Majibu na madai ya uamsho kuhusiana na vurugu na muungano

mara hii wameshaanza kuitamani na daresalama hahaha

Mkuu vile visiwa vikiachiwa huru tutashtukia wimbi la ugaidi usio na kifani! Umemsahau yule jamaa aliyeenda kupigana Tora Bora tokea Zanzibar? Wewe unafikiri ni mahubiri yapi yaliyosababisha aende huko kama sio ya wanauamsho?
 
attachment.php

Huyo jamaa wa pili toka kushoto anaonekana gaidi sio mchezo!
 
Hawa jamaa wanafaidika na muungano maradufu kuliko ss lkn wanakiburi,pegeni kibuti hao magaidi wasitusumbue
 
Wacheni kupotosha Watangayika, kilichozungumzwaa alitoa mfano kabla ya mipaka mipya ya Za'bar kugaiwa na kupunguzwa Dar kulikuwa na km 10 ya Z'bar, lkni baada ya hapo Za'bar ina mipka yke kama iliomo kwnye mabadiliko ya katiba ya mwaka 2010 ya Z'bar.

Sasa na hio sehemu ilobaki Tanganyika mnaitaka? Kasema kwa hilo haliwezekani tena.
Wacheni kuongopeana nyinyi Watanganyika Wazanzibari wanataka nchi yao msiwapotoshe watu, ss hatuna shida na na Dar wala Tanga, au Kilwa.
Almuhimu Jamhuri ya Zanzibar kwanza = Unguja+Pemba+visiwa vidogovidogo+Anga na Bahari iliozunguka visiwa vyetu vinatutosha.

Utata na uzushi mtupu mara kilometa 10 mara maili 10!which is which?HIZO NI DALILI ZA CHOKOCHOKO ZA KIZUSHI.
Unataka kutuambia huyo sultan wenu jamshid alikuwa anatawala mpaka umbali huo ndani ya Dar es salaam? Mbona wakati mkombozi wenu john okelo anaongoza mapambano ya kuikomboa zanzibar hayakuletwa majeshi yake mpaka dar es salaam? hayati sheikh abeid aman karume aliposema mambo fulani fulani ya Tanganyika mwisho chumbe ina maana alikuwa hajui mipaka ya nchi yake!
Nadhani wazanzibari wako kwenye heat na siku si nyingi watanganyika tutawapumulia visogoni!
 
Haiwezekani mtu atoke Dar aende mpaka Unguja akaongee hivyo vineno viwili vilivyochaguliwa na kubandikwa hapa kwa ajili ya ufataani. Weka "interview" kamili tuone nini kilichoulizwa na nini kilichojibiwa. Wacheni hizi fitna za kijinga.
 
Kuna aliyeisoma hiyo makala ya Manyerere baadae ndio akabonyeza vitufe vya Keybord?

Tumeekewa link hii hapo juu. » Blog Archive » Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar

Jihabarishe usiwe mfata mkumbo tu.

Kwenye makala kuna hili jibu.
Nashangaa sasa alipokuja Waziri, Jeshi la Polisi wamemdanganya. Na alipokuja IGP wamemdanganya wamemwambia uongo. Wanamwambia kuwa Jeshi la Polisi limejaribu kuzima fujo, lakini si kweli. Ni uongo huo. CD zipo zinauzwa kila pahali. Wazi kabisa. Zinaonyesha maandamano kitu mbali, na zile fujo kitu mbali kabisa. Hayo matembezi kitu mbali na hizo fujo kitu mbali kabisa.
JAMHURI: Nini chanzo kilichosababisha fujo?
Sheikh Farid: Fujo ilisababishwa na Jeshi la Polisi kukosa utaratibu, kuchukua mazoea yale yale ya uhuni na mabavu. Ndicho kilichofanyika kwa sababu........

JAMHURI: Mambo gani ambayo Zanzibar haitendewi haki ndani ya Muungano?
Sheikh Farid: Ni mamlaka kamili ya kimaamuzi ya kimataifa, ya ndani na nje ya nchi. Hiki ndicho tunachokosa Zanzibar. Wanaita Sovereignty, Zanzibar inakosa sovereign yake kwa hiyo tunataka sovereign state. Kama ni Zanzibar iheshimike, kama ni Rais wa Zanzibar aheshimike, Serikali ya Zanzibar iheshimike ndani na nje ya nchi. Iwe na mamlaka kamili. Na wao wenyewe (Wazanzibari) wataona utaratibu nini watafanya. Kwa hiyo wananchi waulizwe, chepesi tu hakina tabu. Si waliulizwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hakupigwa mtu?
JAMHURI: Je, mtaidai Dar es Salaam?
Sheikh Farid: Hatuna shida nayo hiyo. Tutakuachieni. Sisi watu makarimu sana sie. Tutawaachieni.

JAMHURI: Mbona hamjasikika mkilaani kuchomwa makanisa? Mnaunga mkono kitendo hicho?
Sheikh Farid: Tumeshatoa taarifa nyingi sana. Tatizo unajua hakuna uadilifu kwenye uandishi wa habari. Hakuna uadilifu hata kwenye hii TV yetu iliyopo hapa (ZBC), hata redio zilizoko hapa hakuna uadilifu bwana. Hii ni kwa mtu anachukia kitu anakuwa si mwadilifu. Na haya ndiyo yanayosababisha matatizo kama haya kuzuka. Mtu unamnyima haki yake anafika mahali hawezi kustahamili. Kwa hiyo sisi kiufupi tunalaani vibaya sana suala zima la kuchoma makanisa, dini haisemi hivyo. Si dini yetu wala si nyingineyo, haisemi hivyo.

Halafu sehemu ya kutoa maoni kuna hii.

Nalishkuru hili gazetu kwa kuonesha mfano mzuri wa chombo cha habari kinavotakiwa sio haya magazeti yanayotangaza mambo kwa kusikiliza upande mmoja yaani upande mwengine unashushiwa shutuma bila ya kupewa nafasi ya kujitetea. Sisi wazanzibari sote hatuungi mkono kuchomwa makanisha waliochoma makanisa police wanawajuwa ila kuna ajenda ya siri ya kutaka kustopisha hizi move ila tunawambia mpaka kieleweke muungano hatuutaki na nyinyi watanganyika mudai nchi yenu au hamuna???

Bandugu tujihabarishe, tujiridhishe, tutafute ukweli, tusikurupuke kufata mkumbo wa watu na propaganda za wenye kutaka kuingiza Jamhuri ya Muungano kukidhi matakwa ya kung'ang'ania madaraka.

Mimi si mmoja wa wanaoamini kuwa UAMSHO wamehusika na uchomaji wa Makanisa. Do your home-work!
 
Haiwezekani mtu atoke Dar aende mpaka Unguja akaongee hivyo vineno viwili vilivyochaguliwa na kubandikwa hapa kwa ajili ya ufataani. Weka "interview" kamili tuone nini kilichoulizwa na nini kilichojibiwa. Wacheni hizi fitna za kijinga.

Haya ndiyo madai ya Uamsho kuuvunja Muungano
*Wasema bayana kwamba wanataka Zanzibar iwe 'Sovereign State', ijitawale yenyewe
*Wasema Dar es Salaam ilikuwa ya Zanzibar, maili kumi kuingia ndani, mikataba ipo
*Kiongozi ahoji: Kilomita chache zinakushughulisheni wakati mna mapori tele

Jumuiya ya Uamsho ya Visiwani Zanzibar hivi karibuni ilijikuta matatani, baada ya Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya wafuasi wake. Mwandishi wa gazeti la JAMHURI, Manyerere Jackton, amefanya mahojiano ya ana kwa ana na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed, aliyeeleza lengo kuu la Jumuiya hiyo ya Kiislamu.

JAMHURI: Ni nini chanzo cha vurugu za Mei 26?
Sheikh Farid: Kilichotokea hapa kwa muda mrefu, japo inasikika Jumuiya ya Uamsho ndiyo inayofanya mihadhara, lakini ni Umoja na Jumuiya za Kiislamu ambazo zimekuwa zinaendesha mihadhara. Tumefanya mihadhara zaidi ya mia moja hadi sasa - mikutano zaidi ya mia pamoja na makongamano tofauti. Na lengo zaidi hapo awali lilikuwa ni kuwaelimisha watu kujua Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kuona ni jinsi gani inawabana Wanzibari na haijawapa ile haki yao ya kuujadili Muungano.
Na baada ya hapo kilichokuwa kinazungumzwa zaidi ni kuwaelimisha wananchi kujua haki yao, kujua mustakabali wa nchi yao na umuhimu wa kuuhoji Muungano au kuujua Muungano. Wazanzibari wao kama washirika na Watanganyika wana haki ya kuuhoji Muungano. Sasa hii mihadhara imeendelea kwa muda mrefu na ilikuwa inakwenda misafara ya mbali mingine hadi shamba. Na ilikuwa misafara mikubwa inaweza ikabeba magari mia mbili, mia mbili na zaidi, kuna mapikipiki, watu wanakwenda wanarudi kwa usalama wala hakuna tabu na matatizo yoyote. Hayo yote ndiyo kwa jumla yamefanyika.
Sasa kilichojitokeza hivi karibuni ni kuwa lilifanyika kongamano. Katikati ya lile kongamano watu waliamua kutembea, kama ni matembezi tu lakini si maandamano hasa. Maandamano ni kitu ambacho kimeandaliwa, kina slogan yake, kina ujumbe, kinaenda maeneo maalumu kufikisha ujumbe maalumu. Haikuwa hivyo.

JAMHURI: Je, Polisi walivamia?
Sheikh Farid: Polisi hawakuvamia, hawakuwahi kuvamia. Na walipokuja kwa kweli walikuja matembezi yameanza kutoka maeneo ya Lumumba. Watu wote wameacha baiskeli zao, vifaa vyao palepale na walinzi walibaki eneo lile. Watu wametoka wametembea mpaka hapa Michenzani, katika roundabout, wameshuka chini mpaka maeneo ya Kariakoo. Kwa hiyo watu wakaenda moja kwa moja wakarudi kwenye kile kiwanja walichoanzia. Wakarudi palepale wakataa kitako. Wakawa wanaendelea na shughuli zao. Wakazungumza, wakazungumza mpaka wakamaliza. Walipomaliza kuzungumza wakatawanyika wakaenda majumbani mwao salama salmini.
Nashangaa sasa alipokuja Waziri, Jeshi la Polisi wamemdanganya. Na alipokuja IGP wamemdanganya wamemwambia uongo. Wanamwambia kuwa Jeshi la Polisi limejaribu kuzima fujo, lakini si kweli. Ni uongo huo. CD zipo zinauzwa kila pahali. Wazi kabisa. Zinaonyesha maandamano kitu mbali, na zile fujo kitu mbali kabisa. Hayo matembezi kitu mbali na hizo fujo kitu mbali kabisa.

JAMHURI: Nini chanzo kilichosababisha fujo?
Sheikh Farid: Fujo ilisababishwa na Jeshi la Polisi kukosa utaratibu, kuchukua mazoea yale yale ya uhuni na mabavu. Ndicho kilichofanyika kwa sababu kati ya mmoja wa watu waliohudhuria pale kwenye viwanja palipokuwa na mdahalo ni Maalim Musa Juma, yeye ni mmoja katika wahadhiri wala si kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, lakini ni mwalimu ambaye anahadhiri, anafundisha. Sasa siku ile yeye alikuwa si mzungumzaji, alikuwa mkaribishaji wa wazungumzaji. Walichokifanya wakati wa majira ya saa moja na kidogo usiku, yumo msikitini mwake anasomesha, alikwenda mtu ana shida naye. Alipomwita, kutoka nje kuwafuata wale watu wakamkamata kwenye kiuno, na wengine watano wamekuja wamemzoa wamemshindilia kwenye gari wakampeleka kituo cha Polisi. Wale vijana waliokuwa pale - wanafunzi na watu ambao wanampenda, na sasa kimekuwa kitu sensitive kwa sheikh kumdharau. Sasa hii dharau iliyofanyika, wananchi hawakukubali kwa hiyo wakaanza kupigiana simu wote kwamba Sheikh wetu kakamatwa, twendeni tukamdai kwanini kakamatwa, na tujue. Kama kumchukulia dhamana tumchukulie.

JAMHURI: Lipi jina sahihi la Jumuiya hii? Ni Uamsho au Muamsho?
Sheikh Farid: Hizi harakati zinazoendelea hapa nchini (Zanzibar) zinafanywa na Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Ndiyo wanaofanya hizi harakati zote. Isipokuwa katika utaratibu wa mambo ya mihadhara, Jumuiya pekee ina uzoefu mkubwa kwenye mihadhara ni Jumuiya ya Uamsho.

JAMHURI: Taasisi ya kidini kwanini ijikite kwenye siasa?
Sheikh Farid: Hakuna tatizo lolote. Hakuna tatizo kikatiba, hakuna tatizo kidini yetu, hakuna tatizo kimtazamo sahihi wa wanasiasa. Kote hakuna tatizo. Mtazamo sahihi wa wanasiasa. Tumchukue Rais wetu wa hapa Zanzibar, Mheshimiwa Jumbe ameandika kitabu na kuna sura maalumu anaita "Dini na Siasa". Kaeleza mengi. Kaeleza jinsi watu wengine walivyo katika dini zao, lakini akaelezea ama upande wa Uislamu huwezi kutenganisha dini na siasa. Hilo moja. Basi kama watu wanajua wanasiasa, huyu mwanasiasa anatamka kwenye kinywa chake. Alikuwa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania. Alikuwa pia Makamu wa Mwenyekiti wa CCM na kaeleza wazi kabisa kwenye Uislamu huwezi kutenganisha na siasa.
Ukija kwenye Koran, Uislamu unahesabu kuwa dini ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu, ikiwamo sehemu ndogo inayoitwa "siasa". Siasa kwenye Uislamu au kwenye lugha ya Kiarabu, neno hilo hilo siasa kama lilivyo, maana yake ni "uongozi", kwa hiyo uongozi ni sehemu ndogo, ni mlango katika maisha ya mwanadamu au katika dini ya Kiislamu. Kwa hiyo sisi kuzungumza siasa ni sahihi kabisa.

JAMHURI: Nyuma ya Uamsho kuna msukumo wa kisiasa?
Sheikh Farid: Uamsho haina uhusiano na CUF. Hili suala limeanza ilipokuja hii rasimu ya Katiba, ilipokuja kama rasimu, Serikali nzima iliikataa, Wazanzibari waliikataa wakaona wamedharauliwa. Iliporudi ikaja na dharau nyingine, badala ya kuletwa kama rasimu ikaletwa kuwa ni sheria sasa…kinguvu. Unaposema sheria maana yake ni nguvu, utake usitake. Ikaletwa kama sheria na ilikuwa iletwe kama rasimu. Hilo tatizo la mwanzo. Tatizo la pili, ndani ya rasimu ile kama alivyosema Mheshimiwa Kikwete mwenyewe wakati anazindua Tume, hakuna mjadala wa Muungano mle ndani yake, ni kwenda mbele tu kuuboresha, lakini suala la kutazama mustakabali wa Zanzibar je, inafaidika na Muungano? Hilo hakuna. Imeshapita miaka 48 na hawajawahi kuulizwa huko nyuma. Sasa sisi hapa ndipo tulipoona kuna haja ya kuulizwa, na njia ya kufanya hivyo ni kupitia kura ya maoni.

JAMHURI: Kuna umuhimu wa kuwapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?
Sheikh Farid: Sisi tunachotaka ni kura ya maoni. Wazanzibari waseme wenyewe. Hakuna mtu amepewa kibali cha kumsemea mtu. Hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari. Kila mtu aseme mwenyewe na hiyo ndiyo demokrasia, kwa hiyo sisi kama Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu tunasema iitwe kura ya maoni. Nisiseme mie, mie nitasema kwenye karatasi. Kila Mzanzibari atasema kwenye karatasi. Kura ya maoni ni nyepesi tu.

JAMHURI: Mbona hamjasikika mkilaani kuchomwa makanisa? Mnaunga mkono kitendo hicho?
Sheikh Farid: Tumeshatoa taarifa nyingi sana. Tatizo unajua hakuna uadilifu kwenye uandishi wa habari. Hakuna uadilifu hata kwenye hii TV yetu iliyopo hapa (ZBC), hata redio zilizoko hapa hakuna uadilifu bwana. Hii ni kwa mtu anachukia kitu anakuwa si mwadilifu. Na haya ndiyo yanayosababisha matatizo kama haya kuzuka. Mtu unamnyima haki yake anafika mahali hawezi kustahamili. Kwa hiyo sisi kiufupi tunalaani vibaya sana suala zima la kuchoma makanisa, dini haisemi hivyo. Si dini yetu wala si nyingineyo, haisemi hivyo. Lakini tunashangazwa vilevile, tumechoma makanisa, sisi ameuliwa imam ndani ya msikiti na Jeshi la Polisi…ameuliwa imam ndani ya msikiti, huko Mwembechai kwenu huko Dar es Salaam ameuliwa Muislamu ndani ya msikiti. Acha kuchoma makanisa. Sisi tunalaani uvunjifu wa amani wa aina yoyote - ikiwa wa ubaguzi wa kidini wa kuchoma makanisa, ikiwa wa kuwahujumu watu, tukubali haya si mafunzo maana hata kwenye nyumba yangu wamekuja wamehujumu ndani, wamepiga mabomu ndani ya nyumba, wamevunja mlango.

JAMHURI: Mambo gani ambayo Zanzibar haitendewi haki ndani ya Muungano?
Sheikh Farid: Ni mamlaka kamili ya kimaamuzi ya kimataifa, ya ndani na nje ya nchi. Hiki ndicho tunachokosa Zanzibar. Wanaita Sovereignty, Zanzibar inakosa sovereign yake kwa hiyo tunataka sovereign state. Kama ni Zanzibar iheshimike, kama ni Rais wa Zanzibar aheshimike, Serikali ya Zanzibar iheshimike ndani na nje ya nchi. Iwe na mamlaka kamili. Na wao wenyewe (Wazanzibari) wataona utaratibu nini watafanya. Kwa hiyo wananchi waulizwe, chepesi tu hakina tabu. Si waliulizwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hakupigwa mtu?

JAMHURI: Marekani majimbo yale ni nchi - ni Muungano, mbona majimbo hayana mamlaka kamili kama nchi?
Sheikh Farid: Mbona upo muungano tofauti na huo. Kama Umoja wa Ulaya si upo? Upo vipi? Katika Umoja wa Mataifa si kila nchi ina kiti?

JAMHURI: Huo si muungano ni kama jumuiya tu.
Sheikh Farid: Huo ni muungano, si wameungana katika vitu maalumu? Wamarekani wameamua wao vile. Sisi tumeamua hivi. Wao hatuwasemei. Sie tunaamua tunachotaka sie. Na sisi hawezi kutulazimisha mtu tuamue kwa akili za Kimarekani. Wamarekani wataamua wao wenyewe Kimarekani, haki za Kizanzibari zitaamuliwa Kizanzibari-Zanzibari.

JAMHURI: Ungependa Muungano wa uwe wa namna gani?
Sheikh Farid: Mie ninachosema ule mchakato wa Katiba imekuwa sawa na kumchukua ng'ombe na gari ya ng'ombe halafu ng'ombe ukamweka nyuma gari ya ng'ombe ukaweka mbele. Au mashine ukaweka nyuma, gari ukaweka mbele. Sijui itakwenda vipi. Sasa tunashangaa, watu wataalamu wana akili lakini inaonyesha akili zao zimefika mahali wanatuona sisi wapumbavu. Sisi bwana tunasema ilivyo kitu kinachowafungamanisha Wazanzibari na Watanganyika ni Muungano. Ninyi mnataka kujadili Katiba ya Muungano, hili tatizo la Muungano kwanini msilizungumze mwanzo? Hili la kuzungumza mwanzo. Kwanza, lizungumzwe hili kwanza mpaka likae sawasawa halafu ndiyo tuzungumze Katiba.
Sasa unasema mimi na wewe tunataka kufanya biashara njoo tufunge mkataba mimi na wewe. Si tuzungumze tukubaliane kwanza halafu ndiyo tuandike mkataba kwa sababu Katiba ndiyo umefunga kila kitu. Kitu kinachotufungamanisha tukizungumze mwanzo. Wananchi wapewe fursa wazungumze mwanzo. Watu wanapewa fursa hizo wasiokuwa na nchi mwanzo…hii ni nchi. Hii ni nchi. Ilikuwa ni nchi tena kubwa mpaka Dar es Salaam yote ilikuwa yetu ile, tena mikataba ipo ya kimataifa ya kuonyesha Dar es Salaam yote ile ni yetu sisi. Na kuingia ndani huko maili 10.

JAMHURI: Je, mtaidai Dar es Salaam?
Sheikh Farid: Hatuna shida nayo hiyo. Tutakuachieni. Sisi watu makarimu sana sie. Tutawaachieni. Nashangaa nyie tu hizi kilomita za mraba ngapi zinakushughulisheni nyie wakati mna mapori tele kule juu, na mna ardhi ya kwenda na kurudi, mashamba ya kwenda na kurudi mnang'ang'ania hiki tu!

JAMHURI: Muungano ukivunjika, nini hatima ya Wazanzibari wanaoishi/waliowekeza Bara?
Sheikh Farid: Jawabu moja, wewe huwajui Watanzania wanaofanya biashara Kenya? Uganda? Hatima yao ipo vipi? Sasa ninyi inaonyesha kuna watu wana fikra mbovu katika vichwa wanaona maana yake tukiwa hivi (tukitengana) tutakuwa maadui, hata! Udugu lazima utabakia. Tumeoa kule. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar usingizi wake (mkewe) ni wa kule (Bara) au hujui wewe? Hatuwezi kuachana bwana, watu watabakia, mapenzi yapo, undugu upo, ujirani mwema kabisa, waliokuwapo hapa Watanganyika watabakia, Wakristo hapa watabakia, itakuwa kila kitu kina utaratibu. Si maana yake kwamba mmetengana muwadhulumu wale ndugu zenu (walio Bara). Mkiwadhulumu sawa! Sisi kawaida yetu hatuko hivyo.

…tamati….
 
unaonekana wewe ni kichongo halafu jicho lako moja likapofuwa unashindwa kusoma nini kimeandikwa au jazba tu ya kijina ndio imekujaa na ujinga wa kubwa lao jinga soma mada usikurupuke kama nguruwe mwituu
 
mara hii wameshaanza kuitamani na daresalama hahaha
unaonekana wewe ni kichongo halafu jicho lako moja likapofuwa unashindwa kusoma nini kimeandikwa au jazba tu ya kijina ndio imekujaa na ujinga wa kubwa lao jinga soma mada usikurupuke kama nguruwe mwituu
 
Majibu mujarabu kabisa dhidi ya masuala murua kutoka kwa mwandishi wa jamhuri.

Ahsantum Sheikh Farid
 
yani mimi hiyo mionekano yao tu, kisaikolojia ni watu wakorofi, wabishi na wasiotaka kuelewa. Angalia vizuri ndani ya nyuso zao utaona kuna nyuso za nina sheikh Osama bin Laden, na magaidi mengneyo ya kiarabu.
MY TAKE:
hatua kali dhidi yao zichukuliwe

Hizi ni chuki dhahiri dhidi ya Uislam na Waislam. Jihadhari, unapanda mbegu ambazo huwezi kuvuna. Yatakukuta makubwa ndugu yangu. Sikutishi lkn zingatia haya ninayokwambia. Mdomo uliponza kichwa.
 
hao jamaa wa uamsho nazani wana ajenda yao nyingine tofauti na masuala ya dini, yan wamefika mbali mpaka wwanasema eti dar es salaam ilikuwa sehemu ya zanzibar,shame on you nyie UAMSHO>
 
Wacheni kupotosha Watangayika, kilichozungumzwaa alitoa mfano kabla ya mipaka mipya ya Za'bar kugaiwa na kupunguzwa Dar kulikuwa na km 10 ya Z'bar, lkni baada ya hapo Za'bar ina mipka yke kama iliomo kwnye mabadiliko ya katiba ya mwaka 2010 ya Z'bar.

Sasa na hio sehemu ilobaki Tanganyika mnaitaka? Kasema kwa hilo haliwezekani tena.

Wacheni kuongopeana nyinyi Watanganyika Wazanzibari wanataka nchi yao msiwapotoshe watu, ss hatuna shida na na Dar wala Tanga, au Kilwa.

Almuhimu Jamhuri ya Zanzibar kwanza = Unguja+Pemba+visiwa vidogovidogo+Anga na Bahari iliozunguka visiwa vyetu vinatutosha.

Kabla ya kutoa taarifa kama hizi tujuze elimu yako, wengi UAMSHO wanakurupuka na uelewa wao mdogo kuhusu katiba na TANZANIA kwa ujumla.
 
yani mimi hiyo mionekano yao tu, kisaikolojia ni watu wakorofi, wabishi na wasiotaka kuelewa. Angalia vizuri ndani ya nyuso zao utaona kuna nyuso za nina sheikh Osama bin Laden, na magaidi mengneyo ya kiarabu.
MY TAKE:
hatua kali dhidi yao zichukuliwe

Kuna mwenye ELIMU ya chuo kikuu hapo kweli? Hata katiba hawaijui wanakesha wakiwaza kufanya fujo makanisani. Hawa ni magaidi
 
Kiongozi ahoji: Kilomita chache zinakushughulisheni wakati mna mapori tele

Kauli kama hii ni yaleyale ya waswahili wasemayo choko mchokoe pweza...?!si bure...
 
Back
Top Bottom