Majibu Kwa Tundu Lissu - Imeandikwa na Janeth Rithe Katibu wa Uenezi Taifa ACT Wazalendo

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,273
Imeandikwa na Janeth Rithe, Katibu wa Uenezi Taifa ACT Wazalendo.

Nimesoma maoni ya Ndg. Tundu Lissu kuhusu Uamuzi wa chama cha ACT Wazalendo kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Ninaheshimu sana maoni yake na tunachukulia kwa uzito mkubwa ukosoaji wake kwa maamuzi ya vikao vya chama chetu.

Licha ya kwamba inaleta ukakasi ukosoaji wa maamuzi ya vikao vya chama kutoka Kwa Kiongozi wa chama kingine cha upinzani lakini tunaamini ni ukosoaji wa nia Njema. Sisi kama ACT Wazalendo tumejitahidi sana kujiepusha kutolea maoni maamuzi ambayo viongozi wa CHADEMA wamefanya hivi karibuni licha ya Kuwa na Taarifa nyingi za uhakika kuhusu maamuzi yale. Nitafafanua baadhi ya mambo ambayo ndugu yangu Lissu ametolea maoni.

Lissu anasema kuwa “ACT wame-surrender kwa Magufuli na maCCM. Hakuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inayoamuliwa na Wazanzibari wenyewe; bali ile inayoruhusiwa na Watanganyika, yaani Magufuli na maCCM ya Tanganyika”. Maoni haya yametolewa Kwa haraka bila kutafakari wala kurejea historia ya hivi karibuni.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni zao la Wazanzibari wenyewe kufuatia maridhiano ya Novemba 5, 2009. Wazanzibari walipiga Kura kuidhinisha Mabadiliko ya Katiba yaliyowezesha hilo.

SUK ni suala la Katiba na sio suala la watu kukaa na kujadiliana. Mwaka 2010-2015 CUF ilishiriki SUK sio Kwa kuwa Watanganyika walitaka bali Kwa Kuwa Wazanzibari walitaka.

Watanganyika walipinga sana maridhiano Zanzibar, tena wa pande zote mbili upinzani na CCM kwa sababu ni hulka ya Watanganyika kujiona wao ni watawala wa Zanzibar.

Hata haya maoni ya ndugu yangu Lissu yamejikita katika muono huo huo wa ‘mentality’ za kikoloni Kuwa Wazanzibari hawawezi kujiamulia mambo yao wenyewe mpaka waamuliwe au wasemewe na Watanganyika. Maamuzi ya kuwepo kwa SUK ni ya Wazanzibari na maamuzi ya ACT kuingia SUK Mwaka huu ni kutimiza matakwa ya Wazanzibari ambao wanataka Umoja, Haki na Maridhiano ya kijamii.

Hii hulka ya Watanganyika wa upinzani na wa chama tawala kudhani kuwa wanajua zaidi maslahi ya Wazanzibari kuliko Wazanzibari wenyewe ni hulka ya KIKOLONI. Tuna ushahidi wa kutosha kuwa Bwana Magufuli na CCM hawataki SUK Zanzibar Kwa Kuwa hawataki Wazanzibari kuwa wamoja. Uamuzi wa kuingia SUK ni Uamuzi wa Wazanzibari ambao kwetu sisi ACT Wazalendo umepata baraka zote za vikao vya chama tena bila mkwaruzano ( unanimously decided ). Magufuli na CCM Watanganyika wasipewe sifa wasiostahili kuwa eti wameridhia SUK, huko ni kuwadogosha Wazanzibari kuwa hawana uwezo wa kufanya maamuzi Yao wenyewe.

Ndugu yangu Lissu anasema “Tumemtupia Maalim Seif mfupa mtupu (Makamu wa Kwanza wa Rais hana mamlaka yoyote ya maana kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar!) ili atulie na awatulize Wazanzibari wanaomuunga mkono na jumuiya ya kimataifa iliyochukizwa na dhulma zetu Zanzibar na Tanganyika”. Vile vile maoni haya ni hisia tupu ambazo haziwezi kuthibitishwa na ushahidi wowote. Haya ni Maneno mepesi ambayo mtu yeyote hata muuza kahawa wa Urughu, Iramba anaweza kuyasema.

Lakini pia ni hisia ambazo muda utathibitisha kuwa hazina msingi. Chama chetu kimezungumza na Jumuiya ya Kimataifa kuhusu uharibifu mkubwa wa uchaguzi uliofanyika hapa Tanzania. Niseme tu Kuwa Jumuiya ya Kimataifa inajua Kwa undani nini kimetokea mpaka kufikia Uamuzi huu wa ACT Wazalendo kuingia katika SUK Zanzibar.

Matokeo ya SUK Zanzibar yana maana kubwa sana katika juhudi za Jumuiya ya Kimataifa dhidi ya ukandamizwaji unaoendelea hapa Tanganyika. Litakapodhihiri ndugu yangu Lissu na Watanzania wote wataona nini maana ya Uongozi. Kiongozi ANAONGOZA! Kiongozi HAONGOZWI. Jumuiya ya Kimataifa haitatulizwa bali ipo kazini katika hili la SUK. Niishie hapo.

Itoshe kusema Kuwa Viongozi wetu wa ACT Wazalendo katika hili wanatoa Uongozi badala ya kuongozwa na mihemko ya Wanachama na wafuasi wakiwemo wana harakati.
Ndugu yangu Lissu anasema “Serikali hii ya sasa ni tofauti na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Amani Karume na Maalim Seif. Ya mwanzo ilileta mabadiliko makubwa ya Katiba ya Zanzibar; kwa sababu Karume alikuwa anaunga mkono jitihada za Wazanzibari za kujivua kwenye ‘koti linalobana’ la Muungano”. Naomba kumkumbusha Lissu kuwa Maalim hajawahi kuingia SUK na Rais Karume. SUK ya kwanza Zanzibar ilikuwa Kati ya Dkt. Shein na Maalim Seif.

Ni imani yetu kuwa SUK hii italeta Mabadiliko makubwa kwa Wazanzibari na haswa kuimarisha Umoja wao kupitia maridhiano ya kijamii, kutoa Haki Kwa watu wote walioumizwa na kupoteza maisha Wakati wa uchaguzi na kuweka misingi ya kisheria ya chaguzi za Haki siku za usoni.

Lissu anasema “Hussein Mwinyi ni kibaraka wetu moja kwa moja; tumemweka madarakani kwa bunduki na vifaru vya Bara na kura za Watanganyika waliopelekwa kupiga kura Zanzibar wakati Wazanzibari halali wanakataliwa kupiga kura”. Haya ni maoni tu ya ndugu yangu Lissu. Sisi kama chama na viongozi tunampa Ndg. Hussein Ali Mwinyi kinachoitwa BENEFIT OF DOUBT. Kwa hatua ambazo Dkt. Hussein amezichukua mpaka sasa tangu awe Rais wa Zanzibar anastahili kupewa hiyo benefit of doubt.

Sisi ACT Wazalendo tumerejesha mkono wa kheri katika kurejesha Umoja na Haki kwa Wazanzibari. Maalim Seif anasaidiana na Dkt. Hussein kujenga Zanzibar ya maridhiano. Hukumu anayotoa Ndg. Lissu Kwa Dkt. Mwinyi ni hukumu ambayo yaweza kutosimama muda unavyozidi kwenda.

Lissu anasema “Sasa Maalim Seif Atatumika kama toilet paper ya kusafishia uchafu wa maCCM na madhambi yao dhidi ya Wazanzibari”. Haya ni matusi kwa Kiongozi wa Wazanzibari ambaye amesimamia mapambano ya Wazanzibari maisha yake yote. Sijaamini kama matusi haya yanatoka kwenye maandishi ya ndugu yangu Tundu Lissu. Ushauri wangu kwa Tundu ni kuweka akiba ya Maneno.

Tundu anamalizia kwa kusema haya dhidi ya Maalim Seif “Mimi naamini hatafanikiwa. Masikitiko yangu ni kwamba amekubali kutumika namna hii katika uzee wake. Baada ya miaka karibu arobaini ya kusimamia maslahi ya Wazanzibari, sasa amekubali kutumikia maslahi ya Tanganyika!!!” Hii ni imani yake ndugu Tundu. Mimi ninaamini Kuwa Tundu Lissu amejenga imani hii kutokana na hisia na kutokuwa na taarifa za kutosha. Angechukua muda wa kuzungumza na Maalim Seif au Kiongozi wetu wa chama ndugu Zitto Kabwe angepata taarifa za kutosha ambazo zingemfanya asiandike alichoandika.

Mwaka 1987, miaka 33 iliyopita, Maalim Seif alitoa ahadi mbele ya Wazanzibari ambayo anaiishi maisha yake yote. Maalim hajawahi kuongozwa na tamaa ya mali wala maisha ya Dunia. Anaishi maisha ya kawaida sana. Kwake yeye ni Zanzibar, Zanzibar, Zanzibar. Kila hatua anayochokua ni hatua ya kuilinda Zanzibar na Wazanzibari.

Hajaacha na hataacha kusimamia maslahi ya Wazanzibari. Hata hili la sasa la SUK ni Kwa maslahi ya Zanzibar. Kwa sisi tunaokaa na Maalim kwenye vikao tunajua Mzee huyu ni wa namna gani. Kwa ambao wanamwona Maalim Kwa nje wanaweza kumtafsiri kama hivi ndugu yangu Lissu alivyomtafsiri. Muda ni jawabu. Lissu atameza haya Maneno yake.
-Maalim Seif Shkamoo-

Na Janeth Rithe Katibu Uenezi ACT Wazalendo.


Naomba kuwasilisha.
 
Ok, time will tell,,ila mjue huu ukoo wa mwinyi unakuaga na watu wenye hekima sana,,nadhani kwasasa zanzibar iko katika mikono salama sana..
 
Mbona Tundu Lissu hatupi 'updates' za Maendeleo ya 'Matibabu' yake huko 'Ulaya' aliko? au ameshatusahau Sisi Wafuasi wake tulioko Tanzania hii?
 
Mnahangaika na kichaa Lissu. Lugha yake na uchaguzi Wake wa maneno asingeweza kuwa hata katibu wa Kata. Too local and too emotional. Angebadilisha tu.
 
Mimi nimefurahi sana ulivyomjibu kiherehere ana tabia za kutukana watu na kudharau na kujiona bora kwa kua tu ana kundi la wafuasi mfu wasiojua kupambanua pumba na mchele hongera Act wazalendo!
 
Mimi nimefurahi sana ulivyomjibu kiherehere ana tabia za kutukana watu na kudharau na kujiona bora kwa kua tu ana kundi la wafuasi mfu wasiojua kupambanua pumba na mchele hongera Act wazalendo!
Mambo kibao ya hovyo Chadema wanafanya lakini ACT wanawaheshimu sana: Yule mgombea wao wa Urais kwa Zanzibar aliipigia kampeni CCM kwenye uchaguzi wa 2020., alitumiliwa na ccm na walimuahidi uwaziri kama angefikisha 5% ya kuchaguliwa Zanzibar akawa anajipigie yeye kampeni za urais badala maalim seif kama kilivyotaka chama chake lakini upande mwengine akiwapigia kampeni wabunge wa CCM badala ya wa Chadema.

Kina Mbowe walipewa hizi taarifa lakini kwa sababu chama chao ni legelege mpaka leo hawakuchukua hatua yoyote. Sasa utakuta Ndani ya Chadema tena senior leaders kuna crisis kubwa sana lakini wanabana kimya tu na kujiona kila siku eti chama chao ni Imara.

Kuna maeneo kadhaa kule Zanzibar Chadema walisimamisha wagombea ubunge hewa, walikula njama na CCM eti wapige kampeni ili kupunguza kura za ACT ili mgombea wa CCM apite mana tofauti zilikuwa ni ndogo tu. Sasa kama kuna unafiki huu ni wa kiwango gani? Chadema wamewanuga mkono CCM tokea kwenye Uchaguzi.
 
"Ni imani yetu kuwa SUK hii italeta Mabadiliko makubwa kwa Wazanzibari na haswa kuimarisha Umoja wao kupitia maridhiano ya kijamii, kutoa Haki Kwa watu wote walioumizwa na kupoteza maisha Wakati wa uchaguzi na kuweka misingi ya kisheria ya chaguzi za Haki siku za usoni."
 
Act Wazalendo wanatetea mkate waliopewa na ccm zanzibar kwa kisingizio Cha maridhiano.Hakuna jipya kwa kilichofanyika zanzibar
 
Mnahangaika na kichaa Lissu. Lugha yake na uchaguzi Wake wa maneno asingeweza kuwa hata katibu wa Kata. Too local and too emotional. Angebadilisha tu .....a.
Haahaa lissu amegonga ukweli, maalimu atafaidi marupurupu tu na Sio maslahi ya wazanzibar
 
"Ni imani yetu kuwa SUK hii italeta Mabadiliko makubwa kwa Wazanzibari na haswa kuimarisha Umoja wao kupitia maridhiano ya kijamii, kutoa Haki Kwa watu wote walioumizwa na kupoteza maisha Wakati wa uchaguzi na kuweka misingi ya kisheria ya chaguzi za Haki siku za usoni."
Haahaa ni ndoto, muda Sio mrefu maalim ataanza kulalama wanatengwa ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa
 
Sikuona haja ya TAL kukimbia nchi.aliahidiwa kazi na Rais.
Kweli mabeberu wamevishika vichwa vya baadhi ya watu.hapakuwa na ishara yoyote ya kumfanya yeye KIMBIA NCHI ALIYOZALIWA NA KULELEWA KWA UCHINGU
 
Back
Top Bottom