Maji shingoni, tafadhalini wazoefu katika hili naombeni ushauri.

mjenziwakale

JF-Expert Member
Sep 24, 2015
670
823
Salaam wakuu,

Niende moja Kwa moja kwenye mada. Katika shughuli zangu za ujenzi nimebahatika kupata kazi moja ya ujenzi Wa jengo la hospitali ya wilaya flani hapa nchini, ndo Niko katika hatua za kumaliza msingi Wa jengo Ila nimeishiwa hela kabisaaa na sina chanzo chochote cha kuweza kunisaidia kupata pesa ya kumalizia walau kipengele cha msingi Wa jengo niweze kudai malipo na Kwa taratibu huwezi kulipwa mpaka hatua ya msingi ikamilike. Hivo Nina Mpango nijiondoe katika mkataba huu ili niweze kulipwa kiasi changu cha kazi niliyokwisha Fanya.
Hivo basi naomba nipewe ushauri nifuate hatua gani ili niweze fanikisha adhima yangu.
N.B katika mkataba huu mwajiri ndo kajipa uwezo Wa kusitisha mkataba na Mimi fundi nitalipwa kulingana na kazi niliyokwisha Fanya, Ila Kwa fundi kusitisha mkataba hiki kipengele hakijaainishwa.
Natanguliza shukrani.
 
Huo mkataba utafanikiwa kuusutisha kwa kutumia kigezo za discharge by frustration kutokana na bankrupcy.
Ili uweze kuusitisha huo mkataba itabidi uthibitishe beyond a reasonable doubt kwamba hiyo frustratiom by bakruptcy ni unforeseen, and not self-induced na kikubwa pia itabidi uthibitishe kwamba hiyo bankruptcy iko beyond your controll na pia uthibitishe how it render your future performance impossible.

Baada ya kuthibitisha hayo ndipo mahakama ita terminate huo mkataba kutokana na bankruptcy.

Baada ya kuwa terminated then ndipo unaanza kurise a claim for a remedy of quantum meruit ambapo sasa utafai malipo kulingana na kazi uliyo ifanya.
 
Akilala mbele atakuwa ame repudiate contract na mahakama ikithibitisha hilo basi huyu jamaa atabidi alipe damages kwa hiyo hospital.
Atapata double loss, hapo cha msingi itabidi awataarifu hao waliompa hiyo kaz kama wakishindwa kumuelewa apeleke ombi lake mahakaman
Lala mbele mkubwa watakutafuta wenyewe
 
Back
Top Bottom