Majibu tata kutoka kwa Rais Kikwete kuhusu na Sakata la Tegeta Escrow

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,293
Wakati Raisi wetu akiwa na jopo la waandishi wa habari ikulu akiwapa habari za Ugonjwa wake pamoja na matibabu aliyoyapata akiwa nchini Marekani, kuna swali moja aliloulizwa na muandishi wa habari sijui anaandikia chombo gani cha habari, alimuuliza swali zuri sana muheshimiwa Raisi kuhusiana na sakata la Tegeta Escrwo ambalo limechukua masikio ya Watanzania wote nchini:

Aliulizwa hivi - Je muheshimiwa Raisi nini maoni yako kuhusiana na sakata linaloendelea hapa nchini kuhusiana na wizi wa mabilioni Tegeta Escrow?

Raisi akajibu hvi: Kwakweli mimi sijui kinachoendelea kwakua sikuwepo nchini!

Nitarejea!
 
Kwani ile ripoti ya CAG si ilipitia kwake akai edit ndipo ikaenda kwa PAC, Sasa hajui nn ni mwizi mkubwa.
 
Jana alikuwa anaonyesha fani yake mpya ya utabibu wa tezi dume. Niliona alikuwa anaelezea ugonjwa huo na mkurugenzi wa mawasiliano akawa anachukua notes nadhani tayari kwa kutoa tamko rasmi juu ya umahiri wa mkulu kuhusu ugonjwa huo.
 
Wakati Raisi wetu akiwa na jopo la waandishi wa habari ikulu akiwapa habari za Ugonjwa wake pamoja na matibabu aliyoyapata akiwa nchini Marekani, kuna swali moja aliloulizwa na muandishi wa habari sijui anaandikia chombo gani cha habari, alimuuliza swali zuri sana muheshimiwa Raisi kuhusiana na sakata la Tegeta Escrwo ambalo limechukua masikio ya Watanzania wote nchini:

Aliulizwa hivi - Je muheshimiwa Raisi nini maoni yako kuhusiana na sakata linaloendelea hapa nchini kuhusiana na wizi wa mabilioni Tegeta Escrow?

Raisi akajibu hvi: Kwakweli mimi sijui kinachoendelea kwakua sikuwepo nchini!

Nitarejea!

Inawezekana kweli hajui na wala hukuna cha kushangaza hapo kwa JK. Bado anasubiri aambiwe ili achanganye na zake, baadaye atawajuza watz alichoambiwa na habari itaishia hapo hapo!!
 
Huo ni upuuzi, yeye asichokijua nini kwenye hili sakata wakati kuna barua moja ya kuhimiza ulipwaji wa pesa hizo ilitoka ofisini kwake?
 
Huo ni upuuzi, yeye asichokijua nini kwenye hili sakata wakati kuna barua moja ya kuhimiza ulipwaji wa pesa hizo ilitoka ofisini kwake?
Watoto mlozaliwa kwa njia ya uzinzi mnamatatizo sana ya kiakili, kwa akili yako ya kipimbi ulitaka atoe maamuzi bila hata ya kuwa briefed na wasaidizi wake! mtaumia sana
 
Kuna mtu aliuliza hapa jukwaani kama kuna uhusiano juu ya Tezi D na Escrow.... Pengine akisogea pande hizi atatusaidia kujibu na hili
 
Ni sahihi kabisa, hawezi kujua mambo ya Escrow alikuwa busy kufanya mitihani ya mwisho ya shule ya Tezi dume :becky:
 
Bado pia nilimsikia akisema kua madaktari wake wamemshauri anatakiwa akae wiki 3 au 4 ili arejee kwenye hali yake ya kawaida kwahiyo ni kwamba Raisi bado ana Nusu Kaputi Mwilini kwahiyo kwanjia 1 au nyingine hakuwa na kumbukumbu nini kinaendelea Tanzania japokua hii issue ya Escrow dunia nzima inaielewa na Raisi wetu hajui!

Nitarejea!
 
Sio jambo la kushangaza, Rais amesema yaliyoko ndani ya moyo wake, ni kweli kwamba hajui chochote.
 
Back
Top Bottom