Majibizano ya Mh.Rais na Mkurugenzi wa TBA leo Chamwino yanaonesha jinsi Rais asivyofuata ushauri wa Wataalamu wake, Rais asivunje sheria

Mkuu barafu , Katiba na Sheria zinaruhusu Mheshimiwa Rais kushauriwa lakini hazimlazimishi kuukubali ushauri wa mtu au Taasisi yoyote ile iwayo. Yawezekana Mheshimiwa Rais anayajua mengi kuhusu hilo na kukataa kwake ushauri unaouzungumzia ni kusimamia anachokijua na kukiamini.

Ibara ya 37 (1) ya Katiba inasomeka:
37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote.
Kaambiwa ni kwa mujibu wa sharia jengo la umma kuwa na lift halafu logical unajenga hospital bila lift kweli? Maadam speaker kashangilia historia itawahukumu
 
Mkuu barafu , Katiba na Sheria zinaruhusu Mheshimiwa Rais kushauriwa lakini hazimlazimishi kuukubali ushauri wa mtu au Taasisi yoyote ile iwayo. Yawezekana Mheshimiwa Rais anayajua mengi kuhusu hilo na kukataa kwake ushauri unaouzungumzia ni kusimamia anachokijua na kukiamini.

Ibara ya 37 (1) ya Katiba inasomeka:
37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote.
Kwani lazima uandike chochote? Una uelewa kweli wa unachoandika?
 
Hapana, hii ni tabia yake tu kwamba anafikiri ukiwa Rais basi una majawabu kwa kila kitu. Anashidwa kujua kuwa maadili (ethics) ndiyo msingi wa kila fani ikiwemo siasa na ujenzi. Leo anamwambia mkurugenzi aweke mahabusu ethics za kujenga jengo la ghorofa la umma, tena hospitali; kesho mkurugenzi huyo akiwaamuru wajenzi wapunguze ratio ya zege kupunguza gharama itakuwaje!!!?
Wahenga walisema: "Akili nyingi huondoa maarifa."
Hivi kuwa waziri wa ujenzi miaka kadhaa ndiyo uwe unaelewa kila kitu, kweli!!!? Kuna tatizo kubwa Sana kwa Rais kuliko tunavyofikiria.
Mh.Rais hana tatizo,tatizo ni kwanini hatuna mbadala wa specifications.
Hivi kwa mfano wangeitoa hiyo lift na kuweka RAMP (ground-1st floor) kuna shida gani?
Faida za kujenga ramp kwa jengo la floor moja ni nyingi kuliko kujenga lift.
 
Hii OPD ya muhimbili ilijengwa mwaka gani? Je design na sheria za ujenzi za miaka hiyo wakati inajengwa bado ni relevant mpaka sasa?
Mkuu hebu fikiri kidogo OPD na hiyo hospitali kuwa na lift kipi kinaleta maana ya haraka, kwa fikra za kawaida tuu...

OPD maana yake ni idara inayo shughulika na wagonjwa wa nje hivyo kwa kujengwa hivyo haina athari sana ,

Tofauti inapokuja hii ambayo hospitali inatakiwa kulaza wagonjwa hapo na taratibu zingine..
 
Nilikuwa namfuatilia Rais Dr.John Pombe Magufuli kwenye kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali ya Uhuru,Chamwino-Dodoma.Yalizuka majibizano kidogo kati yake na Mkurugenzi wa TBA kuhusu gharama za ujenzi na "specifiations" za majengo ya hospitali hiyo.

Kwa muda ambao Mkurugenzi ameutumia kumshauri Rais kitaalamu na Rais kuukataa ushauri ule,inaonyesha kuwa huko faraghani Mh.Rais anabeza ushauri wa watu wengi wenye utaalamu na kuamua kwa matakwa yake.Hii inatupa picha kuwa "Rais hashauriki kirahisi".Ni hatari sana katika kufikia maamuzi ya mwisho yeye kama Rais na mtia saini wa mwisho wa mambo makubwa ya Kitaifa.

Rais alibeza jengo la Hospital litakalokuwa na ghorofa moja kuwa na lifti,akisema ni kuongeza gharama zisizo na maana,na yeye hayupo tayari kuona pesa za walipa kodi zinatumika ovyo(Wagogo wakiongozwa na Ndugai wakapiga makofi na kushangilia),hivyo hataki jengo liwe na lifti,maana haiitajiki.

Mkurugenzi wa TBA akamjibu Mh.Rais kuwa kwa mujibu wa sheria,majengo yote ya umma yanapaswa kuwa na lifti,hii ni moja ya specifications ya jengo lolote la umma na haswa hospitali,lakini Rais akamgeukia Mkurugenzi kumuuliza kama nyumba yake ina lifti,jamaa akajibu nyumba yake sio mali ya umma,Mh.Rais akasema kuna majengo Dsm ya umma na hayana lifti,Mkurugenzi amkamjibu kuwa huo ni ubunifu wa majengo ya zamani,ila kwa sasa yote yana lifti.

Mh.Rais akadakia kuwa jengo la Ikulu ya Chamwino halina lifti,jamaa akamjibu kuwa lina lifti sababu ni jengo la umma.Mwisho wa siku Mh.Rais akakosa hoja na akalazimisha jengo lijengwe bila lifti,na akaamuru jeshi lifanye kazi hiyo maana TBA walipewa wakasuasua.

Ukifuatilia mazungumzo haya,utaona jinsi Rais Magufuli asivyotaka kushauliwa,anaonekana kujua kila kitu na yupo radhi kuvunja sheria za ujengaji wa


majengo ya umma kwa mgongo wa kuokoa pesa za walipa kodi.






Ukweli ni kuwa ushauri wa kitaalamu wa Mkurugenzi wa TBA lazima ufuatwe,hospitali hata iwe na ghorofa moja ni lazima iwe na "specification" ya lifti,hospitali ni jengo la umma,lakini pia inahudumia wagonjwa ambao hawana uwezo wa kutembea na kupandisha ngazi.

Mh.Rais,hospitali ya Uhuru inahitaji lifti ili kusaidia wagonjwa waliovunjika viungo,mama wajawazito,wagonjwa wengine mahututi na hata msaada kwa manesi wanahudumia wagonjwa toka ward moja kwenda nyingine.Maiti kutolewa ghorofa ya kwanza kuja chini itahitaji lifti.

Kuokoa kodi za wananchi haina maana ya kuwapa vitu vibovu na visivyo na viwango.Ni heri aghali yenye ubora kuliko nafuu isiyo na ubora.Zingatia ushauri wa wataalamu ili kuendesha nchi kwa kufuata sheria na taratibu,unapoambiwa na msaidizi wako kuwa jengo la umma lenye ghorofa bila lifti ni uvunjifu wa sheria za ujenzi wa majengo ya umma na wewe ukalazimisha sheria ivunjwe hadharani kwa kisingizio cha kuokoa kodi za wanyonge,ni mfano mbaya wa utii wa sheria bila shuruti.

Majibizano yako na mkurugenzi wa TBA ambaye ndio mtaalamu wa mahali anapokuwakilisha,yameonyesha jinsi ambavyo unaweza kupuuza sheria bila kuzingatia madhara yake.Sisi tunaokufuatilia na kuona kazi yako,tunadhani kuna mengi unayoshauriwa na unapuuza,kupuuza sheria hadharani ni mwanzo wa kuliangamiza Taifa na ni mfano mbaya kwa wasaidizi wako,maana unajenga msingi wa wao pia kupuuza sheria na taratibu.

Tunakutakia kazi njema,nia yako njema katika kulijenga Taifa iakisi pia utii wako katika sheria na katiba uliyoapa kuilinda.

barafu wa Jf


wagogo hawajielewi kabisa, wanaambiwa jengo lisiwe na LIFT wanapiga makofi.
Ila huyu mkurugenzi kamuaibisha sana JIWE, kwa kibberu tunasema ame mu- outsmart!

View attachment 1269061
 
Hivi ushawahi kuona mgonjwa aliyezidiwa au mtu mwenye umri mkubwa akipanda ngazi!
Hivi mfano mgonjwa aliyeko kwenye wheelchair akitaka kwenda gorofa la kwanza mtambeba mgongoni

Ova
Solution ni kujenga Ramp (Ground-1st floor)
Upo.....!
 
Tuwe waungwana, sisawa Uujibizana na Rais hadharani kwa Kumkosoa hata kama amekosea. Huu ni ustaarabu wa kawaida tuu, kwa Mkubwa wako Kicheo. Zipo njia zinazokubalika ki protokali.
Mkuu unamaanisha mkurugenzi wa TBA angenyamaza kimya?

Au unamanisha angetoa majibu ya uongo?

Au angesema ndiyo mkuu nitafanya utakavyo licha ya kuwa kanuni za ujenzi wa majengo haziruhusu hili?


Nafikiri tunapaswa kuzitendea haki taaluma zetu na kusimamia misingi ya taaluma zetu.
 
Back
Top Bottom