Maji ya Mgodi wa North Mara yana sumu - Utafiti wa wana sayansi

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
MAJI ya Mto Tighite ambayo yanalalamikiwa na wananchi wa Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara, yamethibitika kuwa hayafai kwa matumizi ya binadamu kwa kuwa yana sumu inayoua pole pole viumbe hai.

Uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakishirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi cha Norway, umewekwa hadharani jana mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na kuonesha kemikali ilivyo nyingi katika mto huo.

Viongozi wa dini ndio waliwaomba wataalamu hao kufanya utafiti huo kutokana na malalamiko ya wananchi wa eneo hilo kuwa mgodi wa North Mara unatiririsha maji ya kemikali kwenye mto huo na baadhi yao na mifugo wamedhurika.

Katika utafiti huo, wataalamu hao walibaini kuwa maji hayo yana aina ya madini mazito ambayo yamezidi kiwango cha Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo yanamwathiri binadamu anayeyanywa au kuoga.

Watafiti ambao wamebaini sumu hiyo ni Asgeir Almas wa Chuo cha Norway na Mkabwa Manoko wa Chuo cha Dar es Salaam ambao kwa pamoja waliwasilisha utafiti wao mbele ya kamati hiyo na kuonesha madhara kadhaa.

Wataalamu hao walibaini ongezeko la madini hayo kwenye maji ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2002. Lakini pia kuna madini ambayo madhara yake yanasababisha nguvu za kiume kupungua.

Hata hivyo, haikuthibitishwa kisayansi kuwa maji hayo ndiyo yaliyosababisha magonjwa kwa wakazi wa eneo hilo na wanyama, hivyo wataalamu hao walipendekeza ufanyike utafiti mwingine juu ya watu na wanyama ambao inasemekana wameathiriwa na maji hayo.

Baadhi ya kemikali ambazo zilitajwa kuwepo kwenye maji hayo ni Arsenic ambayo iko kwenye udongo na maji na kwamba iko juu ya kiwango cha WHO na inaua pole pole.

Wataalamu hao walisema tatizo hilo linatakiwa kuangaliwa kwa karibu, kwani linaweza kusababisha madhara makubwa ikiwamo vifo katika siku zijazo. Wataalamu hao ambao walionekana kuwa waangalifu kwenye mapendekezo yao, walisema hawana uhakika kama chanzo cha madhara hayo kwa binadamu ni sumu hiyo ila walionesha kuwa kwa viwango vya WHO kemikali iliyoko kwenye mto huo inachangia madhara kwa binadamu.

Viongozi wa dini walitoa ripoti hiyo wakati serikali ikichukua vipimo Juni mwaka huu lakini bado haijatoa ripoti yake, lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mazingira, Job Ndugai, alisema serikali itawasilisha ripoti hiyo katika mkutano ujao wa Bunge.

Ndugai ambaye kamati yake ilizuru tena mgodi huo wa North Mara wiki iliyopita, alisema hali bado haijatengamaa katika eneo hilo, licha ya uongozi wa mgodi kuchukua hatua kama walivyoshauri awali.

“Lakini hali bado si nzuri na hili tunakwenda kulijadili na serikali, kuona hatua za kuchukua haraka likiwamo suala la kupima afya za wanyama na watu ambao wameathirika,” alisema Ndugai.

Katika tamko la viongozi hao wa dini walisema baada ya kuzuru eneo hilo wiki iliyopita, walizungumza na wananchi na kugundua kuwa eneo hilo sasa lina uhaba mkubwa wa maji kwa vile wananchi wamesusa maji ya Tighite na mito ya asili iliyoko eneo hilo inasadikiwa pia kuathiriwa na sumu hiyo.

Viongozi hao wa dini ambao ujumbe wao ulikuwa chini ya Mwenyekiti Mwenza Shekhe Salum Fereji, wa Mkoa wa Mwanza, walipendekeza serikali iwe karibu na wananchi katika eneo hilo na uchunguzi wa Mkemia Mkuu majibu yake yatolewe haraka.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shelukindo, alisema mapendekezo yote ambayo yametolewa na viongozi wa dini na hisia za wananchi watazifikisha serikalini kuhusu suala hilo.


Source:
HabariLeo
 
Taarifa hii ina amsha maswali mengi sana:

Hivi serikali yetu inathamini kweli maisha ya wananchi wake?

Kwanini mkemia mkuu mpaka leo hii hajatoa taarifa ya uchunguzi wake?

Je, viongozi wa dini wasingechukua hatua hiyo, taarifa ya mkemia mkuu wa serikali ingesema ukweli wowote?

Je, Spika Sitta atajisikiaje baada ya kusoma taarifa hii Bungeni kwa kuwa alimtoa kwa ubabe Mzee Cheyo kwa kumwambia hajui kitu na ilhali alikuwa anatetea wananchi ambao wamezungukwa na hayo matatizo?

Je, wananchi ambao wameathirika kwa kupungukiwa na nguvu za kiume ama watakaopoteza maisha yao hapo baadaye, Kampuni ya Barrick itawafidia?

Teweli Teweli aliyesimama kidete utetea huu uchafu atakuja na kauli gani?

Kwanini Kampuni ya Barrick wasifukuzwe kwa kusababisha madhara makubwa kwa wananchi wa eneo husika?

Mrahaba wa asilimia 3 una thamani sawa na maisha ya maelfu ya watu watakaopoteza maisha yao? Kuna haja ya kuendelea kuchimba madini ambayo yanasababisha maafa kwa wananchi?

Viongozi wa serikali walio-side na Uongozi wa Mgodi wa North Mara, kwanini wasijiuzulu kwa kuwa walitaka kuficha ukweli na huku wananchi wakiendelea kuathirika na wengine watapoteza maisha yao.

Jeshi la Polisi ambalo liliwahi kutumia nguvu na vitisho kwa kuwaweka ndani wananchi na viongozi wa kata inayohusika waliokuwa wakipiga kelele kuhusu sumu hiyo, viongozi Jeshi la Polisi wako tayari kuwajibika?
 
Wasemaji wa Barick watakuambia kuwa ni makosa ya wananchi na sio ya kampuni hili la kigaidi. Serikali na wabunge ambao wengi wamekula 10 percent yao watakuambia kuwa wanalishughulikia hili tatizo.

Kikwete atatabasamu tu na kuwaambia kina mama wa north mara wazae watoto warrrrrrrreeembo ili washiriki kwenye umisi wakati huo huo Zitto akiishauri serikali kutaifisha (na kisha kulipa mabilioni ya dola) mgodi wa north mara.
 
Kwa nini tusubiri ripoti ya mkemia mkuu wa serikali? Unategemea nini toka kwake? Ripoti nii ni tosha kabisa. Ushauri wa bure wananchi wa Teghethe waelezwe kuhusu Bopal disaster huko India ambapo kampuni moja ya madawa ilishindwa kuitunza vizuri gesi yenye sumu na kulipuka na mwishowe kusabisha vifo vya watu kadhaa. Kampuni husika Union Carbide ya marekani ililipa US $ 470 milioni kama fidia kati ya US $ bilioni 3. Ninyi mnagoja nini wakati ni huu.
 
Wao watalipa ili kuendesha uchaguzi wa CCM na kuondoa upinzani tarime ili waweze kuwamaliza vyema . Watawalipa FFU kuzima haki za watu na hii ndiyo CCM yao
 
Wao watalipa ili kuendesha uchaguzi wa CCM na kuondoa upinzani tarime ili waweze kuwamaliza vyema . Watawalipa FFU kuzima haki za watu na hii ndiyo CCM yao

Kama ndo hivyo hiyo kesi ifunguliwe mapema kabla ya harakati za uchaguzi hazijaanza. Upinzani Tarime utaondolowa na dola ngapi???? Mashujaa wa Tarime hawana bei. Sijui kama FFU wanaweza kitu kama watu wenye cause wakiamua, Shah wa Irani alikuwa na sophiscated weapons lakini aliondolewa na wanaharakati wenye mawe tu bila silaha yoyote.
 
Back
Top Bottom