Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,370
- 39,186
Tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi:
Serikali yasema ni uzushi mtupu
(Kutoka gazeti la Uhuru)
NA MWANDISHI WETU
BAADA ya serikali kufuatilia kwa kina tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali zilizotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, imebaini ni za uzushi na upotoshaji wa makusudi wa ukweli.
Tamko la serikali lililotolewa jana jijini Dar es Salaam lilieleza tuhuma za Dk. Slaa zinalenga kujengea umaarufu vyama vya siasa vya upinzani kwa kudhoofisha umoja wa kitaifa.
Kwa ujumla, tuhuma za Dk. Slaa dhidi ya viongozi wa umma hazina ukweli wowote, bali zina lengo la kuchochea chuki dhidi ya serikali na kutaka kudhoofisha umoja na mshikamano wa taifa letu, ilieleza sehemu ya tamko hilo.
Septemba 15, mwaka huu, Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, akiwa na viongozi wa muungano wa vyama vya siasa vya upinzani, alitoa tamko hadharani linalowataja watuhumiwa wa ufisadi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Temeke, Dar es Salaam.
Miongoni mwa tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa ni ubadhirifu wa mali za umma dhidi ya taasisi mbalimbali kama Benki Kuu ya Tanzania (BoT), NBC, NMB, mikataba ya ubinafsishaji na ununuzi wa mali za umma.
Serikali imefafanua kuwa, waliotajwa kuingiza fedha za kigeni nchini na baadaye kulipwa na BoT, walikuwa wameagiza bidhaa kutoka nje ya nchi miaka ya 1980, ambapo BoT ilipokea malipo yao kutoka NBC.
Tamko hilo lilisema BoT ilishindwa kuwalipa kwa wakati, baada ya kupokea fedha hizo NBC kwa sababu haikuwa na fedha za kutosha za kigeni.
Tuhuma kwamba kulikuwa na shinikizo kwa kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington, Marekani, kupewa kazi ya kukagua hesabu za kampuni za uchimbaji dhahabu, serikali ilisema si kweli.
Ilieleza kuwa kampuni hiyo ilipatikana kwa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi wa umma na hakukuwa na shinikizo lolote.
Juu ya rushwa katika mkataba kati ya serikali na Alex Stewart, serikali ilisema suala hilo liko mahakamani, hivyo haina uwezo wa kulizungumzia.
Kuhusu tuhuma za uuzaji wa rasilimali za taifa, ununuzi wa ndege ya Rais, ubinafsishaji wa NBC na NMB, serikali ilisema hazina msingi wala ushahidi wowote, bali zinajaribu kujenga mazingira ya kujipatia umaarufu usiostahili.
Serikali imetafsiri tuhuma hizo kuwa jaribio la kuwavunja moyo wananchi, kuhusu manufaa ya utekelezaji wa programu iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 na kama ilivyotafsiriwa katika bajeti ya mwaka 2007/2008.
Serikali inawahakikishia wananchi kuwa inapinga vitendo vya rushwa nchini kwa nguvu zake zote na msimamo wake ni thabiti kuhusiana na suala hili, ilieleza sehemu ya tamko hilo.