Kuendeleza swali la FieldMashall, " Ni kipengele Gani Cha Sheria kilikuruhusu Kupata Information za Dr Masau?"
Because Data Protection Act forbid for third part person kupata Information za Mtu Mwingine without His Consent '
Hakuna Data protection bila kuwa na haki za Mgonjwa au Mteja, ukienda kwa Mwanasheria akasema amesajiriwa na anaweza kukutetea ukiwasiliana na Tanganyika Law Society watakwambia kama kweli huyo mtu kapita na ni wakili anayetambulika, hakuna siri kwenye haki za mgonjwa au Mteja wanatoa habari za madaktari au wanasheria wao.
Mfano ukiuliza wakili Nimrod Mkono kwenye bodi yenye dhamana ya kusajili wanasheria ambayo ni Tanganyika Law Society watakwambia kuwa Mkono alisajiliwa 31-08-1977 na namba yake ya usajili ni 71.
ukiuliza wakili yeyote mfano Murtaza Ahmed Lakha alisajiliwa 24.06.1968 na nambari yake ni 32, aliyeanza ni PIROJSHAW 20.4.1931 hakuna siri wala data Protection.
tizama Tanganyika Law Society.
http://www.tanganyikalawsociety.or.tz/members.htm
Dua.
Kuna uongo unarudiwa rudiwa kuwa Masau alikuwa akitibu Marekani na ana kitengo chake ST LUKES hospital kama kuna PARTNERSHIP between THI na ST.LUKES hospital ,hilo nitabisha hadi kiama.
Umesema kuwa kuna watu wanafanya masters UK na kufanya mafunzo ya utabibu hao hawaja qualify kuwa madaktari wako kwenye mazoezi hata CV zao hawawezi kusema kuwa walikuwa wakitibu ST.THOMAS HOSPITAL watasema tulifanya mazoezi ya vitendo kwenye hospital fulani.
Kama ukifanya MBA cranfield au Manchester University na ukaenda kufanya Field Loyyds Bank au Barclays au ukaandikia Dissertation juu ya London Stocks Exchange huwezi kuandika kwenye CV yako kuwa ulikuwa mfanyakazi wa Barclays UK au London Stock exchange, unaweza kusema kuwa nilifanya Field sehemu fulani lakini sio kusema kuwa wewe ulikuwa UK kama mfanyakazi wa Barclays uk na hata familia yako iko UK.
VISA za hao wanaofanya masters zitasema wazi kuwa ni Student VISA, lakini akiwa anafanya kazi kama Daktari atakuwa na visa ya WORK PERMIT au wanaweza kuwa na kitu kinaitwa HSMP.
DR.Masau hakuna anayesema hajasoma Uchina na Muhimbili watu tunabisha kuwa hajatibu Marekani na hawezi kutibu bila idhini ya TEXAS MEDICAL BOARD na hao hawana rekodi zake kama alikuwa daktari wao. aliyekwenda kwenye source ni KUHANI kwani amekwenda kwenye bodi husika,Mwanakijiji kuendelea kumuhoji Mtuhumiwa ukitarajia kupata ukweli juu ya tuhuma zake si kutafuta suluhu na ukweli, zaidi ni kuendelea kumlinda Masau, tafuta INDEPENDENT BODY ifanye kazi hiyo.
Field Marshal.
Kuna watu wanaishi Marekani bila vibali kama watu wa South American kwa mamilioni lakini huo sio utaratibu wa sheria za uhamiaji wa Wamarekani,Tunazungumzia Taratibu za kutibu Marekani, hatusemi kuwa unaweza kuishi kwa njia za panya au kutibu bila leseni, Kuhani anatuonyesha Formality za kuweza kutibu mjadala huu utamsaidia kijana aliye Muhimibili na ana DREAM ya kwenda kutibu Marekani kama Professsional sio njia za panya, ukisema kuwa unaruhusiwa unaweza kuwadanganya vijana wengi kwa kauli yako, labda mganga wa kienyeji anaweza kufanya shughuli zake bila Kibali MAREKANI lakini si medical Doctor.
Sikubaliani na kauli ya DR.Masau kuwa kawafanyia oparesheni wagonjwa 1800 wastani wa wagonjwa mia sita kwa mwaka,sikubali kuwa aliwahi kuishi MAREKANI kama Daktari aliishi akiwa na status ya uanafunzi,hakuwa akilipwa kama ni mtalaam wa tiba aliishi kwa allowance za kiuanafunzi na kama alipata wasaa alibeba box.
Kutokana na kuwa hakuwa professional medical Doctor ndio maana anafanya mambo yake kiholela holela na kiubabaishaji sana.