Maji ya Bahari ya Hindi Hayatoshi Kumwosha RPC Kamhanda Damu ya Daud Mwangosi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maji ya Bahari ya Hindi Hayatoshi Kumwosha RPC Kamhanda Damu ya Daud Mwangosi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Sep 9, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Mwandishi D.Mwangosi ameuawa kikatili na jeshi la Polisi-Iringa chini ya uongozi wa RPC Kamhanda; ila RPC huyo ajue kuwa anastaafu vibaya damu ya D. Mwangosi iliyomikononi mwake haitaoshwa hata kwa maji yote ya bahari ya Hindi.

  Aidha, ijulikane kuwa polisi wamekuwa tayari kumwaga damu ya watu wasionahatia kwa ajili ya kulinda maslahi ya mafisadi wachache waliojificha chini ya mwamvuli wa CCM. Polisi wameuwa waislam, wameuawa wakristo, wameuwa wanasisa, wameuwa wakulima, wameuwa wafanyakazi, wameuwa wateteao haki zao maeneo ya migodini. Polisi wameuwa watu wasionahatia vijijini na mijini; wameuwa barabarani, wameuwa maofisini, wameuwa misikitini (Mwembechai Msikitini miaka ya 90).

  Damu na matone ya damu ya waliouwa haiosheki mikononi mwao hata kwa maji yote ya bahari ya Hindi, Atlantic, wala Pacific.

  Katika Biblia Takatifu MWANZO 4:9-10 "BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika aridhi"
  Swali ili hili,Mungu wa Yakobo anawauliza watawalawa CCM na Polisi wao, "Wako wapi ndugu watanzania niowaweka chini yenu muwalinde?" Lakini ninyi kupitia tume zenu na kamati mnazoziunda kila mnapouwa mnamjibu Mungu wa Mbinguni sawa na Kaini alivyomjibu Yehova. Angalieni jibu la BWANA wa mbingu na nchi kwa Kaini.

  Nawaomba, watu wote mtakasoma thread hii, msihiriki kuwaambia polisi na wanaowatumikia kuwa Mungu amesema, ISAYA 42: 14-16 BWANA hatonyamaza tena, maombi ya watakatifu, wajane na yatima waliotokana na mauaji mnliyofanya hadi leo hii Mungu anyewawazia watu wake mawazo yaliyomema, amesikia kilio chao ameyaona machozi yao. HATONYAMAZA, hatonyamaza, hatonyamaza, hatonyamaza....na wote tuseme -Ameni!
   
 2. m

  mwitu JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 857
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Rpc kamuhanda ashitakiwe ikiwezekana anyongwe
   
Loading...