Majibu kwa Ontario kuhusu kuitwa tapeli wa Biashara ya Forex kupitia TMT

habarini wandugu..

naomba jumanne usiku kila mtu awepo online..

nitatoa ushahidi wangu kuhusu utapeli wa forex chini ya TMT..

naandaa ushahidi wote, screen shot zote, maelezo ya mkurugenzi wa tiss aliyetajwa amefukuzwa mlangoni tu kwa mkwara wa ontario.. nitaweka pia maelezo ya BOT kuonesha vibali vya TMT na forex, maelezo ya nacte kuhusu training za TMT kama zimefata utaratibu

maelelezo ya wote walionguza accounts.. audio inayoeleza maelekezo yanayotolewa kwenye training kuhusu broker wao wanaemtaka..

picha ya range rover ontario aliyepiga nayo picha na kudanganya ya kwake..

jumatatu asubuhi nitaenda BOT, TISS na Nacte kukusanya ushahidi kamili... ili dogo aje ajibu hoja kwa facts, maana ana tabia ya kuweka s mapicha picha ya magari ya watu.. na picha picha za graphs za uongo uongo ili kutapeli wa Tanzania maskini...
Itakua vema
 
Nilichogundua mnaoponda huyo Ontario most of you ni loosers mliofikilia ukianza mambo ya forex ni sawa na kushinda biko, ushauri Wangu kung'uteni vumbi matakoni muanze safari upya kuja kutoa shitholes zenu hapa haisaidii!
 
Forex haifundishwi na TMT peke yake Kuna hawa watu wanaitwa Dar Forex mbona hawazungumziwi,so hapo ndo utajua kuwa hawa jamaa wanataka kummaliza ONTARIO na kamwe hawatoweza ndo kwanza wanamuongezea speed,kwa usalama wa akili zao wangeeacha tu maana ONTARIO ndo anazidi kupamba moto na mtakufa na chuki zenu maniner
Mkuu mbona umejibu ukiwa umeghadhibika hivyo?
Hayo nilimuliza Mletamada, je ndie ww uliejibu?
Unadhani ulichojibu ndicho nilichouliza? Halafu mbona umenitusi bila sababu za msingi?
 
Dah nimesoma mstari kwa mstari. .neno kwa neno. .hakika umeandika kile nilichokuwa natamani kukisema muda mrefu saaana...
Hongera brother mimi nipo arusha sijawahi kufaidika na training za Ontario ingawa nilihudhuria..ila baada ya kumpata mtu sahihi anaejua kufundisha tena nilianza na mtaji mdogo wa $500 tu..namtumia templer. ..lkn leo nazungumzia $7000...
Trainer wengi wanachotafuta ni kamishen tu...
 
Mi sikuingiaa fx,lakin watu si walifurahia tu,,hivi niliteteaje maana hata sikumbuki,,halaf hata mi sijaponda kabisa maana sijui chochote kuhusu forex
Hili jibu lako limenichekesha sana... nikama petro alivyoulizwa afu akajibu hiv......
 
Dah nimesoma mstari kwa mstari. .neno kwa neno. .hakika umeandika kile nilichokuwa natamani kukisema muda mrefu saaana...
Hongera brother mimi nipo arusha sijawahi kufaidika na training za Ontario ingawa nilihudhuria..ila baada ya kumpata mtu sahihi anaejua kufundisha tena nilianza na mtaji mdogo wa $500 tu..namtumia templer. ..lkn leo nazungumzia $7000...
Trainer wengi wanachotafuta ni kamishen tu...
Hongera sana kwa kujielewa na kuondoka kwenye minyororo ya ONTARIO na TMT yao. Mwalimu mzuri hakupi hayo masharti ya kipuuzi eti ingia kwa broker fulani kisha huyohuyo broker anapandisha spread makusudi kuwaliza wajinga wengi. Hivi ONTARIO na akili yake changa hivyo atakufundisha nini?

Hongera sana mkuu
 
Ukiona manyowa keshaliwa, wewe ni muhanga wa The bold bila shaka.

Hivyo vibuku tano vyenu mwenzenu na mke kaopowa hapahapa JF.

Hakiyanani vile Tanzania kufa masikini ni jambo la kujitakia tu.
Mimi sijawahi lipia baada ya yeye kuniunga nikawa naona malalamiko kwa watu eti why walipie kwa mwezi halafu uchambuzi wa story usiishe ndani ya mwezi baada ya kuona hivyo nikawa naskilizia tu hadi akiniremove mwenyewe ,siibiwi kijinga Mimi wewe.
 
Nimesoma kwa umakini sana post ya ONTARIO kuhusu kuitwa tapeli na namna alivyojisafisha >> Nakemea vikali ujinga, uongo, Uhuni na utapeli unaoenezwa na baadhi ya JF members

Naomba kuzungumza machache tu kumsaidia kama feedback:-

1. Kwanza nakupongeza ni kijana mdogo lakini umefanya kazi kubwa ya kutafuta maisha.

Je, umewahi kujitathimini juu hicho ulichokiita heshima kwa watu wote? Nadhani wewe ni mmoja ya watu wenye dharau za hali ya juu sana. Kwenye magroup yako tumeshuhudia ukifokea watu wazima mpaka wengine wamekuuliza sisi ni wanao tukiwa humu?

Kwa kifupi jichunguze, jishushe kwa umri wako huo ulipaswa kuwa mtu wa watu huku ukimwaga shikamoo za kutosha kwa watu kuliko kukaa unaunguruma unguruma tu kama kicheche mnyama.

2. Kupitia TMT unajua wazi jambo baya mnalowafanyia wateja wenu. Mnamakubaliano na Broker wa South Africa JP MARKETS kuwa mtapewa kamisheni kwa kumpelekea watu. Kitendo hiki kilifanya apandishe sana Spreads kwa watanzania ili aweze kupata za kuwalipa. Kukuhakikishia hili, mmekuwa mkitoa link ya kujiunga yenye reffaral kwanini?

Hilo linaweza kuwa si shida, shida inakujia hapa wewe na mwenzio Cre mnabroker wengine ambao ndiyo mnatumia wenye spreads ndogo huku mkiwaingiza mkenge wateja wenu. Bisha nilete ushahidi zaidi.

3. Broker yeyote yule duniani anapata faida kutokana na losses za wateja wake. Kwa kulitambua hilo mwenzio Msouth Cre aidha kwa bahati mbaya ama makusudi amekuwa akitoa call za uongo na kusababisha watu wengi sana kuunguza akaunti.

Unajua kuwa katika watu wote mliofundisha zaidi ya 85% wote wamechoma akaunti? Kama unabisha hili niyaanzisha uzi wa kuitisha wote waliochoma akaunti waje watoe ushahidi.

Right mngelikuwa na moyo wa uvumilivu kusikiliza maoni ya watu mliowafundisha ungekufa na presha aisee. Mnatukanwa mno na asilimia kubwa ya wanafunzi wenu sababu ni moja tu:-

Conflict of Interest. How?
Lengo lenu la nje kutoa elimu ya forex bure limegubikwa na uroho mkubwa na tamaa kubwa ya pesa.

Mifano:-
i. Suala la Broker.
Mngelikuwa na nia nzuri tu ya kusaidia watu msingelazimisha watu kutumia JP Markets ambaye anaspread za 63 ili hali kuna brokers wengi wana spreads za 6 -19 tena bila kamisheni. Hapa mna tamaa kubwa ya pesa iliyojificha ndani. Yes unaweza fundisha bure lakini mzigo wa spreads hizo unafanya mtu akatwe zaidi ya $25 kila anapoexcute trade 1 yenye lot size ya 1.

ii. Bei ya training na uhalisia wa mazingira.
Mmekuwa mkilalamika kuwa mnajitolea na hela mnayopata ni ndogo mno haitoshi kitu. Mmejinasibu mnapenda mazingira mazuri n.k lakini semina zako unaendesha kishamba sana. Unashindwa hata kutoa copy za form zako za viapo vya residential na ile ya kujiunga inawatwisha mzigo wanafunzi wako?

Mfano, nilipata habari za Mbeya mliwasumbua sana vijana wa Mbeya watafute hotel ya 5Star ikiwa na ukumbi na malazi ya juu. Wakashinda siku nzima wakapata hoteli kama tatu nzuri tu. Lakini kwa uroho na tamaa ya pesa mkaishia kuwarundika Mfikemo Bar tena kwenye kichumba kidogo sana na wengi walilalamika sana nje hawakuwa hata na mazingira mazuri ya kusomea.

Acheni kusema mnajitolea bure, watu mia wakilipa laki moja kila mtu unazungumzia million 10 kwa training ya siku 5 tena ya kizembe kabisa utasemaje unajitolea bure? Mungu anawaona. Kuweni wakweli kuwa mnapata faida kwenye hiyo pesa na kamisheni za broker.

4. Hivi umewahi kufanya hata utafiti ujue majeraha ya wanafunzi uliowafundisha? Kwa taarifa yako hata hao wanaokuletea ushuhuda hawajawaprofitable walibahatisha tu siku moja ama wiki moja ama mwezi mmoja. Lakini ukweli ni kuwa wanafunzi wengi sana mliofundisha wamejeruhiwa sana kifedha. Wengine wametumia ada kwa kuaminishwa watawin na wamepoteza. Yaani mngekuwa mnaweza kuvumilia watoe maoni usingeamini bahati mbaya mtu akiuliza kitu mnamremove haraka sana kwenye group lenu.

Kwa ukweli tu ufundishaji wenu ni mbovu. Na huenda ni makusudi ili mpate faida za broker ndiyo maana mnakuwa wakali wanafunzi wenu wakitumia broker mwingine. Yaani kwenye wanafunzi wote mliofundisha nionyeshe hata mmoja tu ambaye alikuja hajui kitu mkamfundisha na akawa profitable trader. Onyesha mmoja tu. Ninachojua asilimia ya watu wachache ambao wameweza kutrade vizuri ni wale walikuja na knowledge ya Forex kubwa tu, wengine wamekimbia ForexIndustrySwahili.

Najua unajua kabisa kipi unapaswa kumfundisha mwanafunzi ili aqe trader mzuri zaidi ni ukitoa uroho wa tamaa ya pesa tu uliojificha ndani.

Mwisho, wewe unasimama kama shujaa uliyeitangaza forex na kwamba hata waliokuwa wanaijua na kula kimyakimya wamejitokeza na kuanza kujitangaza na kufundisha kwa hili nakupongeza sana ila mapungufu yako ndiyo hapo hapo juu kama utaona la maana chukua na ulifanyie kazi.

Narudia tena wewe ni shujaa hayo juu ni mapungufu tu hakuna binadamu asiye na mapungufu wanashindwa tu kukuambia sababu ya pungufu lako la kiburi na kujikweza.
Forex ni biashara nzuri kwa mtu akiielewa hakika inalipa.
---------

Nyongeza;

* Nimesoma comment nyingi mnamtukana ONTARIO mnakosea sana. Tulichofanya hapa ni kumpa mrejesho ili ajirekebishe.

* Mimi nimelose zaidi ya $10,000. Lakini kwenye forex kulose tunaita investiment expenses. Kitendo cha kulose kiliniumiza sana na kunifanya nitafute mwalimu mzuri, nashukuru sasa nakula matunda.

* Kuna watu wanasema broker anapata faida hata kama hujalose hawa hawajui forex. Kwa kuwasaidia tu je, mnajua kuwa broker nao wanatrade? Hebu ingia google search kitu kinaitwa broker winners and losera group jisomee.

* Mimi nikikutana na Ontorio hata leo naweza mpa hata million 5 za shukrani si kwa kunifunza ila kunifumbua macho kuwa kuna forex. Unajua wanachofunza ni too general hawana mwongozo mzuri. Wanafunzi wote wa Ontorio aliofunza na mwalimu alonifunza mimi akafundisha watano tu tena kutumia indicator tu ya Moving Avarage watapiga pesa kuliko wanafunzi alofunza ONTARIO.

Tusimtukane please wala kutukana TMT wachukue haya mapungufu wajirekebishe. Forex ni biashara tu kama zingine na inalipa sana tu.

Mimi sitaleta ushahifi hapa ushahidi wote anao yeye ontorio na wanafunzi wake. Kuleta hapa ni kumdhalilisha zaidi, wakati ameona na amejifunza.


Asante.

Zaidi soma=>Shahidi namba 2: Majibu kwa Ontario kuhusu kuitwa tapeli (Forex)
HAHAHAHAHAHA NAONA MMESHA ONGEA NA ONTARIO UKAOMBBA MSAMAHA
 
Mimi na huyo Ontario ata anikate kichwa sitii mguu kwenye huo upuuzi wa kupenda dola kuliko shilling yangu ya Tsh...! Kwanza ni kukosa uzalendo pili huyo jamaa twende turudi jamaa lazima kuna angle anawatumia kugonga pesa.
ukipata dola si unachange to tsh au
 
Back
Top Bottom