Maji shingoni mitandao - simu toka kwa kikwete

Sep 13, 2010
8
0
Wana JF leo hii asubuhi saa mbili na nusu hivi, nimepokea simu toka kwenye mtandao wangu wa zain, ikasema "helo subiri mhe kikwete anataka kuongea na wewe kisha nikamsikia kikwete akijieleza na kuomba kura"

Je hii yawezekana mitandao imeingia kwenye kampeni? anu JK kaamuru apigiwe debe? hii ni vipi jamani na namba ilikuwa unknown lakini sauti ya JK kabisa. nimepiga zain wanadai hakuna kitu kama hicho - what is this??????????

kweli ccm maji shingoni - kweli sasa nimeamini Slaa anamnyima usingizi JK.
 
shilingi ngapi zinatumika? zisingeweza kusomesha bure japo dara moja mwaka mzima?? iko right yangu ya privacy?
 
haaaaa imewekwa kwenye mtandao sauti hizoooo! duuu VERY EXPENSIVE!
 
Kama uchaguzi huu utakuwa huru na hakutakuwa na wizi wa kura, Thithiem itapigwa chini vibaya sana mijini na vijijini.
 
Wana JF leo hii asubuhi saa mbili na nusu hivi, nimepokea simu toka kwenye mtandao wangu wa zain, ikasema "helo subiri mhe kikwete anataka kuongea na wewe kisha nikamsikia kikwete akijieleza na kuomba kura"

Kweli yamemfika bila ubishi.........na ukweli ni kuwa hata kuchakachua kura zetu safari hii atashangaa mkono wa Mwenyezi Mungu unavyoziba mianya yote ya wizi wa kura...........
 
Zisikupe tabu kwani hizo zinaitwa robo calls na hata marekani pia wanatumia lakini mara nyingi huwa ni kwenye simu za nyumbani tena kwa gharama ya mwenye kampeni lakini kinachonishangaza ni kitendo cha sisi kulipia gharama ya simu kwa niaba ya jk hii inamaanisha kwamba anafanya kampeni zake kwa kutumia gharama zetu kwamba tumpe pesa zetu kwa ajili ya kampeni zake na siku ikifika nimpe kura. Kura yangu umeikosa na nitawapigia zain kudai pesa zangu kwa maana wao ndio walinipigia simu kwahiyo wanawajibika kuilipia.
 
No matter the election result Jk anatakiwa kuwa amepata funzo kubwa sana mwaka huu 2010.Awe Nje au ndani ya utawala we expect to see very new JK. kama hatabadilika basi atakuwa ana ugonjwa mbaya sana ambao yeye , sisi na watu wake wa karibu bado hatujaujua
 
Amefanya kampeni kwa garama kubwa sana ametumia kila aina ya njia ili ajitangaze, ametumia mabango yote mjini kujitangaza LAKINI UKWELI UPO PALEPALE WATU WAMEMCHOKA WANANCHI WAMEAMKA WANATAKA MABADILIKO YA KWELI WAMECHOKA KUNYONYWA NA CCM.

JK KUBALI MATOKEO ILI UWESHIMIKE

EWE MWANANCHI WA TANZANIA ULIFIKIA UMRI WA KUPIGA KURA NA UMEJIANDIKISHA MIEZI,SIKU ZIMEKWISHA SASA YAMEBAKI MASAA MACHAHE SANA KESHO KWA AMANI NA UTULIVU AMKA MAPEMA NENDA KAPIGE KURA YAKO YA URAIS KWA DR. SLAA NA WABUNGE PIA WA UPINZANI. TUNATAKA MABADILIKO YA KWELI
 
Sasa kama hakuomba kura jana na audience yote ile mbona anakuwa anajikanyagakanyaga! tumueleweje?
 
Kweli yamemfika bila ubishi.........na ukweli ni kuwa hata kuchakachua kura zetu safari hii atashangaa mkono wa Mwenyezi Mungu unavyoziba mianya yote ya wizi wa kura...........
Yap, you put it right, Mungu yu upande wetu, si siku zote tutanyanyaswa na kuibiwa, safari hii mkono wake utatushindia, na atamkumbuka mnyonge wake tanzania aliyerubuniwa kwa miaka mingi sana.
 
Mafisadi achana nao. Tukisema nchi hii sio maskini watu wengine hawaelewi. Tunachokosa ni viongozi wenye kiu ya kutumikia taifa. Raslimali tunazo na uwezo wa kuwa na maisha bora upo kabisa
 
No matter the election result Jk anatakiwa kuwa amepata funzo kubwa sana mwaka huu 2010.Awe Nje au ndani ya utawala we expect to see very new JK. kama hatabadilika basi atakuwa ana ugonjwa mbaya sana ambao yeye , sisi na watu wake wa karibu bado hatujaua

Angekuwa kwenye kipindi cha kwanza basi labda angebadilika lakini kwa kuwa ni kipindi cha mwisho, then, he has nothing to lose my friend, ila ninahofia kulipiza visasi na matusi atakavyotubeza kama akishinda!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
peleka kura yako kesho kwa slaa..............kamwe ccm hawawezi kubadilisha mioyo ya watz walioamua mabadiliko......
 
Wana JF leo hii asubuhi saa mbili na nusu hivi, nimepokea simu toka kwenye mtandao wangu wa zain, ikasema "helo subiri mhe kikwete anataka kuongea na wewe kisha nikamsikia kikwete akijieleza na kuomba kura"

Je hii yawezekana mitandao imeingia kwenye kampeni? anu JK kaamuru apigiwe debe? hii ni vipi jamani na namba ilikuwa unknown lakini sauti ya JK kabisa. nimepiga zain wanadai hakuna kitu kama hicho - what is this??????????

kweli ccm maji shingoni - kweli sasa nimeamini Slaa anamnyima usingizi JK.

Hata mimi jana nilipokea hiyo cm mida ya saa 9 alasiri nikaambiwa nisubiri kidogo mhe dr jk anataka kuongea na mm,mara nikasikia sauti yake nikashangaa kuona leo natafutwa na rais,nimechoka kabisa kwa stahili hii ikulu ataisikilizia kwaoooo ukwereni kesho jamani kura kwa dr slaa jamani.
 
No matter the election result Jk anatakiwa kuwa amepata funzo kubwa sana mwaka huu 2010.Awe Nje au ndani ya utawala we expect to see very new JK. kama hatabadilika basi atakuwa ana ugonjwa mbaya sana ambao yeye , sisi na watu wake wa karibu bado hatujaujua

Wala HATABADILIKA. Kwani atakuwa na haja na nyie tena? keshaukwaa Urais na hatogombea kipindi kingine tena!

Hakuna sababu ya kufanya majaribio na kuona kama atabadirika au la. Ni kumnyima kura tu. Kwishnehii
 
nami ndo namaliza kusoma sms kutoka kwa
jmkikwete anomba kura yangu kesho,eti kipindi kilichopita nilimpa heshima kubwa wa kuwa rais wa tanzania na akafanya mambo mengi.nimpe tena kura yangu kwa mara nyingine.
Pole kikwete, kwa taarifa yako sikupiga kura awamu iliyopita kwa sababu sikuwa na sifa,kesho nitaenda kupiga kura kwa mara ya kwanza na kura yangu nampa dr slaa.
Unajivunia wanafunzi wa vyuo kusoma kwa mkopo wakati mkopo wenyewe hawapati wanaosthili na badala yake wanapata watoto wa vigogo.
Na kwa kijua ni watoto wa vigogo ndio wanapata mikopo hiyo unatangaza kwenye kampeni zako kuwa mikopo hiyo ni kama bure kwani hawalazimishwi kulipa.
 
Back
Top Bottom