Majibu ya Dr. Masau wa THI kwa maswali mbalimbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya Dr. Masau wa THI kwa maswali mbalimbali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Langfordltd, Jul 14, 2008.

 1. L

  Langfordltd New Member

  #1
  Jul 14, 2008
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Original story posted by Mzee Mwanakijiji


  Mwanakijiji,
  Asante kwa message yako.
  Nilikuwa sijui mtandao wenu hadi majuzi nilipoongea na Mr. Mstsimbe na kuniambia kuhusu suala hilo. Baada ya hapo nilifanikiwa kuingia kwenye mtandao wenu na kukuta mambo mengi sana.

  Kifupi ni kuwa nisingependa kujiingiza kwenye malumbano au majadiliano yenu na wala sipingi nyie kuendelea na mijadala yenu na hasa kwa vile wote siwajui na mnatumia majina ya kuficha. Lakini kwa ufupi ni kuwa:

  1. Nimekwenda Texas Heart Institute wakati huo nimeshakuwa Registered na Medical Council of Tanganyika in 1995 as a Thoracic and Cardiovascular Surgeon baada ya kuwa nimesomea Shahada ya Udhamili katika Upasuaji wa Kifua, Moyo na Mishipa ya Damu (Masters of Medicine in Thoracic and Cardiovascular Surgery) na kufanya kazi Muhimbili katika fani hiyo hadi nilipokwenda Texas mwishoni mwa mwaka 1996.

  2. Nilikuwa sponsored na University of Texas Health Science Center-Houston kwenda Texas Heart Institute kwenye Cardiovascular Surgery Fellowship Program. Nilikuwa Texas Heart Institute kwenye hiyo program kuanzia January 1997 hadi June 2000 na katika kipindi hicho nilishiriki katika kufanya operation za upasuaji wa moyo zaidi ya 1800 (vielelezo vyote vipo).

  Wakati nikiwa Texas Heart Institute sikuwa chini ya Texas Medical Board na hivyo sikuhitaji kuwa na Licence kutoka Texas Medical Board na wala sijawahi kuwasiliana nayo kwani ingekuwa na maana tu kwangu iwapo ningetaka kubaki na kufanyia kazi huko Texas. Mimi lengo langu lilikuwa ni mafunzo na kurudi nyumbani.

  Lakini ingawa niko nyumbani bado na-maintain ushirikiano mzuri na Texas Heart Institute na Texas Children's Hospital kiasi kwamba mara nyingi nakuja (pamoja na kwamba familia yangu ipo Texas) na naendelea kushiriki katika kufanya operation pale ninapoomba au kuhitaji. Na taasisi hizi mbili ni moja wa supporters wakubwa wa Tanzania Heart Institute.

  3. Mimi ni mwanachama wa Society of Thoracic Surgeons na mmoja wa wajumbe katika Kamati maalumu ya Chama hicho -Workforce of International Relationship of the Society of Thoracic Surgeons kutoka mwaka 2002 -2008

  4. Mimi ni Mwanachama mwanzilishi wa program maalum ya upasuaji wa moyo duniani- Founding Member of the International Cardiac Surgery Program under the World Heart Foundation.

  5. Nimekuwa Chairman of the National Organizing Committee of the 5th African Heart Seminar 2008 under the Course Directors: Prof. Charles Yankah of Berlin Heart Institute and University of Berlin, German and Dr. Willie Koen from Christian Barnaard Memorial Hospital, Cape Town- South Africa.

  6. Next Month September 2008 invited special guest by European Association for Cardiothoracic Surgery and the Society of Thoracic Surgeons and American Association of Thoracic Surgery for laying grounds for the formation of African Society of Thoracic Surgeons/ African Heart Foundation.

  Mwisho, nawatakieni majadiliano na malumbano mema.

  Dr. Masau
   
  Last edited by a moderator: Aug 12, 2008
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mimi nilikuwa nataka aeleze kwa nini halipi kodi? Na ni kweli ana historia ya kutolipa kodi hata kwa Mwarabu wa Mikocheni?
   
 3. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2008
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kuna watu watatamani dunia ipasuke waingie huko wajifiche. Duh hii ni kali haya tulikuwa tunagubikwa hapa na porojo. Mwenyewe kasema sasa. Bring another Theory...
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Aug 9, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Pundit, suala la kodi ni dogo sana ukilinganisha na suala linalohusu maisha ya mtu, na madai ya kuweza kuwa a possible murder suspect na madai ambayo yamelenga kuharibu hadhi yake mbele ya jamii. Unapofikia mtu anasema wagonjwa wasije kwako kwa sababu ya kuwa hujasomea kazi hiyo, that is a very fine line ambayo kwa kweli kucross it takes audacity of daring.


  Kuhusu kodi ana kesi mbili zinaendelea and I think it'll be wise to let the legal procedure follow its course. Lakini swali kwamba alikuwa anafanya kazi na kujitangaza kuwa yeye ni msomi wa fani fulani inayohusu uzima na kifo cha mtu wakati haikuwa hivyo, ni swali ambalo lilihitaji majibu ya moja kwa moja. Don't you agree?
   
 5. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Usipoweza kuaminika katika suala "dogo" la kodi, utaaminika vipi katika suala kubwa la maisha ya binadamu?

  Nchi nyingine Daktari akiwa na viskendo skendo vya kutolipa kodi ananyang'anywa license yake ya ku practise kwa mujibu wa ethics za profession.
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Aug 9, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kusoma professional backround ya Dr. Masau mwaka 2000 alipotangaza kuanzisha huduma ya upasuaji wa moyo Tanzania. Nikasema, huyu jamaa anataka kuwa anatupasua mioyo yetu hapa bongo atakuwa ana ujuzi kweli? Baada ya kupata dossier yake wakati ule na kuipitia sikuwa na shaka kuwa kweli anao uwezo wa kutupasua mioyo yetu, na wala sitakuwa na wasiwasi kumwachia anipasue moyo wangu.

  Ndiyo maana uvumi huu ulipoanza kuwa jamaa ni kihiyo, nilishangaa sana, na sikukubaliana nao. Nilisema kuwa labda tuzungumziea matatizo yake mengine tu lakini siyo ya utaalamu, kwani katika kona hiyo mwenzetu kabobea.

  Nyani Ngabu huwa anasema "Ndivyo Miafrika Tulivyo," nadhani ni kweli kuwa hatumkubali mwafrika mwenzetu kuwa na utaalamu huo. Nakumbukua miaka ya sabini ile wakati Charles Njonjo (mkikuyu wa Kenya) alipoapa kuwa hatapanda ndege inayoongozwa na mwafrika, na vile vile alikataa kuwa hataoa mwanamke wa kiafrika. Ni kama vuile sote tumekuwa akina Njonjo sasa
   
 7. M

  Mkora JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Tatizo kuna watu wanaishushia hadhi baraza kwa Choyo zao tuu
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Aug 9, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Pundit, nadhani wengi wetu hayo madai ya kulipa kodi hayakutushtusha kama yale ya kuwa hajasomea upasuaji wa moyo kama anavyodai na kwamba kuna watu wengi wamekufa chini yake. Hayo ya kodi mimi wala sijali sana lakini yale aliyoleta K kwa kweli yanatisha!!!!
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Not sure how far Masau is willing to go na hii
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Aug 9, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  This is what I'm talkin bout!! Wewe umeenda moja kwa moja kwenye source na source imesema vielelezo vipo. Mwenye kubisha na abishe.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Aug 9, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Wewe beef yako nini....kwamba kasomea upasuaji wa moyo au hajasomea au kwa nini halipi kodi?
   
 12. L

  LeoKweli JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2008
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nina wasiwasi na elimu yako, Kama umeleta majungu ya kufikia hapo ninadhani na wewe ni mmoja wao wa wale Vihio, kwahiyo unadhani kila mtu ni kihio
   
 13. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unaona sasa hiki kitu! Eeeh, Dr. Masau, unaona unavyozidi kuharibu! You're in a hole, the first thing you wanna do is stop digging, alright!

  Ningekuwa sijakaa Marekani hata mimi labda ningempa kibali cha kufungua hospitali. Na ndio maana nasema watu wa Afya ni vigumu sana kumshuku mtu kama Masau.

  Ni hivi, hakuna kiumbe cha Mwenyezi kinachoweza kugusa mgonjwa - achilia mbali kupasua - kugusa mgonjwa wa mafua Marekani kama huna kibali cha uganga. Period. Simple as that. Period.

  Nimekaa kiwanja mvua kibao, and trust me, I didn't spend my life in America watching the Grammies, alright, I'll tell you that for sure. And in the modern world of google you don't even have to subscribe to the morning paper so as to learn the system.

  I don't think there is any way whatsoever that foreign doctor, unlicensed in America, can come here and perform an operation, so Dk. Masau, enough with the obfuscation. Please, sir, please!

  Wale watu pale Afya, oh yeah, utawapelekesha, lakini sio mtu aliyeishi Kiwanjani mvua nenda mvua rudi, so please save me that spin, ok. Thank you.

  Kwa sababu hoja yake ina udhaifu anaposema huwa anakuja na kurudi hapa kufanya operation anapotaka - wakati hana kibali - basi hata hayo mengine ya operation 1800 wakati anajifunza nashindwa kumwamini.

  You have to have a license to practice in America. That's mandatory in the story!
   
 14. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  kodi .....
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Aug 9, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  So, tatizo ni kibali cha ku practice medicine in America au kwamba hajasomea upasuaji moyo? Watu msitake kuvuruga hoja hapa. Direct accusations zimetolewa, the accused has responded na kusema vielelezo vipo. Next step, aombwe aweke vielelezo vyake hapa ili ubishi wa kwamba yeye kasomea au hakusomea upasuaji moyo tuuzike.
   
 16. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0


  Isnt it ironic sababu kubwa ya kuwepo kwa thread ndefu uliyoanzisha humu ya Dr Masau ni kuhusu yeye KUTOLIPA KODI

  lakini hiyo umeona haina umuhimu wa kumuuliza umeamua kurukia hii ya credentials zake

  typical init?
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Aug 9, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Good to know that at least you are sticking to your issue and not flipping, flopping, and flailing in all directions......
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Aug 9, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Watu wengi kufa kwa sababu yeye hajasomea upasuaji moyo ni muhimu kuliko yeye kutolipa kodi. Uhai wa mtu kamwe hauwezi kulingana na kukwepa kulipa kodi.
   
 19. Pangu Pakavu Tia Mchuzi

  Pangu Pakavu Tia Mchuzi Member

  #19
  Aug 9, 2008
  Joined: Jun 3, 2006
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Hata Afya kuna walioishi Marekani kama wewe! na wametambua qualifications zake na kumpa licence.

  Convince us that Afya people were wrong and YOU ARE THE ONE WHO IS RIGHT!... Yaani unawazidi hata jamaa wa Tanganyika Medical Board! Duh!
   
 20. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2008
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Wanafunzi wanaosomea uzamili UK katika Hospitali Uingereza hawana haja ya kuwa Registered wanapochukua mafunzo yao kwani vyuo ndio vinakuwa vinatambuliwa. Wanapochukua mafunzo huwa wako live kwenye kuwatibu wagonjwa n.k. tena utakuta wana vibandiko vimeandikwa Student ....na wanakuwa na wasimamizi wao. (wakimaliza kusoma na wanapotaka kufanya kazi ndio ngoma huanza na maswali kede kede ...Je wale waliosomea USA wanaweza kutupa mwanga?)

  Swala lingine Je, Kuhani amesomea hiyo fani?
   
Loading...