Maji Marefu aomba radhi kuhusu kauli ya Dk. Ulimboka

maji yakimwagika watu hutafuta visingizio tele. Hata Liwalo na Liwe hakujua kwamba anajibatiza jina jipya, damu na machungu ya ubatizo wake vilipojiri akaanza oooo, eeeee, uuuuu.....Ni janja ya nyani kula mahindi mbichi tu.
 
Huu ni upunga zeze hivi siyeye mwenye alizungumza maneno haya?leo anakuja kukana?akushirikisha ubongo wakati anatoa hiyo kauli?Lakini sishangai coz hata Arumeru Mashariki alikana kwenda kwenye kambi ya CDM
 
Wadau jana niliangalia bunge,huyu jamaa ni kweli aliongea hayo aliyoongea na aliambiwa na spika asiongee mambo ya madaktar akang'ang'ania zaid,kisha akakalishwa chini,aliponyanyuka akasema amechanganyikiwa kwa kuwa amezushiwa kifo,
lakini alisema madaktar wasimtibu ULIMBOKA wao si wamegoma?????
Sasa kama anasema alinukuliwa vibaya alinukuliwa na nani???na alitaka watu wamnukuu vipi,maana it waz live show kwakweli jaman,na hao waandish kama wamekubali kuhubiriwa bila kumhoj zaidi?????
 
403882938.jpg

421463554.jpg


Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu", akizungumza na waandishi habari mjini Dodoma jana, amekanusha madai kuwa alilieleza Bunge kuwa mkasa uliompata Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari na Kamati ya kufuatilia haki zao, Dkt. Steven Ulimboka, kuwa alistahili, SI YA KWELI na KUOMBA RADHI Madaktari nchini kwa jinsi alivyonukuliwa vibaya wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni tarehe 28 Juni 2012.

Jana, Mbunge huyo
alinukuliwa
na vyombo vya habari kuwa alisema, "kipigo alichopata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dkt. Steven Ulimboka, kinastahili ili naye apate machungu wanayopata wagonjwa wengine mahospitalini."

Kauli hiyo ilisababisha tafrani kidogo bungeni, ambapo Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda alilazimika kuingilia kati kumzuia Ngonyani asiendelee kutoa kauli hiyo kwa vila suala la madaktari bado liko Mahakamani.


Hawa waganga wanaloga mpaka mama zao si watu wa kuaminiwa kabisa

 
Bongo , bado sana , si huyo mchawi tu..bali wasaniii wa bongo fuleva na taarab kibao bungeni...ndio maana asilimia kubwa ya bajeti inaishia kwenye uendeshaji wa serikali tu na si shughuli za maendeleo
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana na hasa wapiga kura wa Jimbo la Korogwe Vijijini ni nani aliyewaloga hata mkampeleka Mchawi/Mshirikina, mcheza tunguli, msoma nyota, mbashiri Bungeni?? Vijana waliosoma mpaka University hawapo au aliwaloga?? Na chama kilichomteua kilifikiria nini?? Nchi inaongozwa na wachawi na washirikina na waganga halafu tuendelee kivipi??? Mungu uliyeumba Mbingu na nchi iponye Tanzania. Amen!!!
 
Back
Top Bottom