Majibu ya ACT-Wazalendo kwa hoja za Tundu Lissu

IMG_5518.JPG
 
1. Usiangalie upande m1 wa shillingi. Lowasa alitajwa na CDM kuwa ni fisadi papa. Lakini Lowasa huyo huyo mlimteua kugombea urais wa JMT. Je ulichukua hatua gani kwa uamuzi huo wa chama chenu?

2. Lakini pia kumbuka Sumaye ni waziri mliyemtukana aina zote za matusi. Lakinj mlimpokea katika chama chenu na kumpa uongozi wa mwenyekiti kanda ya Pwani. Je kwa uamuzi huo wa chama chenu ulichukua hatua gani?

3. Lazaro Nyarandu mlimwita mzee wa twiga. Lakini mlimpokea katiki chama chenu na kumpa uongozi mbalimbali na kisha kumteua kuwa mgombea ubunge. Je kwa uamuzi huo wa cdm ulichukua hatua zipi?

Au unaziona kasoro za ACT tu?
Yaani hakuna mtu wa ajabu kama huyo sijui mnamwita Lissu.
 
Chadema huwa ni perfect siku zote hawajawahi kukosea jambo,Lissu alisema katika nchi hii upinzani wa kweli ni Chadema na Cuf tu wakati huo walishakuwa na ugomvi na cuf kwa mambo kama haya kuwasema wenzao ila ukiwakosowa wao utaambiwa umenunuliwa.
 
Wakuu niseme tu sina imani na nyie! Mtu akishakosa msimamo kwangu huwa anakua phased out! Am done with you guys!
Unaweza kuwa na msimamo usio kuwa na tija, zaidi ya kukusaidia ukakupoteza kabisa,
Na kwa Lisu na msimamo wake na maneno machafu yanayotoka choo cha mdomo wake asahau kuwa kiongozi mkubwa wa nchi hii.
Ni mtu mwenye roho mbaya na anafundisha nyumbu wake kuwa na riho mnaya katika nchi hii,
Aende akaungane na yule jamaa huko sijui anaitwa Marandu wakaoshe matako ya farasi huko marekani.
 
Nyama ya Nguruwe ukishasema haram itabaki kua haram hata uikaange,uichemshe au uichome bado itakua haram,,,hata uipike kwa viungo vingi bado itabaki kua haram.
 
Kama unazini na mwanamke ambaye ni HIV + kwa kutumia condom kisha baada ya muda mfupi unanogewa na kuamua kuvua condom kisha baada ya miezi kadhaa unajikuta nawe ni HIV +, sasa hapo utamlaumu nani.?

Maalim tayari umri umeshamtupa mkono na kumbe kwa mazingira ya sasa hakufaa kabisa kuwa kiongozi kwa sababu ni mtu ambaye hana msimamo na amefikia uamuzi huo baada ya kuona hana chochote cha kupigania tena baada ya ccm kumfanya their punching bag ktk kila uchaguzi.

Seif has now turned into a villain and definitely a spent force. He cannot assure the Zanzibaris that the next election will be free and fair as ccm will continue to stage mock election after every five years.
 
Unaweza kuwa na msimamo usio kuwa na tija, zaidi ya kukusaidia ukakupoteza kabisa,
Na kwa Lisu na msimamo wake na maneno machafu yanayotoka choo cha mdomo wake asahau kuwa kiongozi mkubwa wa nchi hii.
Ni mtu mwenye roho mbaya na anafundisha nyumbu wake kuwa na riho mnaya katika nchi hii,
Aende akaungane na yule jamaa huko sijui anaitwa Marandu wakaoshe matako ya farasi huko marekani.
Ana maneno machafu kuliko yule anayedhalilisha wanawake majukwaani?
 
Imeandikwa na Janeth Rithe, Katibu wa Uenezi Taifa ACT Wazalendo

Nimesoma maoni ya Ndg. Tundu Lissu kuhusu Uamuzi wa chama cha ACT Wazalendo kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Ninaheshimu sana maoni yake na tunachukulia kwa uzito mkubwa ukosoaji wake kwa maamuzi ya vikao vya chama chetu. Licha ya kwamba inaleta ukakasi ukosoaji wa maamuzi ya vikao vya chama kutoka Kwa Kiongozi wa chama kingine cha upinzani lakini tunaamini ni ukosoaji wa nia Njema. Sisi kama ACT Wazalendo tumejitahidi sana kujiepusha kutolea maoni maamuzi ambayo viongozi wa CHADEMA wamefanya hivi karibuni licha ya Kuwa na Taarifa nyingi za uhakika kuhusu maamuzi yale. Nitafafanua baadhi ya mambo ambayo ndugu yangu Lissu ametolea maoni.

Lissu anasema kuwa “ACT wame-surrender kwa Magufuli na maCCM. Hakuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inayoamuliwa na Wazanzibari wenyewe; bali ile inayoruhusiwa na Watanganyika, yaani Magufuli na maCCM ya Tanganyika”. Maoni haya yametolewa Kwa haraka bila kutafakari wala kurejea historia ya hivi karibuni.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni zao la Wazanzibari wenyewe kufuatia maridhiano ya Novemba 5, 2009. Wazanzibari walipiga Kura kuidhinisha Mabadiliko ya Katiba yaliyowezesha hilo. SUK ni suala la Katiba na sio suala la watu kukaa na kujadiliana. Mwaka 2010-2015 CUF ilishiriki SUK sio Kwa kuwa Watanganyika walitaka bali Kwa Kuwa Wazanzibari walitaka. Watanganyika walipinga sana maridhiano Zanzibar, tena wa pande zote mbili upinzani na CCM kwa sababu ni hulka ya Watanganyika kujiona wao ni watawala wa Zanzibar. Hata haya maoni ya ndugu yangu Lissu yamejikita katika muono huo huo wa ‘mentality’ za kikoloni Kuwa Wazanzibari hawawezi kujiamulia mambo yao wenyewe mpaka waamuliwe au wasemewe na Watanganyika.

Maamuzi ya kuwepo kwa SUK ni ya Wazanzibari na maamuzi ya ACT kuingia SUK Mwaka huu ni kutimiza matakwa ya Wazanzibari ambao wanataka Umoja, Haki na Maridhiano ya kijamii. Hii hulka ya Watanganyika wa upinzani na wa chama tawala kudhani kuwa wanajua zaidi maslahi ya Wazanzibari kuliko Wazanzibari wenyewe ni hulka ya KIKOLONI.

Tuna ushahidi wa kutosha kuwa Bwana Magufuli na CCM hawataki SUK Zanzibar Kwa Kuwa hawataki Wazanzibari kuwa wamoja. Uamuzi wa kuingia SUK ni Uamuzi wa Wazanzibari ambao kwetu sisi ACT Wazalendo umepata baraka zote za vikao vya chama tena bila mkwaruzano (unanimously decided ). Magufuli na CCM Watanganyika wasipewe sifa wasiostahili kuwa eti wameridhia SUK, huko ni kuwadogosha Wazanzibari kuwa hawana uwezo wa kufanya maamuzi Yao wenyewe.

Ndugu yangu Lissu anasema “Tumemtupia Maalim Seif mfupa mtupu (Makamu wa Kwanza wa Rais hana mamlaka yoyote ya maana kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar!) ili atulie na awatulize Wazanzibari wanaomuunga mkono na jumuiya ya kimataifa iliyochukizwa na dhulma zetu Zanzibar na Tanganyika”. Vile vile maoni haya ni hisia tupu ambazo haziwezi kuthibitishwa na ushahidi wowote. Haya ni Maneno mepesi ambayo mtu yeyote hata muuza kahawa wa Urughu, Iramba anaweza kuyasema. Lakini pia ni hisia ambazo muda utathibitisha kuwa hazina msingi.

Chama chetu kimezungumza na Jumuiya ya Kimataifa kuhusu uharibifu mkubwa wa uchaguzi uliofanyika hapa Tanzania. Niseme tu Kuwa Jumuiya ya Kimataifa inajua Kwa undani nini kimetokea mpaka kufikia Uamuzi huu wa ACT Wazalendo kuingia katika SUK Zanzibar. Matokeo ya SUK Zanzibar yana maana kubwa sana katika juhudi za Jumuiya ya Kimataifa dhidi ya ukandamizwaji unaoendelea hapa Tanganyika. Litakapodhihiri ndugu yangu Lissu na Watanzania wote wataona nini maana ya Uongozi. Kiongozi ANAONGOZA! Kiongozi HAONGOZWI. Jumuiya ya Kimataifa haitatulizwa bali ipo kazini katika hili la SUK. Niishie hapo. Itoshe kusema Kuwa Viongozi wetu wa ACT Wazalendo katika hili wanatoa Uongozi badala ya kuongozwa na mihemko ya Wanachama na wafuasi wakiwemo wana harakati.

Ndugu yangu Lissu anasema “Serikali hii ya sasa ni tofauti na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Amani Karume na Maalim Seif. Ya mwanzo ilileta mabadiliko makubwa ya Katiba ya Zanzibar; kwa sababu Karume alikuwa anaunga mkono jitihada za Wazanzibari za kujivua kwenye ‘koti linalobana’ la Muungano”. Naomba kumkumbusha Lissu kuwa Maalim hajawahi kuingia SUK na Rais Karume. SUK ya kwanza Zanzibar ilikuwa Kati ya Dkt. Shein na Maalim Seif. Ni imani yetu kuwa SUK hii italeta Mabadiliko makubwa kwa Wazanzibari na haswa kuimarisha Umoja wao kupitia maridhiano ya kijamii, kutoa Haki Kwa watu wote walioumizwa na kupoteza maisha Wakati wa uchaguzi na kuweka misingi ya kisheria ya chaguzi za Haki siku za usoni.

Lissu anasema “Hussein Mwinyi ni kibaraka wetu moja kwa moja; tumemweka madarakani kwa bunduki na vifaru vya Bara na kura za Watanganyika waliopelekwa kupiga kura Zanzibar wakati Wazanzibari halali wanakataliwa kupiga kura”. Haya ni maoni tu ya ndugu yangu Lissu. Sisi kama chama na viongozi tunampa Ndg. Hussein Ali Mwinyi kinachoitwa BENEFIT OF DOUBT. Kwa hatua ambazo Dkt. Hussein amezichukua mpaka sasa tangu awe Rais wa Zanzibar anastahili kupewa hiyo benefit of doubt. Sisi ACT Wazalendo tumerejesha mkono wa kheri katika kurejesha Umoja na Haki kwa Wazanzibari. Maalim Seif anasaidiana na Dkt. Hussein kujenga Zanzibar ya maridhiano. Hukumu anayotoa Ndg. Lissu Kwa Dkt. Mwinyi ni hukumu ambayo yaweza kutosimama muda unavyozidi kwenda.

Lissu anasema “Sasa Maalim Seif Atatumika kama toilet paper ya kusafishia uchafu wa maCCM na madhambi yao dhidi ya Wazanzibari”. Haya ni matusi kwa Kiongozi wa Wazanzibari ambaye amesimamia mapambano ya Wazanzibari maisha yake yote. Sijaamini kama matusi haya yanatoka kwenye maandishi ya ndugu yangu Tundu Lissu. Ushauri wangu kwa Tundu ni kuweka akiba ya Maneno.

Tundu anamalizia kwa kusema haya dhidi ya Maalim Seif “Mimi naamini hatafanikiwa. Masikitiko yangu ni kwamba amekubali kutumika namna hii katika uzee wake. Baada ya miaka karibu arobaini ya kusimamia maslahi ya Wazanzibari, sasa amekubali kutumikia maslahi ya Tanganyika!!!” Hii ni imani yake ndugu Tundu. Mimi ninaamini Kuwa Tundu Lissu amejenga imani hii kutokana na hisia na kutokuwa na taarifa za kutosha. Angechukua muda wa kuzungumza na Maalim Seif au Kiongozi wetu wa chama ndugu Zitto Kabwe angepata taarifa za kutosha ambazo zingemfanya asiandike alichoandika.

Mwaka 1987, miaka 33 iliyopita, Maalim Seif alitoa ahadi mbele ya Wazanzibari ambayo anaiishi maisha yake yote. Maalim hajawahi kuongozwa na tamaa ya mali wala maisha ya Dunia. Anaishi maisha ya kawaida sana. Kwake yeye ni Zanzibar, Zanzibar, Zanzibar. Kila hatua anayochokua ni hatua ya kuilinda Zanzibar na Wazanzibari. Hajaacha na hataacha kusimamia maslahi ya Wazanzibari. Hata hili la sasa la SUK ni Kwa maslahi ya Zanzibar. Kwa sisi tunaokaa na Maalim kwenye vikao tunajua Mzee huyu ni wa namna gani. Kwa ambao wanamwona Maalim kwa nje wanaweza kumtafsiri kama hivi ndugu yangu Lissu alivyomtafsiri. Muda ni jawabu. Lissu atameza haya Maneno yake.
Nyie wapuuzi ndiyo mlitaka tuandamane tuvunjwe miguu kumbe mnawaza maslahi yenu binafsi kuliko ya wananchi
 
Kwenye huo Umoja wenu wa kitaifa wale waliouawa na kufanywa vilema na serikali hio mnayoshirikiana nayo leo mnawapa faraja gani?

Katika kushirikiana huko ni yapi mliyokubaliana kama hatua za kuleta maridhiano au ni kupewa vyeo waandamizi wachache wa ACT?

Mlisema kwamba huu Haukuwa uchaguzi bali uchafuzi,je sasa umekuwa uchaguzi halali?na kama si halali wale waliudhulumiwa na kuenguliwa kihuni kwenye nafasi mbalimbali mmewafikiriaje?

Mnasema kwamba Zanzibar mnaamua mambo yenu mwenyewe wakati mara kadhaa Maalimu mwenyewe amekuwa akilalamika kwamba Magufuli katuma wanajeshi huko Zanzibar kuhakikisha ACT haishindi,Je alikuwa mwongo?

Ni maajabu gani mnategemea kufanya ili kushinda uchaguzi wa 2025 kama chama cha upinzani?ambayo yatakuwa tofauti na mwaka huu?

Asante
Hawa ni wasaka tonge kama alivyofanya James Mbatia kushangilia kuwa anaenda kuwa KUB bungeni matokeo yake hajapewa hata diwani mmoja.
 
Imeandikwa na Janeth Rithe, Katibu wa Uenezi Taifa ACT Wazalendo

Nimesoma maoni ya Ndg. Tundu Lissu kuhusu Uamuzi wa chama cha ACT Wazalendo kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Ninaheshimu sana maoni yake na tunachukulia kwa uzito mkubwa ukosoaji wake kwa maamuzi ya vikao vya chama chetu. Licha ya kwamba inaleta ukakasi ukosoaji wa maamuzi ya vikao vya chama kutoka Kwa Kiongozi wa chama kingine cha upinzani lakini tunaamini ni ukosoaji wa nia Njema. Sisi kama ACT Wazalendo tumejitahidi sana kujiepusha kutolea maoni maamuzi ambayo viongozi wa CHADEMA wamefanya hivi karibuni licha ya Kuwa na Taarifa nyingi za uhakika kuhusu maamuzi yale. Nitafafanua baadhi ya mambo ambayo ndugu yangu Lissu ametolea maoni.

Lissu anasema kuwa “ACT wame-surrender kwa Magufuli na maCCM. Hakuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inayoamuliwa na Wazanzibari wenyewe; bali ile inayoruhusiwa na Watanganyika, yaani Magufuli na maCCM ya Tanganyika”. Maoni haya yametolewa Kwa haraka bila kutafakari wala kurejea historia ya hivi karibuni.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni zao la Wazanzibari wenyewe kufuatia maridhiano ya Novemba 5, 2009. Wazanzibari walipiga Kura kuidhinisha Mabadiliko ya Katiba yaliyowezesha hilo. SUK ni suala la Katiba na sio suala la watu kukaa na kujadiliana. Mwaka 2010-2015 CUF ilishiriki SUK sio Kwa kuwa Watanganyika walitaka bali Kwa Kuwa Wazanzibari walitaka. Watanganyika walipinga sana maridhiano Zanzibar, tena wa pande zote mbili upinzani na CCM kwa sababu ni hulka ya Watanganyika kujiona wao ni watawala wa Zanzibar. Hata haya maoni ya ndugu yangu Lissu yamejikita katika muono huo huo wa ‘mentality’ za kikoloni Kuwa Wazanzibari hawawezi kujiamulia mambo yao wenyewe mpaka waamuliwe au wasemewe na Watanganyika.

Maamuzi ya kuwepo kwa SUK ni ya Wazanzibari na maamuzi ya ACT kuingia SUK Mwaka huu ni kutimiza matakwa ya Wazanzibari ambao wanataka Umoja, Haki na Maridhiano ya kijamii. Hii hulka ya Watanganyika wa upinzani na wa chama tawala kudhani kuwa wanajua zaidi maslahi ya Wazanzibari kuliko Wazanzibari wenyewe ni hulka ya KIKOLONI.

Tuna ushahidi wa kutosha kuwa Bwana Magufuli na CCM hawataki SUK Zanzibar Kwa Kuwa hawataki Wazanzibari kuwa wamoja. Uamuzi wa kuingia SUK ni Uamuzi wa Wazanzibari ambao kwetu sisi ACT Wazalendo umepata baraka zote za vikao vya chama tena bila mkwaruzano (unanimously decided ). Magufuli na CCM Watanganyika wasipewe sifa wasiostahili kuwa eti wameridhia SUK, huko ni kuwadogosha Wazanzibari kuwa hawana uwezo wa kufanya maamuzi Yao wenyewe.

Ndugu yangu Lissu anasema “Tumemtupia Maalim Seif mfupa mtupu (Makamu wa Kwanza wa Rais hana mamlaka yoyote ya maana kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar!) ili atulie na awatulize Wazanzibari wanaomuunga mkono na jumuiya ya kimataifa iliyochukizwa na dhulma zetu Zanzibar na Tanganyika”. Vile vile maoni haya ni hisia tupu ambazo haziwezi kuthibitishwa na ushahidi wowote. Haya ni Maneno mepesi ambayo mtu yeyote hata muuza kahawa wa Urughu, Iramba anaweza kuyasema. Lakini pia ni hisia ambazo muda utathibitisha kuwa hazina msingi.

Chama chetu kimezungumza na Jumuiya ya Kimataifa kuhusu uharibifu mkubwa wa uchaguzi uliofanyika hapa Tanzania. Niseme tu Kuwa Jumuiya ya Kimataifa inajua Kwa undani nini kimetokea mpaka kufikia Uamuzi huu wa ACT Wazalendo kuingia katika SUK Zanzibar. Matokeo ya SUK Zanzibar yana maana kubwa sana katika juhudi za Jumuiya ya Kimataifa dhidi ya ukandamizwaji unaoendelea hapa Tanganyika. Litakapodhihiri ndugu yangu Lissu na Watanzania wote wataona nini maana ya Uongozi. Kiongozi ANAONGOZA! Kiongozi HAONGOZWI. Jumuiya ya Kimataifa haitatulizwa bali ipo kazini katika hili la SUK. Niishie hapo. Itoshe kusema Kuwa Viongozi wetu wa ACT Wazalendo katika hili wanatoa Uongozi badala ya kuongozwa na mihemko ya Wanachama na wafuasi wakiwemo wana harakati.

Ndugu yangu Lissu anasema “Serikali hii ya sasa ni tofauti na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Amani Karume na Maalim Seif. Ya mwanzo ilileta mabadiliko makubwa ya Katiba ya Zanzibar; kwa sababu Karume alikuwa anaunga mkono jitihada za Wazanzibari za kujivua kwenye ‘koti linalobana’ la Muungano”. Naomba kumkumbusha Lissu kuwa Maalim hajawahi kuingia SUK na Rais Karume. SUK ya kwanza Zanzibar ilikuwa Kati ya Dkt. Shein na Maalim Seif. Ni imani yetu kuwa SUK hii italeta Mabadiliko makubwa kwa Wazanzibari na haswa kuimarisha Umoja wao kupitia maridhiano ya kijamii, kutoa Haki Kwa watu wote walioumizwa na kupoteza maisha Wakati wa uchaguzi na kuweka misingi ya kisheria ya chaguzi za Haki siku za usoni.

Lissu anasema “Hussein Mwinyi ni kibaraka wetu moja kwa moja; tumemweka madarakani kwa bunduki na vifaru vya Bara na kura za Watanganyika waliopelekwa kupiga kura Zanzibar wakati Wazanzibari halali wanakataliwa kupiga kura”. Haya ni maoni tu ya ndugu yangu Lissu. Sisi kama chama na viongozi tunampa Ndg. Hussein Ali Mwinyi kinachoitwa BENEFIT OF DOUBT. Kwa hatua ambazo Dkt. Hussein amezichukua mpaka sasa tangu awe Rais wa Zanzibar anastahili kupewa hiyo benefit of doubt. Sisi ACT Wazalendo tumerejesha mkono wa kheri katika kurejesha Umoja na Haki kwa Wazanzibari. Maalim Seif anasaidiana na Dkt. Hussein kujenga Zanzibar ya maridhiano. Hukumu anayotoa Ndg. Lissu Kwa Dkt. Mwinyi ni hukumu ambayo yaweza kutosimama muda unavyozidi kwenda.

Lissu anasema “Sasa Maalim Seif Atatumika kama toilet paper ya kusafishia uchafu wa maCCM na madhambi yao dhidi ya Wazanzibari”. Haya ni matusi kwa Kiongozi wa Wazanzibari ambaye amesimamia mapambano ya Wazanzibari maisha yake yote. Sijaamini kama matusi haya yanatoka kwenye maandishi ya ndugu yangu Tundu Lissu. Ushauri wangu kwa Tundu ni kuweka akiba ya Maneno.

Tundu anamalizia kwa kusema haya dhidi ya Maalim Seif “Mimi naamini hatafanikiwa. Masikitiko yangu ni kwamba amekubali kutumika namna hii katika uzee wake. Baada ya miaka karibu arobaini ya kusimamia maslahi ya Wazanzibari, sasa amekubali kutumikia maslahi ya Tanganyika!!!” Hii ni imani yake ndugu Tundu. Mimi ninaamini Kuwa Tundu Lissu amejenga imani hii kutokana na hisia na kutokuwa na taarifa za kutosha. Angechukua muda wa kuzungumza na Maalim Seif au Kiongozi wetu wa chama ndugu Zitto Kabwe angepata taarifa za kutosha ambazo zingemfanya asiandike alichoandika.

Mwaka 1987, miaka 33 iliyopita, Maalim Seif alitoa ahadi mbele ya Wazanzibari ambayo anaiishi maisha yake yote. Maalim hajawahi kuongozwa na tamaa ya mali wala maisha ya Dunia. Anaishi maisha ya kawaida sana. Kwake yeye ni Zanzibar, Zanzibar, Zanzibar. Kila hatua anayochokua ni hatua ya kuilinda Zanzibar na Wazanzibari. Hajaacha na hataacha kusimamia maslahi ya Wazanzibari. Hata hili la sasa la SUK ni Kwa maslahi ya Zanzibar. Kwa sisi tunaokaa na Maalim kwenye vikao tunajua Mzee huyu ni wa namna gani. Kwa ambao wanamwona Maalim kwa nje wanaweza kumtafsiri kama hivi ndugu yangu Lissu alivyomtafsiri. Muda ni jawabu. Lissu atameza haya Maneno yake.
Utoporo! Can a round peg fit in a square hole? CCM have achieved their objective: "Divide et emperor". They are all now in teeth.
 
Wewe si mwanachama wa ACT wala si Mzanzibar, unakuwaje uwe na uchungu wa kumbishia Lisu? Huoni kuwa hata wewe huna haki kama unaona Lisu hana hiyo haki? Logic yako
Mimi sijambishia mzee, yeye ndiye anayebishanana ACT-Wazalendo huku akiwa siyo mwanachama wao! Anataka kuendeleza chuki zake kwa kushindwa ucahguzi. Hamad anasema wao wanasonga mbele, yeye anataka warudi nyuma. Angalia Hama alivyosema leo

Nitoe wito kwa Wazanzibar wote wakubali kunyoosha na kupokea mkono wa maridhiano tumeze machungu yaliyotokana na uchaguzi historia yetu imejaa kila aina ya majeraha ni wakati wa kuzika historia hiyo na kushikamana kuijenga Zanzibar yetu. Maridhiano yatafungua milango ya kuwezesha Serikali kuchukua hatua ya marekebisho na kujenga upya pale palipovunjwa..., sisi viongozi tuonyeshe njia kwa wananchi wetu kwa kutibu majeraha kwa waathirika kwa kuwaonyesha kwa vitendo kwamba tunayo nia ya dhati ya maridhiano ili tujenge Zanzibar moja yenye kuheshimu haki na kulinda misingi ya demokrasia,” amesema makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
 
Back
Top Bottom