Majeshi yetu kugeuka wauaji wetu siyo dalili nzuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majeshi yetu kugeuka wauaji wetu siyo dalili nzuri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Mar 19, 2012.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Katika siku za hivi karibuni kumeanza kuzoeleka kasumba kwa majeshi yetu kuua raia kwa kisingizio cha kujihami, serikali isipolishughulikia tatizo hili kwa haraka na uadirifu ipo siku tutashudia mauaji ya haraiki kwa kisingizio cha kujihami pale wananchi watakapo amua kuchukua sheria mikononi.

  Nakumbuka enzi za Mwalimu askari walifundishwa kuwapiga miguu wananchi pale ilipolazimika kujihami. Mbinu hii ya askari kwetu ilianza kusahaurika pale mwembechai pale ambapo wananchi walilengwa kichwani na mgongoni walipokuwa wakikimbia, hata mauaji mengi yanayofanywa na polisi na majeshi mengine marehemu huwa wamepigwa juu ya kiuno na mara nyingi hupigwa kwa nyuma wakiwa wanakimbia kuokoa maisha yao.

  Nadhani kuna mbunge atajitokeza kuleta hoja binafsi kuomba tume maalum ya kuchunguza mauaji ya raia na majeshi yetu vinginevyo tutegemee maafa
   
Loading...