Majibu kwa Lizaboni, kuhusu upotoshaji wa makusudi wenye dhamira mbaya dhidi ya Rajab Luhwavi na CCM

Status
Not open for further replies.

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
LIZABONI NA DHANA ZA KITOTO

Utangulizi
Siku ya tarehe 13/07/2016, Mwana JF na kijana mwenzetu mpendwa maarufu kama Lizaboni, alikuja na hoja aliyoipa kichwa cha habari “Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara”. Nikiwa kama kada Mwaminifu na mwenye upeo wa fikra za kimapinduzi nimeona si vema kukaa kimya. Nimeona ni vema kutumia fursa hii kuupasha Umma juu ya upotoshaji huu ili siku zote “Jamii Forum” libaki kuwa jukwaa huru lenye taswira chanya katika maendeleo badala ya kujikita katika Udaku kama inavyoonekana na kumpendeza Lizaboni.

Hoja Dhaifu kutoka kwa Kijana wetu Lizaboni.
Nilipozikagua hoja za Ndugu yangu Lizaboni, nikaona zimejikita katika maeneo makuu matatu yenye dhamira za kitoto kama ifuatavyo:-

Hoja za kizushi zinazojengwa kwa dhana ya mabadiliko ya hila za wanaotafuta uongozi. Napenda Umma wa WanaCCM na Watanzania wote wajue kwamba:-
Ziara za Naibu Katibu Mkuu Comrade Rajab Luhwavi zilifanyika kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi isipokuwa maeneo mawili tu; ambapo alifanya ziara kwa maelekezo ya Katibu Mkuu kwa kuwa yalikuwa na mivutano iliyohitaji kutulizwa.

Comrade Luhwavi alikutana na Watumishi wa CCM kwa madhumuni ya kuwashukuru baada ya juhudi zao kubwa zilizofanikisha kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kwa niaba ya Katibu Mkuu, Luhwavi aliwasilisha shukrani hizi kwa Watumishi wa CCM.

Comrade Luhwavi alikutana na Watumishi wa CCM kwa madhumuni ya kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzitolea ufafanuzi.
Comrade Luhwavi alikuwa na jukumu la kufikisha ujumbe wa umuhimu wa Wafanyakazi wa Chama kupata Bima ya Afya.

Fedha za Uchaguzi
Majukumu ya Msingi ya Comrade Luhwavi kama Naibu Katibu Mkuu ni pamoja na masuala ya utumishi, utawala, na operesheni maalum na sio kufanya malipo.
Comrade Luhwavi hausiki, wakati wa kawaida au wakati wa uchaguzi na malipo ya fedha kwa kuwa Katiba ya CCM inampa Mamlaka hayo Katibu wa Uchumi na Fedha kwa kila Ngazi kusimamia utaratibu huo. Kwa Makao Makuu, yupo Katibu wa Uchumi na Fedha (Mweka Hazina) akisaidiwa na Mhasibu Mkuu na Mkaguzi Mkuu wa ndani, hivyo haupo uhusiano wa Naibu Katibu Mkuu kutumia Fedha za uchaguzi kama alivyooeleza Lizaboni. Hivyo haupo uhusiano wa Naibu Katibu Mkuu kutuma fedha wala kupeleka fedha za uchaguzi kati ya Jimbo moja au Wagombea wa Uchaguzi.

Katiba ya CCM inampa mamlaka Katibu Mkuu na Makatibu wa Mikoa, Wilaya, Kata na Matawi mamlaka kamili ya Kikatiba ya udhibiti wa fedha na mali za Chama kwa kushirikiana na Katibu wa Uchumi na Fedha. Hivyo, anachokisema Lizaboni hakina nafasi kwa Naibu Katibu Mkuu Bwana Luhwavi kutokana na mfumo wa utawala wa CCM.

CCM si kama vyama vingine ambavyo mtu mmoja anajitwalia madaraka yote. CCM ina mfumo wa Kikatiba ambao utatoa Mamlaka kamili na uongozi wa pamoja kwa kila ngazi. Hivyo, hakuna uwezekano wowote wa mtu mmoja kuhodhi madaraka yote.

Kuhusu Rais John Pombe Magufuli kupewa Uenyekiti:
Wasiomwelewa Comrade Luhwavi wanapaswa wajifunze, laa sivyo watapata shida. Luhwavi amekuwa Mtumishi wa Chama kwa miaka zaidi ya 22 sasa. Kabla, aliwahi kutumikia Umoja wa Vijana kutoka 1983 hadi 1987 kama Katibu wa Vijana wa Wilaya kwa muda mrefu, Mwenyekiti wa Vijana Mkoa, Mkuu wa Idara, Mjumbe wa Baraza Kuu na nafasi nyingine za uongozi na utendaji wa CCM. Kupitia utumishi huo katika nafasi mbalimbali na kwa muda mrefu, amejifunza na kuyajua mengi ndani ya Chama na Serikali zake. Inawezekana, kujua huku, ndiko kunakowatia hofu waroho wa madaraka tena wale ambao hawana uwezo. Si rahisi kwa Mwanachama wa CCM kama Luhwavi, aliyelelewa na kukomaa katika misingi ya Kimapinduzi ya Chama chetu, ashindwe kutambua kwamba ni muda muafaka kwa sasa kukabidhiwa jukumu la Uenyekiti wa Chama chetu kwa Rais John Pombe Magufuli hasa muda huu baada ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu.

Kwa bahati mbaya sana, yeye au aliyemtuma au kwa umoja wao, hawaelewi na hawataki kujifunza namna Chama Cha Mapinduzi kilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu na nini nafasi ya Comrade Luhwavi katika kazi hiyo ngumu ya kuipigania Dola. Sisi Makada wa Mstari wa mbele, tunamtambua aliyekuwa akiongoza Operesheni zote zilizosaidia CCM kuibuka Mshindi na Dkt. Magufuli kuwa Rais kupitia Chama chetu. Wanamapinduzi kama Luhwavi daima huzingatia kuweka historia ya vizazi ili waje kujifunza. Kwa historia aliyoiasisi ya kukabiliana na bughdha zote za upinzani kama Mkuu wa Operesheni ya Uchaguzi Mkuu 2015, historia hii itahitimishwa kwa kuhakikisha Mkutano Mkuu Maalum unafanyika na kumteua Mwenyekiti mpya kwa utaratibu wa mbio za kupokezana vijiti. Poleni msiolitambua hili.

Hoja ya uteuzi kutozingatia Makada wa CCM, nachelea kusema kwamba upeo mdogo au makengeza ya upotoshaji wa makusudi hauwezi kuliona jambo hili. Lakini, senti zilizotumika kama pamba, zimeziba masikio; huku ukosefu wa uerevu umeziba macho hivyo hakuna kusikia au kuona, wala kusoma vyombo vya habari vyote vilivyodiriki kuponda teuzi zote. Mathalan, Lizaboni atueleze kisa cha kutenguliwa uteuzi wa yule Mkurugenzi aliyebainika kugombea ubunge kupitia chama fulani kichanga. Lizaboni anaweza kujiongeza kwa kutembelea Post ya Barafu ya tarehe 29/06/2016 humuhumu Jamii Forum kwa kichwa cha habari “Kwa uteuzi huu wa DC Longido, UKAWA wajiandae kupoteza Jimbo” au Post ya Mwanahabari Huru ya tarehe 7/7/2016 yenye kichwa cha habari; “Makada wa CCM waibua mjadala: Ni baada ya Teuzi za Juzi zinapingwa”.

Atueleze kama ni nani mpotoshaji wa umma baina ya hoja dhaifu za Lizaboni kwamba uteuzi wa Magufuli hauzingatii Ukada wa CCM dhidi ya maudhui ya Picha na sentesi ya kwanza tu katika Post hizo za Barafu na Mwanahabari Huru ktk Forum hii au vyombo vyote vya habari vilivyopiga kelele kila teuzi kwa kuwa zinazingatia heshima kwa Makada wa CCM.

Hitimisho
Huu ni upotoshaji wa makusudi wenye dhamira mbaya dhidi ya Chama Cha Mapinduzi, Comrade Luhwavi na Wazalendo waliopewa jukumu la kuyalinda na kuyatetea Mapinduzi ya wakulima na wafanyakazi. Ujumbe wa Lizaboni umejazwa dhana za kihafidhina kutoka kwa wanyonyaji waliojivika ngozi za kizalendo ambapo mtekelezaji ametekeleza pasipo kujua dhamira yao kwamba pengine ni uroho wa vyeo wasivyoviweza. Tunatambua, Lizaboni si Mwanachama wa CCM, mwepesi kutumika kama “tooth pic” na wa kumuonea huruma. Kwani, mara nyingi, asiyejitambua huishia jehanamu.

Ujumbe wa Lizaboni na Manyapara wake, umegubikwa na wingu la giza nene linaloashiria kutoijua CCM au inavyofanya kazi. Ndiyo maana, hawajui kama ukiacha nafasi ya Uenyekiti wa Vijana Mkoa wa Singida, Comrade Luhwavi hajawahi kufikiria wala kudiriki kuomba kazi za utendaji au uongozi ndani ya CCM. Nafasi zote alizozipata zinatokana na yeye kujulikana ndani ya CCM kwa tabia na vitendo vyake vya kimapinduzi na si vinginevyo. Sifa hizi, ndizo zilizomfanya kuaminiwa kupewa jukumu la kusimamia Operesheni zote zilizoiletea CCM heshima kubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Mnaodhani Unaibu Katibu Mkuu au Ukatibu Mkuu wa CCM unaombwa, shime, nendeni kwa Mwenyekiti Mtarajiwa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mkamuombe awape vyeo hivyo pasipo kujifedhehesha kwa kujaribu kutumia jukwaa hili au lingine lolote kuhujumu fikra na taswira njema za watu wema. Nasisitiza tena, Comrade Luhwavi anajulikana sana kwa tabia na vitendo vyake, ziara zake hakuna kiongozi wa kitaifa asiyejua dhamira na maudhui yake. Sisi kama Makada wa mstari wa mbele, tuko tayari kumsaidia mwana Mapinduzi mwenzetu.

Wote mnatambua uwezo na fikra za Comrade Luhwavi kwamba ni sawa na “kamusi au kitabu” kutokana na kujua kwake. Lizaboni omba clip za ziara hizo Redio Uhuru au Gazeti kongwe la Uhuru ili pate ukweli, labda pengine utakuwa miongoni mwa waungwana na raia mwema.

=======

Mjadala huu unaendelea hapa=>DC wa Kinondoni Ali Hapi ama unashiriki kwenye mkakati huu dhidi ya Magufuli au unawajua wahusika'
 
Lizaboni tungesema sisi ni wewe ni shakubimbi usingekosa jibu lakini hao ni wakunyumba wanasema hivyo.
Sasa unafiki hadi ndani ya nyumba unayoishi na kula itakuwaje kwa jirani? AIBU HIYO, MZUSHI MKUBWA. Kweli kuna matatizo ndani ya ccm lakini umemsingizia mengi kiongozi wako, na sasa utafukuzwa rasmi group 46
 
Hahahaha lizaboni nilishangaa maana Toka nimemjua hapa sijawahi kuona ameweka walaka Kama ule nahisi alitumwa tu.
"Akili za kuambiwa changanya na zako"
Subirini Lizabon atafunguka. Mchezo umeanza. Hizi ni kambi mbili. Bandiko la huyu bwana lina mtetea Luhwavi. (yawezekana akawa yeye mwenyewe anaona mambo yameisha tibuka hivyo akaamua kutoka kimtindo huu).
Lizabon njoo ujibu tuhuma zinazokukabili. Kama kweli hukuwa na nia ya kupotosha umma tadhali njoo tusikie tena upande wako.
 
LIZABONI NA DHANA ZA KITOTO

Utangulizi
Siku ya tarehe 13/07/2016, Mwana JF na kijana mwenzetu mpendwa maarufu kama Lizaboni, alikuja na hoja aliyoipa kichwa cha habari “Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara”. Nikiwa kama kada Mwaminifu na mwenye upeo wa fikra za kimapinduzi nimeona si vema kukaa kimya. Nimeona ni vema kutumia fursa hii kuupasha Umma juu ya upotoshaji huu ili siku zote “Jamii Forum” libaki kuwa jukwaa huru lenye taswira chanya katika maendeleo badala ya kujikita katika Udaku kama inavyoonekana na kumpendeza Lizaboni.

Hoja Dhaifu kutoka kwa Kijana wetu Lizaboni.
Nilipozikagua hoja za Ndugu yangu Lizaboni, nikaona zimejikita katika maeneo makuu matatu yenye dhamira za kitoto kama ifuatavyo:-

Hoja za kizushi zinazojengwa kwa dhana ya mabadiliko ya hila za wanaotafuta uongozi. Napenda Umma wa WanaCCM na Watanzania wote wajue kwamba:-
Ziara za Naibu Katibu Mkuu Comrade Rajab Luhwavi zilifanyika kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi isipokuwa maeneo mawili tu; ambapo alifanya ziara kwa maelekezo ya Katibu Mkuu kwa kuwa yalikuwa na mivutano iliyohitaji kutulizwa.

Comrade Luhwavi alikutana na Watumishi wa CCM kwa madhumuni ya kuwashukuru baada ya juhudi zao kubwa zilizofanikisha kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kwa niaba ya Katibu Mkuu, Luhwavi aliwasilisha shukrani hizi kwa Watumishi wa CCM.

Comrade Luhwavi alikutana na Watumishi wa CCM kwa madhumuni ya kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzitolea ufafanuzi.
Comrade Luhwavi alikuwa na jukumu la kufikisha ujumbe wa umuhimu wa Wafanyakazi wa Chama kupata Bima ya Afya.

Fedha za Uchaguzi
Majukumu ya Msingi ya Comrade Luhwavi kama Naibu Katibu Mkuu ni pamoja na masuala ya utumishi, utawala, na operesheni maalum na sio kufanya malipo.
Comrade Luhwavi hausiki, wakati wa kawaida au wakati wa uchaguzi na malipo ya fedha kwa kuwa Katiba ya CCM inampa Mamlaka hayo Katibu wa Uchumi na Fedha kwa kila Ngazi kusimamia utaratibu huo. Kwa Makao Makuu, yupo Katibu wa Uchumi na Fedha (Mweka Hazina) akisaidiwa na Mhasibu Mkuu na Mkaguzi Mkuu wa ndani, hivyo haupo uhusiano wa Naibu Katibu Mkuu kutumia Fedha za uchaguzi kama alivyooeleza Lizaboni. Hivyo haupo uhusiano wa Naibu Katibu Mkuu kutuma fedha wala kupeleka fedha za uchaguzi kati ya Jimbo moja au Wagombea wa Uchaguzi.

Katiba ya CCM inampa mamlaka Katibu Mkuu na Makatibu wa Mikoa, Wilaya, Kata na Matawi mamlaka kamili ya Kikatiba ya udhibiti wa fedha na mali za Chama kwa kushirikiana na Katibu wa Uchumi na Fedha. Hivyo, anachokisema Lizaboni hakina nafasi kwa Naibu Katibu Mkuu Bwana Luhwavi kutokana na mfumo wa utawala wa CCM.

CCM si kama vyama vingine ambavyo mtu mmoja anajitwalia madaraka yote. CCM ina mfumo wa Kikatiba ambao utatoa Mamlaka kamili na uongozi wa pamoja kwa kila ngazi. Hivyo, hakuna uwezekano wowote wa mtu mmoja kuhodhi madaraka yote.

Kuhusu Rais John Pombe Magufuli kupewa Uenyekiti:
Wasiomwelewa Comrade Luhwavi wanapaswa wajifunze, laa sivyo watapata shida. Luhwavi amekuwa Mtumishi wa Chama kwa miaka zaidi ya 22 sasa. Kabla, aliwahi kutumikia Umoja wa Vijana kutoka 1983 hadi 1987 kama Katibu wa Vijana wa Wilaya kwa muda mrefu, Mwenyekiti wa Vijana Mkoa, Mkuu wa Idara, Mjumbe wa Baraza Kuu na nafasi nyingine za uongozi na utendaji wa CCM. Kupitia utumishi huo katika nafasi mbalimbali na kwa muda mrefu, amejifunza na kuyajua mengi ndani ya Chama na Serikali zake. Inawezekana, kujua huku, ndiko kunakowatia hofu waroho wa madaraka tena wale ambao hawana uwezo. Si rahisi kwa Mwanachama wa CCM kama Luhwavi, aliyelelewa na kukomaa katika misingi ya Kimapinduzi ya Chama chetu, ashindwe kutambua kwamba ni muda muafaka kwa sasa kukabidhiwa jukumu la Uenyekiti wa Chama chetu kwa Rais John Pombe Magufuli hasa muda huu baada ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu.

Kwa bahati mbaya sana, yeye au aliyemtuma au kwa umoja wao, hawaelewi na hawataki kujifunza namna Chama Cha Mapinduzi kilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu na nini nafasi ya Comrade Luhwavi katika kazi hiyo ngumu ya kuipigania Dola. Sisi Makada wa Mstari wa mbele, tunamtambua aliyekuwa akiongoza Operesheni zote zilizosaidia CCM kuibuka Mshindi na Dkt. Magufuli kuwa Rais kupitia Chama chetu. Wanamapinduzi kama Luhwavi daima huzingatia kuweka historia ya vizazi ili waje kujifunza. Kwa historia aliyoiasisi ya kukabiliana na bughdha zote za upinzani kama Mkuu wa Operesheni ya Uchaguzi Mkuu 2015, historia hii itahitimishwa kwa kuhakikisha Mkutano Mkuu Maalum unafanyika na kumteua Mwenyekiti mpya kwa utaratibu wa mbio za kupokezana vijiti. Poleni msiolitambua hili.

Hoja ya uteuzi kutozingatia Makada wa CCM, nachelea kusema kwamba upeo mdogo au makengeza ya upotoshaji wa makusudi hauwezi kuliona jambo hili. Lakini, senti zilizotumika kama pamba, zimeziba masikio; huku ukosefu wa uerevu umeziba macho hivyo hakuna kusikia au kuona, wala kusoma vyombo vya habari vyote vilivyodiriki kuponda teuzi zote. Mathalan, Lizaboni atueleze kisa cha kutenguliwa uteuzi wa yule Mkurugenzi aliyebainika kugombea ubunge kupitia chama fulani kichanga. Lizaboni anaweza kujiongeza kwa kutembelea Post ya Barafu ya tarehe 29/06/2016 humuhumu Jamii Forum kwa kichwa cha habari “Kwa uteuzi huu wa DC Longido, UKAWA wajiandae kupoteza Jimbo” au Post ya Mwanahabari Huru ya tarehe 7/7/2016 yenye kichwa cha habari; “Makada wa CCM waibua mjadala: Ni baada ya Teuzi za Juzi zinapingwa”.

Atueleze kama ni nani mpotoshaji wa umma baina ya hoja dhaifu za Lizaboni kwamba uteuzi wa Magufuli hauzingatii Ukada wa CCM dhidi ya maudhui ya Picha na sentesi ya kwanza tu katika Post hizo za Barafu na Mwanahabari Huru ktk Forum hii au vyombo vyote vya habari vilivyopiga kelele kila teuzi kwa kuwa zinazingatia heshima kwa Makada wa CCM.

Hitimisho
Huu ni upotoshaji wa makusudi wenye dhamira mbaya dhidi ya Chama Cha Mapinduzi, Comrade Luhwavi na Wazalendo waliopewa jukumu la kuyalinda na kuyatetea Mapinduzi ya wakulima na wafanyakazi. Ujumbe wa Lizaboni umejazwa dhana za kihafidhina kutoka kwa wanyonyaji waliojivika ngozi za kizalendo ambapo mtekelezaji ametekeleza pasipo kujua dhamira yao kwamba pengine ni uroho wa vyeo wasivyoviweza. Tunatambua, Lizaboni si Mwanachama wa CCM, mwepesi kutumika kama “tooth pic” na wa kumuonea huruma. Kwani, mara nyingi, asiyejitambua huishia jehanamu.

Ujumbe wa Lizaboni na Manyapara wake, umegubikwa na wingu la giza nene linaloashiria kutoijua CCM au inavyofanya kazi. Ndiyo maana, hawajui kama ukiacha nafasi ya Uenyekiti wa Vijana Mkoa wa Singida, Comrade Luhwavi hajawahi kufikiria wala kudiriki kuomba kazi za utendaji au uongozi ndani ya CCM. Nafasi zote alizozipata zinatokana na yeye kujulikana ndani ya CCM kwa tabia na vitendo vyake vya kimapinduzi na si vinginevyo. Sifa hizi, ndizo zilizomfanya kuaminiwa kupewa jukumu la kusimamia Operesheni zote zilizoiletea CCM heshima kubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Mnaodhani Unaibu Katibu Mkuu au Ukatibu Mkuu wa CCM unaombwa, shime, nendeni kwa Mwenyekiti Mtarajiwa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mkamuombe awape vyeo hivyo pasipo kujifedhehesha kwa kujaribu kutumia jukwaa hili au lingine lolote kuhujumu fikra na taswira njema za watu wema. Nasisitiza tena, Comrade Luhwavi anajulikana sana kwa tabia na vitendo vyake, ziara zake hakuna kiongozi wa kitaifa asiyejua dhamira na maudhui yake. Sisi kama Makada wa mstari wa mbele, tuko tayari kumsaidia mwana Mapinduzi mwenzetu.

Wote mnatambua uwezo na fikra za Comrade Luhwavi kwamba ni sawa na “kamusi au kitabu” kutokana na kujua kwake. Lizaboni omba clip za ziara hizo Redio Uhuru au Gazeti kongwe la Uhuru ili pate ukweli, labda pengine utakuwa miongoni mwa waungwana na raia mwema.
Acha wafu wazikane wenyewe kwa wenyewe...
 
Lizaboni nilikwambia, nilikuwa naaminini Kada uliyeiva lakini umeonesha udhaifu mkubwa sana utafikiri ni mgeni ndani ya chama, siwezi kukutuhumu kama umepewa fedha ua umeahidiwa nini lakini naamini hata wewe utagundua ujinga ulioufanya. Unajiondolea sifa nzuri ulizokuwa nazo kama kada. Umekuwa mpiga zumali sasa na mleta makundi na fitna migongano ndani ya chama kupitia mitandao
 
Wewe utakuwa umetumwa, mbona alichokiandika Lizaboni kiko wazi kabisa na kila mtu anawaona wafuasi wa Luhwavi wanavyohangaika huku uraiani kutaka kukwamisha Rais Magufuli asiwe mwenyekiti wa CCM. Luhwavi baada ya kutimuliwa ikulu, hana uhakika wa kuendelea kuwa na nafasi ndani ya CCM, JEMBE likikabidhiwa chama.
 
Namuunga Mkono Lizaboni
Kama kusemwa yalisemwa hata kabla ya Lizaboni

Hakuna mtoto hapa
Kila mtu anajionea
Kama mpango umeingia doa basi muache unafiki.
Lengo tunataka Magu awe Rais na mwenyekiti wa Ccm hakuna lingine.

Kila mtu anauhuru wakutoa Maoni
Na kueleza kile alicho kiona.
Najua Ccm NI chama kikubwa
Kinasemwa,kinakosolewa,kinapingwa
Sio kama vyama vingine Marufuku kukosoa
Hivyo kumuita Lizaboni mtoto sio vizuri,
Mpinge kwa hoja tu.

RAIS ALISEMA WATOTO NI KINA NANI
WAKATI WA KUZINDUA BUNGE
 
Hakuna tabia mbaya kama unafki, daaah Lizaboni unaumbuka kitoto sana mkuu, yan aibu! aibu! aibu yako!!
Sijaona hoja yoyote hapa ya kukanusha ukweli aliouandika Lizaboni, naona kama
Namuunga Mkono Lizaboni
Kama kusemwa yalisemwa hata kabla ya Lizaboni

Hakuna mtoto hapa
Kila mtu anajionea
Kama mpango umeingia doa basi muache unafiki.
Lengo tunataka Magu awe Rais na mwenyekiti wa Ccm hakuna lingine.

Kila mtu anauhuru wakutoa Maoni
Na kueleza kile alicho kiona.
Najua Ccm NI chama kikubwa
Kinasemwa,kinakosolewa,kinapingwa
Sio kama vyama vingine Marufuku kukosoa
Hivyo kumuita Lizaboni mtoto sio vizuri,
Mpinge kwa hoja tu.

RAIS ALISEMA WATOTO NI KINA NANI
WAKATI WA KUZINDUA BUNGE
Lizaboni amewatoa nyoka pangoni, chezea ukweli, unauma sana.
 
Lizaboni nilikwambia, nilikuwa naaminini Kada uliyeiva lakini umeonedha udhaifu mkubwa sana utafikiri ni mgenj ndani ya chama, siwezi kukutuhumu kama umepewa fedhaua umeahidiwa nini lakini naamini hata wewe utagundua ujinga ulioufanya. Unajiondolea sifa nzuri ulizokuwa nazo kama kada. Umekuwa mpiga zumali sasa na mleta makundi na fitna migongano ndani ya chama.
Mbona mnajikanyaga sana. Halafu mleta mada inaonekana kabisa ID nyingi kwenye mada hii ni zako. Ni kama umetumwa kwa kile unaamini utazima mashambulizi ya Lizaboni. Lizaboni huwa haongopi, mada zake nyingi sana humu zimekuwa ni za kweli tupu
 
Dhumuni kuu la Lizaboni nikutoa ukungu kwa watu
Pia kuwaambia watu mchezo wao mchafu hauwezi timia,
Naona wameona mambo magumu
Lakini ukweli upo palepale
 
Lizaboni sio mwanachama wa ccm...ni mamluki.mnafiki..sokomoko mpenda sifa..anatumika na mafisadi kuchafua chama
 
Status
Not open for further replies.
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom