Majibu ya barua ya JK na serikali yake toka WEF(Davos)….Epukeni punguzo la bajeti ya maendeleo… | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya barua ya JK na serikali yake toka WEF(Davos)….Epukeni punguzo la bajeti ya maendeleo…

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Jan 26, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,546
  Likes Received: 1,327
  Trophy Points: 280
  • Ndugu zangu sijui ni wangapi mnafatilia yanayojiri toka Davos kwa World Economic Forum (WEF)?…au tukishaambiwa na watu wa ikulu kuwa JK kaondoka basi….hatuoji tena nini anafanya huko alikokwenda au nini kimejiri huko?...nashangaa sana hata vyombo vyetu vya habari (hasa hizi tv)vinakuwa shallow sana kufatilia hizi safari za JK na anachofanya anapokuwa huko nje…..tunabaki tu kehesabu tumeliwa kiasi gani na hizi safari zake…..
  • Nimeanza hivi nikitaka kuleta moja ya hoja muhimu haswa kwenye discussions za next bunge session.Kama tunafatilia tutakuwa na taarifa kuwa hivi karibuni serikali ya JK waliandika barua IMF kuwataarifu juu ya mipango yao ya kupunguza bajeti ya serikali katika kukabiliana na athari za euro zone economic crisis.Katika andishi lao,serikali wamesema hatua za kupunguza bajeti zitaathiri miradi ya maendeleo…jambo ambalo linapingwa vikali na wachumi ikizingatiwa kuwa jambo hili litaathiri ukuaji wa uchumi ambao tayari ni legelege……Kinachoshauriwa kikiwa kupunguza matumizi ya serikali yasiyo na tija e.g posho etc.......
  • Katika kile kinachoonekana kuwa ni majibu ya msingi kwa hoja hii kwa seriakali ya JK kutoka kwa wakubwa wa uchumi wa dunia……Mkurugenzi wa IMF (Christine Lagarde), Rais wa bank ya dunia(Robert Zoellick)na Rais wa WTO(Pascal Lamy)wote kwa pamoja wamesema juhudi za serikali zozote za kupunguza matumizi lazima zilenge kukuza uchumi na kuongeza ajira na si kuupunguza :Nanukuu:-`The International Monetary Fund's managing director and top global finance officials are urging the world's political leaders to avoid budget cuts that would hinder economic growth. Christine Lagarde said in a statement that government spending cuts and other fiscal austerity measures should ``promote rather than reduce prospects for growth and employment.''Akamalizia kwa kusema kwamba haya ni matamshi yake na wenzake niliowataja hapo juu na wote kwa pamoja wakatia saini statement yao.Nanukuu:- World Bank President Robert Zoellick and Director-General Pascal Lamy of the World Trade Organization signed onto the statement.
  • (Source:Christine Lagarde joins call for growth, economic reform - The Economic Times).

  • Nadhani hili litakuwa jibu zuri la food for thought kwa kina mh.Zitto watakapokuwa wanajadili masuala ya kupunguzwa kwa bajeti ya serikali yatakapoletwa na serikali katika bunge session next week.Angalizo: serikali ipunguze matumizi yake kwenye issue kama hizi safari za JK zisizo na tija,magari ya serikali,mawizara yasiyo na kazi, mikoa na mawilaya feki etc etc…..na kamwe wasiguse bajeti ya maendeleo ambayo wala hatuyaoni….tunachoona ni safari,posho na mawizara yakilipa watu mishahara bure….
  • Katika hali ya kusikitisha nimeshangaa kuona JK akiongea jambo la ajabu sana (uongo)kwenye plenary session ya Afrika pale Davos……..plenary ilihusisha waziri mkuu Raila, Zenawi,marais makini Chonde(Guinea)na Zuma(SA)….wenzake walijikita kwenye mikakati ya kukuza uchumi wa Africa kwa kujenga ushirikiano….yeye JK akawaambia eti kupambana na ufisadi ndio issue kubwa……(as if yeye anafanya hivyo)……cha kuuzunisha akamaliza kwa kusema kitu cha kwanza kwenye kupambana na ufisadi ni kuwa na uwazi(transparency) na eti yeye kwenye nchi yake(TZ) sasa wana publish mikataba ya madini (wanaweka wazi mikataba)kama new mining code!!! Nanukuu:- However tackling the problem of corruption was still a "major issue", said Tanzanian President Jakaya Kikwete."The first thing to fight against corruption is transparency," he said, adding that his country was now publishing all mining contracts as part of a new mining code. "The best guarantee for an investor is transparency."
  (Source: BBC News - Davos 2012: Africa leaders urge co-operation)
  Is this a joke jamani!!!! Hizi ndizo tija tunazopata watanzania kwa huyu rais wetu anaposafiri nje……amazing eh!!
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Majibu ya wakubwa hao wa IMF na World Bank ni kibano kwa viongozi wetu! Najua akina Zitto,Mnyika na wengine wanapita humu waitumie kama base kuibana serikali.
   
 3. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ajabu kubwa ............

  wakiambiwa punguzeni matumizi wanafikiria bajeti/fedha za maendeleo zipi zipunguzwe na siyo mambo mengine kazi ipo hapa petu Tz.

  Hiyo wanayoiita mikoa mipya itaanza lini kufanya kazi na hizo wilaya zake ????
   
 4. M

  Mzee Busara Senior Member

  #4
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kubeba kipengere kimoja tu kwenye hotuba kunaweza kupotosha maana ingependeza kama tungepata hotuba yote pengine kuna mahala aliongelea pia kipengere cha kupunguza matumizi mengine au jambo linalofanana na hilo.
   
 5. M

  Mzee Busara Senior Member

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbuka kwenye mikutano ya kimataifa kila mtoa mada anapewa eneo la kusema ili kuondoa marudio. kwa hali hiyo Marais wa Afrika wasingezungumza kitu kimoja kwenye mkutano mmoja labda tu kwa maelekezo maalum ya waandaaji.
   
 6. M

  Mzee Busara Senior Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK analaumiwa kwenda Davos hao hapo chini mmewaona. Hakika ningependa kujua ni nchi ngapi za Afrika zimekwenda kushiriki maana tunaambiwa Rais Jk hakuwa na sababu ya kwenda huko.

  kwenye plenary session ya Afrika pale Davos……..plenary ilihusisha waziri mkuu Raila, Zenawi,marais makini Chonde(Guinea)na Zuma(SA)….
   
 7. M

  Mzee Busara Senior Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Bajeti ya Mkullo iliyopita ilieleza kwa ufasaha maeneo ambayo serikali imeamua kupunguza matumizi na kiasi cha fedha kitakachopatikana kutokana na hatua hiyo. Hatua hii ililenga bajeti ya matumizi ambayo si ya maendeleo. chukua bajeti hiyo soma eneo la vyanzo vya mapato ya serikali kwa njia ya kupunguza matumizi.
   
 8. M

  Mzee Busara Senior Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuongeza mapato ya serikali si kwa njia ya kupunguza matumizi tu bali hata ya uzalishaji kwa mtu mmoja mmoja ikiwemo mimi na wewe.

  Kimsingi, hakuna serikali duniani iliayojiri wananchi wake wote wengi wapo nje ya mfumo wa kisekta. serikali ya Tanzania kwa sasa ina watumishi kadri ya 400,000 tu ambao hawawezi kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi bila walio nje ya mfumo wa kisekta.

  Bila kutafuna maneno katika ukanda huu wa Afrika mashariki Tanzania ndio inaongoza kwa wananchi wake kuwa wavivu. Hivyo changamoto za maisha za wananchi zinategemea zaidi serikali. Endapo tutaungana na wenzetu tutamezwa haraka sana na kutawaliwa.
   
 9. M

  Mzee Busara Senior Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania tumejariwa kukosoa kuliko kujikosoa. Uzoefu duniani umeonyesha kwamba wananchi ambao waliendelea mapema kiuchumi ni wale waliotangulia kujikosoa na kuzungumzia mapungufu yao kabla ya viongozi wao. Hili ndilo chimbuko la somo la uzalendo wa kuifia nchi.
   
 10. A

  August JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  huwezi kuwabadili watu kuwa watendaji bila vifaa muhimu vya uzalishaji kama umeme, uwanja sawa wa kufanya biashara wengine wanapewa exemption, wengine wanalipa kodi halali, upendeleo katika utoaji wa vyeo na tenda, uteuzi wa viongozi , vifaa hospitalini, kutokuwa na standard katika transport sector, bara bara mbovu mbovu au foleni nk nk
   
 11. M

  Mzee Busara Senior Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Neno epukeni punguzo la bajeti ya maendeleo haina maana acha kabisa kupunguza bajeti ya mandeleo, kwa tafsiri yangu ningesema punguzeni kwa makini bajeti ya maendeleo bila kuathiri uchumi....
   
 12. M

  Mzee Busara Senior Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tutengeneze uchumi wa kufikirika ambapo tujiulize kuku na yai kipi kilianza? kwenye uchumi mchanga nguvu kazi ndicho kifaa muhimu kuliko vyote kwa kuwa wakati huo huna vifaa. Mfano, China enzi za Mao se Tung ni mfano wa nguvu kazi iliyowapeleka wachina hapo walipo na vifaa vikaja baadaye. Watu wengi sana walikufa katika kipindi hicho cha mpito lakini bila Mao China isingefika hapo.

  Jiulize pia kipi kinatangulia kati ya maarifa na uvumbuzi. huwezi kuvumbua kama huna maarifa.
   
 13. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,546
  Likes Received: 1,327
  Trophy Points: 280
  we hujui unachozungumza.....utapunguzaje bajeti ya maendeleo bila kuathiri uchumi?.......don' t argue here because you can't even associate how development budget is associated with economical growth.......ondoa siasa zako hapa......
   
 14. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #14
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Jk ameenda kutalii hakuna la maana alilofuata huko. Serikali yake imejaa maswahiba ambao hawana uwezo wa kufikiri na wasio na maono.

  Kweli nchi kama tz unawezaje kuamua kushawishi kupunguza budget kwa ajili ya maendeleo!.Ama ladba tafsiri ya maendeleo inapotoshwa. Uchumi gani unaokuwa ukaongezewa kasi ya kukua kwa kupunguza budget ya maendeleo!

  Tanzania kama nchi inayoendelea inahitaji kuwepo na vichocheo dhabiti vinavyochochea ukuaji wa uchumi kwa kuzingatia pato la mtu mmoja mmoja sambamba na kuboresha uzalishaji.Utaboreshaje uzalishaji kama hakuna tija ! .Tija inapatikana kutokana na kuwa na rasilimali watu wenye afya na nguvu pamoja na maarifa ya kutumia rasilimali kuzalisha.Unapopunguza budget ya maendeleo kama huduma za afya ,elimu nk utapata wapi rasilimali watu wenye uwezo wa kuzalisha?

  Kuwa na viongozi kama JK wakati mwingini inasababisha hata kumkufuru Mungu kwa kumlaumu kwa nini tulizaliwa waafrika -Tanzania.Kiongozi asiye na maono ya mbali ni sawa na mbwa asiyebweka akimwona adui.
   
Loading...