaweka noti mpya ya shilingi elfu kumi kwenye mfuko wa shati halafu ukanyeshewa na mvua, ujue shati yako itabaki na rangi ya noti hiyo!! Hizi noti mpya hazina ubora wa kudumu muda mrefu kuliko hizo walizozibadili na hii unaweza kuhakikisha kwa kuzikamata kamata mkononi!!
 
anavyosema haichuji ana maana gani?.....kama ukiisugua kwenye karatasi inaweka rangi nyekundu kwa nini isichuje. na je, hii inamaanisha ukiisugua kwenye karatasi nyeupe kwa muda wa kutosha si rangi itaisha au?

jaribu kuweka kwenye maji utapata jibu????????????
 
jamani tayari watu wameshalizwa na feki na sielewi inakuwaje juu ya uthibiti wa hili,ok ni ngumu kudhibiti ila si lazima tuwe na noti ya sh 10000 kwani marekani na hata china bado pesa ya mwisho ni sh 100,so sioni umuhimu wa kuwa na 10000 kama pesa ya mwisho kwetu wakati kuna mataifa wanatumia 100 kama pesa yao ya mwisho na uchumi ni strong
kuhusu gharama nadhani wangeweza wazi pia tuelewe na tujiridhishe kweli kwani wabongo bwana hawachelewi kuweka 10% zao hapo

mapinduziiii daimaaaaaa:twitch:
 
Kutoa rangi zinatoa hata ukiweka katika mfuko wa shati ukipata manyunyu ya mvua kidogo inatoa rangi,hili limenitokea katika noti ya 10000.
 
Hahahaaaaa teknologia maalum ya intaglio printing ndio inafanya zitoe rangi na ni hali ya kawaida! Hahaaa! Hili jamaa cjui linatuona mafala sisi!? Ah nchi yangu. Hawa watu tuwarecord jamani itakuja siku tutawawajibisha tu,kama sio wao basi vizazi vyao.
 
Huyu Beno ni mtu wapi?? au ni babake yule wa UVCCM au?? maana alipoingia pale nikadhani kaja mtu kumbe ukishaingia hapo lazima uwe mwizi na muongo!!
 
Back
Top Bottom