SoC01 Maji safi yaweza kuwa si salama kwa matumizi

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 13, 2021
6
6
Maji ni sehemu ya kundi la chakula na yana umuhimu mkubwa sana kiafya katika kufanikisha kazi mbalimbali mwilini .

Viungo vingi vya mwili ili viweze kufanya kazi vizuri vinahitaji maji , zaidi ya asilimia 60 ya uzito wa mwili wa binadamu ni maji ,Hivyo maji husaidia mwili kufanya kazi mbalimbali .

Kiafya mtu mzima anashauriwa kutumia walau kiasi cha lita moja na nusu kwa siku huku watoto wanapaswa kupewa maji kulingana na uhitaji .

Kuna faida nyingi sana kiafya zitokanazo na matumizi ya maji safi na salama .
Unywaji wa maji ya kutosha hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo ,

utafiti uliofanywa Marekani kwa muda wa miaka sita unaonesha watu wanaotumia maji ya kutosha walau glass tano kwa siku hujiepusha na hatari ya kupata maradhi ya moyo kwa asilimia 41 zaidi ya wale wanaokunywa glass mbili au chini ya hapo , maji pia husaidia kuondoa sumu mwilini kwa kuondoa uchafu wote kwa njia ya haja kubwa na ndogo, mwili unapokua na maji ya kutosha humfanya mtu kufanya mazoezi ya kutosha na hivyo kupata faida ya mazoezi ipasavyo , maji pia husaidia kupunguza uzito kwa sababu maji hayana mafuta, karoli wala sukari.

Lakini muhimu hapa si maji tu bali maji yanayofaaa kwa matumizi ya binadamu , ni muhimu sana kutumia maji safi na salama ili kulinda afya yako kwani matumizi ya maji yasiyofaa huweza kuleta athari mbalimbali kiafya ikiwemo kupatwa na maradhi.

Uchafuzi wa maji ni hatari kubwa ambao watu kutumia maji yasiyofaa kwa binadamu kama ambavyo ripoti zinaonyesha kuwa wengi huathirika pakubwa kutokana na maji yasiyofaaa kwa matumizi huku watoto wakiwa wahanga wakubwa zaidi .

Ripoti ya umoja wa mataifa inakadiria kuwa watoto 4000 hufa kila siku kutokana na kutumia maji machafu.

kuna uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya maji yasiyofaa pamoja na kudorola kwa afya za watu.

Watu hufikiria maji ni salama iwapo tu hayana wadudu lakini kuna kemikali zingine ambazo hazihitajiki hata kidogo kwenye maji anayopaswa kutumia binadamu ambazo huingia katika maji kutokana na shughuli mbalimbali za binadamu hivyo yakitumika huweza kuleta athari za kiafya kwa binadamu’

Wakati mwingine maji huonekana safi na salama ilihali sio salama kwa matumizi yanaweza kuwa na wadudu lakini kemikali ambazo sio rahisi muda mwingine kutambua hilo hivyo anaitaka jamii kuwa makini kuhakikisha wanapata na kutumia maji safi na salama yanayofaa kwa matumizi ya binadamu.

Kama ambavyo ripoti zinaonyesha kuwa watoto ndio wahanga wakubwa zaidi katika kutumia maji yasiyofaa kwa matumizi miongoni mwa maradhi ambayo huwapata watoto ni pamoja na typhoid, kipindupindu,kuhara na polio.

Hakika watoto wapo katika hatari kubwa na wanaathirika pakubwa na uchafuzi wa maji ambao hupelekea kutumia maji yasiyofaa pasi na wao kufahamu Hivyo yawapasa wazazi, walezi na jamii kuhakikisha kila mmoja anahakikisha watoto wanapata na kutumia maji safi na salama ili kuwalinda watoto ambao ni taifa la kesho.

Kumekua na jitihada nyingi za kupambana na uchafuzi wa mazingira ambao huwa chanzo ya kutopata maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu lakini bado tuna safari ndefu ya kwenda kabla ya kufikia tunapopahitaji , tunahitaji mazingira safi kwa hewa tunayovuta, maji tunayokunywa na udongo tunaopandia chakula chetu wakati rasilimali hizi zinapochafuliwa ardhi yetu na maisha yetu yanakua hatarini muhimu ni kila mmoja kuhakikisha anayalinda mazingira ili yawe salama kwa watu wote.
 
Back
Top Bottom