Majibu ya Dr. Masau wa THI kwa maswali mbalimbali

kwi kwi kwi...

Kuna siku nilishiriki kumpleka ndugu yangu aliyepata ajali MOI... well na mimi nimeshiriki kumtibu... please regconise me... Field Marshall ES... nasisi tuunde MOI hospital yetu...
 
Nimesoma hii thread na nimegundua kuwa wengi wa wachangiaji hawataki kujituma hata kutafakari yale mawazo tofauti na ya kwao. Kuhani, Maumau na Sober wamefanya kazi nzuri ya kuelekeza huu mjadala katika upande sahihi na wala sio ushabiki. Tunapozungumzia tiba, hapa hakuna siasa, hakuna CCM wala CHADEMA, kama ni spade itaitwa spade na wala si vinginevyo.

Mimi sina wasiwasi na usomi wa Daktari Masau pale Muhimbili na huku Uchina, Japokuwa facts zinasema amewahi kuishi Texas lakini hajawahi kuwa Daktari aliyekuwa na mamlaka ya kufanya shughuli za kidaktari kwa mujibu wa sheria za Texas. Endapo, by implication alijionesha kuwa ni Daktari aliyekuwa anapractise huko Texas basi alikuwa anadanganya, kwa hiyo ni kinyume na miiko ya kazi yake.

Pili, Masau kama daktari alipaswa kuonesha kiwango cha juu cha tabia njema na uaminifu. Endapo kama aliingia mkataba halali na NSSF kwa ajili ya pango (rent) alitakiwa alipe kwa wakati bila kulimbikiza. Aidha, ni vema Daktari Masau aoneshe mahesabu yake ya kila mwaka kama alikuwa anawithhold fungu la rent ambayo iko kwenye dispute. Ili kuthibitisha kuwa yeye ni mtu wa tabia njema basi ni vema wakati kesi yake ipo mahakama angeli-deposit hicho kiasi cha pesa anazodaiwa katika akaunti ya mahakama kuonesha kuwa nia yake ni njema na pesa zipo. Kinyume cha hapo kama hizo pesa hazipo basi suala la uaminifu limemtupa mkono na anafungua milango ya watu kutaka kujua na mengine zaidi.

Mwisho, ninatoa wito kwa wataalam wetu wazidi kujitokeza kwa wingi kuanzisha asasi zao binafsi lakini kwa kuwa na mipango itakayokuwa endelevu na itakayozingatia pamoja na mambo mengine taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuangalia basic business ethics na kufanya risk analysis. Tusijibweteke kwa kufanya mambo kiholela na yanapokwenda kombo tunaanza kutaka huruma, ulimwengu huo ulikwishapita.
 
Watanzania ninaowajua mimi ndio za kwao kusagia wenzao. Nyie mmefanya nini mpaka mumwone daktari wetu mbabaishaji?

Tatizo la Watanzania wengi ni wivu na choyo mbaya. Watanzania walio wengi wangelitaka wao ndio wawe juu ya kila kitu. Nyumbani kuna watu wanasema raha ya utajiri ni kuzungukwa na maskini, ni ujinga uliozidi kiasi. Bora kuwa maskini miongoni mwa matajiri kulikuwa kuwa tajiri kwenye mazingira ya TZ.

Huyu Dr. anatakiwa kusaidiwa na wala sio kukashifiwa kama wanavyofanya wengine hapa.

Tusitegemee maendeleo mpaka pale tutakapoanza kuheshimu vilivyo vyetu. Lazima tufanye juhudi ku promote vijana wetu. Tuache kutukana wasomi wetu hata pale ambapo hawajafanya jambo lolote baya.

Kikubwa tuachane na wivu na uchoyo uliozidi kiasi. Mimi nawajua watu ambao wanashindwa hata kuwasaidia ndugu zao kwa kuogopa eti watawazidi. Ni ujinga ujinga na ujinga ambao mpaka unaathiri hata maendeleo ya nchi.

Watu kama Dr. Masua ni watu wa kusaidiwa ili wafikie malengo yao.
 
Mtanzania,

Mimi nakwambia wivu umetujaa vibaya sana hasa watu waliopo serikali hata sijui walilishwa nini!

Angekuwa mzungu au hata angekuwa ametoka Kenya au Uganda, huyu bwana asingepata vikwazo vyovyote. Sisi tunaofanya utafiti tunajua sana haya mambo. Unaomba kibali cha kufanya utafiti sehemu fulani, utazungushwa mpaka mvi zikutoke. Lakini hebu shirikiana na mzungu hapo, tena jina lake tu liwepo katika utafiti huohuo, utakuta mkuu wa kitengo anakusaidia kufukuzia hiyo permit yako mpaka unashangaa.

Sasa huyu mtu kasoma udaktari wake Muhimbili, huko huko wanakujifanya wanajua kuliko dunia nzima, kasoma China, kapata fellowship ya hiyo taasisi ya Texas, lakini kuna watu wanamuona maimuna, hamnazo, ila wao ndio wanajua!! Makubwa, na sijui bwana haya mambo tutayatatuaje. Tatizo la roho mbaya na wivu hauna tiba, dawa yake ni kuchapa kazi tu, acha hao wenye roho za sebuleni waendelee kukuzodoa, shauri zao!
 
Matatizo ni wapambe! Huyu mheshimiwa ameeleza kuwa alisajiliwa Tanzania kama surgeon. Kwa vile wakati huo hapakuwa na zana za kufanyia upasuaji mioyo, sidhani kama aliweza kufanya huo upasuaji hadi alipokwenda Texas. Huko nako alishiriki na wala hakuongoza upasuaji kwa hiyo hakuwa na haja ya kutafuta usajili. Aliporudi, alianzisha hiyo institute kwa kutumia usajili wake wa hapa Tanzania na si kwingenepo. Kwa vile watanzania tunapenda kuwamwagia watu misifa ( kila mtu kigogo, askofu, bingwa aliye bobea n.k.) bila sababu ndiyo yote hayo yanayopingwa na wakina Kuhani yakaanza kujitokeza (Kuwa alikuwa daktari bingwa Marekani wakati si kweli). Palikuwa hakuna haja ya kurembesha wakati qualification muhimu alikuwa nayo, nayo ni kusajiliwa Tanzania. Hayo mengine ni hyperbole na ndiyo maana hayakukaa vizuri.

Shutuma ninayoiona nzito ni hiyo ya kudai watu wengi wamekufa katika institute yake. Hii bila kujali amesajiliwa wapi ndiyo kwa mtazamo wangu linastahili kufanyiwa kazi. Na kama ni uongo, basi Kuhani anastahili kuomba msamaha kwa herufi kubwa.

Amandla!
 
mtanzania,

Mimi Nakwambia Wivu Umetujaa Vibaya Sana Hasa Watu Waliopo Serikali Hata Sijui Walilishwa Nini!

Angekuwa Mzungu Au Hata Angekuwa Ametoka Kenya Au Uganda, Huyu Bwana Asingepata Vikwazo Vyovyote. Sisi Tunaofanya Utafiti Tunajua Sana Haya Mambo. Unaomba Kibali Cha Kufanya Utafiti Sehemu Fulani, Utazungushwa Mpaka Mvi Zikutoke. Lakini Hebu Shirikiana Na Mzungu Hapo, Tena Jina Lake Tu Liwepo Katika Utafiti Huohuo, Utakuta Mkuu Wa Kitengo Anakusaidia Kufukuzia Hiyo Permit Yako Mpaka Unashangaa.

Sasa Huyu Mtu Kasoma Udaktari Wake Muhimbili, Huko Huko Wanakujifanya Wanajua Kuliko Dunia Nzima, Kasoma China, Kapata Fellowship Ya Hiyo Taasisi Ya Texas, Lakini Kuna Watu Wanamuona Maimuna, Hamnazo, Ila Wao Ndio Wanajua!! Makubwa, Na Sijui Bwana Haya Mambo Tutayatatuaje. Tatizo La Roho Mbaya Na Wivu Hauna Tiba, Dawa Yake Ni Kuchapa Kazi Tu, Acha Hao Wenye Roho Za Sebuleni Waendelee Kukuzodoa, Shauri Zao!

Shocking!!!!!!!!!!!
 
Kama kuna mtu anayemuona huyu Dr. maimuna, basi amekosea. Ukweli ni kwamba wengi wa wasomi wetu hawaridhiki na usomi wao. Huyu Daktari qualifications zake za Muhimbili na China zinatosha lakini wapambe wakazidharau na kung'ang'ania za Marekani ambazo hanazo. Hao wenye Ph.D fake ni wasomi tosha maana wana masters lakini hawaridhiki hadi kujivika udaktari. Hao viongozi wetu wa dini hawaridhiki hadi wanapojitwisha uaskofu! Hao matajiri wetu hawaridhiki hadi wanapotuadaa kuwa benzi lake ni special order kutoka kiwandani. Kuna haja ya kuwa modest, na pale wapambe wanapokumwagia masifa yasio yako kuwaambia thanks but no thanks!
 
Mtanzania,

Mimi nakwambia wivu umetujaa vibaya sana hasa watu waliopo serikali hata sijui walilishwa nini!

Angekuwa mzungu au hata angekuwa ametoka Kenya au Uganda, huyu bwana asingepata vikwazo vyovyote. Sisi tunaofanya utafiti tunajua sana haya mambo. Unaomba kibali cha kufanya utafiti sehemu fulani, utazungushwa mpaka mvi zikutoke. Lakini hebu shirikiana na mzungu hapo, tena jina lake tu liwepo katika utafiti huohuo, utakuta mkuu wa kitengo anakusaidia kufukuzia hiyo permit yako mpaka unashangaa.

Sasa huyu mtu kasoma udaktari wake Muhimbili, huko huko wanakujifanya wanajua kuliko dunia nzima, kasoma China, kapata fellowship ya hiyo taasisi ya Texas, lakini kuna watu wanamuona maimuna, hamnazo, ila wao ndio wanajua!! Makubwa, na sijui bwana haya mambo tutayatatuaje. Tatizo la roho mbaya na wivu hauna tiba, dawa yake ni kuchapa kazi tu, acha hao wenye roho za sebuleni waendelee kukuzodoa, shauri zao!

Kitila,

Competence pia zinachangia! Sijafanya research lakini mimi nafahamu vipanga wengi hawakwenda Seriakalini... serikalini wameenda watu wengi wa Makarai (C) evarage people... ingawa wapo wachache wazuri.
 
Wakuu,

Imebidi nisome thread yote ndo niingie.

Sijaona kwanini tunalumbana. Nilivyoelewa Dar Masau alikuwa QUALIFIED hapa nchini hata kabla ya kwenda Marekani. Huko inaelekea alienda kuongeza ujuzi na AKASHIRIKI (unaweza kuitafsiri utakavyo) ambayo naamini haikuhitaji leseni kwa kuwa alikuwa kwenye PROGRAMME maalum ambayo inatambulika kisheria.

Ninaamini kushiriki tu hata kama ni kwa kuangalia au kutumwa (dhihaka yenu) mkasi kwa wagonjwa 1800 (evidence zipo) sio JOKE!!!. Hiyo yenyewe ni qualification wandugu, ni kama post qualification baada ya kuhitimu TZ.

Vitu vingine mnavyovishikilia na kuvisimamia HA VI HOLD WATER. Tuwe objective jamani.

Swali lilikuwa na Nyani Ngabu amesisitiza kuwa tunakubali amesomea na ni mtaalamu wa upasuaji mioyo?. Wote mmekubali. Sasa tatizo lipo wapi?

Maumau, Sober na Kuhani, sioni hoja kubwa humu, jamaa ni qualified period!

Wenu

Fairplayer
 
Mtanzania,

Kuliko kubabaisha vyema kutofanya lolote!

Mkuu Kasheshe,

Lugha kama uliyoandika hapo juu mimi nimeisikia sana Tanzania, tena mara nyingi ikielekezwa kwangu. Bahati nzuri wengine hatukati tamaa, watu hao hao waliokuwa wanatuita wababaishaji leo wanaanza kujigonga gonga.

Iweje miradi yote ya Waswahili wenzetu iwe ya ubabaishaji wakati Wazungu wakija wanapapalikiwa hata kama hawana utaalamu wa kutosha?

Tatizo la TZ ni sisi wenyewe, tunashindwa kukaa na hao tunaowaita wababaishaji na kutafuta njia za kuwasaidia ili wasiwe wababaishaji.

Angalia effort ambayo Dr. Masua kaweka kwenye hiyo project yake lakini watu wanamwona mbabaishaji tu.

Nakubaliana na Kitila na naona kachomelea hasa misumari ya ukweli kwenye hoja yake. Hatuthamini vilivyo vyetu.
 
Kitila Mkumbo,Mwanakijiji,GT,Kuhani,Maumau,.....

..of course ingekuwa vizuri sana kama Dr.Masau angerudi na licence ya ku-practice USA.

..pia naona hakuna anayeulizia kama alipata licence ya ku-practice China. hapa utajua kuna watu wana malengo yao zaidi ya uwezo na usomi wa Dr.Masau.

..pia kuna anayefahamu Madaktari wasiokuwa na leseni, au Madaktari wanafunzi, kama alivyokuwa Dr.Masau USA, wanapata mafunzo ya namna gani ktk hiyo Program aliyokuwa enrolled.

..ninavyoelewa mimi Madaktari waliohitimu nje ya nchi wanaporudi nyumbani hulazimika kuonyesha VYETI vya kuhitimu, siyo LESENI za kufanya kazi huko walikosomea.

..nashauri tujielekeze ktk kutafuta njia ya kutumia ujuzi aliokuwa nao Dr.Masau. kuna mabingwa wengi tu pale Muhimbili ambao wamehitimu ngambo lakini hawana leseni za ku-practice huko walikohitimu.
 
Kuhoji credentials ni muhimu maana ni maisha ya watu yanayozungumziwa. Kutokana na hao wakina Tomasi ndiyo ukweli unapowekwa wazi. Isiwe ili mradi mtu ametoka majuu basi akubaliwe tu kwa kuhofia kuwa tukimuudhi atarudi alikotoka. Ni lazima tuanze kuthamini maisha na resources za watanzania wenzetu kwa kuhakikisha anayepewa majukumu kweli anastahili! Si wivu wala uchoyo. Ni wajib.
 
Nashukuru kwa MKJJ kuanzshisha hii thread kama kutupa attention inayohitajika, na tayari 24 karubu zinakamalika na tushaipa umuhimu wake, naomba Mods muuinganishe na ile ya THI ili tupate mtiririko wa mjadala vizuri
 
mioyo 1800 tangu 1997 - 2000; very possible; I attended several heart attack victims (myself as a patient); real in a day that group of Doctors used to attend (Surgery) about 20 more patients; but such operation differ, either bypass, adding a pace maker etc etc!

Kwa suala la Dr. Masau, such a shining examples of motivated doctors; if i was a Government official responsible for this issue, i cud have taken a fair solution discussing issues to solve differences and make something constructive come out!

Sijui kwenye serikali hawa watu wame-discuss vipi na Dr Msau, lakini mie naona issue hii siyo problem ni license; the guy is a real professional who can be utilized!!

Mimi nipo hapa Texas kwa miaka 11. Watanzania wenzangu ukweli ni kwamba Dr. Massau anasema ukweli na malumbano ya utalaamu wake hayana msingi. Kama mnataka kuzungumzia mambo mengine sawa lakini ukweli ni kwamba huyu jamaa kabobea na mimi namfahamu kwa miaka yote hapa Texas na familia yake.

Tatizo dogo alilonalo ni la kitabia, ni mbinafsi kidogo na kitu hicho ndicho kibaya tu ambacho nimekiona. Siyo mfisadi na hapendi makuu kwenye maisha na si mtu wa kujilimbikizia pesa lakini ni mbinafsi na hilo si siri. Iliuweze kufanya udoctor binafsi unahitaji kufanya mitihani na kufanya hospitali ili upate Residency lakini kama hutafanya kazi marekani haina maana kwani kila nchi inasheria tofauti. Kwa ufupi watu wanaojaribu kusema Dr Massau hajasoma au si muhitimu ni kichekesho kwani ukienda Texas Medical Cnt ambayo ni kubwa kuliko zote duniani na kuuliza Dr Massau kwa madaktari wengine wanamjua na ukifanya kazi hapo na ni Mtanzania wanakuuliza kama unamjua Masau. Msemeni kwa mangine lakini education na qualification mtachemsha na kuonekana wajinga na washabiki.

Kuna member hapa kazi yao ni kutafuta ujiko kwa udi na uvumba. Kama wewe hukusomea hiyo taaluma utajuaje kwamba moja ya kigezo cha kutambulika ni kupasua mioyo ya watu au kuzalisha akina mama wajawazito kwa wale waliosomea midwifery. Lazima u-prove kwamba umetekeleza hayo ili upewe shahada tatizo ni kujifanya unafahamu kila nyanja. Usomi wa Madaktari au Midwifery ni tofauti na Engineering au Lawyers, sasa kama waliofanya kazi na Masau wanakiri amebobea kwa nini kuna watu bado hawaamini? - Wivu wa kipumbavu kwani wao hawawezi kufanya ambayo Masau amefikia kinachowasukuma kama alivyosema Kitila Mkumbo hapo juu.

Kuonyesha yeye hababaiki amekata rufaa kuona kwamba sheria inatendeka, serikali yetu imeshindwa kupata kodi kwa wezi kutoka nje na kuwapa holiday tax kama vile wao ni miumgu watu. Natumaini waliangalia jana sherehe za Olympics jinsi wenzetu wa China walivyokuwa wanajivunia kule walikotoka na kule wanakoelekea wakati sisi tunajidharau na kuwaponda wazawa wetu na kuwakumbatia MAFISADI kina Sinclair bin Mwizi. Ni sawa na Charles Njonjo mwingine lakini hivi sasa yuko Magogoni.
 
Kitila Mkumbo,Mwanakijiji,GT,Kuhani,Maumau,.....

..of course ingekuwa vizuri sana kama Dr.Masau angerudi na licence ya ku-practice USA.

..pia naona hakuna anayeulizia kama alipata licence ya ku-practice China. hapa utajua kuna watu wana malengo yao zaidi ya uwezo na usomi wa Dr.Masau.

..pia kuna anayefahamu Madaktari wasiokuwa na leseni, au Madaktari wanafunzi, kama alivyokuwa Dr.Masau USA, wanapata mafunzo ya namna gani ktk hiyo Program aliyokuwa enrolled.

..ninavyoelewa mimi Madaktari waliohitimu nje ya nchi wanaporudi nyumbani hulazimika kuonyesha VYETI vya kuhitimu, siyo LESENI za kufanya kazi huko walikosomea.

..nashauri tujielekeze ktk kutafuta njia ya kutumia ujuzi aliokuwa nao Dr.Masau. kuna mabingwa wengi tu pale Muhimbili ambao wamehitimu ngambo lakini hawana leseni za ku-practice huko walikohitimu.

Unfortunately kutokuulizia leseni yake ya uchina ni dalili ya ulimbukeni wetu! Leseni ya Tanzania na shahada za Muhimbili na uchina zilionekana hazitoshi bali huko kukaa kwake Marekani!
 
GT,

..hii iachwe hapa hapa kwasababu ime-base solely ktk kuangalia vyeti na uzoefu wa kitaalamu wa Dr.Masau.

..hii thread inatokana na majibu "rasmi" ya Dr.Masau kuhusu qualifications zake.

..ile thread nyingine ni msitu mkubwa wa malumbano yasiyokuwa na msingi.
 
Kitila Mkumbo,Mwanakijiji,GT,Kuhani,Maumau,.....

..of course ingekuwa vizuri sana kama Dr.Masau angerudi na licence ya ku-practice USA.


..ninavyoelewa mimi Madaktari waliohitimu nje ya nchi wanaporudi nyumbani hulazimika kuonyesha VYETI vya kuhitimu, siyo LESENI za kufanya kazi huko walikosomea.

.

Mzee unauliza kisha unajijibu au ndo una resolve issues kwa contradictions. Amesema wazi kuwa hakuhitaji ku practice Marekani ndo maana hakuomba leseni.

Mi naona hii mada inajifia na hakuna jipya....repetitions tu na maswali ambayo majibu yake yametolewa. Mods merge, naona watu wana concentrate kwenye non issues wakati kuna issues za akina Dr wa zamani wa BOT na Radar haipewi uzito wa kutosha.

Maoni tu.

Fairplayer
 
GT,

..hii iachwe hapa hapa kwasababu ime-base solely ktk kuangalia vyeti na uzoefu wa kitaalamu wa Dr.Masau.

..hii thread inatokana na majibu "rasmi" ya Dr.Masau kuhusu qualifications zake.

..ile thread nyingine ni msitu mkubwa wa malumbano yasiyokuwa na msingi.


Unaamana ile ya kuonyesha kuwa Dr Masau ni mwongo na si mlipa rent ni msitu usiokuwa na msingi? zile 2.3 billion anazodaiwa na NSSF hazina maana?

anyway hakuna tabu mkuu mindhali kama hii ipo kuquestion credentals za Masau then poa tuu sasa itabidi wengine tuingie tena machimboni ili tujue whats what
 
Fundi Mchundo,

..kuna mambo mengi sana yamejificha ndani ya huu mjadala mzima.

..nina wasiwasi kama Wapasuaji wote walioko pale Muhimbili wana licence kutoka nchi walizosomea.

..pia si walidai wale wagonjwa watapelekwa Muhimbili. je huko Muhimbili wamehakikisha kuna Madaktari wenye licence za USA ambayo Dr.Masau hana?


FairPlayer,

..nadhani tuko upande mmoja wa hoja, labda nimeshindwa kujieleza tu.
 
Back
Top Bottom