Majibu bora kisiasa kwa maswali magumu kijamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu bora kisiasa kwa maswali magumu kijamii

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Lekanjobe Kubinika, Feb 22, 2011.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Source: Yahoo friends.
  Sijui kama ndiye huyu mwanajamii au ni ukoo wake kijamii, maana nimekutana na wengi na hawataki kufafanua mahusiano yao na mm tumjuaye.

  Swali: Mheshimiwa Rais je unawajua wamiliki wa kampuni ya Dowans?


  Jibu:
  Nasema mimi sijui, ni kina nani sijui,
  Wanatoka wapi sijui, walifikaje sijui,
  Kama nawafahamu sijui, kama wananijua sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Mheshimiwa Rais, lakini waliingia nchini na kupata Mkataba wa Richmond na kuleta majenereta katika kutekeleza mpango wako wa kupunguza tatizo la umeme nchini kweli huwajui?


  Jibu:
  Nasema mimi sijui!, kwanini walikuja sijui,
  Uhusiano wao siujui, Kama nao Richmond sijui,
  Waliingia kwa lipi sijui, na walirithishana vipi sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Lakini ulisema kuwa Richmond ni kampuni Hewa kama Kamati ya Mwakyembe ilivyoonesha na kudai, na ukatoa pongezi! Unawaeleza vipi Watanzania kuwa Taifa liko tayari kuheshimu mkataba wa kampuni ya kitapeli?


  Jibu:
  Nasema tena sijui!Kama kampuni hewa sijui,
  Kama ni matapeli sijui, Kama walibebwa sijui,
  Wahusika kina nani sijui, Mwakyembe alijuaje sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!
  Tulikoanzia sijui, tumefika vipi sijui,
  Nahusika vipi sijui, nimuulize nani sijui,
  Niwaridhishe vipi sijui, nianzie wapi sijui!
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Lakini Rostam Aziz ametajwa kuhusika kuanzia mwanzo wa sakata hili na yeye mwenye amekiri kuhusika na hili kwanini usimuulize ili ujue?


  Jibu:


  Nitamuanza vipi sijui, Rostam huyu sijui,
  Kama mwingine sijui, anahusika vipi sijui
  Nimuamini nani sijui, kama ni kweli sijui!
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Lakini, inawezekana vipi usijue wakati una vyombo vingi vya usalama ambavyo vingeweza kukupata taarifa mbalimbali za kiinteligensia kama walivyoweza kuzipata kule Arusha na kuvunja maandamano ya Chadema? Kwanini hujapatiwa taarifa za kiinteligensia kuhusu Dowans?


  Jibu:


  Intelligensia mimi sijui, nani anipe sijui,
  Kwanini wanipe sijui, nifanye nayo nini sijui,
  Wasiponipa sijui, kama nadaganywa sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Nani awaagize sijui, kama nini mimi sijui,
  Au makamu sijui, Waziri Mkuu sijui,
  Wajitolee tu sijui, au ni Bunge mimi sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Sasa msimamo wako wewe binafsi kama Rais ni upi, Dowans walipwe au wasilipwe?


  Jibu:


  Msimamo gani sijui! Kama ninao sijui,
  Nilikuwa nao sijui, nitakuwa nao sijui,
  Kama walipwe sijui, na wasilipwe sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Wizara ilipe sijui, Au Tanesco sijui,
  Au huko hazina sijui, au hapa Ikulu sijui,
  Bunge litenge fedha sijui, au Mahakama sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Sasa mheshimiwa inaonekana hujui mambo mengi tu; kuna mambo mengine yoyote unayoyajua?


  Jibu:
  Kwanini masikini sijui, Kagoda ni nani sijui,
  Meremeta nani sijui, Dipu Grini nani sijui,
  Mbona elimu duni sijui, wanagomea nini sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Sijui mimi sijui, mengine mengi sijui,
  Ya kilimo siyajui, ya Sayansi siyajui,
  Mambo ya maji sijui, umeme ndiyo sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!
  Kama napendwa sijui, kama nachukiwa sijui,
  Nafurahiwa sijui, au nakejeliwa sijui,
  Kama ninachekewa sijui, au nakebehiwa sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Mheshimiwa swali la mwisho; asante sana kwa kutupa nafasi hii na kwa hakika umetuelewesha na tumeelewa kuwa hujui mambo mengi sana. Labda uwaambie Watanzania, je wewe ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?


  Jibu:


  Sijui mimi sijui, ninarudia sijui,
  Kama miye sijijui, mtajuaje sijui
  Kama najua sijui, kama sijui sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji -BGM)
  <IMG width=1 height=1>
   
 2. P

  Pokola JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Iliwahi kupostiwa hapa JF, kama nina kumbukumbu nzuri
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Inawezekana iliwahi kupostiwa sikuiona. Hata hivyo naamini kuna wengine hawakuiona kama mimi watanufaika hapa, maana majibu kama hayo nakumbuka yanafanana na yaliyotolewa kwenye sikukuu ya chama tawala mwezi wa pili juzi tu.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hata mimi ndo kwanza naiona hapa! good
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Swali: Ulifikaje magogoni kama kila kitu hujui, mheshimiwa?

  Jibu
  Nilifikaje sijui, Nilifika lini sijui
  Walionifikisha hapo siwajui
  Nitatoka lini sijui
  Nikuulize, sijui hapa tunafanya nini?
   
 6. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  JIBU: mimi sijui, kama imewahi sijui
  kama unakumbukumbu sijui
  Nasema mimi sijui
   
 7. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kama ni raisi tumepoteza!!!
   
 8. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hata mimi sijui,kama nliwahi kuiona sijui kama imewahi kubandikwa humu sijui,nasema sijui
   
Loading...