BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,323
- 7,963
"Wakati mradi unaanza kutekelezwa ili kujengwa handaki katikati ya mto ni lazima maji yachepushwe kwa njia nyingine ili yaendelee mbele yakupe nafasi ya sehemu kavu kujenga handaki hili lenye urefu wa mita 700 lenye gharama ya Tsh. Bilioni 235," alisema Makamba.
Ameongeza kuwa mageti ya kuziba mchepusho wa maji ya kujaza maji yamewasili na tayari yameshafungwa na ni miongoni mwa hatua tatu muhimu zilizofanyika katika utekelezaji wa mradi huo hivyo anaona fahari kuutangazia umma hatua hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO), Maharage Chande, amesema kuwa bwawa hilo linauwezo wa kuhifadhi lita bilioni 33.2 za maji na kama zikitumika na mitambo yote itaweza kuendesha mitambo kwa kipindi cha mwaka mmoja.