Majibu ya Dr. Kawambwa juu ya 'maswali ya kuchagua darasa la 7' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya Dr. Kawambwa juu ya 'maswali ya kuchagua darasa la 7'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DT125, Aug 26, 2012.

 1. D

  DT125 JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nimemsikiliza Dr Kawambwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia elimu nchini kwenye serikali hii ya JK nimesikitika sana na mwisho kubaini kabisa hastahili uwaziri. Anaeleza wamelazimika kutoa maswali ya kuchagua mitihani ya masomo yote kwa sababu ya kurahisisha usahihishaji wa mitihani wakiwa na lengo la kupunguza ghalama kwani watoto wanaofanya mitihani hiyo kwa sasa ni wengi tofauti na tulipopata uhuru, sababu ya pili ni kuwahisha zoezi ili waende zao sekondari. Waziri huyu ipo siku atafuta maswali ya kujieleza hata sekondari kwa sababu hizo hizo ikiwemo kuwawahisha kuingia zao kidato cha tano, na baadae kuwawahisha vyuo vya elimu ya juu na wale wa vyuo vikuu kuwawahisha kwenye ajira. Kwani kote idadi imeongezeka ukilinganisha na kipindi baada tu ya kupata uhuru.
   
 2. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kawambwa ni kilaza wa mwisho, sidhani kama anajua maswali ya kuchagua yanapima nini kwa mwanafunzi.
  Ieleweke kila aina ya maswali hupima vitu tofauti. Kifupi Kawambwa ni jinga flan tu aliebebwa kwa undugu na wala hapaswi kuwa waziri wa elimu.
  Aje hapa nimfundishe blooms taxonomy na validity of a test ili aelewe kuwa ni upuuzi mtihani mzima kuwa maswali yakuchagua ni upuuzi tena UPUUZI MKUBWA.
   
 3. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Kwani huyu Dr Kawambwa ni DR wa nini?

  Namsikilizaga hata bungeni anavyojibu maswali nachokaga kabisa.

  Alishawah kuwa mwalimu hata wa chekechea?
   
 4. N

  Ngoshanzagamba Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni balaa wizara ya Elimu ni chaka la wanyang'anyi kila mpuuzi hujichia....Toka Chemistry with Physics had kwenye multiple choice ni mwendelezo wa unyang'anyi wa elimu kwa watoto wetu...kama tatizo ni wanafunzi wengi/suluhu ni kuongeza idadi ya waalimu kwenye kusahihisha...Kwa bahati mbaya mitihani husahihishwa kipindi cha likizo cha watoto hivyo hakutakuw na matatizo yeyote...Nani atabisha kuwa watoto watamaliza kidato cha nne bila kujua kusoma na kuandika?.....Kuwa mhadhiri si kweli kuwa unakuwa unaelewa misingi ya ualimu na taaluma....wizara hiyo alitakiwa apewe mwalimu...mtu mwenye base ya ualimu(fani/taaluma)....
   
 5. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red,nimekumbuka ule usemi "ukiona elimu ni ghali jaribu ujinga"huko ndiko wanakotupeleka hawa kenge/mafisadi, haingii akilini elimu yetu ivurugwe eti kisa kuepuka gharama na kurahisisha mambo.Kila Waziri katika hii wizara anakuja na vituko vyake,mwingine mara Physics with Chemistry,mara michezo ifutwe.Naruhumia sana hiki kizazi.Nina hasira sana, ngoja niishie hapa nsije nikaanzisha mengine,lakini inaudhi sana!
   
 6. +255

  +255 JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Wizara ya Elimu huwa inaonewa sana, huwa watu wabovu ndo huwa wanapewa kuingoza mwisho wa siku kila mtu lazima aharibu kabisat kitu ... Angalia enzi za Mama Sitta, Mungai, Magembe na sasa huyu Kawambwa toka aingie kavuruga kabisa system ya kupata mikopo..
   
 7. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Kwa kweli hii habari imenisikitisha sana na kunikasirisha kwani mwanangu atafanya mtihaniwa darasa la nne na ndo wamepata hizo taarifa wiki iliyopita ya multiple choice kwa kwenda mbele . Nimeambiwa kuna lalamu maalum na kunajinsi ya kujaza kwenye chumba ili computer iweze kusoma....poor kikwete anachezea maisha ya watoto wetu....
   
 8. e

  enzihuru Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sababu ya viongozi wote wa CCm kuhujumumna kuua elimu ni kujenga mazingira ambayo ni watoto wao tu ndio wataweza kukubalika kielimu na kutawala nchi kwa kigezo cha ubora wa elimu kwani watoto wao hawasomi hizo shule zao uchwara zinafuata sera mfu za elimu.Haiingii akilini kigezo cha idadi ya watahiniwa kuwa sababu kwani wangeweza kuongeza wasahihishaji na hivyo kupunguza suku za kazi hiyo.Hivi China au India (ambapo watoto ni zaidi ya milioni mia hamsini)wakisikia sababu zake hawatahoji udaktari wake.Namshauri asitoe view kama madaktari na maprofesa wetu wa nguvu za giza kama Dr. Tangatanga na Prof. Majimaji.
   
 9. Ze Heby

  Ze Heby JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 3,638
  Likes Received: 1,878
  Trophy Points: 280
  Maskini Tanzania...Watu kama hawa ni maadui zako wakubwa!
   
 10. C

  CHOMA Senior Member

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maamuzi ya Waziri huyu ni matokeo ya utekelezaji wa masharti ya wanaoitwa Wahisani wa Wizara hiyo.Wanataka waonekane hakuna mwanafunzi anayepata SIFURI kwenye somo la HISABATI kwa sababu wanafunzi hawahitajiki kabisa kusoma wala kukokotoa maswali ya somo hilo.Hata kama atachagua kuandika majibu yake herufi a ,b na c kwa swali la 1 hadi 50 hataweza kupata SIFURI.Kwa hiyo tutatengeneza wanafunzi goigoi wa HISABATI.Serikali imechoka kutumia gharama kwenye elimu ndio maana Waziri anasema watapunguza gharama za elimu kwa kufanyia mazoezi utaratibu huo unaopeleka Taifa letu kaburini kwenye kipindi hiki cha Sayansi na Teknolojia.Tujiandae kuvuna tunachopanda.
  Tafadhali wanaoipenda na kuitakia mema nchi hii tuungane kupiga vita kwa nguvu zote ili tuliokoe Taifa letu.Umoja ni nguvu utengano ni dhaifu.Tutakuja kuulizwa kesho mbele ya Mwenyezi Mungu tulifanya nini kuliokoa Taifa letu.
   
 11. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka katika bajeti Yake kuna mbunge mmoja simkumbuki jina alikuwa wa chadema lakini aliuliza kwanini wanatoa multiple choice mitihani ya darasa la Saba,ila alibase kwenye hisbati.. Kumbe sababu ya multiple choice ndo hiyo??? Kweli hakuna waziri hapa
   
 12. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,611
  Likes Received: 2,040
  Trophy Points: 280
  Tena mdau DT125, mie mwenyewe nilishangaa kweli wakati akijibu with confidence kwamba ANAOKOA GHARAMA pia INARAHISISHA USAHIHISHAJI kwa walimu kwa kuwa majibu yanafanana hivyo msahihishaji inakua rahisi kusahihisha. Akamalizia kwa kutoa mfano wa IDADI YA WANAFUNZI 1961 na idadi ya sasa na kusema kwamba wanafunzi ni wengi si rahisi kwa wasahihishaji kupata muda wa kutosha kusahihisha maswali ya kujieleza (HAPA NDIO AKANIBOA KABISA MAANA KAMA WANAFUNZI WAMEONGEZEKA KISAYANSI NA WASAHIHISHAJI LAZIMA WAONGEZEKE BASED IWE UWIANO WA WANAFUNZI WALIOONGEZEKA). Maswali design hii yanabidi yatolewe chuoni ambako walishapitia huku chini kwani kwa mwanafunzi wa shule ya msingi ukimpa mtihani design hii humjengi kiakili
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Tumekwisha! Kama mambo yenyewe ndo haya, nchi yetu inaelekea kuzimu kielimu. Unatungaje mtihani mzima multiple choice? Utapima vipi uwezo wa wanafunzi kusoma, kuhesabu, kuandika na kujieleza kwa walau insha fupi fupi na kumalizia sentensi fupi fupi bila kuwepo maswali ya aina hiyo? Upumbavu tu unaofanyika! Hawa jamaa kweli wamechoka.... Hata kufikiri!
   
 14. m

  mwamola Senior Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Atumie salary arrears yangu ya promotion ambayo ameshashindwa ama kugoma kunilipa ili aitumie kuwalipa wasahihishaji wa mitihani hiyo.
   
 15. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,768
  Likes Received: 1,948
  Trophy Points: 280
  kikwrte ni janga la tifa
   
 16. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #16
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Hamjaisikia tathmini yao kuwa kiwango cha elimu kimepanda
  kulinganisha na kipindi cha nyuma. Mambo ya ajabu kabisa...
   
 17. m

  manduchu Member

  #17
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hili linchi kila siku aheri ya jana. kila aneyeingia kwenye elimu anakuja na madudu yake. naona kama tuna kalaana hivi, nchi inayocheza na elimu ya watu wake hakika itaendelea kuwa masikini, na hapo utasikia wakisingizia tuko masikini kwa ajili ya wakoloni.
   
Loading...