‘Maji ya chupa huathiri akili’

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
215,419
2,000
‘Maji ya chupa huathiri akili’

Imeandikwa na Evance Ng’ingo; Tarehe: 11th December 2010 @ 23:55

WATUMIAJI wa maji ya chupa yanayouzwa mitaani ambayo si salama yanaweza kusababisha matatizo ya akili.

Akizungumza katika uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Maji ya Chupa aliyofanya nchini, Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Professa Tolly Mbwete alisema kuwa tatizo hilo linasababishwa na kutopimwa kwa maji hayo.

Mbwete alisema kuwa Shirika la Ubora wa Viwango nchini (TBS) hupima ubora wa maji mara chache hasa wakati yakiwa yanazinduliwa na baada ya hapo ufuatiliaji wake huwa mdogo.

Ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza, alisema inapaswa kuundwa kwa chombo huru kitakachokuwa na jukumu la kufuatilia utengenezwaji wa maji ya chupa na kutoa taarifa kwa TBS na Ewura mara kwa mara.

Alifafanua zaidi kuwa kwa kuundwa kwa chombo hicho kutawafanya watengenezaji wa maji hayo kuwa makini na kufanya uzalishaji wake kuwa bora kwa lengo la kulinda afya ya mtumiaji.

Alisema kuwa hata maandishi yaliyopo katika lebo za chupa za maji hazionekani na maneno ya keni madogo kiasi cha kwamba mnywaji anakuwa hawezi kuyasoma.

Alisema kuwa zipo baadhi za kampuni na hoteli ambazo huweka lebo za biashara zao katika chupa za maji ambazo hawajazalisha kitendo ambacho kinapoteza maana halisi ya lebo za chupa za maji.

Pia alitoa wito kwa Serikali kufuatilia wasambazaji wa maji ya kuuza na kuwa wanatakiwa kufuatiliwa ili kubaini ubora wa maji hayo na usalama katika maeneo wanapoyachota.

Mbwete alisema kuwa hata watumiaji wa maji yanayosambazwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) hayana ubora kwa kuwa kutokana na uchakavu wa miundombinu ya usambazaji maji husababisha kiasi kikubwa cha maji kufika kwa mtumiaji kikiwa tayari
kimechanganyika na uchafu.

Pia alipinga tabia ya kukatika kwa maji kwa kisingizio cha kufanyiwa matengenezo kwa mitambo na kuongeza kuwa inatakiwa mitambo mingine kuwa tayari muda wote ili mmoja ukiharibika mingine ifanye kazi.

Uzinduzi huo wa ripoti ulihudhuriwa na maprofesa mbalimbali na pia alikuwepo Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya.
 

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,633
1,195
Waafrika ni kama domestic livestock! Huko vijijini toka kabla ya uhuru maji ni yale yale kwenye mashimo na chemi chemi tunazo changia kwa pamoja na mifugo!
 

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,360
2,000
Nilishawahi kusikia inabidi uyaweke juani kwanza reaction ya mionzi ya jua ifanyike ndio yawe salama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom