Majibu: Kwanini Nyerere hakuvaa sare za CCM?

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
KWA karibu wiki nzima iliyopita, wanachama na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakisambaza ujumbe mfupi wa maneno (sms) unaodai kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere hakuwahi kabisa kuvaa sare za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambazo ni suruali nyeusi na shati la rangi ya kijani "kwa sababu alikuwa amekichoka".

Katika hali hiyo, waongo hao pia walidai alikuwa hazitaki sare hizo kwa sababu alikuwa na kinyongo nacho kwa kwenda kinyume cha malengo na misingi yake, hivyo wapiga kura wa mwaka 2015 wanapaswa waking'oe madarakani na kuiweka Chadema ili kumuenzi.

Nadhani nitumie fursa hii ndogo kutoa ufafanuzi wa jumla kwa wote waliotumiwa meseji hiyo ya kijinga,waliosoma thread mbalimbali zilizojadili hilo ama kuulizwa kwa namna yeyote ile.

Wakati Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM kuanzia Februari 5, 1977 hadi Agosti 16, 1990 alipong'atuka, sare hizo za chama zinazotumika sasa zilikuwa hazijaanza na hata kufikiriwa kwa namna yoyote.

Badala yake, suarali hizo nyeusi na shati hilo la kijani lililoshonwa katika sura inayofanana na kombati hasa za mgambo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), zilikuwa ni sare tu za Umoja wa Vijana (UVCCM) na chipukizi wake. Halikuwa vazi la TANU wala la CCM.

Sare zinazotumika sasa ambazo ni suruali au sketi nyeusi pamoja na mashati hayo ya kijani zimeanza kutumika wakati tayari ameng'atuka Uenyekiti wa Taifa wa CCM na kubaki tu mwanachama namba moja aliyekuwa na kadi Na. A 1.

Hata aliposhiriki kwenye vikao kama vya Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) au Mkutano Mkuu wa Taifa pia hakufanya hivyo akiwa mjumbe isipokuwa mgeni mwalikwa ambaye siyo lazima avae sare.

Katika kipindi chote alipokuwa Rais wa chama kilicholeta Uhuru cha Tanganyika African National Union (TANU) na hata Mwenyekiti wa Taifa wa CCM hadi alipong'atuka, wajumbe wa vikao vya chama walikuwa wakishona sare hususan mashati kutokana na vitenge vilivyobuniwa maalum kwa ajili ya tukio husika.

Mfano ulipofanyika Mkutano Mkuu wa Taifa wa uchaguzi mkuu au pengine NEC, Makao Makuu ya Chama yalikuwa yakitoa kitenge maalum na kuwasambazia wajumbe nchi nzima ili kila mmoja ashone shati lake. Hapakuwa na sare hizi nyeusi wala za kijani kama sasa. Zote zilianza wakati Mwenyekiti wa Taifa wa CCM akiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi baada ya mwaka 1992.

Zilianza baada ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa nchi ya vyama vingi vya siasa tofauti na mwanzo ilipokuwa ya mfumo wa chama kimoja ambacho pia kilitajwa kwamba ni CCM.

Zilibuniwa kwa sababu ya kuwatambulisha wana CCM wanapokuwa kwenye vikao vyao wenyewe, mikutano yao na hata vinginevyo ili kuepuka kuingiliwa kwa namna yoyote ile na mtu asiyehusika na shughuli zao.

Mtu anayesema vinginevyo au kumhusisha Mwalimu kukidhi matakwa yake ya kisiasa kwa kutaka kuwadanganya wapiga kura, kumtumia kwa utapeli au kuwataka wapiga kura waje waiweke madarakani Chadema mwaka 2015 kwa madai kuwa CCM ilishatengwa mpaka na mwasisi wake ni mzandiki na juha wa kisiasa.

Chadema wamekuwa wakihaha na kutafuta namna na mbuni mbalimbali za kuungwa mkono hasa katika kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015, kwa kueneza uzushi huu wanaamini kuwa itakuwa ndio kujisafishia njia ya kwenda ikulu, jambo ambalo hakika ni mwendawazimu wa kufikiri, labda mtu asiye fikiri sawasawa ndiye anayeweza kurubuniwa kwa njia hiyo.

Mtu anayetaka kujua ukweli akaingie maktaba yoyote yenye picha za vikao vya TANU au vya CCM vya wakati ambao Mwenyekiti wa Taifa alikuwa Mwalimu Julius Nyerere.

Hapo atakuta kwa mfano, wajumbe waliokuwa ni maofisa wa majeshi kama JWTZ, JKT, Jeshi la Polisi au Jeshi la Magereza kwa sababu kilikuwa kipindi cha mfumo wa chama kimoja tu cha siasa utakuta wamevalia sare zao halisi za kijeshi kama ilivyo nchini China, Korea Kaskazini, Vietnam au Kyuba hadi hivi leo.

Wachache kati yao ni pamoja na Jenerali Mirisho Hagai Sarakikya, hayati Jenerali Abdallah Twalipo, Jenerali David Musuguri, hayati Jenerali Mwita Kyaro, hayati Luteni Jenerali Silas Mayunga, hayati Meja Jenerali Mwita Marwa na kadhalika.

Mbali na CCM kutokuwa na sare katika kipindi hicho chote, hata Chadema yenyewe licha ya kuanzishwa na Mzee Edwin Mtei tangu mwaka 1992, lakini ni majuzi tu wakati Mwenyekiti wa Taifa wa sasa, Freeman Mbowe alipokuwa akigombea urais mwaka 2005 ndipo alipokuja na mavazi ya khaki na kutangaza kwamba hatayavua "mpaka kieleweke".

Hakusema kwamba yanakuwa sare za chama hicho lakini ilipofika mwaka 2010 ndipo idadi kubwa ya wanachama wakayafanya kuwa maalum kwa ajili hiyo.

Leo kwa mfano mtu akiuliza kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema aliyetangulia kabla ya Mbowe, hayati Bob Makani amewahi kuvaa sare hizo za khaki jibu lake ni "hapana", lakini haimaanishi kwamba alikuwa hakipendi chama hicho isipokuwa vinginevyo.

Mbali na Makani, hakuna pia picha yoyote inayomuonyesha mwasisi wa Chadema, Mzee Edwin Mtei akiongoza kikao chochote cha Kamati Kuu, Baraza Kuu la Taifa, Mkutano Mkuu wa Taifa au pengine akihutubia popote wakati wote alipokuwa Mwenyekiti wa Taifa huku akiwa na kombati hizo za khaki.

Narudia tena kuwa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere hakuwahi kuvaa sare hizo za CCM zinazotumika sasa siyo kwa sababu alikuwa hakipendi chama chake na kudai hivyo ni ujinga wa kufikiri.
 
hivi wewe kama JK Nyerere kwa mapenzi yake na roho yake aliamua kutovaa jezi za ccm wewe binafsi inakupunguzia nini au unapata madhara gani .... sifahamu unajipendekeza nini kutetea kitu usichokijua

unless otherwise you are running out of conciousness and soon you will turn to be a moron
 
Waliosema hivyo ni wanafiki wakubwa wasio penda maendeleo ya taifa letu
mnakosa hoja za msingi mnaanza kuongelea mavazi.
 
Kweli naona CCM wameamua kutekeleza agizo la mwenyekiti wao kujibu kila kinachoongelewa kuhusu CCM, jibuni na hoja ufisadi,wizi wa epa,kagoda,meremeta na jinsi vigogo wa serikali wanavyotorosha twiga wetu kwenda arabuni, pia hela mlizoficha uswis yapo mengi ya kujibu muhimu zaidi ya kutetea nguo zenu za kijani.......Tanzania tuna shida ya huduma bora na maisha mazuri sio sare zenu jamani.......kha!
 
Kweli naona CCM wameamua kutekeleza agizo la mwenyekiti wao kujibu kila kinachoongelewa kuhusu CCM, jibuni na hoja ufisadi,wizi wa epa,kagoda,meremeta na jinsi vigogo wa serikali wanavyotorosha twiga wetu kwenda arabuni, pia hela mlizoficha uswis yapo mengi ya kujibu muhimu zaidi ya kutetea nguo zenu za kijani.......Tanzania tuna shida ya huduma bora na maisha mazuri sio sare zenu jamani.......kha!

Haya yanayozushwa na tuhuma za "namna hii" zinazoelekezwa CCM kila uchao ni ushahidi tosha kuwa CHADEMA wamekosa sera na hoja za msingi za kuwavuta watanzania katika Chama Chao hivyo kujikita katika hoja dhaifu na zisizo na mashiko za namna hii, lakini kwa kuwa ni tuhuma na mara zote tuhuma ikiachwa bila kujibiwa watu huwa wanaiamini tuhuma hiyo na kuisadiki.

Wananchama wa CCM, wanao wajibu wa kufafanua na kutoa ufahamu kwa watu juu ya tuhuma mbalimbali zinazoikabili CCM kwa kadri ya Ufahamu wao.
 
Haya yanayozushwa na tuhuma za "namna hii" zinazoelekezwa CCM kila uchao ni ushahidi tosha kuwa CHADEMA wamekosa sera na hoja za msingi za kuwavuta watanzania katika Chama Chao hivyo kujikita katika hoja dhaifu na zisizo na mashiko za namna hii, lakini kwa kuwa ni tuhuma na mara zote tuhuma ikiachwa bila kujibiwa watu huwa wanaiamini tuhuma hiyo na kuisadiki.

Wananchama wa CCM, wanao wajibu wa kufafanua na kutoa ufahamu kwa watu juu ya tuhuma mbalimbali zinazoikabili CCM kwa kadri ya Ufahamu wao.

Lakini Mkuu inaonekana ufahamu wa kufafanua tuhuma kwa ccm ni mdogo kulinganisha na ufafanuzi juu ya masuala ya CDM, sasa kama muda mwingi tutakuwa tunaijibu CDM ni lini tutajibu hoja zinazohusu maendeleo ya NCHI yetu?
Kama CHADEMA wamekosa sera za kuwavutia wananchi vp CCM wanatumia msuli mkubwa kupambana na hoja wanazoita dhaifu, WATANZANIA wa leo ni waelewa unapoongea wanapima, wanachuja, wanapembua kama unawadanganya wanajua kama hoja za CDM ni zaifu wala CCM haina shida ya kuumiza kichwa, wananchi wataamua.
 
Mbona kwenye kinyanganyiro cha kumpachika mkapa mwalimu alikuwepo?na mbona wanachama tulivaa sare hizo?bado swali lipo pale pale!!kwa nini hakuwahi kuvaa sare hizo?ziwe kitenge,kofia,overall au chochote?ukweli ni kuwa sare za chama zilikuwepo enzi za mwalimu ila hakuwahi kuzivaa!!!hizo blaa blaa nyingine hazina kichwa wala miguu,cha msingi tujiulize kwa nini hakuvaa basi!!hizo porojo za Tanu na Taa sijui jwtz sijui jenerali nani haziwezi kubadili ukweli!!ngoja nikutumie hela ya kangara moja uzimulie hangover ndiyo inayokusababisha umwage povu hapa,kwanza hoja yenyewe haina maana hata chembe,kama alivaa au hakuvaa haitusaidii chochote,tungejadili mabilioni ya uswis au ile ya misumari badala ya vipuri na jinsi gen mboma anavyotafuna tanesco hapo tungekuwa tunatenda haki,ccm mmekifanya chama cha porojo na wizi tuuu,wakati mwalimu alikijenga kwa misingi ya utaifa!!kwenda kule.
 
Mimi nafikili hili swala la kuvaa sare ni dalili ya ubaguzi katika jamii kisakologia. Kuvaa sare kunamaanisha "NINYI NA SISI". Mbaya zaidi, Ni kutowatendea haki watu mamilioni nchini ambao wanakwenda kwenye sanduku la kupigia kura kuchagua chama na viongozi wa kitaifa si kwa kigezo cha kuona wavaa sare bali kwa kigezo cha sera na utendaji wa chama na viongozi wake.

Ni dalili ya kufilisika kifikra na kisiasa pale jamii inapoanza kufikili na kuona kuwa, kuvaa vazi la langi au aina fulani ni mtaji wa kisiasa na inaonyesha wewe ni nani katika jamii na unakubalika vipi, au pale wananchi wanapojaa kwenye mikutano ya kisiasa basi huko ni kukubalika hata kama ujumbe ni ngonjera na nyimbo zilezile.

Watanzania kwa sasa hatuutumikishi ubongo wetu katika kujenga hoja na maswali magumu na kuyatafutia majibu mbadala badala yake tunaridhika kuwa kwenye "comfort zone" za kimaskini katika mawazo na fikra.

Ndiyo maana hata wanasiasa wetu wako kwenye "comfort zone" za kimaskini katika mawazo na fikra. Kwa mawazo haya, Siyo kitu cha kushangaza pale wanasiasa wa vyama vyetu vikuu nchini wanapoanza kujadili kwa wiki nzima achilia mbali sekunde tano kuhusu kadi ya chama. Silly politics.

Nchi inahitaji jamii yenye mawazo na fikra pevu katika kupambana na changamoto za karne ya 21 na hii itatokea kama Wananchi wataondokana na hizi siasa za matukio na mufilisi.

Twenty years on, ajenda bado ni ruswa na ufisadi huku chorus ikiwa, kadi au pandikizi la kisiasa.

Wananchi deserve more than this silly politics...

Ama kweli, kama ndiyo siasa hizi, basi bado tuko mbali sana
 
waliobaki kwenye chama cha mafisadi ni kwa ajili ya kupokea makombo ya akina ridhiwan kwenye bahasha za kaki
 
Lakini Mkuu inaonekana ufahamu wa kufafanua tuhuma kwa ccm ni mdogo kulinganisha na ufafanuzi juu ya masuala ya CDM, sasa kama muda mwingi tutakuwa tunaijibu CDM ni lini tutajibu hoja zinazohusu maendeleo ya NCHI yetu?
Kama CHADEMA wamekosa sera za kuwavutia wananchi vp CCM wanatumia msuli mkubwa kupambana na hoja wanazoita dhaifu, WATANZANIA wa leo ni waelewa unapoongea wanapima, wanachuja, wanapembua kama unawadanganya wanajua kama hoja za CDM ni zaifu wala CCM haina shida ya kuumiza kichwa, wananchi wataamua.

Ni kweli kuwa uelewa wa wananchi umeongezeka kwa kuwa wengi wamepata ELIMU angalau hata ya msingi na sekondari lakini idadi ya wasomi pia hivi sasa ni kubwa maradufu ukilinganisha na siku za nyuma, hii ndio kusema kuwa CCM imefanya kazi yake ipasavyo ya kuandaa sera ya upatikanaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari lakini pia ni kudhihirisha kuwa CCM imeisimamia vyema serikali yake katika kutimiza Ilani yake na Sera zake juu ya Elimu.

Lakini pamoja na Uelewa huo wa watu wetu, ni ukweli usiopingika kuwa wapo wananchi ambao wanaamini katika uzushi huu na propaganda chafu dhidi ya CCM, basi isingelikuwa ni busara kuwaelisha na kuwapa ufahamu wa sawasawa watu hawa..?? nadhani jambo la kusema kwa wananchi ni nini kimefanywa linasemwa sana na viongozi wa chama hasa katibu wa itikadi na uenezi Ndugu NNauye, na hili dogo la kuwaambia hawa wazushi kuwa mmesema jambo lisilo kichwa wala miguu, tunaweza wengine katika sisi kulisema na kulifafanua.
 
olyset net NYERERE HAKUWA NA NDIMI MBILI;;;
Aliamini ktk CCM, kwa kauli zake na matendo, hakuwa mnafiki, hakushindwa kudhihirisha kile kilichopo moyoni mwake, ni mwanaCCM wa kwanza na imara kuwahi kutokea...!

Uzushi huu hauna sura wala umbile. Hoja yako hii Ni hoja iliyokosa uthibitisho na dhaifu mbele ya wenye akili ya kufikiri.
 
Last edited by a moderator:
Hujui unachoongea TandaleOne,
Kifupi tu ni kua Mwalimu alikua na falsafa za "TAIFA KWANZA, CHAMA BAADAE".
Huo unaoongea hapo ni uongo, uzandiki, ujuha na uzushi tu.
 
Last edited by a moderator:
Hivi lile VAZI LA TAIFA limefikia wapi? (though to me was a childish idea).

Nchimbi aliunda TUME YA VAZI La taifa na ikazunguka mikoa yote ya Tanzania kutafuta maoni. We want to know matokea ya TUME hiyo maana imeteketeza pesa za walalahoi wa Tanzania. Au ulikuwa ni mradi wa Nchimbi? baada ya kuhamia Internal affairs umekufa?

Huyu Nyerere mimi ninaona tunamtukutza sana (No disrespect to him). Nyerere kwamba hakuwahi kuvaa sare za CCM, so what? Inanikumbusha kauli ya Mkapa kwamba Vicent Nyerere sio ukoo wa Nyerere kwasababu Nyerere hakuwahi (Mkapa) kunitambulisha hata siku moja.

Hizo ndiyo light touch politics za Tanzania.
 
Hujui unachoongea TandaleOne,
Kifupi tu ni kua Mwalimu alikua na falsafa za "TAIFA KWANZA, CHAMA BAADAE".
Huo unaoongea hapo ni uongo, uzandiki, ujuha na uzushi tu.
MWALIMU HAKUWA WA NDIMI MBILI., Kumzushia juu ya hili ni kumvunjia heshima kiongozi wetu huyu...!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom