Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Katika hali isiyo ya kawaida na ya kuhatarisha jamii maji ya bahari ya Hindi yameibukia katika mitaro ya Mjimkongwe na eneo la soko kuu la Zanzibar na kuonekana kuwashangaza wananchi na kukumbwa na hofu.
ITV ilishuhdia maji hayo ya baharini yakiibukia katika mitaro ya soko kuu la Zanzibar liliko darajani na pia katika baadhi ya mitaa ya Mjimkongwe huku wananchi wakiendelea na shuguli zao kama kawaida ikiwemo biashara katika soko hilo, aidha baadhi ya mitaa ya Mjimkongwe yakionekana kujaa na kuzagaa maji hayo na usafiri wa abiria ukiendelea kama kawaida.
Wakizungumza na ITV baadhi ya wananchi na wafanyabiashara katika eneo hilo la darajani wameonekana kushangazwa na kuhofia hali ya hatari endapo maji hayo ya baharini yakizidi kasi na kiwango chake kuongezeka na kushauri serikali iliangalie suala hilo kwa maksudi na kuepukana na magonjwa.
Hata hivyo afisa uhuisano wa manispaa ya Zanzibar Mohamed Nassor Ali amesema hali hiyo ni ya kawaida na sio ya kutisha au hatari yeyote kwa wakazi wa maeneo hayo na maji hayo hujaa na kuizidi kiwango kwa muda mfupi tu.
Pamoja na kuwepo kwa uhakika wa manispaa, bado wakazi wengi wa Zanzibar wanaendelea kuwa na hofu ya maisha yao mbali ya kuona iko siku huenda samaki aina ya papa ataibukia hapo na maji hayo ya bahari yakazidi kasi na kubomoa mindombinu na kusababisha maisha ya watu kupotea.
Chanzo: itv