Majibu dhidi ya Makala ya waziri wa CUF aliyeporomoshea matusi CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu dhidi ya Makala ya waziri wa CUF aliyeporomoshea matusi CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Oct 15, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  KUPITIA gazeti hili toleo la Jumatano iliyopita, Waziri wa Afya na Mjumbe wa CUF Taifa, Mheshimiwa Juma Duni Haji aliandika makala kujibu makala zangu kama tatu nilizoandika kuhusu Chama cha CUF, na maadili yanayotiliwa shaka kuhusu madhumuni ya Vision for Change (V4C), mjadala mpana wa mapato na matumizi na tuhuma nyingine ya kuwa CCM B.

  Namshukuru Mheshimiwa Juma Duni Haji kujitokeza, ingawa ni katika hali ambayo sikuitarajia.

  Alikuwa ni kama anajibu hoja, lakini aliporomosha matusi na maneno ambayo si mazuri kwa umri wangu, maadili yangu na ya Watanzania. Siwezi hata kufikiri kuyarudia kuyaandika humu.

  Bahati mbaya niliuliza malengo ya Vision for change, na kusema CUF ‘wanakopi na kupesti’, wao hawana fikra. Niliuliza masuala ya mapato na matumizi, lakini mheshimiwa Duni badala ya kujibu hayo akashambulia mtu mmoja mmoja kwa vitu ambavyo kabisa havihusiani na hoja za msingi za makala hizo.

  Niwaombe kupitia makala hii wote mliotukanwa katika makala iliyopita kusamehe, pengine waziri alipata jazba baada ya kusoma falsafa hii ambayo daima nitasema ukweli ili taifa letu linufaike, liendelee kudumu.

  Kifupi tu niseme, namheshimu sana Mzee Juma Duni Haji, sio tu kwa kuwa ni Waziri wa Afya au Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa, bali kwa maadili ya Kiafrika kwa umri wake anastahiki kuheshimiwa.
  Lakini pamoja na kumheshimu siogopi kumuuliza maswali kadhaa yanayohusu mustakabali wa taifa letu na malengo ya CUF kwa kuwa amejitokeza.

  Ningetarajia Juma Duni Haji aone aibu kujitokeza akizungumzia Vision for Change, dira ya mabadiliko, ambayo ni kaulimbiu ya chama kipya cha ADC.

  ADC ni chama kilichopata usajili wake wa kudumu Agosti 28, 2012 huku kaulimbiu yake ikiwa ni ADC-Dira ya Mabadiliko.
  Lakini CUF walioanza na ‘Vision for Change ‘wameiba’ kaulimbiu hiyo ya ADC na wanazunguka huku na kule kuhubiri chama cha wenzao kwa jina tofauti. Wanahubiri ADC kwa jina la CUF.

  Ikumbukwe ADC – Dira ya mabadiliko imesajiliwa rasmi na kisheria kwa Msajili wa Vyama.

  Ukiachilia mbali kuiga mbinu na mikakati toka Movement for Change (M4C) ya CHADEMA, CUF pia wamekiibia hiki chama kidogo kipya kaulimbiu yake. Hii haikuonekana kwa Waziri huyu, badala yake akaona aporomoshe matusi.

  Ilikuwa ni fursa nzuri kwake kutoa ufafanuzi kwa wananchi kwanini chama cha CUF kinawakamua sana wabunge wake, kinawachangisha kila mwezi sh 1,250,000 (milioni moja na laki mbili na nusu) kwa ajili ya maendeleo ya chama, ilhali vyama vingine vya CCM na CHADEMA vinachangisha laki moja tu.

  Hivyo kuwa Mbunge wa CUF inabidi kweli ujinyime kwa ajili ya chama.

  Juma Duni Haji alipaswa kueleza mapato na matumizi hayo, pesa lukuki hizi hutumikaje kuendeleza chama, badala ya kunufaisha kundi fulani katika CUF?

  Kabla ya kuwa Waziri wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Juma Duni Haji alikuwa Mkurugenzi wa Fedha, Rasilimali na Uchumi wa CUF, ndiye aliyesimamia kukusanya michango ya sh mil. 30 kila mwezi kutoka sehemu ya ruzuku ya chama chake kwa miaka mitano, hivyo kufikia 2010, chama kilitarajiwa kuwa na makusanyo ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane (1,800,000,000).

  Kwa kuwa idadi ya wabunge wa CUF (walikuwa 32), ambao kwa ajili ya uchaguzi kila mmoja alichangishwa shilingi milioni nane, ilifanya mchango wao kuelekea Uchaguzi Mkuu kuwa sh 256,000,000.

  Hivyo kwa hesabu ya haraka CUF walikuwa na zaidi ya shilingi bilioni mbili bila kuhesabu akiba zingine za ruzuku na michango ya wanachama wengine.

  Lakini Watanzania wanakumbuka kuwa CUF kilifanya kampeni za kinyonge sana, tena kwa hali ngumu, kikawa na magari mabovu jambo lililomlazimu mgombea wa urais wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba kuanza kusukuma magari. Juma Duni Haji ajitokeze awaambie Watanzania, yeye alipokuwa Mkurugenzi wa Fedha, Rasilimali na Uchumi alipeleka wapi pesa mpaka Lipumba akawa na gari ya kusukuma wakati wa kampeni?

  Hizi ndizo hoja za kifalsafa za kujibu sio kutoa matusi.

  Wanafalsafa wengine hawatanielewa nisipokuuliza, kwanini ulipokuwa Mkurugenzi wa Fedha Rasilimali na Uchumi, hujawahi kuwaambia wanachama, mapato na matumizi ya pesa zilizochangwa kupitia simu za mkononi kupitia mfuko ulioitwa “nipe tano”?

  Waziri unataka tusikuulize kuwa pesa za chama zinazodaiwa kupelekwa Mwanza kwa mfanyabiashara mwenye unasaba na wewe zikapotea na wengine walipohoji mkawatimua, akiwemo Rwakatare, haya nayo tusikuulize kwa kuwa tunaogopa matusi?
  Kutukana ni uamuzi wako, pengine ni tabia ambayo kwa umri ulionao si vema tukakukosoa, jamii yenyewe itapima, lakini suala la mapato na matumizi ni la msingi ili ukisaidie chama kiache kufikiriwa kuwa ‘kinakopi na kupesti’ mawazo ya vyama vingine.

  Juma Duni Haji, unapaswa kuwaambia wanachama wa CUF, kama ulipokuwa Mkurugenzi wa Fedha, Uchumi na Rasilimali ulifanya manunuzi yanayodaiwa kuwa ni hewa ya shamba huko mkoani Lindi, na ukatolea taarifa kuwa chama kimenunua shamba Lindi.

  Lakini viongozi wa CUF wa Mkoa wa Lindi, akiwemo Mwenyekiti ambaye kwa sasa ni mbunge, Salumu Baruany, walikuwa hawajui shamba hilo lipo wapi. Je, ni kosa kuulizwa haya?

  Unawaambia Watanzania kuwa “ndoa ya CCM na CUF” imeleta utulivu Zanzibar, na eti kuwa kuna amani. Ungefanya vema kuwaeleza Watanzania hicho kinachoitwa uamsho kinadai nini? Kwanini kipo, kinachochewa na kufadhiliwa na nani? Je, kina uhusiano mzuri na serikali au la? Nani anaratibu shughuli za uamsho kama kuna amani inayotokana na “ndoa ya CUF na CCM’?

  Baada ya Uchaguzi wa Bububu mbona ndoa imetetereka kuna nini? Hadi imefika wakati mwakilishi wa Bububu anaapishwa matangazo ya moja kwa moja ya televisheni ya Zanzibar yanakatwa kwa kuwa Waziri wa Habari na Utangazaji ni wa chama chako? Watanzania kweli tusiulize, ila tukiuliza inakuwa nongwa? Hayo ndiyo tungejadili hapa.

  Juma Duni Haji umenukuu vizuri sana katiba ya CUF, nikapenda. Umesema “Madhumuni ya Chama cha wananchi CUF kama yalivyo katika katiba yake ni, “kuwaunganisha Watanzania wakatae uonevu, kudhalilishwa, kunyanyaswa, kubaguliwa au maovu mengine yanayoweza kufanywa dhidi ya heshima ya utu wa binadamu, yawe yanayotendwa na serikali, kikundi cha watu walio na uwezo kwa ajili ya mabavu yao au kwa ajili ya kujinufaisha kwao kiuchumi au kisiasa na kiitikadi au kwa kujali dini, kabila jinsia au rangi zao.” (Kifungu cha 6[1] Katiba ya CUF - uk.12).
  Kwa kifungu hicho tu, jibu hoja za kiuchumi za mapato na matumizi, na ueleze kwanini CUF inaiga Movement for Change (M4C), na kwanini inahubiri “Dira ya Mabadiliko” ambayo ni kaulimbiu ya Chama cha ADC? Ina maana CUF haiwezi kubuni bila kutegemea akili za vyama vingine? Aidha mapato na matumizi hayahusu maisha ya watu binafsi na nyadhifa zao na wake zao kutoka vyama vingine.


  Makala hii Imeandikwa na Josephat Isango wa Tanzania Daima
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Vyama vya siasa Tanzania vimekuwa kama vikundi vya taarabu mipasho tu, kwa staili hii kweli mtaing'oa CCM madarakani kweli.
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Naona kama majungu vile!! Hivi tutaacha lini kuongelea mambo yasiyo ya msingi? kila kukicha siasa za maji taka. Hata huyu aliyeandika haya bado anayendeleza yale yale si bora angekaa kimya ili watanzania wenyewe tukamhukumu Mzee Duni wenyewe? Hivi suala la Chama kufanya kambeni za kinyonge si ni ahuweni kwa mpinzani? Suala la kuwatimua wanachama kweli linamhusu mtu mwingine zaidi ya chama husika au ndo tuamini kuwa hyu aliyeandika haya ni LWAKATARE na hivyo bado ana kinyongo na kufukuzwa? Nilidhani amani inayoongelewa Zanzibar baada ya serikali ya umoja wa kitaifa ni ya kisiasa, sasa hapa Uamsho ni chama cha siasa? Mapato na matumizi ya chama kingine unayahoji wewe wa CDM? kazi ipo jamani, basi tusubiri na Juma Duni haji naye atakapokuja na madai ya matumizi na mapato ya CDM, CCM, TLP na wengine sijui tutasema siasa zimemshinda.

  Upeo wa wanasiasa wetu bado sana.
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Umeona mkuu, sasa sijui huyu kasema nini hapa, maneno mengi lakini kilichomo kichefuchefu.
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Molemo hebu ongeza font na kuipanga vizuri kidogo hii makala ili tuweze kuisoma na kutoa michango yetu. Kwa hivi ilivyokaa inakuwa vigumu kuisoma.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kumbe V4C imeibwa na CUF kutoka chama cha ADC
   
 7. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hapana, nadhani ungekemea kwanza ile makala ya mtu mzima mzee Haji

  Kuhoji mapato na matumizi ni haki ya msingi, ndio maana wenye hekima hawajifaragui kuhoji vitu ambavyo vikianza kuchunguzwa vitawaibulia na wao issues

  Hii itasaidia sana kufunga midomo watu wanaobwabwaja hovyo huku wenyewe wakiwa wachafu
   
 8. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CUF hawana la kujivunia katika siasa za taifa hili. Tunahitaji haki, uhuru na mabadiliko ya kweli katika taifa letu wao wanaishia kuangalia maslahi yao binafsi na chama chao.
   
 9. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi CHADEMA huwa siwaelewi kabisa! DUNI alikuwa anajibu hoja ya 'CUF kuwa CCM-B' kama CHADEMA wanavyodai, halafu huyu analeta habari za SHAMBA hewa na UAMSHO! $@#$ mbona husemi Mbowe alipokiuzia CHAMA magari mabovu!
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Chadema hawajajibu.Bali mwandishi wa habari Josephat Isango amejibu matusi ya waziri.
   
 11. M

  MASIKINI MASIKINI New Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimsingi watanzania hatutaki vyama vya siasa vyenye lengo la kugawana MAULAJI Ya watanzania. kama CUF wanavyotaka,kama ilivyo huku zanzibar na hawa akina DUNI wametulia baada ya kuahidiwa ulaji. TUNAHITAJI WATCHING DOG OF OUR GOVERNMENT
   
 12. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Ukweli kwanza nashkuru kwa Makala hii...ila ningependa kufahamisha kua Vison For Change ipo katika Ilani ya CUF mwaka 2010..Suala kua CUF wamekopi na kupesti ni hao CHadema wenzako na ADC mana rangi za vyama zao na za CUF hazina tofauti na suala la kukatishwa matangazo kuapishwa mwakilishi ni kua wananchi wengi hawamtambui kama mwakilishi halali....ukitakata usitake ZNZ yetu wenyewe tuachilieeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 13. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ndiyo wale wale....
   
 14. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Utajiujua mwenyewe ukweli unauma
   
 15. p

  promi demana JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Cuf ni chama cha ponda.
   
Loading...