Maji ya chupa ya Kilimanjaro yameanza kupotea sokoni Dar

Hill water ndo yanaongoza kwa kuuzika huku dar, yakifatiwa na afya, masafi etc maji ya Kilimanjaro yapo kwa uchache sana Madukani, cjui bonite hawana stock ya maji au watu hawayanunui tena

85% ya wakaazi wa Dar ni masikini wa kutupa!! Wengi huishi chini ya mstari wa dola moja kwa siku sasa watawezea wapi maji ya 1ltr kwa 1000-1500?

Hill water ni 500 tu unapata lita so ni kawaida ndo maana huwezi kuta biashara ya miguu na utumbo wa kuku iringa au Arusha.
 
Hill Water ndo yanaongoza kwa kuuzika huku Dar, yakifatiwa na Afya, Masafi etc.

Maji ya Kilimanjaro yapo kwa uchache sana Madukani, sijui Bonite hawana stock ya maji au watu hawayanunui tena.
Ile ladha ya awali ya maji ya Kilimanjaro haipo tena.

Ndio yalikuwa maji pendwa kwa miaka mingi ila nadhani kuna aidha mchanganyaji aliondoka au wameamua kubania mchanganyiko wa awali na ndio unaowaondoka sokoni. Sio Dar tu ila mpaka mikoani.

Nimekuwa nawaza kuanzisha thread kuwasema ila nashukuru nimepata lift hapa kuyasema niliyoyasema.

Kilimanjaro water is collapsing dramatically.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom