Maji ya kisima changu yanabadilisha vitu vinakuwa na rangi nyeusi

Occupy

Member
Jul 4, 2022
9
13
Habari wakuu, Moja kwa moja kwenye mada.

Wiki iliyopita nilikamilisha uchimbaji na ujengeleaji wa KISIMA changu kwa matumizi ya nyumbani na maji yamepatikana kwa wingi japo Yana chumvi kidogo.

Sasa shida imeanza, Maji ukiyaangalia meupe na masafi lakini ukipikia vyakula kama ndizi zinaiva hali ya kuwa zimekuwa nyeusi sana. Ukipikia maharage yakiiva yanakuwa na rangi nyeusi au zambarau tofauti na rangi mloizoea ya maharage yakiiva.

Tangu tuanze kuyatumia maji haya kunawa na kuoga ngozi zetu zimebadilika rangi tumeanza kuwa weusi.

Baadhi ya vyombo vya plastic vyenye rangi nyeupe tunavyotumia kuchota maji haya vimebadilika na kuwa na weusi. Kwa sasa tumeacha kuyatumia Kwanza. Nipo Tabora.

MSAADA WA MAWAZO/USHAURI.

Natanguliza shukrani.
 
Unatakiwa ujisalimishe kwa watu wa Bodi ya Bonde la Kati ili wachukue sampuli na kuona wingi wa madini uliomo kwenye kisima chako.

Usichukulie poa mkuu mnaweza kuugua ugonjwa wa mifupa. Nimesema kujisalimisha kwa sababu umechimba kisima kinyemela bila kupata kibali kutoka kwao.

Hivyo kunaweza kuwa na faini lakini mwisho wa siku utatakiwa kulipia kila mwaka. Unaweza kusema chumvi ni kidogo kumbe imezidi kiwango kinachoruhusiwa!
 
Umechimba kisima chako mwenyewe?
Je umepeleka hayo maji kufanyiwa vipimo maabara?

Usitumie maji ya kuchimba ardhini bila kuyapima maabara utaua familia huenda kuna mwamba wenye kemikali hatarishi
Ni tabia ya watu wengi kupuuzia hili jambo la msingi.maji ni kitu hatari sana kama yatatumika kiholela,si tu kwa familia yake.watu wote watakaohusika na matumizi ya maji ya hicho kisima.
 
Nchi hii ina watu wapuuziaji afya sana
Muda mwingine sio upuuzaji wa afya Bali ni kutokuwa na Elimu na baadhi ya vitu.
Hata mimi nilikuwa sijui kuwa ukitaka kuchimba kisima ili uweze kutumia hayo maji kwa usalama lazima uyapeleke maabara yakapimwe.
Nimejua hili muda mfupi kidogo baada ya eneo nililopo kuchimbwa kisima.
Watu hatujui na wala hatupewi elimu
 
Muda mwingine sio upuuzaji wa afya Bali ni kutokuwa na Elimu na baadhi ya vitu.
Hata mimi nilikuwa sijui kuwa ukitaka kuchimba kisima ili uweze kutumia hayo maji kwa usalama lazima uyapeleke maabara yakapimwe.
Nimejua hili muda mfupi kidogo baada ya eneo nililopo kuchimbwa kisima.
Watu hatujui na wala hatupewi elimu
Afadhali umejua
 
Back
Top Bottom