Maji mtera na kuapnda bei ya umeme Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maji mtera na kuapnda bei ya umeme Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kubingwa, Jan 14, 2012.

 1. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nchi ya kufikirika,Tanzania.
  Tuliambiwa kuwa kupanda kwa gharama za maisha kunatokana na kuporomoka kwa uchumi ulaya na marekani.Na hivi karibuni Iran,mzalishaji mkubwa wa mafuta duniani ,marekani imeiwekea vikwazo na kama haitoshi Iran nayo inatishia kuufunga ule mfereji ambao meli huingilia na kutokea zikiwa zinakwenda kuchukua mafuta nchi za kiarabu.

  Swali la kwanza:
  Hali itakuwaje Tanzania endapo vikwazo vya marekani kwa Iran vitakapoanza kuiathiri dunia?, maana hata Nigeria hali nako si salama.

  Swali jingine:
  Mafuriko yote haya na mvua zinaoendelea kunyesha huko home ina maana bwawa la mtera limekauka na kama halijakauka itakuwaje litakapo kuja kauka kipindi cha kiangazi?

  Maisha bora kwa kila Mtanzania ndo kupanda kwa bei ya mafuta na umeme? Serikali kupitia EWURA hakuna jipya,siasa zimejaa tu na kama wanalipa deni la Dowans si waseme tu,siri za nini?

  Swali la Mwisho: Kwa nini wenye migodi walipe nafuu na mlalahoi alipe zaidi?
   
 2. f

  frontline1 Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hili ni tatizo kubwa, wa tz tunaumasikini wa fikra otherwise tungetumia fursa ya vikwazo kwa Irani kama nafasi yakupata soko la gas yetu na mafuta yetu. badala yake tunaona hali hii kama tangazo la tanzia!

  sikuzote gharama za maisha zikipanda anayeathirika ni mlaji wa chini kabisa bse wakubwa wao wana exemption kibao, allowances kibao, nyumba maji, umeme, maid n gari wanapewa na serikali!

  2nahitaji mapinduzi ya fikra !
   
Loading...