Majibu rasmi ya BoT juu ya nyumba ya Ndulu

You must have something wrong in your brain kufikiri kwamba a 1 million dollar (US $) house ni kitu cha kawaida kwa mtumishi wa serikali especially in TZ. In reality hata president wa Tanzania hastahili nyumba yenye gharama hiyo.

Hiyo reply ya BOT inataka kutuaminisha kwamba contractors ndio waliopanga bei, na wao wakachagua yule wa chini. Hivi yule wa chini angekuwa $5 mil. angepewa tu kwa sababu ni chini?

Halafu kwa mtu yeyote anayefahamu taratibu za tendering in TZ na tena huko huko BOT sio rahisi kuamini maelezo yao kwamba hakukuwa na michezo michafu.

Maswali ya kizushi,

1. Hii kampuni Eletrics International Co. Limited mbona imekaa kimazabemazabe well labda wadau mnaoifahamu lakini kwa sababu ni bongo si vibaya kujiuliza nio kampuni ya nani, imewahi kufanya miradi gani mingine, na hapo BOT imewahi kufanya kazi ngapi? Inaweza kuonekana ni kupersonalize the issue lakini history tells me kuna haja ya kujua.

2. Ndulu ameshahamia kwenye nyumba hiyo? Na kabla ya hapo alikuwa anakaa wapi?

3. Liyumba anayedaiwa kwamba aliidhinisha majengo pacha, hakuhusika na hii isije mwishoni mambo yakiwa moto karushiwa tena Liyumba. Mind you mradi wa karibu $450mn jamaa wamemmbebesha Liyumba wht about this $1ml?

- Mkulu Nyambala salute na hands down!

Respect
.

FMEs!
 
Rufiji,

On my posting before defending BOT descision, I had asked the same question! Suala si kula matapishi, bali ni watu kushindwa kujenga hoja na wewe kama si Wacha au yule jamaa mwingine mkadai najifanya machinoo!

Mimi nilisema, ni haki kwa BOT kujijengea nyumba, kutokana na bajeti yake, lakini hapo hapo nikauliza kwa ujumla, kwa nini mfumuko huu wa bei haudhibitiwi?

I am not a hypocrit, and I wish you extend an apology.

Go back and read the whole thread on BOT and see what I stated before kuniita mnafiki!

Reverend,

Let me be clear as I can , I still stand by everything I said and I am not going to apologize as you have requested. In fact , you are the one who should apologize for distorting my position. By the way, can you please explain to me what u' meant by :

Ndiyo maana nikasema, BOT pmoja na kupewa mtaji, wanapesa ambazo ni mapato ambazo zinawekwa katika fungu lao la bajeti na matumizi. Kama taasisi zingine, nao wanamakato ambayo yanakwenda hazina na salio ni lao.

Sawsa kama wametumia salio lao kutoa mikopo kwa wafanyakazi wao, kujenga nyumba mpya, kuongeza mishahara na kununua magari, tatizo liko wapi?

Au tunataka tuanze kusema kila senti itumike kununulia dawati na kisima cha maji? kama ni hivyo, mbona hatuidai CCM iliyonunua magari 200 kutoka Japan na kusema fedha hizo zingetosha kuweka visima na pampu kila kata kijiji Tanzania?

Kwenye hili la ujenzi wa hizi nyumba, hakuna hata mmoja anayeangalia ni gharama gani za kujenga nyumba zilivyo Tanzania na ni jinsi gani uholela wa bei za viwanja na ardhi ulivyo.
 
Hiyo reply ya BOT inataka kutuaminisha kwamba contractors ndio waliopanga bei, na wao wakachagua yule wa chini. Hivi yule wa chini angekuwa $5 mil. angepewa tu kwa sababu ni chini?

Ni kweli wanatuona wote mbumbumbu kwenye tenda si lazima uchukue bei ya chini unaangalia pia ubora hii nafikiri ilishapangwa tuwaambie hivi ili waone wanatumia vizuri pesa za serikali, nonsense.
 
Mie statement hii tu imenichafua
"GAVANA WA Benki Kuu na manaibu wake kwa mujibu wa mikataba ya kazi zao, wanastahili kupewa nyumba ya kuishi kila mmoja."

Hivi niulize waungwana yupi anastahili kupewa nyumba bank officer wa BOT aliyeajiriwa akiumwa na nge (risks) kila siku katika kazi zake au yule aliyeteuliwa ambaye risk yake ni collective risk ambapo watu wa chini wanafanya kazi yeye anafanya maamuzi tu!!!!

Adios

Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote but mh!!!!!! kwa staili hii si mchezo!!!
 
MASWALI YA LULA WA NDALI (RAIA MWEMA)

8.Swali la mwisho ambalo ningependa kujua jibu lake ni kwa Gavana Ndulu kutuhalalishia kwa nini Gavana wa Tanzania akae kwenye jumba lenye gharama inayoshinda jumba la Gavana wa Benki Kuu ya Marekani, taifa kubwa zaidi lenye uchumi mkubwa na lenye matatizo ya kiuchumi ya kutosha tu?

Swali hilo hapo juu hata mimi nimekuwa nikiliuliza. Hivi Beno Ndulu alizaliwa wapi na kukulia wapi ambako watu washindwe kutambua hali ya maisha ya watanzania walio wengi? Jeuri hiyo ya kuruhusu fedha nyingi hivyo kutumia kujengea nyumba moja ya kuishi familia moja tena itaendelea kutumia fedha za walipa kodi kuitunza na mengineyo (gharama zilizotajwa ni sh. bilioni 1.3 kwa nyumba moja)?

Ndulu anataka kutuaminisha nini anaposema maamuzi ya ujenzi wa nyumba hizo ulitolewa akiwa hajateuliwa kuwa Gavana wa BOT? Anataka tuamini kwamba angekuwepo kabla ya maamuzi angekataa? Ninavyojua BOT ni Taasisi, hivyo alivyoingia tu kama kulikuwa na maamuzi yaliyotangulia kabla hajateuliwa na yalikuwa kinyume cha taratibu si angeyatengua? Sijaona kwa nini Beno Ndulu atuambie habari za kutokuwepo BOT wakati maamuzi ya ujenzi yanatolewa. Ndiyo kawaambia hao waliotoa maelezo hayo ya BOT waseme yeye hakuwepo? Kama ndivyo, umma uondoke na nini katika kipengele hicho? Kwamba Ndulu hahusiki? Ama ni nini hasa nia ya kutueleza kwamba yeye hakuwepo?

Cha kushangaza, maelezo yanasema kwamba wakati anajiunga BOT hatua za awali za ujenzi zilikuwa zimeshaanza. Hapo napo tuamini nini? Kwamba asingeweza kuzuia ujenzi au wanajaribu kutuaminisha nini sisi?

Kifupi Bwana Ndulu na timu yake wamefuja mali ya umma, na binafsi nashauri tu ajiuzulu maana hiyo ni kashfa. Ulishaona wapi Tanzania na hali ya uchumi wake huu tulio nao tujenge nyumba ya kuishi mtumishi kwa gharama ya zaidi ya bilioni moja jamani?

Bajeti yetu kila mwaka tunaokoteza maana huwa tuko na mapungufu katika makusanyo ya mapato yetu ikilinganisha na mahitaji kwa mwaka. Hivyo, Serikali hulazimika kuwalilia wahisani (nchi za Kaskazini) kutujazia pengo la bajeti yetu; pamoja na mazingira hayo anatokea mtu mmoja tu na wenzake eti wanafanya makubaliano yakujenga nyumba kwa kiasi hicho cha fedha!!

BOT hao hao wakiwa wasimamizi wa uchumi wa jumla wa nchi yetu, wanapitisha azimio la kupeana mikopo mikubwa kiasi cha kushangaza. Hivi wao ndiyo pekee watumishi wa umma? Si huku ni kuongeza pengo kati ya wasio nacho na wenye nacho? Kwa nini taasisi hiyo muhimu na yenye kutia chachu maendeleo ya nchi inaendeshwa kama familia fulani hivi? Wakuu wanaowajibika na usimamizi wa matumizi ya fedha za umma (Wizara ya fedha na uchumi) wako wapi hadi haya yote yanatokea?

Mimi siamini eti Ndugu Mukulo alikuwa hajui BOT kutumia fedha nyingi kiasi hicho hadi juzi ndipo kafahamu hivyo. Mbona wanalazimisha sisi wananchi kutuaminisha kwamba Serikali inafanya mambo kama maigizo hivi? Inakuwaje Waziri anayesimamia fedha za umma asijue tena Wakala wa Serikali aliye chini yake (Agency-BOT) ametumia fedha hizo pasipo ulazima wowote wa kufanya hivyo? Hivi Mukulo anapotuambia kwamba Serikali imeshangazwa kusikia matumizi hayo ya fedha anataka tuamini nini? Anaposema anafanya uchunguzi wa uhalali wa matumizi hayo ya fedha za umma, je anafikiri ni halali kutumia sh. bilioni 1.3 kujenga nyumba moja ya kuishi mtumishi wa umma, kiasi cha yeye kusema tu anaangalia uhalali wa matumimizi hayo. Hapo haihitaji hata uchunguzi, maana Kama waziri wa fedha anao uzoefu wa kutosha kabisa kuhusiana na ujenzi wa miradi ya nyumba nchini. Sasa hapo achunguze nini? Ama ni kwenda kujiandaa kuja kudanganya umma ili unyamazie ufujaji wa mali za umma wa namna hiyo?

Hayo ni maswali ya nyongeza kwenye maswali yaliyotangulia kuulizwa na mtoa thread hii! Tusubiri majibu na nyongeza ya maswali ya wadau wa JF!!!
 
Hawawezi kufahamu yanayotokea kwenye Benki Kuu lakini anayosema Yahaya watayajibu within hours.
 
Ni kweli wanatuona wote mbumbumbu kwenye tenda si lazima uchukue bei ya chini unaangalia pia ubora hii nafikiri ilishapangwa tuwaambie hivi ili waone wanatumia vizuri pesa za serikali, nonsense.

Wanajaribu kuyazoa maziwa yaliyokwishamwagika. Serikali kupitia Mkulo eti yadai imeshtushwa na matumizi hayo makubwa ya BOT huku BOT yenyewe ikijikanyagakanyaga kwa maelezo hafifu. Nilisema mwanzoni kabisa kuwa Prof. katika haraka yake ya kujibu mapigo, amefungua pandora box na mpaka sasa tunachoshuhudia ni just the tip of an iceberg. Mbinu na timu zilizowezesha EPA bado ziko pale pale intact ukiacha ya watu wawili watatu kutolewa kafara na wengine kuongezewa ulaji. BOT na TANESCO ni miongoni vya visima ambako CCM inachota hela, tena hiyo hela inachotwa kwa jeuri ya kutisha - ukihoji umekwisha, na wengi wamepoteza maisha (RIP)
 
- Nilisema huko nyuma kuwa mengine tunajitakia wenyewe, yaani huyu Ndulu amefanya kazi na Mama Meghji, Mramba, yona, Nyirabu, Balali, mpaka Liyumba sasa kelele za nini jamani mbona tunataka kuonea buji huku tunajua gombe ni nani?

- Nani aliyempa kazi ya ugavana Ndulu in the first place? Hii ndio michirizo ya EPA, Kagoda na the rest sasa tuone mwenye ubavu amguse kama hakutoa siri na huku uchaguzi umefika, kila kona imejaa mijizi tu! siku moja tutaamka asubuhi na kukuta hakuna serikali yote imeibiwa!

Respect.

FMEs!
 
Patamu hapo hakuna wa kumgusa Ndullu au ataamua kulonga...Huyu alikuwepo wakati wa wizi wa EPA na Twin Towers hivyo na yeye utendaji wake hakustahili kupewa nafasi hiyo lakini bado aliteuliwa, sasa na yeye kaamua kuonyesha makucha yake ya kifisadi kwa kujenga nyumba mpya wakati ile ya Gavana ilikuwepo tena na hadhi nzuri kabisa. Kapitisha mikopo hadi milioni 100 kwa maafisa wa juu...Kweli Tanzania imeoza!
 
Kama ataweza hata kuelewa bilioni moja ni nini! Wengi hesabu zetu zinaishia milioni na huko vijijini laki moja! Labda uwaeleze ni laki moja 10,000!

Amandla.......
Teh, teh haaaahhh!!
Kweli wazee! Tunalazimika kucheka hata mahali penye kuuma; najitahidi kupunguza hasira zangu juu ya maamuzi ya wakubwa hao wa BOT! Kijini wapi mtu akajua hesabu ya bilioni moja? Ni ajabu akina Ndulu kutungua pesa za wazee wetu kirahisi kiasi hicho! Sijui Ndulu na wenzake walizaliwa na kulelewa wapi kiasi cha kuwa na ujasiri huo wa kukataa nyumba eti kwa sababu tu haina bwawa la kuongelea. Kwa maana nyingine ni kwamba, nyumba isiyokuwa na bwawa la kuogelea iliachwa na kusababisha kujengwe nyingine yenye bwawa kwa gharama ya sh. bilioni 1.3! Haki hiyo jamaani??

Mbona tunafanywa vilaza kiasi hicho? Hawana aibu hata kutoa maelezo yao hayo yenye hoja dhaifu kuyaleta kwa umma kufafanua ubadhilifu wao mkubwa katika kutumia fedha za umma!
 
Patamu hapo hakuna wa kumgusa Ndullu au ataamua kulonga...Huyu alikuwepo wakati wa wizi wa EPA na Twin Towers hivyo na yeye utendaji wake hakustahili kupewa nafasi hiyo lakini bado aliteuliwa, sasa na yeye kaamua kuonyesha makucha yake ya kifisadi kwa kujenga nyumba mpya wakati ile ya Gavana ilikuwepo tena na hadhi nzuri kabisa. Kapitisha mikopo hadi milioni 100 kwa maafisa wa juu...Kweli Tanzania imeoza!

- Mkulu please, uliza mtu yoyote wa serikali jinsi ilivyokuwa kivumbi kwa Nyirabu kukubaliwa na US kua balozi wetu kule DC, wanyamwezi walitaka maelezo ya kina kuhusu kuungua kwa BOT na hasa section ya mafaili ama sivyo wasingemkubali aende kule waligoma kata kata kuwa hawawezi kupokea utambulisho wake, ikabidi kuwabembeleza na kuwalipa sana kina Andrew Young na Jesse Jackson waingilie kati ndio Nyirabu akakubaliwa kwenda,

- Lakini ilikuwa ni aibu ya mwaka, yaani serikali ya nje inakuwa concerned na ubovu wa kiongozi wetu kuliko sisi wenyewe, sasa kavbla hujamaliza kushangaa ya musa ndio unakuja kupigwa na haya ya firauni pumbavu kabisaa, I mean baada ya EPa na Kagoda, ilitakiwa kuondoa uozo wote huko BOT hawa kina Ndulu wote ni masalia ya mijizi tu iliyokubuhu sasa finally limeshikwa hands down halina hata pa kutokea, sasa jiulize huko nyuma limeiba hela ngapi?

- I mean don't give me this nonsense kwamba huu ndio wizi wake wa kwanza, ukishika mwizi ujue ndio kwanza ameshikwa lakini sio mara ya kwanza kumbuka Tiger Woods! Haya majizi ya hela za wananchi kule U-China hayana nafasi katika jamii, guess huwa wanayafanya nini? Garademiti! Umesikia juzi walivyomfanya muingereza waliyemkamata na kuuza unga hawana masihara eti!

- Huyu Ndulu ingekwua huko China, saa hizi tungekwua tunaongea mengine!

Respect.

FMEs!
 
Muda mrefu sijaweka michango yangu lakini hii sasa too much!

1.nyumba ya hiyo hapo pichani kama haina dhahabu ndani ni ngumu kugharimu $1M hizi ni pesa nyingi watanzania,kwa pesa hiyo ikizingatiwa zimejengwa na serikali ile wanayosamehewa kila kodi pale bandarini pia zimejengwa wakati kwa mkupuo ilitakiwa isizidi $500,000.kuonesha hivyo nitaweka experience yangu hapa ukumbini.

may mwaka tumekamilisha ujenzi wa nyumba kubwa zaidi ya hiyo (or better).total costs at around $450,000

ilijengwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.

ufuatao ni mchanganuo wa gharama kwa upesi-upesi ili muone vitu vinavyo-maliza fedha kwenye ujenzi.gharama nyingi ziko rounded to the nearest thousand,ule ufisadi wa kuweka 13,298,241.32 siupendi unaumiza macho watu tu!
kiwanja

plot purchased at $10,000.obviously purchased 10 years ago!
pre-building consultancy was done at roughly $5,000

Total area Main house area stands at 480sqm.

rooms were 7.,1 master bedroom,1 guest room 4 normal rooms,1 spare room(later converted to mini home theater).all rooms were equipped with AC,Bathrooms,walk in closets.

also included was a 70sqm servant quarters+50sqm fully equipped garage.

sasa turudi kwenye proces nzima.

nyumba ilijengwa through hatua kuu kama 5 hivi kufuatana na funds na mahitaji.

Hatua ya kwanza.($162,000)
1.msingi na ukuta wa nje(total costs $25,000)
2.kupandisha juu-matofali na Kuezeka vigae(total costs($45,000)
3.madirisha na milango(nyumba ina milango 20 costing $20,000).Madirisha 35(costing $32,000).
4.mabomba+wiring+electric installations+100kW generator(alone cost $27,000),total was $40,000

Hatua ya pili.($135,000)

1.finishing,imported tiles ($50 per sqm*600sqm=$30,000)+fees za wale wazulumaji wa bandarini na transport(almost $20,000)+total $50,000.
2.Imported Sanitary tools(sinks,Jacuzzi,etc)-total cost=$30,000.it was a total of 10 washroom sinks(@$500),5 kitchen sinks(@$500)10 shower systems,10 toilet sets and other minor sanitary things.add up shipping feees and again jamaa bandarini.
3.kitchen cabinets+closets instalations(material sourced locally & abroad)-cost for 3 cabinets(1 big=,1 medium=and 1 small) was $20,000.costs for 7 walk in closets was $10,000.
4.Kuviweka hivyo hapo juu we had a courtesy of personal professional installation from the companies we bought the things(only $15,000 for their personnel including round-trip ticket and other minor costs)

Hatua ya tatu($20,000)
1.Paintwork and decorations-it involved lights fixtures,paint and minor decors(costs were $20,000

Hatua ya nne($110,000)
1.Home electronics,
2 Two Multi door GE fridges($10,000),kitchen appliances(microwaves,ovens,hoods,etc)-$5000,4 plasma sets ($20,000).2 Bose Home theater system ($20,000),Sony Projector +Sound system set($12,000).5 AC at $8000
2.Security system+home server+3 computer sets ($18,000).
3.Home furniture for the whole house,10 beds,2 sofa sets,2 dining tables sets+curtains an all (sikumbuki details lakini it was in the neighbourhood of $36,000)
4.garage doors+motor+control System($8,000)

Hatua ya Tano (almost $6,000)
1.Landscaping,sorry watanzania,had to hire a college buddy to do this,this Italian is fantastic.as a friend had to part away with $6,000.

Trip za hapa na kule,nchini na nje katika muda wote wa ujenzi=$15,000

Total estimated was $450,000.makorokoro mengine nimesahau hela zilikopotelea..,mliojenga mwalijua hilo!BUT we end up spending more than $480,000.

kwa hiyo nyumba ya Gavana HAPO JUU ku-cost $1M NAKATAA KATA KATA.unless they provide a very detailed account as to why all that money was spent in such a regular house.

GAVANA,PROF.NDULU hizo pesa zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi nyingi zimeliwa!!!sema ukweli,come clean before you force Tanzanians to come all out on you!!
 
Beijing defends execution of corrupt officials

BEIJING — Execution for corruption is proportionate and accords with "China's national condition," a senior official said Thursday, as a disgraced former party chief from Shanghai, now confirmed to be behind bars, awaits trial.

The ruling Communist Party has vowed to root out corrupt officials before a key congress later this year to ensure that tainted members cannot rise any further. It has warned that the problem is so severe it may threaten the party's rule.

Last month, the former head of the Chinese food and drug safety watchdog, Zheng Xiaoyu, was put to death for corruption amid a series of health scares concerning Chinese products.

"As for the death penalty, different countries have different situations and different cultural backgrounds," Gan Yisheng, head of the party's Central Commission for Discipline Inspection, said at a news conference.

"We still execute people who have committed serious economic crimes on consideration of China's national condition and cultural background. I don't think we can be criticized for this," Gan said. Zheng was put to death for the "serious nature" of his crimes, he added.

China does not publish execution figures, but human rights groups estimate that they number from about 5,000 to 12,000 annually. Corruption has become rampant since market reforms opened the economy in the 1980s. Chen Liangyu was toppled from his post as the head of the Communist Party in Shanghai last September after an official investigation into the misuse of money in the city's social security fund.
Last week, he was formally expelled from the party and handed over to the judicial authorities.

Gan did not say when Chen would be tried, indicating only that he was in detention and in good health.
"It's up to the legal authorities to decide when he will be brought to trial," he said. "According to the law, it does not matter who you are, once you've been handed over to the law, you'll be held in detention. Chen Liangyu is of course not immune."

Chen was the first member of the party's elite Politburo to be purged for corruption since 1995. A dozen other officials and businessmen have since been implicated by the inquiry. Gan defended the Chinese system where members are investigated by the party internally and may be punished by it with little or even no consultation with the legal authorities.

"To say China has two types of laws is biased, and is a distorted understanding of Chinese law," he said.

- Tizama watu walio serious hawa hawana mchezo huko hawa kina Ndulu wataendelea kutusumbua tu hapa bongo na hawa viongozi wetu tunaoita watu wa watu, ulisikia walivyomfanya Rais wao aliyekua mtu wa watu kule Indonesia, mpaka leo anasota jela!

Respect.

FMEs!
 
Hivi bado waziri wa fweza na katibu wake mkuu pamoja na Gavana bado wana kazi 2010? Just asking?

Wabunge eeeeeeeeeeeeeeee mko wapi jamani?
 
Watanzania wajue wanaibiwa.HUYU NDULU with his $15K salary could afford a $300,000 without hurting a muscle,since he has a free ride,and paid up bills.his salary is virtually spent on minor issues.

KWA NINI AWABEBESHE MZIGO HUU watu wenye per capita GDP chini ya $2000 kwa mwaka?!this i can't understand.
 
Teh, teh haaaahhh!!
Kweli wazee! Tunalazimika kucheka hata mahali penye kuuma; najitahidi kupunguza hasira zangu juu ya maamuzi ya wakubwa hao wa BOT! Kijini wapi mtu akajua hesabu ya bilioni moja? Ni ajabu akina Ndulu kutungua pesa za wazee wetu kirahisi kiasi hicho! Sijui Ndulu na wenzake walizaliwa na kulelewa wapi kiasi cha kuwa na ujasiri huo wa kukataa nyumba eti kwa sababu tu haina bwawa la kuongelea. Kwa maana nyingine ni kwamba, nyumba isiyokuwa na bwawa la kuogelea iliachwa na kusababisha kujengwe nyingine yenye bwawa kwa gharama ya sh. bilioni 1.3! Haki hiyo jamaani??

Mbona tunafanywa vilaza kiasi hicho? Hawana aibu hata kutoa maelezo yao hayo yenye hoja dhaifu kuyaleta kwa umma kufafanua ubadhilifu wao mkubwa katika kutumia fedha za umma!

Na ukitaka wakuelewe zaidi uwaambie kuwa kila mtu anayeishi (baba,mama, watoto,wajukuu n.k.) kwenye kijiji hicho pamoja na kila kuku, bata, mbuzi na ng'ombe watakatiwa sh. laki moja kila mtu na zitabaki za kuwawekea mabati kwenye shule na kliniki yao!

Amandla.......
 
Muda mrefu sijaweka michango yangu lakini hii sasa too much!

1.nyumba ya hiyo hapo pichani kama haina dhahabu ndani ni ngumu kugharimu $1M hizi ni pesa nyingi watanzania,kwa pesa hiyo ikizingatiwa zimejengwa na serikali ile wanayosamehewa kila kodi pale bandarini pia zimejengwa wakati kwa mkupuo ilitakiwa isizidi $500,000.kuonesha hivyo nitaweka experience yangu hapa ukumbini.

may mwaka tumekamilisha ujenzi wa nyumba kubwa zaidi ya hiyo (or better).total costs at around $450,000

ilijengwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.

ufuatao ni mchanganuo wa gharama kwa upesi-upesi ili muone vitu vinavyo-maliza fedha kwenye ujenzi.gharama nyingi ziko rounded to the nearest thousand,ule ufisadi wa kuweka 13,298,241.32 siupendi unaumiza macho watu tu!
kiwanja

plot purchased at $10,000.obviously purchased 10 years ago!
pre-building consultancy was done at roughly $5,000

Total area Main house area stands at 480sqm.

rooms were 7.,1 master bedroom,1 guest room 4 normal rooms,1 spare room(later converted to mini home theater).all rooms were equipped with AC,Bathrooms,walk in closets.

also included was a 70sqm servant quarters+50sqm fully equipped garage.

sasa turudi kwenye proces nzima.

nyumba ilijengwa through hatua kuu kama 5 hivi kufuatana na funds na mahitaji.

Hatua ya kwanza.($162,000)
1.msingi na ukuta wa nje(total costs $25,000)
2.kupandisha juu-matofali na Kuezeka vigae(total costs($45,000)
3.madirisha na milango(nyumba ina milango 20 costing $20,000).Madirisha 35(costing $32,000).
4.mabomba+wiring+electric installations+100kW generator(alone cost $27,000),total was $40,000

Hatua ya pili.($135,000)

1.finishing,imported tiles ($50 per sqm*600sqm=$30,000)+fees za wale wazulumaji wa bandarini na transport(almost $20,000)+total $50,000.
2.Imported Sanitary tools(sinks,Jacuzzi,etc)-total cost=$30,000.it was a total of 10 washroom sinks(@$500),5 kitchen sinks(@$500)10 shower systems,10 toilet sets and other minor sanitary things.add up shipping feees and again jamaa bandarini.
3.kitchen cabinets+closets instalations(material sourced locally & abroad)-cost for 3 cabinets(1 big=,1 medium=and 1 small) was $20,000.costs for 7 walk in closets was $10,000.
4.Kuviweka hivyo hapo juu we had a courtesy of personal professional installation from the companies we bought the things(only $15,000 for their personnel including round-trip ticket and other minor costs)

Hatua ya tatu($20,000)
1.Paintwork and decorations-it involved lights fixtures,paint and minor decors(costs were $20,000

Hatua ya nne($110,000)
1.Home electronics,
2 Two Multi door GE fridges($10,000),kitchen appliances(microwaves,ovens,hoods,etc)-$5000,4 plasma sets ($20,000).2 Bose Home theater system ($20,000),Sony Projector +Sound system set($12,000).5 AC at $8000
2.Security system+home server+3 computer sets ($18,000).
3.Home furniture for the whole house,10 beds,2 sofa sets,2 dining tables sets+curtains an all (sikumbuki details lakini it was in the neighbourhood of $36,000)
4.garage doors+motor+control System($8,000)

Hatua ya Tano (almost $6,000)
1.Landscaping,sorry watanzania,had to hire a college buddy to do this,this Italian is fantastic.as a friend had to part away with $6,000.

Trip za hapa na kule,nchini na nje katika muda wote wa ujenzi=$15,000

Total estimated was $450,000.makorokoro mengine nimesahau hela zilikopotelea..,mliojenga mwalijua hilo!BUT we end up spending more than $480,000.

kwa hiyo nyumba ya Gavana HAPO JUU ku-cost $1M NAKATAA KATA KATA.unless they provide a very detailed account as to why all that money was spent in such a regular house.

GAVANA,PROF.NDULU hizo pesa zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi nyingi zimeliwa!!!sema ukweli,come clean before you force Tanzanians to come all out on you!!

Mimi hapa ndipo ninaposhindwa kuelewa. Nyumba ya $450,000 kweli unawakatia waliokutayarishia michoro, mahesabu ya nguzo n.k ka measly $5,000? Yaani hawa jamaa gharama yao ni sawa na jokofu na pungufu ya mlango wa gereji! Bila shaka mafundi walilamba zaidi ya hii maana naona watalamu wa kazi tamu uliwaachia zaidi ya $20,000!

Inasikitisha lakini ndivyo ilivyo. Wataalamu wanaothaminiwa bongo ni madaktari (ukifanya mchezo unaondoka) na mawakili ( ukifanya mchezo utajisaidia kwenye ndoo.) tuu!

BTW Tanzania GDP per capita (2007) ilikuwa ni $369.7. ref:

http://data.un.org/CountryProfile.aspx?crName=United%20Republic%20of%20Tanzania

$ 2000 hatujawahi kugusa. GDP per capit (PPP) ni kama $1,300 tu!

Amandla......
 
Haya jamani tumuombe mwenyezi mungu aturehemu watanzania na viongozi wetu mwaka 2010 ujinga na upumbavu utuondoke.

Vichekesho!! Yaani kuna watu wazima eti wanasema hizo fedha si za serikali ni za BOT, ambako zimepatikana kwenye biashara za BOT. Sasa owner wa BOT ni nani?? Si serikali ya jamhuri??

wakati mabilioni yakitumika kwa nyumba mbili, in parallel serikali yetu hii kwenye hospitali kubwa ya mkoa yafanya hivi:::::

Ndesamburo aipiga jeki hospitali ya Mawenzi

na Grace Macha, Moshi

WODI ya wazazi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi inakibiliwa na uhaba wa nafasi na vifaa hali inayohatarisha afya za wajawazito na wale waliokwishajifungua.

Hayo yalielezwa jana kwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo wakati alipoenda hospitalini hapo kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya ambapo alitoa mashuka 200 na viti 10 vya kubebea wagonjwa vyenye magurudumu manne. Pia alikabidhi mashuka 200 na viti vya kusukuma 10 kwenye vituo vya afya vya Majengo na Pasua vyote vikiwa na thamani ya sh milioni 5.

Muuguzi kiongozi wa wodi hiyo, Kandida Mafoi alimweleza mbunge huyo kuwa kwa sasa wanakabiliwa na uhaba wa vitanda hali inayowalazimu kuwalaza kinamama waliojifungua wawili mpaka watatu pamoja na watoto wao kwenye kitanda kimoja.

Alisema uhaba huo wa vitanda umekuwa ukiwalazimu kuwaruhusu mapema hata kabla ya kutimiza muda unaoshauriwa kitaalam unaowataka kukaa chini ya uangalizi wa wauguzi kwa saa 24.

Mafoi alisema hata kwenye chumba maalum cha kujifungulia, pia si salama kwani hakuna hewa ya kutosha kutokana na udogo wa chumba kwani kuna vitanda vinne maalum kwa ajili ya kuzalishia.
Mbunge huyo alishuhudia wengi wa kinamama hao wakiwa wamelala wawili kwenye kitanda kimoja ambavyo vingi havikuwa vimetandikwa mashuka, huku vifaa vyao vikiwa vimehifadhiwa madirishani.
Mafoi alisema pia wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa vifaa vya kufanyia usafi ikiwemo sabuni.
 
Muda mrefu sijaweka michango yangu lakini hii sasa too much!

1.nyumba ya hiyo hapo pichani kama haina dhahabu ndani ni ngumu kugharimu $1M hizi ni pesa nyingi watanzania,kwa pesa hiyo ikizingatiwa zimejengwa na serikali ile wanayosamehewa kila kodi pale bandarini pia zimejengwa wakati kwa mkupuo ilitakiwa isizidi $500,000.kuonesha hivyo nitaweka experience yangu hapa ukumbini.

may mwaka tumekamilisha ujenzi wa nyumba kubwa zaidi ya hiyo (or better).total costs at around $450,000

ilijengwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.

ufuatao ni mchanganuo wa gharama kwa upesi-upesi ili muone vitu vinavyo-maliza fedha kwenye ujenzi.gharama nyingi ziko rounded to the nearest thousand,ule ufisadi wa kuweka 13,298,241.32 siupendi unaumiza macho watu tu!
kiwanja

plot purchased at $10,000.obviously purchased 10 years ago!
pre-building consultancy was done at roughly $5,000

Total area Main house area stands at 480sqm.

rooms were 7.,1 master bedroom,1 guest room 4 normal rooms,1 spare room(later converted to mini home theater).all rooms were equipped with AC,Bathrooms,walk in closets.

also included was a 70sqm servant quarters+50sqm fully equipped garage.

sasa turudi kwenye proces nzima.

nyumba ilijengwa through hatua kuu kama 5 hivi kufuatana na funds na mahitaji.

Hatua ya kwanza.($162,000)
1.msingi na ukuta wa nje(total costs $25,000)
2.kupandisha juu-matofali na Kuezeka vigae(total costs($45,000)
3.madirisha na milango(nyumba ina milango 20 costing $20,000).Madirisha 35(costing $32,000).
4.mabomba+wiring+electric installations+100kW generator(alone cost $27,000),total was $40,000

Hatua ya pili.($135,000)

1.finishing,imported tiles ($50 per sqm*600sqm=$30,000)+fees za wale wazulumaji wa bandarini na transport(almost $20,000)+total $50,000.
2.Imported Sanitary tools(sinks,Jacuzzi,etc)-total cost=$30,000.it was a total of 10 washroom sinks(@$500),5 kitchen sinks(@$500)10 shower systems,10 toilet sets and other minor sanitary things.add up shipping feees and again jamaa bandarini.
3.kitchen cabinets+closets instalations(material sourced locally & abroad)-cost for 3 cabinets(1 big=,1 medium=and 1 small) was $20,000.costs for 7 walk in closets was $10,000.
4.Kuviweka hivyo hapo juu we had a courtesy of personal professional installation from the companies we bought the things(only $15,000 for their personnel including round-trip ticket and other minor costs)

Hatua ya tatu($20,000)
1.Paintwork and decorations-it involved lights fixtures,paint and minor decors(costs were $20,000

Hatua ya nne($110,000)
1.Home electronics,
2 Two Multi door GE fridges($10,000),kitchen appliances(microwaves,ovens,hoods,etc)-$5000,4 plasma sets ($20,000).2 Bose Home theater system ($20,000),Sony Projector +Sound system set($12,000).5 AC at $8000
2.Security system+home server+3 computer sets ($18,000).
3.Home furniture for the whole house,10 beds,2 sofa sets,2 dining tables sets+curtains an all (sikumbuki details lakini it was in the neighbourhood of $36,000)
4.garage doors+motor+control System($8,000)

Hatua ya Tano (almost $6,000)
1.Landscaping,sorry watanzania,had to hire a college buddy to do this,this Italian is fantastic.as a friend had to part away with $6,000.

Trip za hapa na kule,nchini na nje katika muda wote wa ujenzi=$15,000

Total estimated was $450,000.makorokoro mengine nimesahau hela zilikopotelea..,mliojenga mwalijua hilo!BUT we end up spending more than $480,000.

kwa hiyo nyumba ya Gavana HAPO JUU ku-cost $1M NAKATAA KATA KATA.unless they provide a very detailed account as to why all that money was spent in such a regular house.

GAVANA,PROF.NDULU hizo pesa zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi nyingi zimeliwa!!!sema ukweli,come clean before you force Tanzanians to come all out on you!!
Pangupakavu,
BOT haikununua hivyo viwanja. Ilipewa bure na serikali ya Tz kama ilivyo wizara yeyote au idara ya serikali.
 
--------------------------------------

MAJIBU YA HOJA ZA LULA KUTOKA BENKI KUU

TAARIFA KWA UMMA

BOTgoldLogo10.jpg

TAARIFA KUHUSU UJENZI WA MAKAZI YA VIONGOZI WAKUU WA BENKI KUU YA TANZANIA

GAVANA WA Benki Kuu na manaibu wake kwa mujibu wa mikataba ya kazi zao, wanastahili kupewa nyumba ya kuishi kila mmoja. Hapo awali Gavana alikuwa anaishi Barabara ya Mahando kiwanja namba 387Masaki na Naibu Gavana Barabara ya Msese kiwanja Namba 43.

Awali Benki Kuu ilikuwa na viongozi wakuu wawili, Gavana na Naibu wake mmoja. Baada ya mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2006, Benki Kuu ina viongozi wakuu wanne; Gavana na Manaibu wake watatu. Kila mmoja wao, kwa mikataba iliyowekwa anastahili kupata nyumba ya kuishi.

Mwaka 2006, kabla ya uteuzi wa viongozi wa sasa wa juu, Benki Kuu ilifanya uamuzi wa kujenga nyumba mbili zaidi kwa makazi ya viongozi walioongezeka. Iliamuliwa nyumba hizi zijengwe kiwanja namba 57 Barabara ya Mtwara Crescent na kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe maeneo ya Oysterbay.Viwanja vyote viwili vilikuwa ni mali ya Benki Kuu vilivyokuwa na magofu yaliyopigwa marufuku kuishi wanadamu (condemned).

Timu ya wataalamu waelekezi ikiongozwa na M/S SKY Architects Consultants iliajiriwa kutengeneza michoro na ramani za nyumba hizo. Michoro miwili ilichaguliwa, moja kwa kila nyumba ili wataalamu hao watengeneze ramani kamili ya ujenzi. Nyumba zote mbili zilipangwa ziwe za ghorofa moja, vyumba vitano vya kulala, wenyeji na wageni, sebule ya wageni, sebule ya familia, mahali pa kulia na vyoo na mabafu yanayoendana na idadi ya vyumba. Majengo ya nje ni pamoja na nyumba ya kuishi watumishi, gereji ya magari, bwawa dogo la kuogelea, ukuta na vyombo vya usalama na kibanda cha walinzi.

Huduma zilizogharimiwa katika ujenzi wa nyumba hizi ni pamoja na mashine ya umeme (generator), mashine ya kupoza hewa na matenki ya kuhifadhi maji. Wakati huohuo, shughuli zingine zilizofanyika ilikuwa ni kutengeneza mahali pa kuegesha magari pamoja na bustani.

Wataalamu hawa baada ya uchoraji huu walifanya tathmini ya vifaa vinavyohitajika na maelekezo kwa wazabuni ili itumike kualika zabuni. Taratibu zote za manunuzi zilifuata sheria ya manunuzi katika kuwaalika wazabuni na kuteua wakandarasi. Kila nyumba ilikuwa ni mradi unaojitegemea na kila moja ilifanyiwa zabuni peke yake.

Izingatiwe kuwa ujenzi wa nyumba hizi ulipangwa na kuamuliwa kabla ya uteuzi wa Profesa Benno Ndulu kujiunga na Benki Kuu Septemba 2007.

Tangazo la kuwaalika wazabuni kwenye kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe lilichaapishwa katika gazeti la Daily News la Februari 26,2008. Wakandarasi wote wa daraja la pili au la juu zaidi walialikwa kuwasilisha zabuni na walitakiwa kulipa ada ya shilingi 50,000. Wakandarasi 12 walituma maombi na kuchukua hati za zabuni.Lakini kati ya hao 10, waliwasilisha maombi yao kabla ya kufikia tamati ya kupokelewa maombi hayo Machi 25,2008.

Zabuni hizi zilifunguliwa na Bodi ya Zabuni ya Benki Kuu na kufanyiwa tathimini ikishirikisha mtaalamu mwelekezi wa mradi huo na Idara ya Miliki ya Benki Kuu. Mapendekezo kutoka kwa wakandarasi yalikuwa na viwango vya gharama kuanzia Shilingi 1,399,184,549.00 hadi shilingi 1,847,763,537.00 kwa kiwango cha juu. Baada ya tathmini ya zabuni hizo na kufanya masahihisho ya tarakimu zilizowasilishwa, mzabuni aliyeshinda kwa kuwa na gharama ya chini kuliko wote alikuwa ni M/S Eletrics International Co. Limited. Gharama yake baada ya masahihisho ilikuwa ni Shilingi 1,274,295,025.26.

Taarifa ya tathimini hiyo ilipitia tena kwenye Bodi ya Wazabuni na ndipo ilipofikia uamuzi wa kumteua M/S Eletrics International Co. Limited kwa bei ambayo haitabadilika (fixed price) ya Shilingi 1,274,295,025.26 ya kukamilisha ujenzi huu katika wiki 32.Mkataba wa ujenzi na mkandarasi huyo ulitiwa sahihi Juni 03,2008 na kazi ya ujenzi ikaanza mara moja. Mkandarasi huyu aliteuliwa na Bodi Zabuni (DSM) ya Benki Kuu ikaridhia kuwa M/S Remco (International) Limited ishughulikie maswala aya vipoza hewa; M/s Ginde EAP Services Ltd ishughulikie maswala ya maji safi, mabomba na maji taka na M/s Pomy Engineering Co.Ltd ishughulikie maswala ya umeme. Makampuni yote hayo yamesajiliwa Tanzania.

Wazabuni wa nyumba Namba 57 Mtwara Crescent nao pia walialikwa kwa mfumo huohuo wa ushindani wakianza na wakandarasi watano (5) ambao waliwasilisha maombi yao na kuishia na uteuzi wa M/s Holtan Builders Ltd ambayo gharama yake ya Shilingi 1,272,348,512.00 (fixed price) ilikuwa ni ya chini kuwashinda wengine na makubaliano ya kukamilisha ujenzi katika muda wa wiki 24. Mkandarasi huyo alitumia kampuni zifuatazo kwa shughuli zingine: M/s Jandu Construction & Plumbers Ltd kwa shughuli za mabomba, maji safi, na maji taka, M/s Barkley Electrical Contractors Ltd kwa maswala ya umeme na M/s Remco (International) Ltd kwa shughuli za vipoza hewa. Mkandarasi ndiye mlipaji wa gharama za shughuli hizi zote zinalipiwa kutokana na gharama ileile iliyokubalika kwa mkandarasi mkuu.

Watendaji wote wa miradi hii wanaonyeshwa kwenye mabango ambayo bado yapo kwenye viwanja hivyo. Uteuzi wa Gavana Ndulu, Manaibu Gavana, Dkt. Enos Bukuku na Bw.Lila Mkila ulifanyika wakati mipango ya awali ya kujenga nyumba hizi ilikuwa imeshaanza. Benki Kuu ilikodisha nyumba mbili, mojakiwanja namba 480 Barabara ya Bray, Masaki na nyingine kiwanja namba 591,Msasani Peninsular kwa matumizi ya viongozi hao wawili ambao walikuwa bado wanaishi kwenye nyumba zao mbali na ofisi.

Kati ya Oktoba 2007 aliporipoti kazini kama Naibu Gavana hadi Aprili 2008, Profesa Ndulu aliishi kwenye nyumba yake iliyoko Mbezi Beach, na Naibu Gavana Mkila naye pia aliishi nyumbani kwake kabla ya kuhamia kwenye nyumba hizi zilizokodishwa.

Benki Kuu iliamua kumhamisha Naibu Gavana Juma Reli kwenda Barabara ya Mahando Masaki ili kuruhusu matengenezo ya nyumba aliyokuwa anaishi Kinondoni Barabara ya Msese. Naibu Gavana Dkt.Bukuku anaishi kwenye nyumba yake na Benki Kuu inatoa posho ya nyumba kulingana na mkataba.

Nyumba hizo mbili zilizojengwa chini ya miradi iliyotajwa, sasa hivi zimekamilika.Gavana wa Benki Kuu, Profesa Ndulu alihamia nyumba namba 12 Barabara ya Tumbawe Desemba 17,2009 na Naibu Gavana Mkila alihamia nyumba namba 57 Mtwara Crescent Desemba 4,2009

Kama ilivyo kiutaratibu, ukaguzi wa mahesabu yanayohusu miradi hiyo utafanyika kisheria. Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ndiye mkaguzi wa mahesabu ya Benki Kuu; ambaye ameanza kufanya kazi hii tangu mwaka 2007. Yeye ameiteua kampuni ya Ernst & Young kama wakaguzi wa kumsaidia kutekeleza jukumu hili.

IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA UMMA NA ITIFAKI
BENKI KUU YA TANZANIA

...ten thousand Blue Blistering Barnacles.............Muddo SIK!!
 
Back
Top Bottom