AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Tarehe 1/5/2017 zilifanyika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani maarufu kama Mei Mosi katika mji wa Moshi ambapo mgeni Rasmi alikua ni Mh.Dr.John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania.
Katika sherehe hizo ambazo zilifana sana zilihudhuriwa na maelfu ya wafanyakazi kutoka katika sekta mbali mbali.
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) lilivialika pia vyama vya siasa mbali mbali kuja kujumuika pamoja katika sherehe hizo.
Ni Chama Cha Mapinduzi pekee ambacho kiliitikia wito huo wa TUCTA kwa kuhudhuria sherehe zile.
Hata hivyo sikushangaa sana kujitokeza kwa CCM peke yake kwa maana ndicho chama pekee Tanzania kilichokidhi matakwa ya kisheria ya uajiri na chenye mfumo na utaratibu mzuri wa ajira.
CCM ni miongoni mwa waajiri wakubwa Tanzania ikiwa na wafanyakazi wanaokaribia takribani 8000 Tanzania nzima, na wafanyakazi hao wamepewa mikataba ya ajira kwa mujibu wa sheria huku wakipata stahiki zao kama mishahara na kuwekewa michango yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii bila ya longolongo.
Hapa ndipo unapoipata tofauti kubwa kati ya CCM na vyama vingine vya siasa ,wakati CCM ikiwa na wafanyakazi walioajiriwa rasmi vyama vingine vimeajiri vibarua tu.
Vyama hivyo vimeajiri vibarua hao kwa lengo la kuwanyonya na kuwakandamiza kwa sababu havitoi mikataba ya ajira, na pia havipeleki michango katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
CCM ni taasisi kubwa na madhubuti ambayo kimfumo na muundo wake huwezi kuufanananisha na chama chochote cha siasa hapa nchini.
CCM inamiliki taasisi mbalimbali kama vile shule,vyombo vya habari, na sasa hivi kipo katika mpango wa kufungua Chuo Kikuu cha Uongozi ambapo humo watakua wanapikwa makada wake kwenye mambo mambo mbali mbali ya uongozi na miiko na maadili ya utumishi na uongozi.
Wasalaam.
Augustino Chiwinga.