Maji ya shingo Great thinkers | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maji ya shingo Great thinkers

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbimbinho, Oct 5, 2009.

 1. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2009
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa nianze kwa kusema Shikamooni nikiamini wengi wa member ni watu wazima na wenye heshima na familia zao. Mimi bado ni kijana wa miaka 21 na nipo chuo kikuu mwaka wa pili. Nisirefushe sana maelezo, kisa changu ni hiki,

  Miaka kadhaa iliyopita nilipokuwa sekondari nilikuwa na msichana ambaye tulipishana kidato kimoja, na ndiye alikuwa msichana wangu wa kwanza, nami nilikuwa wake wa kwanza, kwa maana kwamba alikuwa bado bikira.
  Nafikiri wengi kama haijawatokea basi mmesikia jinsi mpenzi wa kwanza anavyokuingia moyoni, labda kwa sababu ya ugeni wa fani. Nilitokea kumpenda sana yule binti na nikawa sisikii wala sioni kwake. Tatizo likaja pale alipogundua kuwa nampenda sana, basi akaanza kuniletea pozi nyingi zisizo na mpango. Mara ataibuka tu na kusema, nafikiri tuachane, kwa sababu kama, anataka asome sana, mara hatuwezi changanya mapenzi na elimu, mara mimi ni kiongozi wa dini hapa shuleni hivyo natakiwa kuwa mfano au kuna mtu anampenda, na sababu zisizoeleweka, mimi nikawa naona kuwa kuna kaukweli ndani yake, lakini ilikuwa ngumu kukubali kwa kuwa tayari alikuwa ndani ya moyo wangu, na ingawa nilikuwa mwanafunzi niliweka nadhiri kuwa sitakuja mwacha.(Tuliishi vile bila kukutana kimwili hadi siku moja akaniuliza kama nilikuwa kamili, nikamjibu kuwa wakati wake ukifika atajua.) Basi nikawa nasononeka sana hadi wakati mwingine nikawa napoteza uzito kwa kumuwaza, na uwezo wangu darasani ukawa unashuka, kila nikimfuata anakataa hadi inapotokea marafiki zangu wanapomfuata na kumbembeleza ndipo anakubali. Hii imetokea zaidi ya mara moja . Siku moja mmoja kati ya rafiki yake alinionea huruma na kuniambia kuwa huyo msichana wangu alikuwa anafanya vile pale tu anapojisikia, yaani akiamua kunikondesha ananikondesha, alikuwa anawaambia wenzake ngoja nimchemshe flani, ilikuwa kama aina ya mchezo wake kwangu, hivyo akanishauri niachane nae, lakini bado nilishindwa hadi nilipomaliza kidato cha nne na kuondoka shuleni ndipo nilipomsahau.

  Sasa nipo nje ya nchi ninasoma na imetokea mimi na yule binti tumeanzisha upya mawasiliano tu, siku moja wakati tunaongea nikamuuliza kiutani kwamba alikuwa anaonaje kama turudishe uhusiano wetu??, binti wa watu akakubali bila matatizo, na kwa sasa anaonesha mahaba haswa, haipiti saa kani sms au kupiga kabisa, isitoshe amemwambia mama yake kuwa tumerudiana. Sasa hapo ndipo linapokuja tatizo kwani nilikuwa namtania tu na isitoshe nina mpenzi kwa sasa ambaye tunapendana kiukwelia kwelia.Kumwambia nilikuwa namtania naogopa maana sijui itakuwaje, mbaya zaidi katika maisha yangu huwa najisikia fedheha sana pale nimuonapo mwanamke akillia achilia mbali nikiwa chanzo.

  Ndugu zangu najua nilikosea pale nilipotania kwani nilijua atakataa kwa kuwa alishawahi niambia hanipendi, Naombeni msaada wenu, akili imestaki.((
  Kumwambia siwezi na kuendelea kukaanalo siwezi maana nahisi namsaliti mpenzi wangu.
  Msaada wana JF.
   
 2. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kamsimulie mzazi wako...
   
 3. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,804
  Likes Received: 6,314
  Trophy Points: 280
  You are not serious
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Duh! Pole sana Mkuu, Kaa, Fikiria uchukue uamuzi wa Busara, kama unampenda huyo uliye naye sasa hivi basi achana na huyo binti wa zamani coz utakuja kuumia siku ukija gundua kwamba si Bikira tena.
   
 5. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Marahaba.... na zingatia masomo achana na mapenzi mpaka wakati wako utakapofika.Haya kafanye assignments.
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mbona rahisi sana,

  mwache aubebe msalaba wake wa kilio, mpigie simu mwambie "siku ile nilipokwambia turudiane nilikuwa nakutania!"
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Muulize kasahau nini kwako tena?..si alikuwa hakutaki?
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Oct 5, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Naona umekazania mwili ambao utazikwa na kuoza ikabaki mifupa, umeisahau roho yako itakayodumu milele yote Jehanam kama utakufa katika uasherati! Katafakari: Nini hatima yako ukiwa unahamisha uasherati toka kituo kimoja hadi kingine na mara mauti yatakapokufika?
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Shikamoo mkuu. Mtu ana miaka 21 kwa hiyo wakati wake ni upi? Na wewe ulianza mapenzi na umri gani?
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hiyo idea, ila napata wasiwasi sasa kwamba we tutatumia nguvu nyingi kudadis ishu ya kutunga

  Namshauri kama ana nia ya kweli basi, basi apunguze hadi characters 200
   
 11. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Sijui vijana wa sasa lakini wakati wetu ulikua unamaliza masomo yako ndipo sasa uanze haya mambo.Wakati kabla hatujamalizia mafunzo ya mgambo pale Tabora kuna kijana alianza kujihusiha na mapenzi ambayo yalimsababishia kuharibu masomo yake,Ndio maana namshauri kijana azingatie masomo
   
 12. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280


  Ofcoz sio bikira tena, dada'ake ambaye ni rafiki yangu sana ndiye aliyeniambia.
   
 13. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280


  Ni kweli ulichosema, lakini kwa sasa nafikiri ndo muda muafaka wa kuanza kujifunza haya mambo, na sidhani kama nyakati hizi zinaweza kwenda kikarne ya 20, mambo yanabadilia as tekinolojia hadi kwenye mapenzi siku hizi.
  Ba kuhusu asignment, nshafanya zote currently)
   
 14. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280


  Duh! I wish wud b tht simple, but thank you mkuu, I will try it. Ingawa sometimes nafikiria kubadili namba ya simu, lakini inaniwia ngumu kwa kuwa ni namba itumwayo na watu wengi sana muhimu kwangu.
   
 15. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280


  Nilisha muuliza kwanini kakubali kirahisi wakati alishasema kuwa hakunipenda, akadai kuwa ulikuwa ni utoto na kwa sasa amekuwa na anajitambua.
   
 16. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280


  Muinjilisti Buchanan, nafikiri hukunielewa, ni kwama sikuwahi kutana kimwili na yule binti na sitathubutu ndio maana nimeomba msaada wa namna ya kumdisi, ningeweza hata kunaniihii nae as kupooza machungu na kulipa kisasi as many friendz used to tell me, but naona kama ni ujinga.
  Na isitoshe sijui mienendo yake as we are far apart from each other.
  Ninampenda mpenzi wangu peke yake)
   
 17. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280


  Ahsante MwanaFA kwa msaada wa jibu. Nafikiri huu ndo umri wenyewe maana tukisema tusubiri ndo matokeo yake kudondokea kwa uhusiano usiosahihi maana wrngi huwa na papara katika kuchagua,
   
 18. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Achana na tamaa ...huna uhakika na maisha yako ya kimapenzi...!!
   
 19. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280


  Mwana sikulazimishi kuamini, nimeandika habari ndefu ili iwezeeleweka vizuri, lakini ni ukweli mtupu.
  Wakati mwingine nampotezea kujibu sms zake au simu, lakini ataendelea kupiga na kutuma hadi najisikia vibaya hivyo kuamua kumjibu.
   
 20. KIFARU

  KIFARU Senior Member

  #20
  Oct 6, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 172
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,ila kwa ushauri zaidi achana na mambo ya mapenzi,na maisha hayana kuchelewa,na uamuzi mzuri unafanywa na aliyekomaa kiakili,mapenzi yanaharibu maisha 99%,huo uhusiano unaosema sio sahihi hata ukianza mahusiano ukiwa na 13yrs hadi 24yrs utakua unafanya uchaguzi na maamuzi yasiyokua sahihi kwa sababu ya ukomavu wa kiakili,kila kitu kina muda wake,mapenzi yako na huyawezi maliza,mapenzi hayana formula,mkuu soma sana kisha ukishakomaa akili utamwomba Mungu akujalie mke bora,mtazamo wangu tu
   
Loading...